A good man draws a cycle around him self and cares for those within,his woman his children. Other man draw righteous cycle and bring within their brothers and sister. But some-man have a great destine they must draw around them selves a cycle that include many many more.
China imewaweka chini ya uchunguzi Makamu mwenyekiti Mkuu wa Tume Kuu ya Kijeshi (CMC) pamoja na Afisa mwingine wa ngazi ya juu kwa tuhuma za ukiukwaji wa nidhamu, kwa madai ya kula rushwa.
Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Ulinzi, iliyotolewa leo Jumamosi Januari 24, 2026 inasema kuwa imeamuliwa kuanzisha uchunguzi dhidi ya Zhang Youxia na Liu Zhenli kwa tuhuma za kukiuka nidhamu na sheria.
Zhang Youxia, mwenye umri wa miaka 75, ndiye jenerali mwenye cheo cha juu zaidi nchini China na Makamu mwenyekiti mwandamizi wa CMC, pia ni mjumbe wa Politburo, chombo chenye ushawishi mkubwa ndani ya Chama cha Kikomunisti cha China.
Zhang Youxia anashikilia wadhifa wa Makamu mwenyekiti wa CMC pamoja na Zhang Shengmin, jenerali kutoka kikosi cha makombora cha China, ambaye alipandishwa cheo Oktoba mwaka jana baada ya mtangulizi wake kuondolewa katika msako mwingine wa rushwa.
Wote wanaripoti moja kwa moja kwa Rais Xi, ambaye amekuwa mwenyekiti wa CMC tangu mwaka 2012, Liu Zhenli, mwenye umri wa miaka 61, ni Mkuu wa Wafanyakazi wa idara ya pamoja ya CMC inayosimamia mipango ya kijeshi.
Uchunguzi huu umeibuka huku kukiwa na fununu baada ya Zhang Youxia na Liu kukosa kuhudhuria kikao rasmi kilichoongozwa na rais Xi wiki hii ambaye amekuwa akiitaja rushwa kama tishio kubwa zaidi kwa Chama, akisisitiza kuwa mapambano dhidi ya ufisadi bado ni magumu.
#MillardAyoUPDATES
“Sikuwahi kudhani kama itafika siku nikasema hili ila leo kwa maumivu sana nalisema “Tuna nia moja kama nchi nzima ya kuwa tunataka maisha bora, kila mmoja wetu anakubaliana na hili wazi kabisa kuwa tunataka tu kuwa na maisha mazuri zaidi ya tuliyonayo, kuuana ili kupata maisha mazuri isiwe moja ya njia za mafanikio”
“Hii sio sawa popote nje na ndani ya moyo hata wa ubinafsi kiasi gani, hii sio sawa Allah atatupa adhabu kali yenye mfano wa asiye hata na tone la huruma ya kukuangalia usoni kwa damu ya kiumbe wake uliyemwaga damu yake ili uwe na maisha mazuri katika ardhi aliyotupatia bure, ni kiasi kidogo sana cha upendo kinachohitajika kulielewa hilo” ——— @IdrisSultan