DAR ES SALAAM - Mchezaji wa Klabu ya Soka ya Yanga, Stepheni Aziz Ki ametoa pesa na lori mbili za ng'ombe kwa ajili ya kunasa 'NDIYO' ya wazazi wa Mwanamitindo na Mfanyabiashara Hamisa Mobetto ambaye tayari amekwisha mvisha pete ya uchumba.
#HabarileoUPDATES
ARUSHA - Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma (@mwanafa), amewataka wakandarasi wanaojenga uwanja wa michezo Arusha kuhakikisha wanakamilisha mradi huo kwa wakati, kabla ya ukaguzi wa mwisho wa Shirikisho la Soka la Afrika (CAF).
Uwanja huo unatarajiwa kutumika katika mashindano ya AFCON 2027, ambayo Tanzania itakuwa mwenyeji pamoja na Kenya na Uganda.
“CAF wanakuja kufanya ukaguzi wa mwisho mwezi Julai 2026, na tunataka mradi huu ukamilike Mei 2026, miezi miwili kabla ya ukaguzi huo,” alisema Mwinjuma.
Aliongeza kuwa mradi huu ni wa kipaumbele kwa serikali, huku akisisitiza kuwa Rais Samia Suluhu Hassan, ameonesha dhamira kubwa kuhakikisha uwanja huo unakamilika kwa wakati.
“Rais anajua umuhimu wa uwanja huu kukamilika ili tusiwe nyuma kwenye ratiba ya CAF ya kuandaa AFCON 2027. Ndio maana ametuelekeza tufuatilie kwa karibu na kuhakikisha kila kitu kinalipwa kwa wakati,” alisisitiza.
Imeandaliwa na Mwandishi Wetu
Zaidi tembelea //habarileo.co.tz
#HabarileoUPDATES
DAR ES SALAAM - Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephane Aziz Ki, ameoa rasmi mwanamitindo Hamisa Mobetto katika hafla ya ndoa iliyofanyika leo, Februari 16, 2025, katika Msikiti wa Masjid Nnuur, Mbweni, Dar es Salaam.
Ndoa hiyo imefungwa na Sheikh Mkuu wa Dar es Salaam, Walid Alhad Omar, akisaidiana na jopo la masheikh wengine. Akizungumza baada ya ndoa, Sheikh Walid aliwatakia wanandoa hao maisha mema na kuhimiza jamii kuepuka zinaa.
Sherehe rasmi ya ndoa hiyo inatarajiwa kufanyika Februari 19, 2025, katika ukumbi wa Superdome, Masaki, Dar es Salaam.
Jana, Aziz Ki alilipa mahari ya ng’ombe 30 na Sh30 milioni, mahari iliyokabidhiwa kwa familia ya bi harusi na Rais wa Yanga, Mhandisi Heris Said, kwa niaba ya bwana harusi.
Imeandaliwa na Mwandishi Wetu
Zaidi tembelea //habarileo.co.tz
#HabarileoUPDATES
DAR ES SALAAM - KAMPUNI ya Barrick nchini imechangia Sh trilioni 3.6 katika mapato ya serikali kupitia kodi, mrabaha na tozo kwa kipindi cha miaka minne kuanzia mwaka 2020 hadi 2024.
Meneja wa Barrick nchini, Melkiory Ngido alisema hayo jijini Dodoma mwishoni mwa wiki mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakati akiwasilisha maendeleo ya kampuni tanzu baina ya Barrick na Serikali ya Tanzania ya Twiga Minerals.
Ngido alisema takwimu za miaka minne kuanzia mwaka 2020 hadi 2024 zinaonesha Kampuni Barrick imewekeza zaidi ya dola za Marekani bilioni 4.24 (Sh trilioni 11) katika shughuli zake ndani ya nchi na imeilipa serikali dola bilioni 1.5 (Sh trilioni 3.6) kupitia kodi, mrabaha na tozo.
Ngido alisema Barrick tangu ilipoanza kuendesha shughuli zake mwaka 2019 imeendelea kuchangia kukuza uchumi wa kijamii kupitia uwekezaji, ajira, na miradi ya kijamii.
Imeandaliwa na Mwandishi Wetu
Zaidi tembelea //habarileo.co.tz
#HabarileoUPDATES
DODOMA – Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limetangaza nafasi za ajira kwa vijana wa Kitanzania wenye sifa zinazohitajika, likiwataka kuwasilisha maombi yao kupitia mfumo rasmi wa ajira wa jeshi hilo kabla ya Februari 28, 2025.
Kwa mujibu wa tangazo hilo, nafasi zinazotangazwa ni kwa ngazi ya Konstebo, ambapo waombaji wanapaswa kuwa na elimu ya kidato cha nne au sita.
Aidha, nafasi maalum zimetengwa kwa wenye ujuzi wa udereva wa magari makubwa, ufundi bomba, uuguzi, urubani wa helikopta, na taaluma ya zimamoto na uokoaji.
