People respect you more when they don't see you often. Even parents. Trust me. It's strange how distance rearranges love, how absence restores what closeness erodes. When people are deprived of your presence, they start seeing you clearly again, not through habit but through awareness. Proximity dulls perception. Space sharpens it. That's just how the human mind works.
Kuna ile huna haraka na maisha. Unaona muda wa kupumzika unao. Una matumaini mno na kesho kuliko leo. Unatamani mno kile usichokifanya. Unajipanga lakini huanzi. Ukianza kidogo umeacha. Unachoka haraka. Unaahirisha utekelezaji. Inaitwa kukosa nidhamu.
Ukishakosa nidhamu unakotamani kwenda utapajua vizuri lakini hufiki. Miaka inaenda lakini hakuna mahali unaenda. Unaamka asubuhi mara jioni hii hapa. Unaianza Januari mara Juni hii hapa. Hakuna kitu kimebadilika. Utakapoanza kuona umuhimu wa leo kuliko kesho, ukaacha kujipanga sana kila kitu kinaanza kubadilika.