VIDEO:
Msanii wa muziki nchini, Godfrey Tumaini, maarufu kama Dudubaya, amejibu agizo la kukamatwa kwake lililotolewa na Serikali kwa kutangaza kuwa anaenda kujisalimisha mwenyewe katika Kituo Kikuu cha Polisi (Central Police Station) jijini Dar es Salaam
Hatua hiyo ya Dudubaya inakuja muda mfupi baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, kuzungumza na wanahabari leo Ijumaa, Septemba 4, 2026, na kuliagiza Jeshi la Polisi nchini kumtafuta na kumfikisha mbele ya vyombo vya sheria msanii huyo kwa madai ya kukaidi wito wa serikali.
Waziri Katambi alieleza kuwa Dudubaya alitakiwa kufika wizarani kujibu tuhuma za makosa ya jinai yanayomkabili lakini alishindwa kufanya hivyo kwa mara ya pili, na badala yake akaonekana kwenye mitandao ya kijamii akitoa kauli za kukaidi mamlaka.
Kupitia video aliyoichapisha kwenye ukurasa wake rasmi wa mtandao wa kijamii wa Instagram mara baada ya kupokea taarifa za kusakwa kwake, Dudubaya amekiri kulipata tamko la Waziri Katambi lililoagiza akamatwe
Hata hivyo, msanii huyo ameweka wazi kuwa yeye si mtu wa kukimbia mkono wa sheria. Amefafanua kuwa amekuwa na urafiki wa karibu na wa muda mrefu na Jeshi la Polisi tangu alipoanza tasnia ya muziki, akibainisha kuwa mwanamuziki yeyote hawezi kufanya tamasha la hadhara bila kupata ulinzi thabiti wa askari polisi.
โMimi ni Mtanzania. Mimi siwezi kukimbia polisi,โ amesema Dudubaya katika video hiyo akisisitiza uzalendo wake
Kama MWAIPOPO kusema ATAWAUWA wananchi ni NIA njema Unawezaje kusema Tundu lissu anaesema Lazima tuupinge mfumo kandamizi kwa maandamano ni UHAINI???
Awamu ya SITA ina VIONGOZI WAPUMBAVU sana
Taarifa iliyotufikia ni kuwa Polepole yupo mateka kwenye ghorofa la Abdul lililopo Ukonga - inabidi kujipanga vizuri kuwakomboa mateka! Kumbukeni aliwahi kumlipua Abdul na genge lake
In this video Humphrey Polepole who has been missing since his violent abduction was revealing that Abdul Halim - Samiaโs son- was keeping trolls in his compound in Masaki
Today we received information that Polepole has been transferred and kept incommunicado in Abdulโs compund in Ukonga
Abdul is a menace,
#FreePolepole
Miezi mitano iliyopita Dudubaya alituambia Wanachadema tuwe makini na Ishengoma ni kibaraka wa Abdul.
Sasa baada ya Abdul kuona kwamba ushahidi waliotoa Mahakamani kwenye kesi ya Uhaini dhidi ya Mhe. Lissu hautoshi kumtia hatiani Mhe. Lissu ndo kampa kazi huyu Ishengoma ili aje kusema Mhe. Lissu ndo aliwatuma kufanya uhaini.
Abdul ni zero brain ndo maana hata watu ambao anawatumia kwenye mambo yake ya kiwaki na wao hawana akili kama yeye.๐ฎ๐ฎ
Unayeitwa Waziri mwenye dhamana ya kulinda raia na mali zao, unaweza kweli kuongea upumbavu kwa kiwango hiki na bado ukawa ofisini ? So sad.
Kwa kauli kama hii, hukupaswa kuwa ofisini hata kwa dakika moja. Dhamana ya kulinda maisha ya watu si mahali pa uzembe, dharau wala kauli zisizo na weledi.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 355
Katuga: Mkutano ulikuwa na lengo la kuelimisha watia nia kuhusu no reforms no election, ni sahihi?
Golugwa: Sahihi kabisa
Katuga: Unaweza ukamuelimisha mtu aliyepitisha azimio la no reforms no election?
Golugwa: Ndio unaweza kabisa.
Katuga: Jana ulisema ulialika na viongozi wakuu ambao hawakuwa watia nia?
Golugwa: Nilikuwa na wajibu wa kuwapigia simu viongozi wakuu
Katuga: wewe ulimualika Makamu Mwenyekiti Bara na Zanzibar, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar na wajumbe wa Sekretarieti?
