@godbless_lema Mimi ninaomba mnaomzungumzia @zittokabwe mwachane naye,
Hapaswi kujadiliwa bali apuuzwe na kunyimwa ushirikiano wowote,
Ilisjajulikana njia na tabia yake,
Mkalieni kimya apotee
Baba Askofu Kalikawe Lwakalinda Bagonza SIYO PIGO KWA Tundu A. M. Lissu ! Tumepigwa Wote.
Nimesikia baadhi ya watu wanasema Tundu Lisu amepata pigo mahakamani baada ya mahakama kuamua kwamba mashahidi watakaotoa ushahidi katika kesi ya uhaini, watakuwa wa siri. Yeye hatawajua na umma hautawajua, hautawaona, na hata familia zao hazitajulikana. Hili Si pigo kwa Lisu. Ni pigo kwa mahakama na pigo kwa haki. Zingatia.
1. Tunazo mahakama tatu: Mhimili wa dola, mahakama ya umma na ya Mwenyezi Mungu. Hii ya mwisho haina rufaa na ndiyo pekee yenye mashahidi wa siri. Jaji ni Mwenyezi Mungu. Uamuzi wa leo unaigeuza mahakama ya dola kuwa ya Mungu. Haikubaliki.
2. Serikali iliyotaka kupinduliwa ni yetu wananchi. Si ya Rais wala chama. Umma una haki kuwajua na kuwahoji mashahidi waliotusaidia kuzuia serikali yetu isipinduliwe na huyu mhaini. Kuwaficha mashahidi ni kuwanyima haki ya kutambuliwa uzalendo wao.
3. Uhaini ni kosa kubwa (high crime). Mahakama huendesha kesi hizi kwa wazi na kuwaadhibu wakosaji kwa wazi ili kutoa fundisho kwa wengine. Leo tunaficha mashahidi, kuna siku tutaficha wahaini na kuwanyonga mafichoni. Haiwezekani kuipindua serikali sirini. Aliyeshauri mashahidi wa kesi hii wawe siri afutiwe matokeo ya elimu yake. Sina tatizo na Jaji aliyekubaliana na ushauri huu. Kuna kupigwa upofu feki unaoitwa “maelekezo toka kinyume cha chini”.
4. Mtuhumiwa wa uhaini ana haki zake. Moja ni kuwajua wanaomshtaki (ambao ni sisi Jamhuri), na kuwajua wanaoshuhudia uhaini wake. Kwa kuwa ni mtuhumiwa na kwa msingi wa uamuzi wa kulinda mashahidi, hata yeye angefichwa tusimjue ili ikitokea akashinda kesi, tusiendelee kumwona na kumnyanyapaa kuwa ni mhaini. Tungemwona tu baada ya kuhukukiwa. Kwa kuwa tunamjua mtuhumiwa, tuwajue mashahidi.
5. Kuingiza au kuonekana unaingiza mizengwe mahakamani ni kuifanyia uhaini mahakama yetu. Mtu mmoja aitwaye Tundu Lisu asifanywe kuwa ana nguvu na umuhimu wa kulazimisha mahakama yetu inajisiwe. Mahakama ina wajibu wa kuitetea heshima yake. Umma una haki ya kutetea uhuru wa mahakama.
6. Kutumia siasa kutatua masuala ya kisheria au kutumia sheria kutatua masuala ya kisiasa ni kufanya uchochezi na kuchonganisha siasa na sheria. Katika mwaka wa uchaguzi, ni kuwachagulia wananchi viongozi kinyume na matakwa yao. Tunaandaa uongozi wa kutawala miili badala ya mioyo. Kuna watu wengi saaana wako tayari kumchagua Rais Samia akiwa na mpinzani kuliko akiwa peke yake.
7. Yanayoonekana kupitia chaguzi ndani ya vyama ni kielelezo halisi cha hali ya nchi yetu. Huu si uchaguzi, si uchafuzi, ni urasmishaji wa rushwa katika taifa letu. Baada ya kupata viongozi kupitia mtindo huu, hatuwezi kupata kiongozi wa kupambana na rushwa. Wapi hapajafikiwa na rushwa katika taifa letu?!
8. Tuliwahi kuwa na gaidi feki. Ikiwa tumeruhusu mashahidi wawe siri
na ushahidi uwe siri, basi tutakuwa na mhaini feki. Pia tunaye kijiweni msaliti feki anayedaiwa ni mchanga katika chama chetu “kinachochukia” rushwa. Ufeki
huu utatufanya tuone kila kitu ni feki. Nimeishaitwa Askofu feki.
Hukumu hii inasisitiza TURUDI MEZANI. Mahakamani hakuna msaada.
@KumbushoDawson Huyo Dr. Mie simwelewagi kwa kweli, Sijui alipitaje hata hizo awamu 2.
Hii drama ya mke wake ni ya kuomba kura za huruma na wajumbe wameshakula chao
Wameshajua hana kesi, ni kichomi kwao akiwa huru. Watamwacha huru baada ya uchaguzi. Bahati nzuri sana hatokei mikoa ya mpakani, wangeshasema sio raia.
TAARIFA KWA UMMA:
Mheshimiwa Rais (Mst.) @jmkikwete ndiye MTU PEKEE DUNIANI ambaye alifanikiwa “KUMDHIBITI” Mheshimiwa TUNDU LISSU kwa HAKI na HOJA. Alitumia FALSAFA ya “HOJA HAIPIGWI RUNGU”. Tumpe 💐🌹🌷 yake Mheshimiwa KIKWETE.
@Mwabuk2Boniface Asante na Hongereni sana kwa kazi kubwa hii,
Saidieni Mataifa yetu haya.
Bado tunaimba demokrasia mdomoni.
Mungu awatumze na kuwainua zaidi.
Ongezeni nguvu na facts mmwokoe mpinganaji @TunduALissu
The voice of 1970s
Wana wa nchi leo wanapigania Matumbo yao,
Urafi wa madaraka, Rushwa
Unafiki na Usaliti kwa wananchi wao,
Wamekosa mistari ya kusimamia bali wanasimamia Matumbo na familiya zao.
Pumzika kwa amani Mzee wetu,
Mzalendo na Simba wa Mageuzi🇹🇿