Watanzania wanaoishi katika nchi mbalimbali za Ulaya ikiwemo Ujerumani, Bulgaria, Czech Republic, Hungary, Poland, Romania, Slovakia, Uswisi na Vatican wamekaribishwa kushiriki katika clinic maalum itakayofanyika jijini Berlin tarehe 2 hadi 3 Mei mwaka huu.
Akizungumza kuhusu maandalizi ya tukio hilo, Balozi Hassan Iddi Mwameta amesema clinic hiyo inalenga kuwakutanisha Watanzania wa diaspora na wadau muhimu wa maendeleo kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, kwa lengo la kuwakaribisha kushiriki kikamilifu katika fursa za kiuchumi na kijamii zinazopatikana nchini.
Amebainisha kuwa miongoni mwa wadau watakaoshiriki na kutoa huduma ni pamoja na Idara ya Uhamiaji, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), UTT AMIS, taasisi za kifedha na mabenki, pamoja na mifuko ya hifadhi ya jamii na Mamlaka ya Bandari Tanzania.
Kwa mujibu wa Balozi Mwameta, uwepo wa taasisi hizo utatoa nafasi kwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi kupata huduma muhimu karibu yao, huku wakipewa taarifa sahihi kuhusu uwekezaji, fursa za biashara na michango yao katika maendeleo ya taifa. #CloudsDigitalUpdates
Kuhusu suala la vita ya Israel/Marekani na Iran imeisha au haijaisha, lango la Hormuz limefunguliwa au bado?, mazungumzo yamefikia wapi?, @FKihamu anajibu maswali hayo yote. #PBCloudsFM
Bei ya mafuta katika soko la dunia imeanza kushuka huku masoko ya hisa yakipanda, kufuatia makubaliano ya kusitisha mapigano kwa masharti ya wiki mbili kati ya Marekani na Iran, yanayojumuisha kufunguliwa upya kwa njia muhimu ya usafirishaji kupitia Mkondo wa Bahari wa Hormuz.
Bei ya mafuta ghafi ya kimataifa ya Brent imeshuka kwa takriban asilimia 13 hadi dola 94.80 kwa pipa, huku mafuta yanayouzwa nchini Marekani yakipungua kwa zaidi ya asilimia 15 hadi dola 95.75. Hata hivyo, pamoja na kushuka huko, bei za mafuta bado ziko juu ikilinganishwa na kabla ya kuanza kwa vita hiyo, ambapo mafuta yalikuwa yakuzwa kwa wastani wa dola 70 kwa pipa.
Inatarajiwa baadhi ya meli za mafuta zilizokuwa zimekwama huenda sasa zikaanza kupita wakati wa kipindi cha usitishaji mapigano, jambo litakalosaidia kupunguza gharama katika masoko ya nishati katika wiki zijazo.
Gharama za nishati zilipanda kwa kasi kufuatia kusitishwa kwa usambazaji wa mafuta na gesi kutoka Mashariki ya Kati, baada ya Iran kutishia kushambulia meli zinazopita katika Mkondo wa Bahari wa Strait of Hormuz kama hatua ya kulipiza kisasi dhidi ya mashambulizi ya Marekani na Israel, ambapo kwa Tanzania bei iliongezeka kwa takribani shilingi 1000 kwa lita.
#CloudsDigitalUpdates
Akizungumzia maoni ya baadhi ya watoa huduma ya usafirishaji, Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, CPA, Dkt. Habibu Suluo ameeleza ya kwamba, kikokotoo wanachotumia kwa ajili ya kupanga nauli za usafiri, hakioneshi kwamba wasafirishaji watapata hasara kwa sasa kutokana na mabadiliko mapya ya kupanda kwa bei ya mafuta nchini.
Watoa huduma za usafiri wamesisitizwa kuendelea kutoa huduma, na kukaribishwa kwa ajili ya majadiliano na LATRA na si kusitisha kutoa huduma hizo, kwa kufanya hivyo LATRA itachukua hatua ya kusitisha leseni zao. #CloudsDigitalUpdates
Jumla ya sh. trilioni 1.77 zinahitajika kwa ajili ya ujenzi wa madarasa, maabara, ajira mpya za walimu, ruzuku ya mitihani, ya vitabu na uendeshaji kwa wanafunzi zaidi ya milioni tatu wanaotarajiwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka 2028.
Hayo yamesemwa Bungeni, jijini Dodoma leo (Jumatano, Aprili mosi, 2026) na Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba wakati akiwasilisha Mapitio na Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa Mwaka 2026/2027.