Golugwa: Ndio ni sahihi kabisa
Katuga: Je jana ulisema kwenye ushahidi wako kuwa kwenye kikao cha Sekretarieti Naibu Katibu Mkuu Zanzibar kuna kikao hakushiriki cha Sekretarieti wakati wa maandalizi ya kikao cha 3/4/2025?
Golugwa: Sikueleza
Katuga: Waambie majaji kauli kuwa kesi hii ni ya uongo imeletwa kisiasa kwa nia ya kuzuia mapambano ya kudai mabadiliko katika katiba na sheria na kauli kuwa kesi hii ni mwendelezo wa kuendeleza chuki au kunishtaki kwa chuki, chuki iliyojengwa na DCI na IGP; hizi kauli mbili zinafanana au hazifanani?
Golugwa: Zinafanana na zinamhusu mtu huyo huyo mmoja
Katuga: wewe unasema kesi hii ni ya kisiasa ili kumzuia mshtakiwa asiendeleze mapambano ya kudai mabadiliko ya kisiasa, yeye anasema kesi amekuwa akitengenezewa kesi na IGP na DCI kwa chuki dhidi yake, nani anayesema uongo kati yako na Lissu?
Golugwa: Nimeshasema zinafanana hivyo siwezi kuzitenganisha, na kweli ni kesi ya kisiasa hivyo siwezi kusema nani anasema uongo na nani anasema ukweli.
Katuga: Kikao cha 3/4/2025 kati ya aina zile 4 za vikao chenyewe kinaangukia kwenye kikao kipi?
Golugwa: Hakipo kati ya vile vinne ila ulikuwa Mkutano wa ndani wa chama.
Katuga: Mkutano ulikuwa wa kikatiba?
Golugwa: Ndio kwasababu katiba yetu inaruhusu viongozi kukutana na wanachama
Katuga: Wewe ndio ulimwalika Lissu aje kuongea na watia nia?
Golugwa: Sahihi
Katuga: Wewe ndiye uliyemwandikia Hotuba?
Golugwa: Hapana sikumwandikia hotuba
Katuga: Je alikupa Hotuba yake kabla hajaja kwenye kikao?
Golugwa: Hapana hakuweza kunipa hotuba yake
Katuga: Je ulikuwa unajua alichofikiria kichwani mwake?
Golugwa: Wewe wakili unaweza kuingia kwenye kichwa cha mtu? Mimi nilikuwa najua anachoenda kukisema ambacho ni msimamo wa chama
Katuga: Nani alikuwa mwenyekiti wa huo mkutano?
Golugwa: Haukuwa na mwenyekiti
Katuga: Nani alikuwa mgeni rasmi?
Golugwa: Hakukuwa na mgeni rasmi
Katuga: Nani alikuwa wa mwisho kuongea?
Golugwa: Nilikuwa mimi
Katuga: Nani alikuwa wa mwisho kutoa hotuba?
Golugwa: Mwenyekiti wa Chama Tundu Lissu
Katuga: Nani aliongea kwa muda mrefu zaidi?
Golugwa: Mwenyekiti wa Chama Tundu Lissu
Katuga: Nani alikuwa amebeba dhima nzima ya mkutano huo?
Golugwa: Viongozi wote
Katuga: Wakati Lissu anaongea kulikuwa na vyombo vya habari?
Golugwa: ndio vilikuwepo
Katuga: Je Sekretarieti ilimlazimisha Tundu Lissu kuongea na vyombo vya habari?
Golugwa: Haikumlazimisha
Katuga: Je Lissu alitaka hotuba yake iende kwa umma?
Golugwa: Ndio alitaka
Katuga: Je alitaka hotuba ile iende kwa umma wa Watanzania?
Golugwa: alitaka
Part 356 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 354
Mahakama Imesharejea.
Majaji wameshaingia
Mhe. Lissu yupo,
Mawakili wanaendelea kumfanyia Serikali pia nao washaingia kwenye ukumbi wa Mahakama.
Katuga: Shahidi ulisema Tundu Lissu alifunguliwa kesi ya uongo? Swali je, kwenye Ripoti ya SADC kuna maneno kuwa Tundu Lissu ameshtakiwa kwa kesi ya uongo?
Golugwa: SADC wamesema kuwa Tundu Lissu alikamatwa na kushtakiwa kwa kesi ya uhaini.
Katuga: Je ni ripoti gani inasema Lissu alifunguliwa kesi ya uhaini uongo?
