Kwa kuongozwa na sala ya Yesu Kristo katika Yohana 17 nawaalika tusali pamoja Novena ya kuiombea Tanzania Haki na Amani (Siku ya 5):
*SALA YA KUIOMBEA TANZANIA*
Ee Mungu Mwenyezi wa milele, Baba wa mataifa yote na wa watu wote, utuangalie kwa macho ya huruma sisi watu wako wa Tanzania, ambao nasi sasa twahesabika kati ya mataifa ya dunia. Kwa baraka yako uhuru wetu huu usipokonywe, na utuwezeshe kuishi maisha mema zaidi kadiri iwastahilivyo waana wa Mungu.
Tunakuomba nchi yetu iwe ya amani, waliopotea wapatikane na waliotekwa wapate uhuru wao, walioumizwa wapone, na waliouawa wapate uzima wa milele na uovu ukome katika nchi yetu. Tunakuomba ubadilishe nyoyo za watenda maovu na washirika wao katika uovu ili zikuelekee wewe, kwani sisi tulio wanyonge hatuna uwezo wa kuzibadilisha nyoyo ovu.
Uendelee kututawala na kutuongoza. Daima nchi hii iongozwe na viongozi ambao ni chaguo lako. Waangazie watawala hao, sheria wanazotunga kwa kutufaidia kwa mambo mema ya hapa duniani zipatane na Wewe uliyetuumba kwa ajili yako. Wajalie watu wetu wote paji lako la Imani. Tukiwa Mahujaji wa Matumaini, tuthibitishe tusishindwe kupambana na maovu yawezayo kutufikia kutoka nje au ndani, tupe hekima ya kutafuta ukweli katika mambo yote, na kuishi kwa uaminifu katika amri zako.
Ee Mwenyezi Mungu, uongozi wa kweli unatoka kwako, tunakuomba ujalie wale watakaosimamia na kuiishi Demokrasia ya kweli, Haki na Amani katika nchi yetu ili haki ituletee Amani ya kudumu.
Washa nyoyo zetu na mapendo yako ya kimungu yatakayotuwezesha kushinda utengano, ushindani, na chuki ya ukabila au utaifa, na tuunganishe wote katika muungano wa kidugu utakaotuwezesha, kwa msaada wa neema yako, kutufanya tuwe umoja katika Wewe Baba wa wote.
Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana wetu. Amina.
Bikira Maria Mtakatifu Mkingiwa dhambi ya asili. Utuombee.
Atukuzwe Baba....
#MaMaMa #MaombiMaonoMaadili
Tukiwa Igunga wakati wananchi wanachangia tone tone, pamoja watu kuwa wengi wanasukumana mwishoni alikuja mzee mmoja wa umri mkubwa ambae kwa makadirio ana miaka 90+.
Huyu mzee akatoa sh 2,000 ambayo alikua ameifunga kwenye karatasi na ilikua pesa pekee.
Tukio hili liligusa sana hisia zangu maana ukimuona yule mzee ni kama alitoa kila kitu alichokuwa nacho.
Najua kuna wengi na mama mwingine pia alitoa hivyo tukiwa Serengeti.
Kisa hiki nakifananisha na ule mfano wa yesu kwenye biblia akimzungumzia mama alietoa kila kitu.
Huyu mzee alinigusa sana ikabidi nimpe sh 100,000.
Tunawashukuru sana Watanzania kwa jinsi mnavyojitolea kupigania mabadiliko.
Asanteni sana wote.
#NoReformsNoElection
"KISUTU HATOKI MTU"
Naam naleta mrejesho wa mtanange wa akili na mamlaka ndani Viwanja vya Hakimu Mkazi Mahakama ya Kisutu.
Kisutu, Kisutu, Kisutu ndiyo Jina linalo vuma na kuvutia kwa sasa. Dunia nzima inataka kujua kesi ya mwanasheria, mwanasiasa nguli na kiongozi wa upinzani nchini Tanzania Tundu Antipas Mughwai Lissu juu ya hatima yake.
1.UPANDE WA JAMHURI
Uliwakilishwa na jumla ya Mawakili watano, Nassoro Katuga Wakili wa serikali Mkuu, Job Mrema Wakili wa Serikali Mkuu,Tawabu Issa Wakili wa Serikali, Harrison Lukosi Wakili wa Serikali na Cuthbert Mbilinyi Wakili wa serikali.
