Ofisi za Instagram za kazi gani bwana @MsigwaGerson? Kuna changamoto zipi hizo hadi tunahitaji ofisi za Instagram zijengwe Tanzania? Tumieni akili ndogo mlizonazo kushawishi kampuni za kutengeneza magari; Volkswagen, Mercedes-Benz, Ford, Jeep, Hyundai, Honda, BMW, TVS wafanye assembling TZ
Mfano, gari zilizoshushwa kutoka katika meli ya mizigo 9 April 2022 katika bandari ya Dar es Salaam, gari 1,105 (sawa na 27%) ya mzigo ulioshushwa bandarini zilibaki Tanzania na gari 2,936 (73%) zilikwenda nchi jirani amnazo zinatumia bandari ya Dar es Salaam (Sudan, Zimbabwe, Mozambique, Malawi, Zambia).
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (Tanzania Ports Authority- TPA) anasema, kuanzia April 5 hadi April 7 (ndani ya siku 3 tu) bandari ya Dar es Salaam ilipokea meli nne (4) zenye jumla ya magari 8,384 (ukilinganisha na mwaka 2021, walikuwa wakipokea gari 10,000 kwa mwezi mmoja).
Hilo siyo jambo la kujivunia. SERIKALI imeamua kuifanya nchi yetu soko la magari mtumba (used cars) kwa sababu ya kupenda tozo na kodi. Gari ambayo utaagiza kwa $4,175 (Sh9.82 milioni) utalipa kodi TRA sawa na gharama za uagizaji gari hilo. Kwamba kodi ni sawa na gharama za kununua gari.
Serikali ya Tanzania katika gari ambalo mtanzania ananunua, haiweki hata spare tyre au bolt au hata maji ya wiper lakini wanachukua kodi sawa na bei uliyonunua gari. WIZI na UJAMBAZI. Ndiyo maana nafikiri ni wakati sahihi sasa kampuni za magari kuwekeza viwanda vya kuzalisha magari yao Tanzania.
Kenya imetengeneza sera - National Automotive Policy (NAP) iliyoanzishwa mwaka 2019 ili kuimarisha sekta ya utengenezaji magari ndani ya ardhi ya Kenya, ikitaka kuongeza uzalishaji na usanifu maradufu kufika mwaka 2025. na kupunguza utegemezi wa magari mitumba (used cars) kutoka nje ya Kenya.
Sera ya Kenya inatoa mazingira wezeshi kwa wadau wa sekta ya kuuza na kutengeneza magari kufikia uwezo wao kamili na nafasi ya Kenya kama mtengenezaji mkuu wa magari, ukanda wa Afrika Mashariki, eneo ambalo ni soko kubwa (jalala la taka) la magari mtumba (used cars) kutoka Europe na Japan.
Sera inatatua ukosefu wa mifumo maalum ya kisheria, mfumo wa kitaasisi na udhibiti, wamiliki wageni waliothibitishwa kuagiza vifaa na bidhaa, na kudhibiti utitiri wa magari yaliyotumika (used cars). Pia, sera hiyo NAP inatumika kufanya tasnia ya kutengeneza na kuuza magari ya ndani kuwa na ushindani.
Sekta hii ya kutengeneza na kuuza magari imeweza kutoa ajira zaidi ya 100,000 za moja kwa moja (direct) na zisizo za moja kwa moja (indirect) kwa wananchi wa Kenya. Sekta hiyo pia inachangia takribani Ksh30 bilioni (Sh518.38 bilioni) kwa mwaka kwa serikali kupitia mapato halali ya ushuru na kodi.
Wakati majirani Kenya wanafikiria vitu kama hivyo, serikali ya CCM inamuagiza mtumishi wa serikali aende kwenye kipindi cha Radio, awaeleze watanzania kwamba serikali kupitia wizara na waziri wa habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wanawashawishi INSTAGRAM kuweka ofisi zao Tanzania.
Ulimwenguni, tasnia hii ya kutengeneza na kuuza magari imekuwa nguzo ya ukuaji wa uchumi wa viwanda na kichocheo kikuu cha ukuaji wa uchumi mkubwa na maendeleo ya kiteknolojia. Serikali ya Tanzania inatakiwa kuwekeza akili huku siyo kuwa kichekesho cha Ulimwengu. Ujenzi wa ofisi za Instagram?
