#OnThisDay in 2⃣0⃣1⃣9⃣ we visited Tanzania to face Simba SC in a friendly 🇹🇿
An unforgettable experience sharing football and friendship with our Tanzanian friends ❤️🤍
Iko hivi,
Kukakola moja yenye mls 350 ina takriban gramu 39 za sukari, sawa na vijiko 10 vidogo vya chai vya sukari.
Funta Chungwa yenye mls 350 ina takriban gramu 44 za sukari, sawa na vijiko 11 vidogo vya chai vya sukari.
Pipsi yenye mls 350 ina takriban gramu 41 za sukari, sawa na vijiko 10–11 vidogo vya chai vya sukari.
Upande mwingine, chai unayoweka vijiko vidogo, kawaida vijiko vidogo 1 mpaka 3, vina takriban gramu 8–9 za sukari tu.
Mpaka hapa utaona chai ni bora zaidi kuliko soda, kwa sababu ina sukari kidogo sana na haina madhara makubwa ikiwa inakunywa kwa kiasi.
Sasa utamu upo hapa, hizi sukari zinatofautiana, hapa ndipo madhara ya soda yanaonekana.
Sukari iliyopo kwenye soda inaitwa high-fructose corn syrup (HFCS) au sucrose, hii inatengenezwa kutoka kwenye mahindi, ni mchakato mrefu, mahindi yanachemshwa, unga wake unachakatwa na kemikali na ule wanga unabadilishwa kuwa glucose kisha sehemu yake inabadilishwa kuwa fructose, huu utamu wake balaa, ndio sukari ya soda, kifupi soda ule utamu ni kemikali zimechanganywa.
Sasa mwilini hii sukari ya soda huchakatwa na ini, na ukinywa nyingi, yaani zaidi ya unavyohitaji (nguvu unazotunia au mazoezi) ndipo ini hubadilisha kuwa mafuta ili itunze kenye stoo za mwili (nyuma matakoni na tumboni), mtu ananenepa, mafuta yanaongezeka mwilini + sukari na hapo ndipo anasogelewa na magonjwa ya kisukari na moyo.
Sukari ya chai hii tunakoroga yenyewe ni sucrose ya kawaida, yaani table sugar, kwanza tofauti na ile ya soda inayotokana na mahindi hii inatokana na miwa au beetroot, pili hii unakunywa gramu chache tu (8-9) na tatu mwili huitumia sukari hii moja kwa moja kama nishati na hatari ya kubadilishwa mafuta ni ndogo kama unatumia kiasi hiki kidogo.
Kaini alimuua Abeli, kisha akafukuzwa na kwenda kuishi nchi ya mbali na kule akaanzisha uzao wake!!🤔
Je Kaini alimuoa nani kule nchi ya mbali? Alizaa na nani?🤷🏿
Ikiwa Dunia ilikuwa na Adam & Eva
(Watu wawili tu)
Nao wakazaa Kaini & Abeli
(Wakawa 4)
Abeli akafa wakabaki Mtu tatu!!
Kaini Alizaa na nani kule nchi ya mbali?
Kitabu kinasema baadae
Adam & Eva walimzaa Seth na baadae wakazaa watoto wengine (BAADAE)🤔
Hapo lakini Kaini tayari alishaanzisha uzao wake! Je Alianzisha na nani?🤔
Inawezekana Adam & Hawa hawakuwa watu wa kwanza duniani hapa, tayari dunia ilishakuwa na watu kabla yao?🤔
Au inawezekana Eva hakuwa mwanamke wa kwanza kwa Adamu, tayari Adamu alishakuwa na Ma’mtu mwingine kabla na wakazaa watoto?🤔
Au je mwanamke huyo ndo’ yule LILITH?🤔
Kivyovyote vile Kaini alilala na Sister Ake!!
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza ratiba ya Uchaguzi Mkuu wa rais, wabunge na madiwani ambapo siku ya Uchaguzi Mkuu itakuwa ni tarehe 29 Oktoba, 2025.
Akitangaza ratiba hiyo katika hafla iliyofanyika ofisi za Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) jijini Dodoma siku ya Jumamosi, Mwenyekiti wa Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele amesema tarehe 09 hadi 27 Agosti, 2025 itakuwa ni utoaji wa fomu za uteuzi wa wagombea kwa kiti cha Rais na Makamu wa Rais.
“Tarehe 14 hadi 27 Agosti 2025 itakuwa ni utoaji wa fomu za uteuzi wa wagombea ubunge na udiwani, tarehe 27 Agosti 2025 itakuwa siku ya uteuzi wa wagombea kiti cha Rais, Makamu wa Rais, Ubunge na Udiwani”, ameeleza.