Golugwa: Ripoti ya UN iliyotolewa Novemba 2025
Katuga: Unafaham kuwa Tanzania ni nchi huru?
Golugwa: Nafahamu
Katuga: Ilipata uhuru mwaka gani?
Golugwa: 9/12/1961
Katuga: Unafahamu kuwa Tanzania kwa kuwa huru haipaswi kuingiliwa?
Golugwa: Nafahamu
Katuga: Unafahamu kuwa kwa mujibu wa Katiba Mahakama ndio mhimili wa mwisho katika kutoa haki?
Golugwa: Ndio nafahamu
Katuga: Unafahamu kuwa mahakama hii haiwezi kuelekezwa na EU?
Golugwa: Nafahamu ila mamlaka zingine zinaweza kuzungumza
Katuga: Ni kweli ulisema kuwa hii kesi ni ya uongo?
Golugwa: Ndio ni ya uongo
Katuga: Ulisema kwa maoni yako au kwa mujibu wa sheria?
Golugwa: Mtu mmoja hawezi kufanya kosa la uhaini duniani kote haiwezi kutokea haya ni maoni yangu
Katuga: Unafahamu mshtakiwa ameshtakiwa kwa kifungu gani na unaijua ni sheria gani?
Golugwa: Mimi sio mwanasheria ninachojua Tundu Lissu ameshtakiwa kwa uhaini na mtu mmoja hawezi kufanya uhaini.
Katuga: Naomba nimuonyeshe shahidi Kanuni ya Adhabu ili asome kifungu cha 39(2)(d). Je hapo uhaini unaweza kupangwa na kuratibiwa?
Golugwa: Anasoma na anasema mimi sio Mwanasheria kwahiyo siwezi kutafsiri sheria kwa ufasaha kama wewe.
Katuga: Unakubaliana na mimi kuwa mtu mmoja anaweza kuchochea watu wengine?
Golugwa: Mtu akiwa mwenyewe hawezi kujichochwa lazima wawe wengi na sio akiwa peke yake
Katuga: Jana ulisema Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi anateuliwa na Rais, ulimaanisha nini?
Golugwa: Nilitaka kuonyesha kuwa mifumo yetu ya uchagzui mamlaka yake yamehodhiwa na mtu mmoja
Katuga: Unajua kuhusu Ibara ya 74(7) ya Katiba inasemaje?
Golugwa: Waheshimiwa majaji naomba Katiba nisome
Katuga: Anampa Katiba na kumwambia asome
Golugwa: Anasoma, kwa madhumuni ya utekelezaji Tume itakuwa huru katika utekelezaji wa majukumu yake
Katuga: Soma na Ibara ya 74(11)
Golugwa: Anasoma, Tume ya Uchaguzi katika kutekeleza mamlaka yake haitalazimika kufuata maoni ya mtu yeyote au chama chochote cha siasa.
Katuga: Waambie majaji, wakati unasema kuwa uteuzi wa Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume umesema ulikuwa unaonyesha kuwa Tume imeingiliwa kwenye maamuzi yake, umewahi kuona Tume ikiingiliwa kwenye maamuzi yake?
Golugwa: Ndio nimewahi Unanipeleka kwenye vifungu hivyo lakini umeacha vinavyohusu uteuzi. Maneno Tume kuwa huru yapo tu lakini uhalisia sio huru
Katuga: Unafahamu haki yako ikikiukwa unaweza kufungua kesi?
Golugwa: Ndio nafahamu
Katuga: wewe umewahi kufungua kesi ulipoona Tume imeingiliwa?
Golugwa: sijawahi lakini wapo wanachama wetu waliowahi kufungua kesi
Katuga: Jana ulisema maamuzi ya no reforms, no election yalifanyika kwenye mkutano mkuu wa chadema
Golugwa: Ni kweli
Katuga: Mkutano Mkuu unawakuwa na wajumbe wangapi?
Golugwa: Zaidi ya 1000 na zaidi
Katuga: Hao wajumbe wanakuwa ni wanachama au
Golugwa: viongozi wanaotoka kwenye wilaya, majimbo, mikoa na kanda za chama
Katuga: Waeleze majaji kama Mwaka 2025 mlikuwa na majina ya watia nia wa uchaguzi
Golugwa: Wale waliokuwa wagombea wa 2020 na wale waliokuwa wapya ndio walijiorodhesha siku hiyo.
Katuga: Kati ya hao watia nia kulikuwa na watu kati ya hao waliokuwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 2024 ulip?