Wakili Nassoro Katuga ndiyo alikuwa Mzungumzaji Mkuu kwa jopo lao sauti ya taratibu yenye kumbeleleza kiti cha Hakimu.
Wenzie wanne walionekana watulivu huku Wakili Job Mrema akionekana mwenye wasiwasi usoni na udadisi wa kufungua hiki na kile angalau awe bize.
2.THE WOLVES (Mbwa Mwitu)
Walikuwa jumla ya mawakili 22 huku mawakili watatu viongozi wa Jopo Wakili Mzee Mpare Mpoki, Wakili Dr. Lugemeleza Nshala na Wakili Peter Kibatala.
Wingi wa mawakili 22 mbele ya Mahakama ni sababu ya uchache wa mabenchi ya kukalia mawakili kiasi Wakili Jeremiah Mtobesya wa upande wa utetezi alikosa pakukaa akajikuta anaenda kukaa katika benchi la mawakili wa Jamhuri ili aweze kusikiliza kesi.
Mawakili wengine walikuwa bize nyuma kufungua vitabu na rejea mbalimbali kisha kutembeza nyaraka kutoka nyuma kwenda mbele.
3.MSHTAKIWA
Kama Kawaida yake Tundu Lissu aliingia kwa uchangamfu Mahakamani mwenye bashasha, kishindo na kujiamini
Kwanza akazimua ile Kauli mbiu maarufu ya "No Reforms No Election" kisha ikapigwa 'Pipooozi' ukumbi wote ukaitika 'Pawaaaa'.
Kuashiria moto wa kisheria unaenda kuwaka Mahakamani.
Tukio la kuvutia ni pale Hakimu alipoagiza mshtakiwa Tundu Lissu apewe nafasi ndani ya chumba cha Mahakama cha kuteta na Mawakili wake kwa faragha.
Basi watu wote wakiwa wametolewa nje ya ukumbi wa Mahakama, Tundu Lissu amebakia yeye na Mawakili huku askari Magereza wakiwa mbali kidogo kuhakikisha wanaliona lindo lao lakini wanawachia faragha.
Badala ya Mawakili kuanza kumuelewesha mwenendo wa Kesi Mtuhumiwa (Tundu Lissu)
Ni Lissu ndiyo alikuwa amezungukwa na Jopo lote la Mawakili 22 wa utetezi analipiga shule mfano wa kocha wa Arsenal Mikel Arteta akiwa anaongea na wachezaji wake chumba cha kubadilishia nguo half time.
Tundu Lissu anakamata vitabu mbalimbali na vifungu vyake nakueleza vitakavyotumika, namna ya kutengeneza maswali, namna ya kurejea lesi zote za uhaini na mwisho akashika katiba ya Nchi akawa anawaambia "Humu hatoki mtu" × 3
Huku Mawakili wake wote wa Utetezi wakiwa wanatingisha vichwa ishara ya somo kuwaingia akilini.
4.MAGEREZA
Kama kawaida kikosi cha KM kinachosafirisha misafara ya mahabusu au wafungwa maarufu (VIPs) au hatarishi kilifika mapema sana Mahakama ya Kisutu
Wakiwa na Landcruiser hardtop 2 moja yenye vioo vyeusi hadi mbele ndiyo ilimpakia Tundu Lissu,Toyota Hilux single cabin yenye section ya polisi 10 kwa ajili ya kufungua njia mbele na nyuma kabisa palikuwa na basi kubwa la Magereza lililobeba askari maalum wa KM
Kizimbani pekee yake Tundu Lissu alikuwa chini ya ulinzi wa KM wa Magereza 15 wakiwa wamevalia kininja, ukumbi wa Mahakama ulikuwa na maafisa wa Megereza wenye nyota moja hadi 3 kama 7 wakiwa na machale muda wote kuangaza kila pande.
5.WADUNGUAJI
Juu ya Paa la Mahakama ya Kisutu walikuwa KM kama 8 wenye silaha nzito kama siyo AK 47 zile basi irakuwa ni SMG wakiwa wanafanya doria kwa mbwembwe za kupisha mmoja anakuja, mmoja anaenda wakiwa wamevalia Kininja pia na miwani nyeusi kujihami kanakwamba walikuwa na taarifa kuwa vijana wa ulinzi HAMASA wa CHADEMA walikuwa na mpango wa kumtorosha Mwenyekiti wao.