Amesema tarehe 28 Agosti hadi 28 Oktoba 2025 itakuwa ni kipindi cha kampeni za Uchaguzi wa Tanzania Bara. Aidha, tarehe 28 Agosti hadi 27 Oktoba 2025 itakuwa ni kipindi cha kampeni za uchaguzi wa Tanzania Zanzibar ili kupisha kura ya mapema.
Pia, tarehe 29 Oktoba 2025 siku ya jumatano, itakuwa ndiyo siku ya kupiga kura.
Wanamuita Mwanaume wa Kazi, Mfalme wa mizigo na hodari wa maumivu yote.... jina lake la kuzaliwa ni FAW J5P na amekuwa akihudumu Nchini Tanzania tangu mwaka 2017 na hadi sasa waliomtumia ni Mashahidi wa yake yote mazuri na wanaweza kukusimulia kwanini hadi leo ameendelea kuwa chaguo la wengi.
J5P series 340HP 6X4 Tipper ( 19.32 CBM) ni moja ya Malori bora kuwahi kutengenezwa na Kampuni ya FAW na rekodi za mauzo yake Nchini Tanzania zimeendelea kukuwa kila kukicha kutokana na ubora wake ikiwemo ulaji wake mzuri wa mafuta ambao ni lita 40 kwa kilometa 100.
Habari njema kwa Wanunuzi wa Malori haya ni kuwa Kampuni ya FAW Tanzania leo imetangaza kuanzia sasa Mteja yeyote atayenunua Lori hili la FAW atalipata ndani ya wiki moja tu baada ya kufanya malipo tofauti na awali ambako ilikuwa analazimika kulisubiria kwa muda mrefu kutoka China.
Taarifa rasmi ya JIEFANG MOTORS Tanzania ambao ndio Watengenezaji wa Malori hayo, imeeleza kuwa sasa Wateja wanaweza kutembelea Ofisi za FAW zilizopo barabara ya Nyerere mkabala na TAZARA, Dar es salaam ambazo kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa hufunguliwa saa mbili na nusu asubuhi hadi saa kumi na nusu jioni na jumamosi kufunguliwa saa mbili na nusu asubuhi hadi saa sita kamili mchana.
Pia JIEFANG imewakaribisha Watanzania mbalimbali hata wasio na lengo la kununua Lori kwa wakati huo, wafike kwenye Ofisi hizo kujionea umahiri wa Malori hayo ambako watakutanishwa na Wataalamu watakaowaelezea na kujibu maswali yote watakayokuwa nayo, +255767518888 au [email protected] #MillardAyoSHOPPING
Mchambuzi wa Masuala ya Siasa, Deus Kibamba, amaesema 'Unono' wa #Siasa unafanya watumishi wengi wa umma wakimbilie huko kwasababu inaonekana ndio njia pekee ambayo mtu anaweza kutajirika na kuishi mazuri hivyo maeneo mengine yanakosa watu wenye weledi, na kwamba usipodhibitiwa basi nchi itachelewa sana kupata maendeleo
"Tusipodhibiti unono wa kazi ya siasa nchi hii maendeleo tutasubiri sana. Kwasabbabu Prof. wa Chuo Kikuu, Daktari Bingwa wa Upasuaji wanaacha (majukumu) yao wanakimbilia bungeni. Sijasema tuwe masikini, lakini huwezi kuwa nchi ambayo ili Utajirike ni lazima uingie Bungeni tu. Haiwezekani hata kidogo!"
Deus ameyasema hayo Julai 10, 2025, Dar es Salaam akiwa katika Kipindi cha Mada Kuu - TBC
Soma https://t.co/7HvhlUCP9Z
#JamiiAfrica #JamiiForums #Accountability #UchaguziMkuu2025 #Siasa
Serikali ya Tanzania kupitia Waziri wa Kilimo Hussein Bashe, leo April 23 2025 imetoa tamko la kupiga marufuku mazao ya kilimo kutoka Nchi za Afrika Kusini na Malawi baada ya Nchi hizo mbili kuzuia mazao kutoka Tanzania.
“Wakati mazungumzo yanaendelea sisi hatuwezi kuendelea kuishi kuzuiliwa haki yetu hiyo hivyo natangaza rasmi kuanzia usiku huu mambo yafuatayo kwa Nchi hizi mbili South Africa imekua ikiingiza Tanzania 'fresh apples' kwa hivyo kuanzia leo ni marufuku kuingiza fresh apples Tanzania hatutaruhusu zao lolote kutoka South Africa linalohusina na kilimo kuingia Nchini kwetu"
"Kuhusu Nchi ya Malawi mpaka sasa hawajafuta notisi waliyoitoa kwa hivyo ninatangaza rasmi ni marufuku mazao yoyote ya kilimo kutoka Malawi kuingia Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia leo” amesema Bashe.
#MillardAyoUPDATES