#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 500
Mhe. Lissu amemaliza kuteta jambo na Mawakili wake, Mawakili wanarudi kwenye nafasi zao.
Mhe. Lissu anasema Waheshimiwa majaji nashukuru kwa nafasi, naomba mnisikilize kwa umakini na muandike kwa umakini.
Leo ni siku ya 577 nikiwa gerezani kwa kuitwa Mhaini, kosa ambalo kwa katiba ya nchi yetu ndio kosa kubwa kuliko yote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ndio kosa pekee lililotamkwa katika katiba, kosa ambalo kwa mujibu wa kifungu cha 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu, adhabu yake inaweza kuwa kifo baada ya siku 577 za hilo wingu jeusi la adhabu ya kifo kuning’ing’inia juu ya kichwa changu, mmeniita mchochezi kosa ambalo halijapangiwa adhabu.
Mmeniita mchochezi na Wakili wa Serikali Mkuu anahangaika kutafuta adhabu yake ni nini????
Maana yake ni nini waheshimiwa majaji?
Kosa nililoshtakiwa nalo halikuwa kosa na nyie wenyewe mmesema halikuwa kosa, kwahiyo nilikaa siku 577 Gereza la Ukonga bila kosa lolote.
Waheshimiwa majaji kauli yenu kwamba halikuwa kosa mmekubaliana na msimamo wangu na ushahidi wangu.
Kuna kitu kimoja hamjakisema na nitakisema for the record na ushahidi wangu umethibitisha kwamba hii ilikuwa ni kesi ya kisiasa tuu, kugeuza Mahakama ya jinai kuwa uwanja wa mapambano ya kisiasa.
Kwa hukumu yenu ya leo mmethibitisha hilo, ni Political persecution, hivyo inabidi visababu vitengenezwa vya kumfunga huyu mpinzani wao wa kisiasa na visababu vyenyewe ni kosa la uchochezi ambalo nyie Majaji mmelitengeneza, sikushtakiwa kwa uchochezi, nilishtakiwa nje ya uhaini.
Nilishtakiwa kwa kusambaza taarifa za uongo, mmetafuta kosa ambalo halikuwepo, with all due respect mmefanya hivi kwasababu ya maelekezo ya kisiasa, hana kosa ila asiachiwe hivi hivi ataonekana ameshinda, Serikali itaaibika, anayetupa Ujaji ataaibika, ndivyo mlivyofanya leo.
Ninajua mnahukumu, ninajua, I feel it in my heart kwa bahati mbaya sana mmefanya kile ambacho Mahakama kuu ya Kenya ilikifanya mwaka 1954 kwenye kesi ya Jomo Kenyatta.
Mahakama Kuu ya Kenya ilimpata na hatia Mzee Kenyatta ingawa historia ilikuwa inajua kuwa hamna kosa lolote, ndicho ambacho mmefanya leo Waheshimiwa majaji.
Historia haijawa na wema sana kwa Majaji ambao wamegeuza Mahakama zao kuwa mahali pakuadhibia wasiokuwa na hatia ili kuwaridhisha walioko madarakani kwasababu mnaadhibu mtu ambaye mnajua hana hatia na Dunia inajua hana hatia.
Waheshimiwa Majaji Wasiokuwa na hatia kama mimi huwa hawaombi msamaha, unaomba msamaha kama una hatia au kama umekosa.
Huombi msamaha unapokuwa huna hatia, nataka niwe very clear kuwa haya nitakayoyasema yasichukuliwe kuwa naomba msamaha, I am completely innocent lakin kwa vile Wakili mkuu wa Serikali amezungumza naomba nimjibu,
Kwanza kabisa, amesema kwenye kifungu cha 35 ambacho amekiombea adhabu kali amesema adhabu ya juu ni kifungo cha miaka 5 au faini au vyote viwili.
Sheria inapotoa adhabu ya aina hiyo faini au kifungo, Mahakama inatakiwa ifanye nini? katika kesi ya Salum Shaban vs R (1985) TLR 71 ambapo Mahakama hii ilisema pale ambapo Bunge limetoa option ya faini au kifungo, Mahakama lazima itoe kwanza adhabu ya faini kwanza.
Kwahiyo mnapotafakari adhabu kali iliyoombwa na Wakili Mkuu wa Serikali msije mkasahau msimamo huu wa kisheria ikiwemo kesi ya Alice Nyawira Ndungu vs R Criminal Appeal No 40 of 2022, Elias Ndikumana vs R Criminal Appeal No 39 of 2022 na mashauri mengine mengi ambayo nina uhakika mnayafaham.