Pia, nafasi zitatolewa kwa waombaji wenye shahada katika fani mbalimbali, zikiwemo Uhandisi Bahari, TEHAMA, Uhandisi wa Ndege, Lugha (Kiingereza), Sheria, Uchumi, Ukadiriaji Majenzi, na Ualimu wa Usimamizi wa Elimu.
Jeshi hilo limeeleza kuwa waombaji wanapaswa kuwa raia wa Tanzania, kuwa na afya njema kimwili na kiakili, na wasiwe na rekodi za uhalifu. Masharti mengine ni pamoja na kutokuwa na alama za kuchorwa mwilini (tattoos), kutokutumia dawa za kulevya, na kuwa tayari kuhudhuria mafunzo ya taaluma ya Zimamoto na Uokoaji.
Imeandaliwa na Mwandishi Wetu
Zaidi tembelea //habarileo.co.tz
#HabarileoUPDATES
MAREKANI - Mjumbe wa Rais wa Marekani Donald Trump huko Mashariki ya Kati, Steve Witkoff, amethibitisha kuwa mazungumzo ya kusitisha vita vya Ukraine yatafanyika Saudi Arabia wiki hii.
Witkoff ameelekea nchini huko Jumapili pamoja na Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Marekani, Mike Waltz.
“Ninaondoka usiku wa leo,” Witkoff alisema katika mahojiano na Fox News.
“Tuna matumaini kwamba tutapiga hatua kubwa,” aliongeza, bila kufichua ni nani watakaoshiriki mazungumzo hayo au mada zitakazojadiliwa.
Kwa mujibu wa Washington Post, maafisa waandamizi wa Marekani wanatarajiwa kukutana na wenzao wa Urusi jijini Riyadh wiki hii kwa ajili ya mazungumzo ya kusitisha vita vya Ukraine.
Mazungumzo haya nchini Saudi Arabia yanatajwa kuwa miongoni mwa mazungumzo ya kwanza ya ana kwa ana kati ya maafisa wa ngazi ya juu wa Marekani na Russia kwa miaka kadhaa.
Hatua hii inatarajiwa kuwa maandalizi ya mkutano kati ya Rais wa Urusi, Vladimir Putin, na mwenzake wa Marekani, Donald Trump.
Imeandaliwa na Mwandishi Wetu
Zaidi tembelea //habarileo.co.tz
#HabarileoUPDATES
KIEV - Ukraine inatarajiwa kufanya uchaguzi mkuu mwishoni mwa Oktoba 2025, Rais wa zamani wa nchi hiyo, Pyotr Poroshenko, amesema.
Akizungumza na https://t.co/DL9SxvNcLg, Poroshenko alisema kuwa vyanzo kadhaa kutoka ndani ya serikali vimethibitisha kuwa maandalizi ya uchaguzi tayari yameanza.
“Andikeni: [utafanyika] Oktoba 26 mwaka huu,” alisema Poroshenko, ambaye kwa sasa ni kiongozi wa chama cha European Solidarity kinachoshikilia viti 27 kati ya 450 katika bunge la Ukraine.
Imeandaliwa na Mwandishi Wetu
Zaidi tembelea //habarileo.co.tz
#HabarileoUPDATES
UKRAINE: MASHAMBULIZI ya ndege zisizo na rubani ‘droni’ za Urusi zimeharibu kituo cha kuzalisha umeme na mafuta kilichopo, Kusini mwa Ukraine, usiku wa kuamkia leo.
Al Jazeera imeripoti kuwa, kutokana na kuongezeka kwa mashambulizi ya Urusi nchini Ukraine, Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, ameita mkutano wa dharura mjini Paris leo Jumatatu, Februari 17, 2025, ili kujadili namna ya kuisaidia Ukraine katika kukabiliana na mzozo huo.
Kwa mujibu wa Waziri Mkuu wa Ukraine, Denys Shmyhal, vikosi vya Russia vilitekeleza mashambulizi hayo usiku wa kuamkia leo, wakati joto katika maeneo mengi ya Ukraine linatarajiwa kushuka hadi nyuzijoto saba chini ya sifuri (-7°C).
Shmyhal amesema kupitia mtandao wa Telegram kuwa, "Hili lilifanyika kwa makusudi ili kuwaacha watu bila joto katika halijoto ya chini ya sifuri, na kusababisha janga la kibinadamu."
Chanzo: Reuters
#HabariLeoUpdates
DAR ES SALAAM: WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Februari 17, 2025 amemwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 20 ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inayofanyika Kituo cha Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.
Maadhimisho hayo yameambatana na kliniki za huduma katika mikoa 7 nchini yakilenga kutoa elimu kwa wadau muhimu wa masuala ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu.
kaulimbiu ya maadhimisho ni ”Maadhimisho ya miaka 20 ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu- Athari chanya, Ubunifu na Huduma’’.
