UKIRI WA BARAKA ZA SIKU.
NAIBARIKI JUMANNE YANGU.
Familia yangu itasonga mbele haiwezi kurudi nyuma. Kwetu kutakuwa Kwema, hakutakuwa na magomvi wala magonjwa wala vifo, wala ukata. Maisha yetu yatakuwa mazuri kwa kuwa tumebarikiwa na BWANA.
YESU Asante.
WELCOME TO THE NEW SEASON YOUTH CAMP 2026
Welcome to the Youth Camp 2026, which will take place from 17–20 June 2026 at Precious Centre, Kibaha, Coast Region (Pwani), Tanzania.
This is your opportunity to connect with young people from different regions of Tanzania in a unique camp designed for youth with vision, dreams, and a passion for serving God and building a purposeful life.
At this camp, you will have the opportunity to:
✅ Learn the Word of God and grow spiritually. ✅ Build new friendships with young people from various parts of Tanzania. ✅ Participate in life-enriching seminars and discussions. ✅ Gain knowledge on spiritual, social, and economic development. ✅ Discover and develop your talents and gifts.
🏆 There will also be a variety of exciting competitions, including:
⚽ Football (Soccer) 🏃 Running Competitions 👔 CEO of the Year 🎤 Singer of the Year 👗 Fashion Designer of the Year ✨ And many more exciting activities!
Young person, this is your opportunity to begin a new season of positive thinking, greater vision, creativity, and success for your present and future life in the Kingdom of God.
Don’t miss it! Your new season starts here.
KARIBU MSIMU MPYA WA KAMBI YA VIJANA 2026
Karibu kwenye Kambi ya Vijana 2026 itakayofanyika kuanzia tarehe 17–20 Juni 2026 mahali ni Precious Centre, Kibaha, Mkoa wa Pwani.
Huu ni wakati wako wa kuungana na vijana kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania katika kambi ya kipekee iliyoandaliwa kwa ajili ya vijana wenye maono, ndoto na shauku ya kumtumikia Mungu na kujenga maisha yenye kusudi.
Katika kambi hii utapata nafasi ya:
✅ Kujifunza Neno la Mungu na kukua kiroho.
✅ Kujenga mahusiano mapya na vijana kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania.
✅ Kushiriki semina na mijadala yenye kujenga maisha.
✅ Kupata maarifa kuhusu maendeleo ya kiroho, kijamii na kiuchumi.
✅ Kugundua na kukuza vipaji vyako.
🏆 Pia kutakuwa na mashindano mbalimbali yakiwemo:
⚽ Mpira wa Miguu
🏃 Mashindano ya Kukimbia
👔 CEO Bora wa Mwaka
🎤 Mwimbaji Bora wa Mwaka
👗 Mbunifu Bora wa Mwaka
✨ Na mengine mengi ya kusisimua!
Kijana, hii ni fursa yako ya kuanza msimu mpya wa mawazo chanya, maono makubwa, ubunifu na mafanikio kwa ajili ya maisha yako ya sasa na ya baadaye ndani ya Ufalme wa Mungu.
Usipange kukosa! Msimu wako mpya unakuanza hapa.
NENO LA SIKU
Na, Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira – Kanisa la Efatha
TAREHE: 08/06/2026
SOMO: UTAKATIFU
Mambo ya Walawi 20:26 “Nanyi mtakuwa watakatifu kwangu mimi; kwa kuwa mimi BWANA ni mtakatifu…”
Utakatifu si kwa ajili ya watu wengine, bali ni kwa ajili ya Mungu. Unapomsogelea Mungu, anataka kuona utakatifu ndani yako, si madhaifu wala uchafu wako.
Utakatifu haupatikani kwa nguvu zetu, kufunga au kuomba pekee, bali kupitia neema na dhabihu ya Yesu Kristo msalabani. Tunapothamini na kuheshimu kile Yesu alichotufanyia, tunaishi maisha yanayompendeza Mungu.