Kuna maneno yamezungumzwa hapa na Wakili Mkuu wa Serikali, amejigeuza kuwa shahidi, amesema kwamba haya makosa ya uchochezi yamekuwa ni makosa mengi sana kwa mujibu wa taarifa za polisi, na kwa mujibu wa hotuba ya Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman.
Part 501 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
@AmanJovie@edgarwabwire_ The true hero is the Senegalese Coach,
The act of asking players to leave the pitch enforced the need for leveling the ground,
Mane, was left as a negotiating entity, and a team leader able to carry the blame
Bwana Simbachawene wewe si mwanasheria?
Ukamataji kwenye Nchi yetu upo kwa mujibu wa sheria na PGO ya polisi inaelekeza kila kitu..
Huo ambao serikali yenu imekua ikifanya ni utekaji, ndio maana tunataka kujua walipo watu wote waliotekwa..
Je hizo task force za watu wanaovaa kininja na kuteka zinaongozwa na nani? Na kwanini zipo mpaka sasa?
Waliotekwa wako wapi?
Huwezi kuita utekaji kwamba ni ukamataji usiofuata sheria, huo ni utekaji tu.
A Tanzanian friend of mine once told me that former TZ President Benjamin Mkapa was once asked if he had any regrets regarding his leadership - and the answer was YES. He regretted selling state assets. The Government should NOT sell strategic state assets. The Kenya Pipeline is a STRATEGIC STATE Asset and so are many others! It amounts to giving a away something of the nation’s sovereignty!
@UNHumanRights imetoa taarifa ikisisitiza wajibu wa mamlaka kulinda haki za msingi za binadamu, ikiwemo uhuru wa kujieleza, kukusanyika kwa amani na kushiriki katika masuala ya umma, kwa mujibu wa sheria za kimataifa.
Taarifa kamili: https://t.co/3MIfmXnzjC
Muhimu: kuna taarifa kuwa polisi kwa sasa wameambiwa mataifa wanaangalia Tanzanja kwa hiyo mambo ya kudhuru wananchi hadharanu hakuna
Ila hawa wauaji wanapenda sana damu na kutesa kwa hiyo USIBEBWE KIZEMBE na tusiruhusu mtu kuchukuliwa wakati wa maandamano au mtaani! Wasije wakafanya uovu wao gizani! Ni kupambana na hawa madhulmat!
Nadhani imeeleweka?!
#D9 tutoke bila woga hakuna wakutudhuru pia kumbukeni maandamano ni bila kikomo na kukaa ndani usiku ni hatari hawa wauaii hawafai
#d9tanganyikaday #d9tunatoka #samiamustgo
Fortunatus Buyobe amekematwa na askari kutoka Dar Central Police nyumbani kwake jioni hii. Hatujui wanampeleka wapi. Buyobe amekuwa akitafutwa atekwe sababu ya maoni yake. Huu ushenzi haukubaliki. Free Fortunatus Buyobe Now!
Independent human rights experts condemn reported widespread and systematic human rights violations in #Tanzania 🇹🇿 following the general elections on 29 October, including allegations of hundreds of extrajudicial killings, enforced disappearances, and mass arbitrary detentions.
🇹🇿📣 Important Message from @TunduALissu for all Participants of the IDU FORUM 2025 from Ukonga Prison in Dar es Salaam, Tanzania 🇹🇿 .
Tundu, Chairman of @ChademaTZ2 and Executive Vice Chairman of the @idualliance , has sent us a powerful statement about the situation in Tanzania and the struggle for democracy.
👉 We call on all our members and partners to raise this issue in your national parliaments, assemblies, and political groups.
👉Tanzania’s democratic crisis must not go unnoticed — your voices can help generate international scrutiny and pressure for change.
👉Please take a moment to read Tundu’s message — and keep him in your thoughts today.
We have to build a country where people are so proud of their country that when they are handed Firearms they won't turn against their own people (leaders),
Tunatakiwa kujenga nchi ambayo watu ni wapenzi wa nchi yao kiasi kwamba wakipewa mitutu, hawatogeukiana wao wenyewe.
Kwa sasa,
Nimeamua kutoa muda kwa ajili ya kujifunza zaidi harakati tofauti tofauti,
Mageuzi ya kiteknolojia, mapinduzi na sababu zake, huku nikitoa analysis inayo-cover wigo mkubwa wa matukio hayo,
#Tutae
Observers Trash Tanzania Poll:
SADC election observers declare elections a sham
Observers: Polls marred by massive irregularities
SADC observers documents were seized by security
SADC: Team forced to delete mission-related photographs
#CitizenExplainer