6.WAGENI WA KITAIFA NA KIMATAIFA
Kesi yenye mvuto wa aina yake umefanya wazee maarufu Tanzania waachie vitanda alfajiri wawahi Kisutu kushuhudia kesi ya kihistoria kama Dkt. Slaa, Askofu Mwamakula, Jenerali Ulimwengu, Prof. Lwaitama..
7.WAGENI
Kesi ya Tundu Lissu inawaleta majaji wakuu wawili wa Kenya kortini kushuhudia umakini wa Mahakama zetu. Jaji Mkuu Mstaafu wa Kenya Willy Mutunga anazuiwa uwanja wa ndege wa Mwl. Nyerere huku Jaji Mkuu Mstaafu wa Kenya David Maraga anafanikiwa kupita na kutinga katika chumba cha Mahakama wakati Kesi ya Tundu Lissu inaendelea.
Martha Karua alizuiwa uwanja wa ndege na kurejeshwa kwao Kenya. Boniface Mwangi alikamatwa hoteli ya Serena na kupelekwa mahabusu ya polisi. Pia, mwanasheria Agatha naye alifikishwa mamlaka za uhamiaji.
Mabalozi wa Jumuiya ya Ulaya Wanapeana zamu kama kawaida yao. Leo akienda Ujerumani, Canada na Marekani basi awamu ijayo wanakuja ubalozi wa Sweden, Norway, Belgium, na Finland.
8.JESHI LA POLISI
Baada ya kuambiwa na mahakama wawaache wasikilizaji wa kesi waje mahakamani bado Jeshi la Polisi haliamini kama wasikilizaji wa kesi wanaweza kwenda Kisutu wakahudhuria kesi huku kesi zingine zikiendelea bila bughudha, vurugu au fujo Mahakamani
Bado wanaleta Toyota Hilux single Cabin yenye Section ya Polisi 10 Kama 10 Zinakaa kila Upande wa Mahakama, Askari wengine kama 160 wameshuka kukaa barabara zote za kuingia Kisutu huku wengine wakikaba geti Kuu la kuingilia Kisutu
Makachero wa Jeshi la Polisi wakitimba hadi ndani ya chumba cha Mahakama na wanachukua benchi zima la nyuma kwa pamoja na kushuhudia kila kinachoendelea ndani.
9.WANANCHI
Wananchi waliojitokeza Mahakamani kwa hesabu za haraka haraka waliokuwa nje na ndani wanaweza kufika isadi ya watu 2,000. Nilipenda jinsi walivyojiratibu na kujipanga bila kusubiri maelekezo ya Polisi
Walichagua watu wachache wa kuingia ndani ukumbi namba moja kwa kuwa ulikuwa na uwezo wa kubeba watu 80 tu.
Wakachagua watu waakiba (reserve) wakukaa katika banda la kusubiria kesi kuitwa ndani ya parking ya Mahakama na wengi zaidi walikaa nje kwa umoja wakijitenga na Polisi ili kuzuia Vurugu.
Polisi wakajikuta kwa mara ya kwanza wamekosa kazi ya kufanya kisutu wakabakia kuwa mashuhuda na waliondoka Mahakamani bila kukamata mtu hata mmoja au kupiga bomu la machozi kwa sababu ya akili kubwa za wananchi jana.
10.UBWABWA
Si unajua tena kuna watu Duniani wameumbwa kusaidia Jamii na kupinga dhuruma tu. Ndiyo mwananchi mmoja alivyotimba pande za Kisutu na wali nyama wa wakutosha watu 3,000 majira ya saa 7:00 mchana.
Kilichovutia zaidi katika ubwabwa ulikuwa haugawiwi kwa ubaguzi au kwa vigezo kiasi wapita njia pale Mahakamani nao walipanga foleni wakapata chakula..
Baadhi ya manjagu ambao lindo lao lipo nyuma ya Mahakama na upeo mabosi zao ulipokuwa mbali na wao walidaka sahani moja moja Wakajumuika na Watanzania kupiga ubwabwa.
Kila aliyeonja aliishia kusifia roho nzuri ya msamaria mwema huyo ambaye hakutaka atajwe Jina na mpishi alivyojua kutengeneza combination ya mchele, mafuta na chumvi halafu akaja kuua na rosti ya nyama. Kila mtu akajikuta anatoa ahadi ya kurudi Mahakamani 02 June 2025.