WORD OF THE DAY
With, Apostle and Prophet Josephat Elias Mwingira – Efatha Church
DATE: 08/06/2026
SERMON: HOLINESS
Leviticus 20:26 “You shall be holy to Me, for I, the LORD, am holy…”
Holiness is not for other people; it is for God. When you draw near to Him, He desires to see holiness in you, not your weaknesses or your impurities.
Holiness is not attained through our own efforts, fasting, or prayer alone, but through the grace of God and the sacrifice of Jesus Christ on the cross. When we value and honor what Jesus has done for us, we live lives that are pleasing to God.
3. USEMI WAKO
Mithali18:20 “Tumbo la mtu litajazwa matunda ya kinywa chake; Atashiba mazao ya midomo yake.
Usiruhusu shetani aweke neno lake kinywani mwako. Linda usemi wako. Lazima utambue kuwa kuna nguvu katika kinywa chako. Namna unavyosema ndivyo unavyoamuru vitu viwepo na unavutia vitu viwe karibu. Laana na baraka inabebwa na ulimi wako.
Kwa namna unavyosema ndivyo unavyotamka baraka au laana katika ubaadaye wako. Unavyotamka mbingu inakuangalia na inatengeneza yale mazingira ya uliyotamka na unavyotamka vya dunia unaamuru laana katika maisha yako. Unapaswa uliamrishe Neno la Mungu ili kutengeneza ubaadaye wako maana pasipo ukiri wa imani huwezi kuona ubaadaye wako. Imani inabebwa na neno la Mungu na huwezi kutengeneza maisha yaliyobora pasipo imani.
Maisha yetu hayashikiliwi na serikali bali na yanashikiliwa na nguvu kutoka mbinguni. Ni kweli tunapata hapa duniani ila anayetupa sisi ni Mungu na sio wa dunia hii bali inatoka kwa muumba wetu. Ukijua ya kwamba bajeti yako haipo duniani bali ipo mbinguni utaona Mungu akiamrisha watu akuletee vitu na kubadilisha maisha yako.
Zaburi 19:14 “Maneno ya kinywa changu, Na mawazo ya moyo wangu, Yapate kibali mbele zako, Ee BWANA, Mwamba wangu, na mwokozi wangu.”
@ MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA
MAOMBI
1. Mwombe Bwana Yesu; eeh nafsi yako, nia yako na mawazo yako yaelekea njia ya Bwana, na Neno la Mungu likae ndani yako katika Jina la Yesu.
2. Msihi Mungu akili yako, inene akili ya Mungu, maandiko ya Mungu na kinywa chako kiseme kile ambacho unasikia Neno la Mungu pasipo kuangalia mazingira yako.
2. IBILISI ATAINGILIA HATUA ZAKO
Zaburi 119:105 “Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu.”
Unapomruhusu ibilisi aingilia njia zako utaona giza, hutaona njia ya kutoka, wala hutaona mpenyo na hutaona ubaadaye wako, maana ibilisi ameingilia njia zako. Unapoona vitu haviko sawa ujue ibilisi ameingilia kuchanganya njia zako, ndipo biblia inasema “Uzao wa mwanamke utaponda kichwa chake na wewe ibilisi utamponda kisingino.” kisingino ni njia zako, ibilisi hajaruhusiwa kuingia katika akili yako bali ameruhusiwa kukuchanganya katika njia zako. Neno la Mungu lisipokaa katika akili yako ibilisi anakuchanganya katika maisha yako.
Waefeso 5:15-16 “Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu.”
Zaburi 16:11 “Utanijulisha njia ya uzima; Mbele za uso wako ziko furaha tele; Na katika mkono wako wa kuume Mna mema ya milele.”
Unapoweka Neno la Mungu kichwani kwako, unamsababisha Mungu afanye jambo fulani katika maisha yako.
Zaburi 119:59-60 “Nalizitafakari njia zangu, Na miguu yangu nalizielekezea shuhuda zako. Nalifanya haraka wala sikukawia, Kuyatii maagizo yako.”
Lazima utafakari njia zako, usiangalie mtu bali angalia njia zako maana unayepitia magumu na changamoto katika dunia hii ni wewe.
@ MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA
Galatia 3:1 “Enyi Wagalatia msio na akili, ni nani aliyewaloga, ninyi ambao Yesu Kristo aliwekwa wazi mbele ya macho yenu ya kuwa amesulibiwa?”
Watu wenye akili ya Mungu hawasubiri kuambiwa wamekosea hapa bali wanarudi magotini mwa Bwana na kuomba rehema za Mungu.
Mathayo 7:24 “Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba;”
Ili uweze kuepukana na ibilisi, kushika akili yako, hakikisha unaweka Neno la Mungu na maandiko ya Mungu ili ibilisi asiingilie akili yako. Maandiko yajae ndani yako. Mungu anamwambia Joshua “Maneno ya kitabu hiki yasindondoke kinywani mwako” Unapoona vitu haviendi kabisa hakikisha unanena Neno la Mungu, Mfano wewe ni mfanyakazi neno linasema “Bwana atabariki kazi ya mikono yangu” Unanena hilo neno mpaka linakuwa la kwako na ibilisi anashindwa na Neno la Mungu linatimia kwako. Je una Neno gani la kusema? Neno ulilonalo ni Neno la Mungu, litamke mpaka litimie kwenye maisha yako. Shetani hachezi na watu wenye akili bali anacheza na watu wapumbavu.
Luke 6:48 “Mfano wake ni mtu ajengaye nyumba, na kuchimba chini sana, na kuweka msingi juu ya mwamba; na kulipokuja gharika, mto uliishukia nyumba ile kwa nguvu, usiweze kuitikisa; kwa kuwa imejengwa vizuri.”
Mtu yeyote ambaye anatamka Neno na anaongea Neno na ndani yake pamejaa Neno la Mungu anakuwa kama nyumba iliyojengwa kwenye mwamba, ila kama hauna Neno la Mungu utanyumbishwa na kupewa kila maneno mabaya na yule mvamizi. Mtu anapokusengenya na ukayapa nafasi yale maneno ya uwongo, yanabadilika na kuwa kweli na kutawala akili yako na kuanza kujenga chuki na watu ndani yako.
OMBI: Kataa ibilisi asishike akili yako ( Kwa mawazo, maneno na matendo) na kunena juu yako bali wewe ni wa Yesu Kristo na una akili ya Mungu maana wewe ni sura na mfano wa Mungu.
SOMO: MAPENZI YA MUNGU KWAKO
1 Yohana 5:18 “Twajua ya kuwa kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi; bali yeye aliyezaliwa na Mungu hujilinda, wala yule mwovu hamgusi.”
Jiulize unajilinda mwenyewe? akasema yule amjuaye Mungu ujilinda, analinda vitu vya msingi vitatu navyo ni;
1. Mawazo, fikra na nia yake.
2. Hatua zake mwenendo wake hapo ndipo palipo na mahusiano na watu.
3. Maneno ya kinywa chake, namna unavyoongea na kuwasiliana na watu.
1. MAWAZO, FIKRA NA NIA YAKE
Waefeso 4:27 “wala msimpe Ibilisi nafasi.”
Usimpe ibilisi nafasi kwenye akili yako, usiruhusu kabisa kwa sababu kwenye akili ndipo unapowaza, unapoamua, unapotengeneza mipango yako na ndipo kwenye ubadaye wako na ibilisi akiingia katika akili yako utasababisha uharibifu.
2 Wakorintho 4:4 “ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.”
Usipomzuia ibilisi katika akili yako atakupeleka mahali usiamini chochote kinachotokana na Mungu na kuwaza mambo ya dunia hii, kwa kuumiza wengi na kufanya uovu katika duniani. Ukiruhusu ibilisi katika akili yako hautaona uponyaji unaona uharibifu, huoni usaidizi wa Mungu unaona mahangaiko na kupambana katika maisha yako.
Yohana 12:40 “Amewapofusha macho, Ameifanya mizito mioyo yao; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakafahamu kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya.”
