Life is ten percent what happens to you and ninety percent how you respond. Don’t let a bad moment turn into a bad day. You have to say, “No, I’m not going to give away my joy, I am not going to lose my peace. This is the day the Lord has made, I’ve made up my mind to enjoy it.”
Tune into Joel’s message today! "No More Bad Days": https://t.co/kNnMjb1SU6
Watu wanapitia mengi na hawasemi. Si wengi wana ujasiri wa kufunguka na kukuambia wanachopitia. Usilazimishe. Kwa wengine kimya kinasema wanachopitia. Kwa wengine kuepuka kujieleza kunawasaidia kutokudanganya. Heshimu.
Upendo unatukumbusha kutokutazama hali za watu kwa kutumia uhalisia wetu. Upendo unatukumbusha kuuliza. Upendo unatukumbusha kutokuhukumu. Upendo unatukumbusha kuvumilia hali za watu tusizozielewa. Upendo unatukumbusha kutokujipa kazi ya kushauri tusichokielewa.
Life is not perfect and it never will be but if you can still wake up every day & do your best to seize the day, then you know the secret, & you are living it! This is me seizing the day on my morning walk stopping to watch some mallard ducks. #CarpeDiem 🫶🏻 #StarfishClub
Kila mtu, kwa kiwango fulani, ana ule ukurasa wa tabia zake asiopenda kuusoma kwa sauti. Inaweza kuwa historia mbaya, matukio magumu aliyowahi kukutana nayo na asiyopenda kuyakumbuka au inaweza kuwa chochote ambacho kikifahamika unafedheheka. Ufikirie ukurasa huu kama mzimu unaoweka rehani heshima yako na, labda, unapambana kuudhibiti usikudhalilishe na kukufedhehesha. Ukurasa huu unaotamani kuuchana, Carl Gustav Jung, anasema ndio chanzo kikuu cha chuki unayoweza kuwa nayo kwa watu fulani fulani.
Unapomchukia mtu, mara nyingi, ni vile anajaribu kukusomea ukurasa huu au kwa namna fulani anakukumbusha kilichomo kwenye ukurasa huu mchungu. Jung anasema chuki ni kama handaki tunalotumia kufukia zimwi tunaloogopa litatuharibia heshima yetu mbele za watu. Huwezi kumchukia mtu asiyegusa penye kidonda. Huwezi, kwa mfano, kumchukia mtu kwa kukuzushia tabia unayojua huna.
Kuishinda chuki uliyonayo kwa mtu, Carl Gustav Jung anasema unahitaji mchakato wa dhati wa kukabiliana na kipande kibaya cha maisha yako, kipande usichokipenda, kipande kinachokufanya ujisikie aibu, fedheha, dhalili na hasira dhidi yako mwenyewe. Ukiweza kushughulikia kipande hiki ‘unazaliwa upya’, unakutana na ‘wewe’ mwingine, aliyebadilika kiasi cha kutokuogopa ukurasa mchungu wa maisha yako. Ukifika hapo unapata uhuru wa kuishi na historia yako, na hivyo, hutamchukia mtu hata kama kila mkikutana anakusomea ukurasa wa maisha yako usioupenda kuusoma kwa sauti.
Uwezo wa kumnyamazia mtu wako wa karibu kwa muda mrefu bila taarifa yoyote ya nini kinaendelea; uwezo wa kumuacha mwenzio kimya kimya bila mazungumzo ya wazi kutathmini wapi mmepishana; uwezo wa kumuondoa kabisa kwenye maisha yako mtu mliyewahi kuwa karibu, mkishirikishana mambo ya kina kuhusu maisha yenu na ukafanikiwa kujitenga naye, ukamsahau na hata ukikutana naye mnaweza kupishana kama watu wasiofahamiana, ndugu yangu, hiyo sio hali ya kawaida unayoweza kujivunia.
Kinachokusaidia kumpuuza mtu kwa kiwango hicho sio kujitambua, kujua usichokitaka na kuendelea na maisha yako bali kumbukumbu ya maumivu yasiyotibiwa na majeraha makubwa ya kihisia unayoishi nayo yasiyoacha kukukumbusha namna ulivyowahi kutwezwa utu wako huko nyuma, ukaonewa, ukafedheheshwa na kuachwa mpweke asiyeweza kumwamini mtu yeyote lakini mwenye ujasiri wa kumshughulikia ipasavyo yeyote anayetonesha majeraha uliyonayo.