Associated Vehicle Assemblers (AVA) ndiyo kampuni kubwa zaidi ya kutengeneza magari nchini Kenya. Ni kampuni inayofanya kazi kwa chapa kama vile MITSUBISHI Motors, SCANIA, TATA, HINO na TOYOTA. Kampuni hiyo hapo awali ilikuwa ikitengeneza pia magari ya PEUGEOT, FIAT, IVECO na VOLVO (malori)
Associated Vehicle Assemblers (AVA) Ilichukuliwa na Simba Corporation mwaka 2017 kwa ubia na Marshalls East Africa na kukarabatiwa kwa Ksh4 bilioni (Sh69.15 bilioni). Kwa mwaka 2022 walitengeneza magari 7,500. AVA inatengeneza magari ya TOYOTA na MAHINDRA katika kiwanda cha Mombasa.
Mwaka 2021 wametangeneza magari 300 kwa ajili ya Jeshi la Polisi Kenya kwa gharama ya wastani ya Ksh2.5 milioni (43.25 milioni) na kutengeneza daladala (matatu) 3,600 zenye viti 16 (kila moja). Kqa mwaka 2022 wakatengeneza magari 132 ya MAHINDRA kwa Polisi. Magari yote yanaundwa nchini Kenya.
Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya Kenya - Kenya National Bureau of Statistics (KNBS) inasema katika ripoti yake kwamba idadi ya magari yaliyotengenezwa nchini Kenya iliongezeka kutoka magari 3,241 kwa mwaka wa 2018, hadi kufikia magari 4,406 kwa mwaka wa 2019, kati ya miezi ya Januari na Julai tu.
TOYOTA (Japan) wanatengeneza LandCruiser na Hilux, RENAULT (France) wanatengeneza malori. Serikali ya Kenya imetoa agizo Taasisi na Idara za serikali kununua magari kutoka ndani kwa ajili ya shughuli mbalimbali. Hii inapunguza gharama za uagizaji wa magari kwa matumizi ya serikali kutoka nje ya Kenya.
Hii sio tu nzuri kwa kuongeza uwezo wa utengenezaji wa magari (kwa watu wa Kenya) lakini pia ni nzuri katika suala la uhamisho wa ujuzi (skills transfer), katika suala la kuunda ajira kwa watu wao na katika kuunda fursa mpya (creating new opportunities). Wananchi wa Kenya wananufaika. Kwa namna gani?
Kuna watu ndani ya Kenya wanatengeneza brakepads, windscreen, suspensions & shock absorbers. Wote watapata ajira rasmi katika viwanda au kuuza ujuzi wao, kuna watu watauza mipira kwa ajili ya magurudumu, wakulima wataanza kulima zao la mpira (Hevea brasiliensis). Faida itakwenda mbali zaidi.
Zao la mpira ni zao la kimkakati Tanzania linalotumika kutengeneza bidhaa kama matairi, viatu na gloves. Mahitaji ya soko ni 99.7% ambalo kwa sasa mauzo ya zao hilo ni 0.03% pekee. Kama tunaweza kuwashawishi wenye viwanda vya magari kuwekeza Tanzania, wakulima wetu hawajanufaika hapo?
RENAULT wanaunda K-Range heavy-duty trucks, Renault walitumia Ksh58 milioni (Sh1 bilioni) kufanya maboresho ya uzalishaji wao eneo la Thika. Hii ni sawa na pesa ambayo imetumika kukarabati ofisi za Makamu wa Rais Dodoma na Dar es Salaam. Acheni kujipendelea. Acheni ubinafsi.
MMM, Martin Maranja Masese, Mtikila.
Kuna platform inaitwa FREECASH APP — kwenye app hii unaeza earn real money kwa kufanya survey na kucheza games tu.
Kama una tumia Android or iOs — Download app inaitwa Turbo VPN (Au vpn yoyote) or Tafuta Static residential Proxy za USA (Kama unajua jinsi ya kutumia Proxy).