Meli kubwa ya kifahari ya Watalii ikiwa na Watu 829 ndani yake wakiwemo Raia wa Marekani, Uingereza na Mataifa mengine imetia nanga katika Bandari ya Dar es salaam kabla ya kuelekea Msumbiji ikiwa ni moja ya sehemu ilizopanga kuzitembelea.
Baada ya kuipokea meli hiyo, Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es salaam, Mrisho Mrisho ameiambia @AyoTV_ kuwa kwa wastani Bandari ya Dar es salaam hupokea meli za aina hii kuanzia nane hadi kumi kwa mwaka zikiwa zinatembeza Watalii kutoka maeneo mbalimbali ya dunia huku zikipambwa na huduma zote za kifahari zinazopatikana kwenye hoteli zenye hadhi.
#MillardAyoUPDATES