“Tathmini inaonesha kuwa wanafunzi 3,021,177 wanatarajiwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka 2028. Jumla ya gharama zinazohitajika ni shilingi trilioni 1.77 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 23,226; matundu ya vyoo 46,632; maabara 9,366; ajira mpya za walimu 40,192; ruzuku ya vitabu na uendeshaji pamoja na ruzuku ya mitihani na upimaji,” amesema.
Amesema mahitaji hayo yanatokana na uamuzi wa Serikali kuimarisha sekta ya elimu kwa kuzingatia Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 (Toleo la 2023), mitaala iliyoboreshwa, mipango na mikakati mbalimbali ikiwa na lengo la kuzalisha rasilimaliwatu wenye ujuzi na maarifa stahiki yatakayowezesha kumudu ushindani wa ajira na uwezo wa kujiajiri ndani na nje ya nchi.
⁷ Wakuu wa Mikoa wasimamie kikamilifu maandalizi na mapokezi ya wanafunzi wa elimumsingi ya lazima ya miaka 10 watakaojiunga na kidato cha kwanza mwaka 2028 kwa kukamilisha miundombinu na huduma zote muhimu.
“Tunaposema elimu ya lazima kuwa miaka 10, kimsingi tunasema tulikuwa na sekondari kila kata, sasa tunaongelea kuwa na shule ya sekondari kila kijiji. Lazima tujiandae kwa miundombinu pamoja na maoteo ya mahitaji yote ya kutekeleza mpango huo.”
#CloudsDigitalupdates
Inawezekana kwenye macho ya watu wengi, wakaona @darcitybball imefungwa na kibonde lakini @kotinyotz kutoka Pretoria anatupatia uchambuzi wa kina kuhusu mchezo wa leo #CloudsDigitalUpdates
Baada ya msimu wa Malkia wa Nguvu 2026 kuzinduliwa rasmi, makao makuu ya nchi Dodoma 104.4 yamepewa heshima ya kunyoosha na Kukoleza Level kwa kanda ya kati April 25. Fuatilia Clouds FM, Clouds TV na Clouds Digital kufahamu michongo yote ya #MalkiaWaNguvu2026#KolezaLevels
Kwa utafiti mdogo aliofanya @SamSasali kuhusu upatikanaji wa mafuta inaonyesha kuanzia April 1 itakuwa siku ya kwanza ya maumivu kwenye sekta mbalimbali kutokana na kupanda kwa bei ya bidhaa hiyo muhimu #PBCloudsFM
Rais Mstaafu Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jopo la Wazee la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Panel of Elders - POE), na Mwakilishi wa Ngazi ya Juu wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika katika juhudi za kutatua mgogoro wa Sudan Kusini, amekutana leo na timu ya mpira wa kikapu ya Dar City inayoshiriki Michuano ya Ligi ya Mpira wa Kikapu Afrika (Basketball Africa League (BAL) 2026, inayoendelea jijini Pretoria, Afrika Kusini. #CloudsDigitalUpdates
Wananchi wa mkoa wa Iringa wamejitokeza kwa wingi kushiriki misa ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Isimani, marehemu William Lukuvi, iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Jimbo la Iringa, Parokia ya Kihesa, huku majonzi na simanzi vikitawala miongoni mwa waumini na waombolezaji.
Misa hiyo imeongozwa na Askofu wa Jimbo Katoliki Iringa, Romanus Mihali, ambaye katika mahubiri yake aliwakumbusha waumini umuhimu wa kuishi maisha ya uadilifu, upendo na kujitoa kwa jamii, akieleza kuwa marehemu Lukuvi ameacha alama ya utumishi uliotukuka katika jamii na taifa kwa ujumla.
#CloudsDigitalUpdates
Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga linawashikilia watu wanne kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Mwajabu Shabani (30) pamoja na mwanaye wa miezi minne, Mwantumu Abdullah, katika kijiji cha Kisangasavwa, wilayani Kilindi mkoani Tanga.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, ACP Almachius Muchunguzi, tukio hilo la kuuawa kwa mwanamke huyo na mtoto wake mchanga limetokea Machi 28 mwaka huu majira ya saa 9 jioni. #CloudsDigitalUpdates
"Tunasimamia maelekezo ya Serikali kwamba Coco Beach haiuzwi, hata maboresho yatakayofanyika wafanyabiashara watajumuishwa. Na Leo kubwa ni kuwa na mazingira ambayo ni nadhifu na wezeshi zaidi kwa kufanya biashara na yanayovutia zaidi wageni na sisi wenyewe Watanzania"- Mhe. Saad Mtambule, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.
#LiveOnClouds360
#LainiYawana
#Clouds26Nyoosha
Ni miaka 7 tangu Jasiri Muongoza Njia, Ruge Mutahaba atangulie mbele ya haki.
Asante kwa kuifungua Dunia na kuchonga barabara za vijana wengi ambao kupitia maono yako wanaendelea kunyoosha.
Daima utaishi ndani yetu, #Clouds26 tunaendelea kusherekea maisha yako RUGE MUTAHABA.
#Miaka7YaJasiriMwongozaNjia
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (@engmaryprisca) ameshiriki katika Jukwaa la Tisa la Biashara Barani Afrika, linalofanyika Addis Ababa, Ethiopia tarehe 16 hadi 17 Februari, 2026.
Kaulimbiu ya Jukwaa hilo ni: Kugharamia Mustakabali wa Afrika: Ajira na Ubunifu kwa Mabadiliko Endelevu” (Financing the future of Afrika: Jobs and Innovation for Sustainable Transformation.)
Jukwaa hili la kimkakati linawakutanisha Serikali, Wawekezaji, Wafanyabiashara, Taasisi za Fedha na Wadau wa Maendeleo kwa lengo la kubadilishana uzoefu, kuimarisha ushirikiano na kuweka mazingira wezeshi yatakayowawezesha vijana na wanawake kushiriki kikamilifu katika biashara na uwekezaji.
Kupitia ushiriki huu, Tanzania inaendelea kusisitiza dhamira yake ya kuchochea ajira, ubunifu, ukuaji wa viwanda, upatikanaji wa masoko na mitaji, na kuharakisha mabadiliko endelevu ya kiuchumi barani Afrika.
Gen-Z wote wamekubali kuwa uzi ni mkali na unafaa sana kwa mitoko sio tu Damdam Marathon.
#NyooshaLuv na uzi wako wa #Damdammarathon2026 ambao tayari umeanza kutolewa sambamba namba za kukimbilia wewe na yule DamDam wako mliojiandikisha.
VITUO VYETU NI
MLIMANI CITY
KUNDUCHI MALL.
Zimebaki siku 3 jihakikishie sasa nafasi yako na mwenzako ya kukimbia kwenye msimu wa sita wa #DamDamMarathon tarehe 14/2/2026 kwa kujisajili kwa kulipia 50,000 tu kwa watu wawili ambapo mtapata t-shirt,namba za kukimbilia na medali baada ya kumaliza kukimbia.
Kujisajili fanya malipo kupitia SELCOM PAY kwa mtandao wowote wa simu kubonyeza *150*50*1# kisha ingiza lipa namba 61 23 44 25 halafu weka kiasi 50,000 na jina litakuja Clouds Media Group. Baada ya kufanya malipo tuma meseji kwenda namba 0779 888 839 ukiweka majina yenu,size za tshirt na umbali mtakao kimbia.
Uzi wa kibabe sana huu. Umethibitishwa kwa viwango vya juu sana vya ubunifu na hakuna doubt tunang’aa.
Uzi wa Damdam unapatikana VITUO VYETU VYA
-MLIMANI CITY
-KUNDUCHI MALL
ili uweze kuchukua KIT zako mara baada ya kujisajili.
Zimebaki siku 3 jihakikishie sasa nafasi yako na mwenzako ya kukimbia kwenye msimu wa sita wa #DamDamMarathon tarehe 14/2/2026 kwa kujisajili kwa kulipia 50,000 tu kwa watu wawili ambapo mtapata t-shirt,namba za kukimbilia na medali baada ya kumaliza kukimbia.
Tumesalia hatua chache kabla ile button ya SOLD OUT kuweza kubonyezwa 🎬, nafasi zimebaki chache sana #KM 5,10 na 21, maandalizi ya kuelekea kilele cha #Damdammarathon2026 yakishika hatamu viunga vya 88.5 MHZ DAR ES SALAAM.
Jihakikishie sasa nafasi yako na mwenzako ya kukimbia kwenye msimu wa sita wa #DamDamMarathon tarehe 14/2/2026 kwa kujisajili kwa kulipia 50,000 tu kwa watu wawili ambapo mtapata t-shirt,namba za kukimbilia na medali baada ya kumaliza kukimbia.
Kujisajili fanya malipo kupitia SELCOM PAY kwa mtandao wowote wa simu kubonyeza *150*50*1# kisha ingiza lipa namba 61 23 44 25 halafu weka kiasi 50,000 na jina litakuja Clouds Media Group. Baada ya kufanya malipo tuma meseji kwenda namba 0779 888 839 ukiweka majina yenu,size za tshirt na umbali mtakao kimbia.