Golugwa: Sikumbuki.
Part 355 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 353
Upande wa Jamhuri wanaendelea kumfanyia cross examination, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Amani Golugwa.
Katuga: Maneno kuwa haya mashtaka dhidi ya Lissu ni ya uongo ulitaja ukurasa gani wa ripoti?
Mhe. Lissu: Waheshimiwa Majaji naona mawakili wa Serikali wamenogewa na shahidi wangu, wamesahau kuwa saa saba mchana huwa ni muda wa health break.
Watu na majaji kicheko๐๐๐๐๐ hasa hilo neno kunogewa na shahidi wa Lissu
Jaji Ndunguru: Wakili wa Serikali unasemaje?
Anasimama wakili wa Serikali Ajuaye amesimama: waheshimiwa majaji ni kweli tunaomba ahirisho la saa moja tu kwasababu shahi wa leo anahojiwa maswali ya Dodoso
Mhe. Lissu: Wakili wa Serikali umesahau kuwa huwa nafanya consultations?
Jaji Ndunguru: shauri linaahirishwa hadi 14:30
Majaji wanasimama
Inapigwa High Cooouuurrrt.
Tukutane baada ya break.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 352
Upande wa Jamhuri wanaendelea kumfanyia cross examination, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Amani Golugwa.
Katuga: 98.6 ukitoa 2.4 inabaki ngapi?
Golugwa: Waheshimiwa majaji usahihi ni 97.6 na 2.4 jana ilikuwa ni human error lakini inaonyesha wingi wa kura za uongo za CCM
Katuga: Jana ulisema vyombo vya dola viliwapiga waandamanaji, je ni Taarifa ipi ilionyesha kuwa vyombo vya dola viliwapiga waandamanaji?
Golugwa: Taarifa ya Umoja wa Afrika , SADC, iliyotolewa mwaka jana baada ya uchaguzi na vyombo vya habari na hata wewe unajua ila hutaki kukiri kuwa mapolisi walipiga watu
Katuga: Uliwaambia majaji ni ukurasa gani?
Golugwa: Nilitaja ripoti na majaji naamini watasoma ripoti yote
Katuga: Majaji wasipoona kwenye taarifa ya SADC wakakosa hayo maneno, majaji wakuchukulie wewe ni muongo?
Golugwa: hapana wasinione muongo kwasababu nilisema kwa niliyoyasoma na kuyasikia waliyoyasema wakati wanatoa ripoti zao
Katuga: naomba nimuonyeshe shahidi ripoti ya AU na asome wapi inasema Polisi walipiga watu?
Golugwa: Anasoma the mission noted with concerns on the excessive use of force by the Police and Military against the protesters.
Katuga: Wapi hapo wanasema Polisi walipiga waandamanaji??
Golugwa: Wakili usichoelewa hapo ni nini maana ya excesive use of force, unataka kusema Polisi waliwafanyia massage waandamanaji??? Kila mtu na dunia inajua kuwa Polisi waliwapiga waandamanaji na wengine waliuwawa majumbani mwao mpaka watoto kwa kupigwa na Polisi. Hii lugha ya kingereza wewe huelewi Katuga ila majaji wanaelewa. Hii ni lugha ya kikorinto wewe huwezi kuielewa.
Watu wamecheka sana๐๐๐๐๐๐๐๐๐ mpaka majaji wanacheka๐๐๐๐
Hapa Golugwa amecheza kama pele yani makofi kwake tafadhali๐๐๐
Katuga: Ni sahihi kuwa maneno Polisi waliwapigwa waandamanaji hayajaandikwa?
Golugwa: Yapo yameandikwa na ninasisitiza hili kabisa na huo ndio uhalisia uliotokea, watu walipigwa sana, waliuwawa kwa mamia ya watu.
Katuga: Shahidi unajua maana ya maandamano?
Golugwa: Ndio najua
Katuga: Kuharibu mali ya umma wakati wa maandamano ni uhalifu?
Golugwa: Ni uhalifu
Katuga: Kuchoma vituo vya mwendokasi ni uhalifu au maandamano?
Golugwa: Ni uhalifu
Katuga: Kukata watu vidole wakati wa maandamano ni uhalifu au maandamano?
Golugwa: Ni uhalifu
Katuga: Kupiga na kuua askari Polisi wakati wa maandamano ni uhalifu?
Golugwa: ni uhalifu
Katuga: Je ulishiriki au kupanga maandamano ya Octoba 29 ambapo Polisi waliwauwa waandamanaji?