Ukitibu majeraha hayo, huwezi kumwuumiza anayekuumiza kwa kumpuuza na kumwacha kimya kimya bila kumpa taarifa kuwa uhusiano wenu umefikia tamati. Ukitibu majeraha hayo unaweza kushindwana na mtu na ukawa na uwezo wa kujadiliana naye kuwa ukurasa wenu wa kuaminiana umefungwa rasmi. Nafsi ikiponywa unaweza kutofautiana na mtu, ukaumizwa, ukakosewa, ukaufunga vizuri ukurasa wenu wa kuaminiana na bado ukamheshimu na ukampa nafasi ya kuendelea kuwepo kwenye maisha yako kama mtu mwingine yeyote bila kisasi, kinyongo wala kutakiana mabaya.
Utoshelevu wa mtu (contentment) huanza utotoni wakati ambao huna chochote kinachowavutia watu kwako. Wakati ukiwa mtoto uchi, bila elimu, mali, umaarufu, huo ndio wakati wa kujenga hali ya utoshelevu itakayoamua kiwango cha utoshelevu utakachokuwa nacho kwa safari nzima ya maisha. Hatusemi kama ulikosa vitu fulani utotoni basi hutokaa urekebishe. Hapana. Unaweza kuchukua hatua stahiki wakati wowote katika safari ya maisha yako ingawa tofauti na mwenzako aliyepata ‘template’ ya utoshelevu utotoni, wewe utalazimika kutumia muda na gharama kubwa kurudi kwenye mstari.
Utoshelevu wetu unaletwa na thamani tunayoiona ndani yetu hata tusipoambiwa na mtu kuwa tuna thamani. Utoshelevu ni kazi inayoanzia ndani ya mtu na sio matokeo yanayoletwa na kinachotokea nje ya mtu. Naomba urudie setensi hiyo. Utoshelevu ni matokeo ya kujiona unatosha hata kama ulivyonavyo visipokuwepo na unavyovitaka visipopatikana. Utoshelevu ni ile furaha na amani unayokuwa nayo kabla hujakutana na yeyote mwingine. Hali hii, kwa kiasi kikubwa, inategemea mazingira ya kimalezi uliyokutana nayo miaka ya mwanzo ya maisha yako. Ikiwa bahati mbaya uliwekewa mazingira ya kupambania mahitaji yako ya msingi yanayokujenga ujione mtu, ikiwa muda wote ilibidi ulie, ugombane kusikika na kueleweka, utoto wako ulisongwa na upweke wa kutokueleweka, kuonekana na kusikika, ni vigumu mno baadae ukawa mtu mwenye utoshelevu wa ndani hata ungepata kitu gani.
Ukikosa hiyo thamani ndani yako, kishunuzi utajielekeza kwenye vitu ili kujihakikishia heshima. Unaweza kufikiri, kwa mfano, nikifaulu basi watu wataniheshimu. Unafaulu unakuwa wa kwanza darasani halafu unagundua wala haikupi huo umuhimu ulioufikiri ungeupata. Unasoma shahada ya kwanza ngumu ngumu ukifikiri watu watakuheshimu. Unamaliza wanakuuliza ulisoma chuo gani. Unagundua shahada pekee haitoshi bali jina la chuo kilichokutunuku shahada yako. Unasoma shahada ya uzamivu ukifikiri sasa watu watakuelewa. Wasiopenda amani wanakuja kukuuliza,
“Mbona tafiti zako unachapisha kwenye majarida ya kitapeli (predatory)?”
“Mbona maandiko yako hayana jipya?”
“Mbona hunukuliwi?”
“Mbona huna miradi inayofanana na uzamivu?”
Unavurugwa maana sasa kile ulichofikiri kinakuja na utoshelevu hakikuhakikishii heshima uliyofikiri ungeipata ukiwa nacho. Unielewe. Hoja hapa sio usisome. Hoja ni tatizo la kusoma kama nyenzo ya kukupa utoshelevu.
Mwingine anatafuta kuongeza thamani yake kwa pesa. Huyu anafikiri akiwa na mali basi watu watakunyenyekea. Unagundua wapo wengi wanakuzidi na wewe wala huonekani kwenye mazungumzo ya mafanikio. Unaanza sasa kupambana si kuwa na mali bali uwazidi wenzako wote angalau na wewe uonekane. Unaanzisha mradi wa kujitengenezea himaya na umaarufu. Unachokuja kugundua, baadae ukishafanikiwa, ni kuwa wengi wanakufuata kupata ulichonacho. Unaanza kujiona kama badala ya kuwatumia watu, wewe ndiye unayetumika. Unagundua ule utoshelevu uliofikiri unakuja na mali haupo. Unakuwa mpweke. Unakuwa mwenye mali na power lakini mnyonge unaomtafuna ndani kwa ndani.
