@mdudechadematz @SuluhuSamia Mdude bhan et utamkabili hahahahaha yaan Rais akae anawaza Roho ya Kuku kama ww kwelii???! Mbona mnapendaga kujipa ukubwa ambao hamna?? Yaan Rais akae anakuwaza ww kwa lipii ?? Au kuna wa2 wanakudanganya sio?? Huna umuhimu wwote kwenye hili taifa na wla hauona sio tshio pia.
Mhe. Rais Dkt. Samia anaendelea na Ziara yake ya Kikazi Mkoani humo ambapo atakagua na kufungua miradi mbalimbali ya Maendeleo pamoja na kuzungumza na Wananchi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Taarifa ya Kituo cha kupokea na kupoza umeme wa Gridi ya Taifa kilichopo Inyonga Mkoani Katavi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga tarehe 13 Julai, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Bw. Suleiman Abubakar Mombo kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Julai, 2024.
#kishindochamama
Niger 🇳🇪, Bukinafaso na Mali 🇲🇱 zimeunda Muungano wa kijeshi (Alliance of Sahel States- AES.
Hii ni hatua nzuri kuelekea ushindi dhidi ya Ukoloni mamboleo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt, Samia Suluhu Hassan na mgeni wake Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi wakiwa katika Matukio tofautitofauti Wakati wa Uzinduzi wa Maonyesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa Dar es salaam Viwanja vya Sabasaba leo Julai 03, 2024.
Nikimkaribisha Ikulu Mheshimiwa Filipe Nyusi, Rais wa Jamhuri ya Msumbiji.
Tanzania na Msumbiji ni ndugu na washirika tangu harakati za ukombozi wa nchi za Afrika toka kwa utawala wa kikoloni, nchi yetu ikitoa mchango mkubwa wa ukombozi wa Msumbiji. Kihistoria, chama cha FRELIMO kilichowaongoza wananchi kufikia uhuru wa Msumbiji kilianzishwa jijini Dar es Salaam tarehe 25 Juni mwaka 1962, na ndipo yalipokuwa makao yake makuu hadi mwaka 1975.
Ikiwa ni sehemu ya matunda ya uhuru, nchi zetu hizi sasa zinaendelea na kazi ya kukuza uhusiano wetu ili kuongeza tija katika maeneo yanayoboresha maisha ya wananchi wa pande zote mbili, hasa maendeleo ya kiuchumi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na mgeni wake Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi wakati wakishuhudia utiaji saini Hati ya Makubaliano ya kushirikiana katika masuala ya Afya baina ya Tanzania na Msumbiji Ikulu Jijini Dar es Salaam.
tarehe 02 Julai, 2024. Kulia ni Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu akionesha Hati ya Mkataba huo pamoja na Naibu wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Msumbiji Mhe. Manuel José Gonçalves.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na mgeni wake Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi wakati wakishuhudia utiaji saini Hati ya Makubaliano ya kushirikiana katika masuala ya Afya baina ya Tanzania na Msumbiji Ikulu Jijini Dar es Salaam.
1/3. Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema Serikali kupitia Wizara ya Fedha imesikia kilio cha Makandarasi Wazawa na imeamua kupandisha wigo wa thamani ya miradi kwa Makandarasi hao kutoka kiasi cha Shilingi Bilioni 10 hadi kufikia Shilingi Bilioni 50.
Chuo cha Taifa cha Ulinzi – Tanzania, katika Mapokezi ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu tarehe 26 Juni, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja na washiriki wa Kozi ya 12 ya 2023/24 ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi- Tanzania kilichopo Kunduchi Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Juni, 2024.
📍VIDEO:
"Pale (TIC )Kituo cha Uwekezaji tumeshafungua kituo cha kuhudumia wateja kwa pamoja, na sasa tunataka tozo za mamlaka mbalimbali za udhibiti zilipwe mara moja ili kuondoa usumbufu kwa muwekezaji" Prof. @kitilam. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji.