Leo Septemba 22, 2025 nimeshiriki katika mkutano wa hadhara wa Mgombea mwenza wa Kiti cha Urais kwa tiketi ya CCM, Dkt Emmanuel Nchimbi Wilayani Ludewa Mkoani Njombe.
Leo Septemba 18, 2025 nikiwa kwenye kampeni za Uchaguzi Mkuu kutafuta kura za Mgombea urais kwa Tiketi ya CCM, Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan Mkoani Iringa Mtaa wa Kihesa Kilolo.
Jana Septemba 19, 2025 nimetembelea shule za msingi Kambarage na Deo Mwanyika zilizopo Halmashauri ya Mji wa Njombe na kuwazawadia wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo yao kama motisha ya kuendelea kusonga mbele kielimu.
Nikiwa na Mheshimiwa Festo Sanga na viongozi wengine katika harakati za kutafuta kura za Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan ikiwa ni kampeni za Uchaguzi Mkuu Wilayani Makete Mkoani Njombe leo Septemba 19,2025.
Leo Agosti 9, 2025 nimeelekeza Jeshi la Uhifadhi (JU) na Jeshi la Polisi (PT) kuendelea kushirikiana katika utatuzi wa changamoto zinazoikabili Sekta ya Maliasili na Utalii ikiwemo matukio ya ujangili na utoroshaji wa nyara za Serikali.
Leo Juni 9,2025 nimeshiriki katika mapokezi ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Nduli, Mkoani Iringa kwa ajili ya kufungua rasmi Mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA Mkoani humo.
Leo tarehe 4 Agosti, 2025 nimetembelea Maonesho ya Nanenane yanayoendelea kwenye viwanja vya Nanenane Nzuguni jijini Dodoma ambapo nimesisitiza wananchi kutembelea kwenye maonesho hayo ili kupata elimu ya uzalishaji wa mazao na kujifunza utalii wa vyakula.
Leo Wizara ya Maliasili na Utalii imezindua Mkakati wa Taifa wa Usimamizi na Uendelezaji wa Mikoko 2025β2035, ikiwa ni hatua madhubuti ya kulinda, kurejesha na kutumia kwa tija rasilimali hiyo muhimu ya mazingira, ambapo zaidi ya Sh bilioni 54 zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji
Usiku wa Juni 28,2025 nimekuwa mgeni rasmi katika hafla ya utoaji tuzo za 32 za kimataifa kanda ya Afrika na Bahari ya Hindi ambapo pamoja na kutwaa tuzo lukuki, Tanzania imetangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya kuwa kivutio bora Afrika Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan katika picha ya pamoja na Mawaziri mara baada ya kikao cha mwisho cha Baraza la Mawaziri cha Serikali ya Awamu ya Sita kilichofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo Julai 14, 2025.
Leo Julai 14, 2025 nimepokea na kukabidhi vifaa vya kisasa vya kusaidia kupambana na kudhibiti ujangili na kukabiliana na wanyamapori wakali na waharibifu kutoka kwa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kupitia Mradi wa Kupambana na Ujangili na Biashara haramu wa (IWT)