Kufikiri wingi wa vitu huja na heshima ni kujitengenezea mazingira ya kutokuridhika daima. Kufikiri heshima inayotoka nje ndiyo inayokuhakikishia thamani na utulivu wa ndani ni kujitengenezea mazingira ya kuwa mnyonge wa kudumu. Kwa nini? Hukuanza kushughulikia unyonge wa ndani yako kwanza kabla ya kupata hivi vingine. Habari njema ni kwamba, wakati wowote, katika hatua yoyote ya maisha yako, unaweza kuchukua hatua ya kujenga ile thamani yako isiyotegemea elimu uliyonayo, mali uliyonayo, madaraka uliyonayo na umaarufu ulionao. Ukishaanza kuridhika na wewe, ukajifurahia bila kutegemea kibandiko chochote kile cha kijamii, nakuhakikishia hivi vingine vyote —pesa, elimu, madaraka, umaarufu—havitakusumbua. Utavipata na kuvikosa lakini ndani hako utakuwa na utoshelevu.
I am at Oxford for Skoll in the UK this week representing @herinitiative and I will be part of the sidebars co-leading these two discussions on fueling grassroots power and rethinking localization in the midst of Aid cut.
What does hope look like for all of us?
#TheSideBar
Walking in Nature Can Help Optimize Your Health.🌲
Researchers have found walking in nature or 'Forest Bathing' has beneficial immune effects, lower blood pressure, lower stress, more energy & even more benefits...simply due to inhaling molecules called phytoncides secreted by trees and plants.
Most people do not know this but you should wash your avocados before eating them. 🥑
Before you slice into that creamy avocado, give it a good wash with a bit of soap! Even if the skin looks clean, it can harbor bacteria, pesticides, and dirt.
That's because before you get them from the grocery store, there's been hands all over those avocados before you take them home. Just as shopping carts are contaminated with a great deal of bacteria - that goes for avocados as well.
Wash the avocado before cutting with a knife because as the knife goes through the avocado skin it can contaminate the inside of the avocado.
The compound 'gingerol' in ginger root blocks several genes and enzymes in the body that promotes inflammation. They are antioxidant, anti-inflammatory, anti-disease and anti-bacterial.
*Fresh ginger is richest in gingerol. Some supplements could be formulated to have a higher concentration of gingerol than fresh ginger, especially if they use concentrated extracts.
#inflammation #health
The Box Breathing Technique used by the Navy Seals is powerful in reducing stress and anxiety - Just a minute or two will generate a relaxation response.
It can also help prevent and reduce high blood pressure.
Box Breathing can change how to be less responsive to stress and how to calm that response.
Umewahi kuhisi rafiki zako hawana msaada ukiwa na shida? Umewahi kusikia watu wakisema, kwa mfano, usimkopeshe rafiki? Unajiuliza sasa kama huwezi kumkimbilia rafiki wakati wa shida uende wapi? Kumbe haya mambo ya kukwepa kukusaidiana yalishafanyiwa tafiti kitambo.
Mwaka 1973, Mark Granovetter alichapisha andiko maarufu linaloitwa, “The Strength of Weak Ties”, lililotokana na tasnifu yake ya PhD. Granovetter aligundua kitu tunachokutana nacho kwenye maisha yetu ya kila siku. Kwamba msaada wa uhakika unaweza kuupata kutoka kwa watu usiofahamiana nao kivile (acquaintances).
Maisha yako ya kazi (career), mathalani, hubadilishwa na ‘weak ties’, wale watu hamjazoeana kivile, hamkutani sana, hamuwasiliani, wamekuzidi umri na uzoefu, wana taarifa usizonazo, wana kitu usichokuwanacho na mara nyingi huwezi kuwafanya marafiki zako kwa sababu hamfanani.
5 Reasons to Eat Avocado Every Day: 🥑
1. Very Healthy Fat
2. Very high in potassium (800 mg. per cup)
3. Reduces inflammation
4. High in fiber
5. Excellent for a healthy gut. Avocado promotes higher amounts of short-chain fatty acids (a major source of energy for colon cells).
Mungu alimpa Yusufu ndoto ya kule anakompeleka lakini hakumpa undani wa maumivu ya mchakato wa kuifikia ndoto yake.
Jukumu la kujitegeneza na kuvumilia miaka 22 ya misukosuko ya maandalizi ya kuwa vile alivyojiona lilibaki mikononi mwa Yusufu. Mafanikio hayana ‘njia ya mkato.’