#Usipoteze Muda wako kumng'ang'ania Mtu utafikiri ulizaliwa nae, Mtu mliyekutana nae Ukubwani huwezi kujifanya unamjua zaidi ya anavyojijua yeye
#Mtoto wa Mungu
"Wakati ule Yesu akajibu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga."
Natoa moyo wangu
kwa Yesu Kristo,
Natoa akili yangu
kwa Yesu Kristo,
Natoa roho yangu
kwa Yesu Kristo,
Natoa mwili wangu
kwa Yesu Kristo,
Nakabidhi familia yangu
na maisha yangu
kwa Yesu Kristo.
Yesu, ninakutumainia.
Yesu, ninakupenda.
Yesu, nisaidie.
Amina!
Mbunge wa Kigoma Mjini, Clayton Chipando maarufu Baba Levo, amenaswa kwenye video akibishana na maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) waliofika kwa msanii Ommy Dimpoz wakiwa wameambatana na askari Polisi kukamata Gari la msanii huyo kwa kile kilichodaiwa ni ukwepaji wa ulipaji wa kodi
Tukio hilo limetokea wakati maafisa hao walipofika kwa msanii huyo kwa ajili ya kushughulikia suala linalohusiana na tuhuma hizo.
#KitengeUpdates
VIDEO:
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padre Dkt. Charles Kitima, amebainisha kuwa demokrasia halisi katika nchi yoyote inasimikwa kwenye utawala wa sheria, uhuru wa mahakama, uhuru wa kitaaluma wa wasomi, na uhuru wa vyombo vya habari
Akizungumza leo, Septemba 15, 2026, mkoani Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani yaliyoratibiwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Padre Kitima ameeleza kusikitishwa kwake na kupungua kwa uhuru wa kitaaluma nchini, akibainisha kuwa tofauti na zamani ambapo jamii ilikuwa ikisikiliza na kupata miongozo kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, siku hizi maprofesa na wasomi wamekuwa wakiwekwa ndani.
Akitahadharisha kuhusu athari za maisha ya hofu kwa ukuaji wa uchumi na ubunifu, Padre Kitima ameongeza kuwa nchi haiwezi kufikia uchumi unaotegemea maarifa iwapo wananchi na wasomi wanaishi kwa hofu, huku akisisitiza kuwa uhuru wa vyombo vya habari vya kijamii na vya kawaida ni nguzo nyingine kuu.
Hakuna uhusiano ulio mkamilifu. Kila uhusiano huwa na nyakati nzuri na za
changamoto. Wale wanaoweza kuvuka changamoto hizo zote ndio wanaopendana kweli.
Uhusiano wetu sisi kwa sisi (wana ndoa/watarakiwa) unakuwa vivyo hivyo.
Halikadhalika, sisi mbele za Mungu hatupo wakamilifu katika uhusiano wetu na Yeye. Mara zote tumekuwa tukili halifu Neno la Mungu, lakini Mungu mwenyewe kwa upendo wake ametuita turejee kwake (kuturudishia uhusiano wetu na Yeye).
Ukimpenda Mungu ukweli utalishika Neno lake.✍🏾
Baba wa Mbinguni,
Ninakuamini leo
kwa moyo wangu wote.
Ninakuamini kesho kwa
matumaini yangu yote.
Ninakuamini kwa mafunzo
katika maisha yangu.
Ninakuamini kwa maisha
yangu ya mbele na ndoto zake.
Ninakuamini kwa kila kitu
sasa na hata milele.
Asante kwa kuwa nami
na kuniongoza!
Wakikupenda watasema UNAJIAMINI.
Wakikuchukia, watakuita mwenye MAJIVUNO.
Kuna tusi linamaanisha we mkali, Kuna sifa zinamaanisha kejeli.
Muda mwingine si kile unachoambiwa, bali ni sababu nyuma ya kauli zao.
Take notes..👍
𝐓𝐚𝐟𝐚𝐤𝐚𝐫𝐢; Yesu anatutia moyo: Usiogope upinzani wala usifiche ukweli. Mungu anatutunza zaidi kuliko mbayuwayu. Uamuzi wetu wa kumkiri au kumkana Kristo hapa duniani una matokeo ya milele. Hofu ya binadamu inaondolewa na imani katika Mungu.
Baraka za Jumamosi..
Bwana haoni
mambo vile ambavyo
sisi tunaona.
Watu wanahukumu kwa
muonekano wa nje,
lakini Bwana anatazama
moyo.
📖~1 Samweli 16:7
Uwe na Wikiendi Njema..👋🏽