Golugwa: Sikupanga wala sikushiriki
Katuga: Ripoti za SADC na AU wamesema kuwa waandamanaji walipigwa na polisi, Je ni wewe uliyewapelekea hizo taarifa?
Golugwa: Sio mimi ni wao wenyewe waliona waliyoyaona kwasababu wamesema wenyewe kwenye ripoti zao
Katuga: Ulisoma ripoti ya Jaji Chande
Golugwa: Ndio
Katuga: Ulisikia Jaji Chande akisema askari zaidi ya 16 waliuwawa?
Golugwa: Nilisikia pamoja na watu 518
Katuga: Hilo la watu sijakuuliza
Hapa Katuga haoni kabisa uthamani wa watu 518 waliouwawa hataki Golugwa alisemee hili, ndio maana shahidi anasema Katuga ana roho mbaya, haoni thamani ya uhai wa watanzania wenzetu.
Katuga: Jana ulisema kuwa baada ya Lissu kukamatwa waangalizi wa uchaguzi wa kimataifa walisema walisikitishwa na kukamatwa kwake na kuwa aachiliwe Lissu kwasababu mashtaka yake ni ya uongo.
Golugwa: ndio yapo kwenye taarifa zao
Katuga: Ulitaja observer wangapi?
Golugwa: niliowataja kuwa walitoa taarifa zao kuhusu uchaguzi ni AU, EU, SADC, Thabo Mbeki Foundation, na wengine
Part 353 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 351
Upande wa Jamhuri wanaendelea kumfanyia cross examination, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Amani Golugwa.
Katuga: Kwahiyo Chadema haikushiriki kutokana na haki ya kikatba?
Golugwa: Ni kutokana na msimamo wetu wa no reforms no election
Katuga: Akitokea mtu anasema Chadema haikushiriki uchaguzi kwasababu katibu mkuu hakusaini kanuni za maadili ya uchaguzi atakuwa yuko sahihi au sio sahihi?
Golugwa: ni kweli kabisa tulizuiwa
Katuga: Haya majibu ya mlizuiwa na kuwa chadema kutokushiriki uchaguzi ni haki yake kikatiba yanafanana au hayafanani?
Golugwa: hayafanani
Katuga: Ulielezea jana hapa maushenzi katika chaguzi ulizosema mojawapo ni kama vile mawakala kutokupewa viapo, wasimamizi kutokupokea fomu za wagombea wa chadema, kubadili taatifa za wagombea wa chadema uliyaona pia katika uchaguzi wa 2015, 2019, 2020?
Golugwa: ndio nilieleza?
Katuga: Je mambo hayo pia uliyaona kwenye uchaguzi wa 2025?
Golugwa: Hatukushiriki uchaguzi ila kwa niliyoyaona na kuyasikia na kuyasoma yalinishangaza na kuniogopesha
Katuga: Mwaka 2024 na 2015 ni mwaka upi unaanza?
Golugwa: 2015
Katuga: Mwaka 2024 na 2020 upi unaanza?
Golugwa: 2020
Katuga: Jana ulisema yale mambo ya kishenzi uliyoyaona 2024 uliyaonaje mwaka 2015?
Golugwa: Kwa akili ya kawaida na memory ya kawaida tu si mtu unakuwa na kumbukumbu za nyuma?
Watu wanamcheka katuga anauliza swali la kishenzi๐๐๐๐๐
Katuga: Waambie Majaji kama Chadema ilishiriki uchaguzi Mkuu wa 2015
Golugwa: Ndio
Katuga: Mwaka 2015 chadema ilipata wabunge 35?
Golugwa: Ni zaidi ya wabunge 30
Katuga: Katiba ipi ilikuwa inatumika?
Golugwa: Katiba hii hii ya JMT
Katuga: Wewe unasema mwaka 2025 hamkushiriki uchaguzi, yale maushenzi ya 2024 uliyaonaje wakati chadema haikushirki uchaguzi?
Golugwa: Kama nilivyosema, niliyasikia, kuyasoma na kuyaona na vyama vingine vya upinzani aisee yalikuwa ni mambo mabaya sana
Katuga: Jana ulisema mgombea wa CCM hujawahi ona akienguliwa ?
Golugwa: Kabisa kabisa
Katuga: Nani custodian wa wagombea kuenguliwa?
Golugwa: Tume ya Uchaguzi na Chama cha siasa ambacho mgombea ameenguliwa
Katuga: Je taarifa za waaangalizi wa uchaguzi ni sahihi zinatambulika kwa tarehe zilizotolewa?
