Zamani wakati Dr. Leakey anachambua boli, alikuwa kwanza anakupa background ya mchezaji nje ya pitch!
Adivataizi kwanza mkwara wake anakutajia majina saba ya Ronaldo!!
We unajuaga tu anaitwa Ronaldo de lima, yeye anakwambia huyu anaitwa
Ronaldo Luis Nazario Del Souza Pereira De Lima!!
Kukuchanganya zaidi anakupa na hii
Ronaldo alilelewa na babu yake anaitwa Rodrigues Fereira Costa, na alipofikisha miaka 11 aliacha shule na kwenda kuishi na mama yake mdogo Rio de Janeiro huyu ndo alivumbua kipaji chake na leo atakwepo uwanjani kumshuhudia mwanae……Malamamaaeee🙌🙌🙌🙌🙌
Hiyo unaacha kila kitu unaangalia gozi!!
1998 hiyo Brazil wa moto vipi,
Chile anakufa 4-1
De lima anawa-shenyeta kamba mbili.
Wachambuzi wa sikuhizi Bongoflava nyiiingiiiiiii