11.KESI YA MSINGI
Kawaida kesi ya Uhaini inayomkabili Tundu Lissu ilikuja kwa ajili ya kutajwa tu kwa kuwa upande wa Jamhuri walikuwa hawajakamilisha upelelezi wao.
Kesi za kawaida zikiwa zimekuja Mahakamani kwa ajili ya kutajwa Mahakamani zinatumia dakika 5 hadi 7 kumalizika au kuhairishwa
Lakini kesi ya uhaini ya Tundu Lissu imetufundisha kuwa ni ngoma ya mtoto pekee yake ndiyo haikeshi. Kutajwa tu kwa kesi kumetumia muda wa saa moja na nusu. Hatari sana.
Upande wa mashtaka ndiyo ulikuwa wa kwanza kusimama na kujieleza kisha kusema kuwa wanaomba tarehe nyingine baada ya siku 14.
Ilikuwa ni kama walichokoza vita kwa upande wa utetezi na upande wa utetezi wakajibu mapigo kiutu uzima na kwamba wasichukuliwe poa.
Wakaja na hoja 3 kubwa, moja ilikuwa hakuna kuhairisha kama hawasemi upelelezi umefikia wapi na hatua gani, kwa kuwa kulikuwa na amri ya Mahakama ya kutaka kuletwe taarifa kamili kuhusu upelelezi ulipokuwa umefikia.
Hoja pili ilikuwa ni kutaka Tundu Lissu asizingirwe na ulinzi akiwa kizimbani kwa kuwa bado hajakutwa na hatia na kama katiba inavyosema katika ibara ya 13 (6b) (The doctrine of innocence)
Hoja ya tatu ilikuwa ni kuomba Mahakama iruhusu kesi iendeshwe katika Mahakama ya wazi
Na Jamaa hoja zao zote 3 zilitoboa ikiwemo ya kuleta taarifa Mahakamani kuhusu Upelelezi ulipofikia.
MWISHO
Kwa utamu wa hii kesi na namna watu walivyojipanga kwa mapambano ya kisheria, nikiona Wakenya wanasafiri kuja Tanzania kufuatilia hii kesi wala sishangai.
Nashauri serikali isizuie watu Uwanja wa ndege kujakufuatilia kesi ya Tundu Lissu. Tuchukue kesi ya Tundu Lissu kama utalii wa Kimahakama. Tunaweza Kukuta Kisutu imeingiza pesa kuliko Mlima kilimanjaro kwa Kesi hii moja tuhl.
Tukutane Tarehe 02 June 2025
Wenye uhuru nchi hii ni mafisadi na wezi wa mali za umma, wengine wote ni mateka ndio maana wanatekwa na kuuliwa muda wowote mafisadi wakijisikia kufanya hivyo.
Chadema hongereni sana. Wakati CCM inakamua wananchi na Makampuni, wakina Bashite na Waziri Mapete wanakula nchi. Nyinyi mkishirikiana na diaspora mnawalisha wananchi. Hiki ni kielelezo Tosha kwamba mkipata madaraka mtawajali wananchi wenu. Hongereni na Poleni sana
The International Democracy Union; @idualliance
1. Is seriously concerned by and strongly condemns the continued arrest, detention, abduction, torture, disappearances and political persecution of CHADEMA Party leaders, members and activists, and government critics.
2. Reiterates that the high treason charge levelled against Hon Tundu Lissu is politically motivated and lacks any legal foundation; thus, should be immediately and unconditionally dropped and Hon. Lissu set free.
3. Is satisfied that the scheduled October 2025 election will see nothing short of manipulation, rigging and serious violence against the CHADEMA Party and the wider opposition as the government of Tanzania has purposely decided not to change the current flawed constitution and implement major electoral reforms as demanded by the general public and advised by the international community.
4. Calls upon the international community to increase pressure on the government of Tanzania to uphold and respect fundamental human rights, the rule of law, and democracy which can only be so by ushering in constitutional and legal reforms in the country.
5. Support the clear demands for electoral reforms before the 2025 general election demanded by the CHADEMA Party and the wider Tanzania public.
https://t.co/BfIwprpmoa
Siku ya Tisa - Novena kwa Mt Rita wa Kashia - Mwombezi wa Mambo Yaliyoshindikana kumwombea @mdudenyagali arudi salama
Leo tunatimiza novena yetu 🙏🏽
Kesho May 22 ni sikukuu ya MT Rita ya Kashia na tutaendelea na hii novena hadi siku ya 12
Tunaomba kwa imani kuu
Amina!