Golugwa: Ni kweli
Katuga: Je taarifa za waangalizi wa uchaguzi zipo kwenye mitandao ya kijamii?
Golugwa: Zipo kwenye public domain kabisa na kila mtu anaweza kuzisoma
Katuga: Je ulitaja tarehe ya ripoti kutolewa?
Golugwa: Nilitaja mwaka kuwa zilitolewa 2025 mara baada ya uchaguzi mkuu
Katuga: Je ulieleza Mahakama kama Thabo Mbeki Foundation walikuwa observer wa uchaguzi mkuu wa 2025?
Golugwa: Nimesema nilisoma maoni yao kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka 2025
Katuga: CEO wa Thabo Mbeki Foundation ni nani?
Golugwa: Max Boqwana
Katuga: Ilikuwa na page ngapi?
Golugwa: Page 2
Katuga: Naomba nimuonyeshe shahidi taarifa ya Thabo Mbeki Foundation, anamuonyesha aya ya tatu ili Golugwa asome
Golugwa: Anasoma inarejea pia taarifa ya SADC na AU
Katuga: Kwa mujibu wa hiyo aya, ni wapi wansema wao walikuwa observer wa uchaguzi wa Tanzania??
Golugwa: Kwenye aya ya kwanza na sio hii ya tatu naomba niisome , katuga anamzuia Golugwa asisome, shahidi amekomaa na anaongea kwa ukali sana anasema bwana Katuga sikiliza wewe usinilazimishe nisome aya moja tu, tulia nikuonyeshe waliposema kuwa wao walikuwa observer,
Jaji Ndunguru: Shahidi soma aya ambayo unaona na ni relevant, Katuga anasoma aya ya kwanza ambayo inasema Thabo Mbeki Foundation walisikitishwa sana na maovu yaliyotokea kwenye uchaguzi wa Tanzania wa 2025 na kwa jinsi walivyofatilia
Katuga: Wamekuwa wafatiliaje tena sio waangalizi?
Golugwa: Kazi ya observer ni kufuatilia
Watu kicheko๐๐๐๐๐
Katuga: Jana ulisema Rais alichaguliwa kwa asilimia ngapi?
Golugwa: 98.6 na upinzani ni 2.4
Part 352 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 350
Upande wa Jamhuri wanaendelea kumfanyia cross examination, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Amani Golugwa
Katuga: Utakuwa hujui aina za vikao vya aina za Chama.
Golugwa: Ukitaka nikuelezee utofauti wa hilo utaelewa.
Katuga: Lakini neno vikao vya Uchaguzi halipo na aina mbili hazipo.
Golugwa: Kwa maana ya maneno hayo hapo hayapo lakini ukitaka kuelewa utaelewa na nitakuelewesha.
Katuga: Umesema kwenye ushahidi wako neno Ushenzi mara nyingi sana. Kwahiyo ni sahihi wewe ni shahidi wa Ushenzi.
Golugwa: Mimi ni shahidi niliyeelezea Ushenzi wa kweli uliofanyika kwenye chaguzi mbalimbali.
Katuga: Mtu atakaetoa hoja specific atalazimika kuithibitisha kwa mujibu wa kifungu cha ushahidi?
Golugwa: Mimi sio mwanasheria.
Katuga: Hivi ulikuwa na wajibu wa kupokea report za kanda zingine?
Golugwa: Niliratibu makatibu wa kanda zingine kujua maendeleo yao na sio kuzipokea.
Katuga: Ulisema Freeman Mbowe alisema hatutakuwa tayari kwenda kwenye uchaguzi mwingine wowote kabla ya mabadiliko ya mifumo ya Uchaguzi?
Golugwa: Alisema ndio.
Katuga: Mbowe alisema hamtakuja kushiriki uchaguzi hadi hayo mabdiliko yafanyike kuna lingine tofauti?
Golugwa: Niliyoyasema unayajua. Ingawa alisema mengi.
Katuga: Maneno kwamba huu uchaguzi tunaenda kuuzuia kwenye maneno ya Mbowe yapo?
Golugwa: Hayapo.
Katuga: Tunaenda kukinukisha. Yapo au hayapo?
Golugwa: Ukitaka neno hilo hilo hutaliona.
Katuga: Shahidi Mwema sasa nisikilize
Golugwa: Mimi mwema kwako. Hakuna wema wowote. Mimi sio shahidi mwema. Una roho mbaya hauwezi kusema mimi ni shahidi mwema.
