Mfalme Daudi alipotumia madaraka yake kuzini na Bethsheba—mke wa raia mnyonge Uria—kiburi cha dhambi kilimchochea kukimbilia kuficha dhambi kuliko kushughulikia matokeo ya hatia yake. Dhambi huja na ‘busara’ zake. Busara hizo zikamwelekeza Mfalme Daudi kuja na mpango wa amani wa kumpa Uria Mhiti ‘ofa ya kurudi nyumbani kwa mapumziko mafupi.’ Daudi alitaka Uria alale na mkewe wakati wa vita. Daudi alitaka maridhiano na uhalifu wake. Daudi alitumia amani na Uria kama mkakati wa siri wa kufunika dhambi.
Uria, kwa upande mwingine, hakujua kinachoendelea nyuma ya ofa ya Mfalme. Dhambi ilikuwa imetendeka gizani wakati yeye akifanya kazi ya kizalendo kulipigania taifa lake vitani dhidi ya Waamori. Kwake, Uria, kulala na mke wake wakati nchi iko vitani ilikuwa usaliti mkubwa kwa wapiganaji wenzake. Uria alikuwa anawawaza wanyonge wenzake wanaopambana na Waamori wakati Mfalme Daudi anawaza namna ya kufunika dhambi yake na kulinda heshima ambayo hata yeye mwenyewe anajua hakuwa nayo.
Uria aliukataa mpango huo wa amani hewa wakati akijua wazalendo wenzake wanapambana na Muamori. Kukataliwa kwa mkakati huo wa kufunika dhambi kulichochea vibaya mno kiburi cha Mfalme Daudi na kumwingiza kwenye uhalifu mbaya zaidi. Daudi aliagiza Uria awekwe kwenye vikosi vya mbele ili ale jeuri ya uzalendo wake. Kweli mnyonge Uria aliuawa na mfalme akaamini amepoteza ushahidi na angeishi kwa amani na mke wa Uria.
Hapo ndipo Nathan, kiongozi wa dini, alipojitokeza na kusimama kwenye nafasi yake kumkemea vikali Mfalme Daudi. Nathan alinyoosha maneno kuwa, “Mungu anaenda kukuvua nguo.” Kilichomuokoa Daudi ni ule moyo wake wakukubali ametenda dhambi, kujuta na kutubu. Daudi hakuendelea na propaganda za kuzimisha sauti ya kiongozi wa dini anayepigania haki ya mnyonge asiye na yeyote wa kumtetea.
Tunachojifunza hapa ni kwamba Mungu siku zote huwa upande wa mnyonge. Dhambi dhidi ya mnyonge huwa haiachani na wewe mpaka ukubali aibu ya kuikiri na kuijutia. Mungu akikupenda anakupa nafasi yake pili kwa kukuletea mpaka Nathan akuonye. Ukishupaza shingo ukakwepa aibu ya kukiri dhambi lazima ule matokeo ya dhambi. Kilio cha mnyonge hakiendi bure.
[kwa simulizi kamili rejea 2 Samweli 11:1-27; 12:1-23]
@SwahiliBible Wale Mitume na Manabii ambao kanisa letu tukufu limetufundisha kuwakataa na kuwapinga ndio wamekua mstari wa mbele kukemea na kuonya kiasi kwamba wamehatarisha mpaka huduma zao na maisha yao! Pia na wamekuja na jumbe nzuri za faraja na tumaini kwa Mungu. Kanisa letu zuri sasa…!
Kijana unayefanya kazi kwa mazoea, huna nidhamu ya kazi, unachelewa kazini, unaondoka muda unaotaka wewe, huoni haja ya kujifunza mambo mapya, unajua kuliko wanaokutangulia, huheshimu makataa (deadlines); kuna umri utafika wenzako wataaminiwa kwa majukumu makubwa zaidi wakati huo wewe ukipambana na ‘roho’ ya kukataliwa.
Katika vitu ambavyo namshukuru Mungu ameniwezesha kuvi-experience ni kuishi maeneo tofauti ya nchi yetu hii na kuona maisha tofauti wanayoishi watanzania.
By 2006 nilikuwa nimesoma Mafia na Lushoto, shule za serikali lakini nzuri; mambo ya watoto kwenda shule peku nilikuwa #UZI
Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC), inakutana Dar es Salaam leo, kujadili utoaji endelevu wa huduma bora za Elimu na Afya unaofanywa na taasisi za Kanisa hapa nchini. #Upendomedia#Amanikwawote
@cssc_tanzania yaandaa Mkutano Mkuu wa wakuu wa shule na vyuo vya ufundi vya kanisa!
Lengo: Kuimarisha ubora wa elimu kwa kuzingatia mabadiliko ya kisera & teknolojia, Kujenga uongozi, uwajibikaji, na utawala bora. Kupanua huduma huduma ya elimu na mafunzo ya amali.
#ElimuBoraTZ
I've seen CDM's "wajumbes" walking around "majestically" kitaa with their blue caps, red T-shirts and badges! 😀,
They should!
They've given a lesson to the "old party" 😎
@daveisaya Hatujazoea kusikia Wapinzani wanatuhumiana rushwa; au watu fulani kudaiwa kufanyiwa hujua ili wang’oke; au kusikia kiongozi wa chama anakuwa na chuki na mwanachama wake mpaka anahama chama. Hizi zinazoitwa Team fulani kimsingi ni mshangao na tahayaruki.