Imeandaliwa na Ramla Hamidu
#HabariLeoUpdates
RUFIJI, Pwani:: MSEMAJI Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Gerson Msigwa, amesema kuwa Mradi wa Uzalishaji Umeme wa Bwawa la Julius Nyerere (JNHPP) una uwezo wa kuhifadhi lita za ujazo bilioni 32 za maji, huku tuta lake likiwa na urefu wa zaidi ya kilomita moja.
Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ameeleza hayo mwishoni mwa juma kwenye Mkutano na wanahabari ndani ya eneo la Mradi wa JNHIPP na kufafanua kuwa mradi huo ulianza mwaka 2019 na uliishia asilimia 33 kabla Rais Samia Suluhu Hassan kuupokea mradi huo na kuufikisha asilimia 99.8.
"Tuta hili lina urefu wa zaidi ya kilomita moja. Kama lingekuwa jengo, lingekuwa na zaidi ya ghorofa 45, kitu ambacho hakipo Tanzania," amesema Msigwa.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, JNHPP ni kubwa zaidi kuliko Bwawa la Manyara, na ukubwa wake unazidi hata maeneo makubwa kama Wilaya ya Temeke na Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Bwawa hili, linalojengwa katika Mto Rufiji, linatarajiwa kuzalisha megawati 2,115 za umeme, ikiwa ni sehemu ya juhudi za serikali za kuongeza uzalishaji wa nishati na kuimarisha maendeleo ya taifa.
"Thamani ya mradi huu ni trilioni 6.5 na Rais Samia tayari ameshalipa Sh trilioni 6.2 ambayo sawa na asilimia 95.8," amesema Msigwa.
Imeandaliwa na @ismailykawambwa @frankbulilo
Zaidi tembelea https://t.co/vtmow6d4jY
#HabarileoUPDATES
MAREKANI - Washington inatarajia Ukraine kurejesha “uwekezaji” iliyofanya katika mzozo wake na Russia, amesema Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Marekani, Michael Waltz, akizungumza na Fox News Jumapili.
Waltz alisisitiza kuwa kurejesha fedha kwa walipa kodi wa Marekani kutahakikisha msaada wa siku zijazo kwa Ukraine unaendelea.
Kauli yake imekuja baada ya ripoti kudai kuwa Rais wa Ukraine, Vladimir Zelensky, “alikataa kwa heshima” kusaini makubaliano ambayo yangeruhusu Marekani kumiliki asilimia 50 ya rasilimali za madini ya Ukraine, akidai anatafuta makubaliano bora zaidi.
Rais wa Marekani, Donald Trump, alidai kuwa Ukraine inapaswa kulipa msaada wa zaidi ya dola bilioni 300 kwa kutoa “madini adimu yenye thamani ya dola bilioni 500.”
“Wananchi wa Marekani wanastahili kurejeshewa, wanastahili aina fulani ya fidia kwa mabilioni waliyochangia katika vita hivi,” alisema Waltz. “Njia bora ya kuwafanya Wamarekani wajisikie salama kuhusu msaada wa siku zijazo ni kwa Ukraine kushirikiana nasi na kuhakikisha kuwa walipa kodi wa Marekani wananufaika.”
Imeandaliwa na Mwandishi Wetu
Zaidi tembelea //habarileo.co.tz
#HabarileoUPDATES
UGANDA: SERIKALI ya Uganda imetangaza kuiondoa kesi dhidi ya mpinzani, Kizza Besigye kutoka mahakama ya kijeshi na kuihamisha kesi hiyo kwenye mahakama ya kiraia.
Hatua hiyo imetokana na maamuzi kutoka Mahakama ya Juu ambayo yamedai kuwa raia wa kawaida hawezi kufikishwa katika mahakama ya kijeshi, huku pia ikimtaka asitishe mgomo wa kula gerezani.
Besigye, ambaye ni mshirika wa zamani wa Rais Yoweri Museveni na mpinzani wake wa muda mrefu, alianzisha mgomo wa kula Februari 10, 2025 akipinga kifungo chake, ambapo alikamatwa kwa tuhuma za uhaini na madai ya kutishia usalama wa taifa, hatua ambayo ilipingwa na wakosoaji wengi wakiwemo wanasheria na wanaharakati.
Waziri wa Habari, Chris Baryomunsi amesema kuwa alimtembelea Besigye gerezani Jumapili na kumshauri aanze kula ili aendelee kuwa na afya njema wakati akingojea uhamishaji wa kesi yake.
Kwa upande wake, Mke wa Besigye, Winnie Byanyima, ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la UNAIDS ameikosoa ahadi ya serikali huku akisema kuwa ni "inatia mashaka" na haionekani kama utawala wa Museveni utatekeleza ahadi hiyo kwa dhati.
Chanzo: VOA
#HabariLeoUpdates
In this story for @infoNILE, @dsyliver reports that the fishing industry in Lake Victoria 🇹🇿, is facing an unprecedented crisis. Illegal, unregulated, & unreported fishing has slashed daily fish catches & left local communities in poverty. https://t.co/ijoTCbCCkz