Katuga: Ni haki ya Kikatiba kushiriki uchaguzi?
Golugwa: Ni haki.
Katuga: Sio haki kumlazimisha mtu pia kushiriki uchaguzi na kumlazimisha ni kosa kisheria?
Golugwa: Sasa kuwa kosa kisheria hapo ndio siwezi kusema.
NB. NAAMBIWA NA WAKILI HAPA KUWA TOKA ASUBUHI HAYA MASWALI YA JAMHURI SIO KESI NI SIASA TU.
Kesi ni Uhaini wa Kuchapisha na Kusambaza na kuitisha Serikali. Huko hatujafika kabisa.
Katuga: Kwahiyo hizi Haki tulikuwa tunazungumzia za Katiba ya Chadema au ipi?
Golugwa: Kwamba ulikuwa hujui tunazungumzia katiba gani? Ni ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katuga: Jana ulisema kuwa wasimamizi wa Uchaguzi walishirikiana na wagombea wa CCM kubadili fomu za wagombea wa chadema, je ulikuwepo au hukuwepo?
Golugwa: Nilikuwepo
Katuga: Jana ulieleza mahakamani kama ulikuwepo ofisi yoyote ya uchaguzi na ukashuhudia msimamizi wa uchaguzi akibadili fomu ya mgombea wa chadema?
Golugwa: sikusema
Katuga: Je ulitaja jina la mtendaji au msimamizi wa uchaguzi aliyekuwa anabadili fomu za wagombea wa chadema?
Golugwa: sikumtaja
Katuga: Halafu unasema mimi nina roho mbaya?
Golugwa: Ni kweli una roho mbaya na sura pia mbaya
Watu kicheko๐๐๐๐๐
Katuga:Jana ulisema kuwa wasimamizi wa uchaguzi walikuwa wanafunga ofisi ili wagombea wa chadema wasipokelewe fomu zao, ulitaja ofisi au jina la msimamizi wa uchaguzi?
Golugwa: Nilitaja matendo yao hao wasimamizi wa uchaguzi
Katuga: Jana ulisema kuwa mawakala wa chadema hawakukuta viapo vyao kwenye vituo vya kupiga kura, na mawakala wa CCM pekee ndio walipewa viapo, uliiambia mahakama wakala fulani wa chadema hakukuta kiapo?
Golugwa: Nilielezea matukio yote kwa ujumla ambayo mawakala wetu mambo ya kishenzi waliyokuwa wanafanyiwa na wasimamizi wa uchaguzi
Katuga: Umesema wewe huna taaluma ya sheria lakini uligusia sheria za uchaguzi?
Golugwa: Nilizigusia
Katuga: Ulizigusia Kanuni zilizotungwa na waziri wa TAMISEMI?
Golugwa: Nilizitaja na nikasema zilitungwa na mkwe
Katuga: Ulitaja mapungufu ya Kanuni hizo?
Golugwa: Sikuainisha moja moja ila nilitaja kwa ujumla
Katuga: Chadema ilishiriki uchaguzi wa 2025?
Golugwa: Haikushiriki
Katuga: Ni sahihi kuwa Chadema haikushiriki kwasababu ya No Reforms No Election
Golugwa: Ni sahihi na huo ndio msimamo wa Mkutano Mkuu mpaka leo
Part 351 itaendele kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 349
Upande wa Jamhuri wanaendelea kumfanyia cross examination, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Amani Golugwa
Mwinuka: Maudhui ya taarifa yanaweza kuathiriwa na fasili ya mtu.
Golugwa: Yanawezekana. Ukiwa umetafsiri vibaya itakuwa ni vibaya. Na kama ametafsiri vizuri basi ndio itakuwa vizuri.
Mwinuka: Umeeleza chochote kuhusu uwezo wako wa kutafsiri kingereza?
Golugwa: Naweza kutafsiri vizuri tu.
Mwinuka: Title ya ripoti ya Jumuiya ya Madola ikoje?
Golugwa: Nilisema nimeona tamko sio ripoti umesahau tena.
Mwinuka: Kichwa cha habari cha Thabu Mbeki ripoti yake?
Golugwa: Ilisema Ripoti ya Thabu Mbeki kuhusu matukio ya 2025 siwezi kukumbuka neno kwa neno?
Mwinuka: Ripoti ya Afrika Mashariki kuhusu uchaguzi uliangalia?
Golugwa: Sikuangalia hiyo.
Mwinuka: Una imani na ripoti ya Chande?
Golugwa: Sina imani nayo.
Mwinuka: Kwahiyo ulichokieleza kilichopo kwenye ripoti huna imani nacho pia?
Golugwa: Niliyosema kuna mambo nakubaliana nayo lakini sio kukubaliana na ripoti yote.
Mwinuka: Kuhusu sababu za machafuko vipi?
Golugwa: Hata saa mbovu huwa inasema ukweli kwenye kipande cha sababu za Machafuko nakubaliana nayo.
Mwinuka: Kikao cha Tar. 03/04 kwa mujibu wa kikao kile kulikuwa na kinachogusa unyunyu na manukato.
Golugwa: Unyunyu kama neno haikuwepo.
Amemaliza Ignas Mwinuka ameenda Kukaa amemaliza maswali.
Anasimama Ajuaye anasema anafuata Nassoro Katuga.
Katuga: Kuulizwa maswali ya Dodoso ni suala la kisheria na sio roho mbaya ya mawakili wa serikali?
Golugwa: Nakubaliana na wewe lakini wapo mawakili wa Serikali wana roho mbaya wanasingizia watu kesi za uongo. Roho mbaya ipo.
Katuga: Kesi ya Jinai ni ushahidi na sio ushabiki?
Golugwa: Nafahamu.
Katuga: Kuna taarifa zako ziko kwenye public domain?
Golugwa: Nilisema ugomvi wangu na Mkurugenzi wa Jiji la Arusha. Nimesema hilo.
Katuga: Taarifa zako na waandishi ziko kwenye Public Domain?
Golugwa: Zipo.
Katuga: Wewe ni mjumbe wa Kamati kuu ya Chadema?
Golugwa: Ndio toka January 22, 2025.
Katuga: Tar. 29/08/2025 Kamati Kuu iliketi kujadili mambo mbalimbali.
Golugwa: Iliketi lakini sio kujadili mambo mbalimbali.
Katuga: Ulitangaza maazimio ya Kamati Kuu?
Golugwa: Ni kweli
Katuga: Hiyo taarifa ipo kwenye public domain?
Golugwa: Ni kweli
Katuga: Miongoni mwa vitu ulivyotangaza ni kuhusiana na kesi hii?
Golugwa: Kweli
Katuga: Ulisema mmekusudia kumtetea mheshimiwa mwenyekiti wa Chama?
Golugwa: Tulisema viongozi waelekeze nguvu zao hapa wasifanye mambo mengine. Tumtetee Mwenyekiti.
Katuga: Kwahiyo umeleekeza nguvu kumtetea?
Golugwa: Nguvu nyingi kabisa.
Katuga: Kuteuliwa na kuchaguliwa utofauti?
Golugwa: Kuchaguliwa kuna mchakato lakini kuteuliwa anakuteua.
Katuga: Katibu Mkuu wa Chama wa sasa anaitwa nani?
Golugwa: Anaitwa John Mnyika na ameteuliwa na Mwenyekiti?
Katuga: Akitokea mtu akisema aliteuliwa na kuidhinishwa je na Kamati Kuu?
Golugwa: Hatakuwa sahihi.
Nb. Viongozi Wakuu wa Chadema hawaidhinishwi na Kamati kuu.
Katuga: Kuwa Muhasibu tangu 2001 na kufanya kazi za kihasibu toka 2001 kuna utofauti? Si umesema kuna mawakili wa serikali wana roho mbaya.
Golugwa: Wewe kweli kabisa roho mbaya unayo. Ni kweli kabisa.
Katuga: Ulichukua minutes za kikao cha Tar. 03/04?
Golugwa: Kile hakikuwa kikao cha kuandika minutes.
Katuga: Aina za vikao?
Golugwa: Kuna vikao vya uchaguzi na vikao vya kawaida.
Katuga: Vikao vya ndani na hadhara akitokea mtu akisema ni aina ya vikao vya Chadema kama ilivyo vikao uchaguzi na kawaida atakuwa sahihi?
Golugwa: Yuko sahihi. Ni vikao vyote vya Chadema.
Katuga: Ulisema hukumbuki kwamba vikao viko sura ya ngapi ya Katiba?
Golugwa: Sahihi niletewe nitaisoma nione.
Katuga: Kutakuwa na vikao vya aina nne kwa mujibu wa Katiba Soma?
Golugwa: Vikao vya aina nne na vinahitaji maelezo
Part 350 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.