Zaburi 119:99-100 “Ninazo akili kuliko wakufunzi wangu wote, Maana shuhuda zako ndizo nizifikirizo. Ninao ufahamu kuliko wazee, Kwa kuwa nimeyashika mausia yako.”
Unakuwa na akili kuliko waliokufundisha, akili kama imeharibika huwezi kuongea na Mungu, akili ikiingiliwa na shetani huwezi mjua amefananaje? Ukiruhusu akili ya Mungu utajua hii ni akili ya Mungu, hii ni akili ya kibinadamu na hii ni akili ya shetani, hivyo amua ubaki kwenye dhambi uwe na akili ya kibinadamu au uache dhambi upate akili ya kiungu. Ukikaa na hiyo hali uliyonayo utakuwa wa kawaida mpaka unafariki dunia hivyo amua kufa.
Kataa maisha ambayo shetani anamamlaka kwako, lazima uwe na maisha ambayo unajua umekosea na unarudi kumwomba Mungu wako. Ubinadamu wako ukikusukuma kukosea rudi kwa muumba wako tengeneza na Mungu na usonge mbele. Neno la Mungu linasema “Utaijua kweli nayo itakuweka huru” Kweli ya Mungu inakaa ndani yako kwa sababu unatambua makosa yako pale unamkosea muumba wako na kurejea kwake pasipo mtu kukuambia umekosea yaani unatambua mapema makosa yako. Katika biblia tunaona Daudi alitambua makosa yake na kumrejea muumba wake pasipo kuambiwa na mtu yeyote.
@ MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA
Siku ya utakaso, siku ya kuweka wakfu kile alichokiumba tunaona kitu cha ajabu sana ambacho ni ulinzi, Siku ya kwanza ya ndoa yangu niliweka ulinzi. Mfano wa wanandoa wanapoanza maisha yao, cha kwanza Mungu anahakikisha una ulinzi, Mungu aliweka jambo la msingi sana kwetu sisi kufuatisha utaratibu wake.
Pasipo mvamizi hakuna vita, maana wapo wawili na walianza kwa pendo na wataishia kwa pendo la Mungu, ila mvamizi cha kwanza atakachoiiba ni Pendo la Mungu. Bahati mbaya wa mama ndio wa kwanza kuingiliwa na mvamizi katika ndoa yake maana alianza na mama yetu Hawa ambaye alivamiwa na nyoka. Unaposoma biblia unapata picha hali za maisha ambayo ni uumbaji wa Mungu na ulinzi wa Mungu.
Mungu hakuumba hali ya kushindwa, ndio maana alikuja tena kutukomboa katika dhambi na Mungu alisanifu ushindi. Ushindi upo katika maamuzi. Kila ulichoamua kinaweza kukufanya kuwa mshindi au mshindwa.
Mungu alimuumba mwanadamu akiwa mkamilifu na hali ya kushindwa imetokana na mvamizi. Unaona wanandoa wanaanza vizuri na baadaye mmoja wao anaanza kubadilika ujue tayari mvamizi ameingia. Ulinzi haupo pale kukumbembeleza bali upo pale kukushughulikia. Wakati Mungu anashughulika na mvamizi alianza kushughulika na aliyemkaribisha mvamizi ambaye ni Hawa na alimnyang'anya mamlaka ya kuamua.
Nyumba ikiharibika ni wewe mwanaume maana mwanamke ameshanyang'anya mamlaka hivyo shughulika na mkeo usimwonee huruma muhimu ulinzi upo, baada ya hapo Mungu akamwendea Adam akamwambia "utakula kwa jasho mpaka kifo." Ni kweli wanawake wana macho mengi ila linda usalama wa mke wako, wa kwako na kizazi chako kijacho.
Mungu hakutengeneza ubaadaye kwa mwanamke, bali alitengeneza ubaadaye wa mwanaume, mwanamke amepewa kushughulikia ya leo ndio maana akijifungua mtoto anasahau yale maumivu ila mwanaume amepewa kujua alipotoka, alipo na anapokwenda.
@ MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA
Mungu aliumba Mbingu na nchi na ndiye aliyefanya na vyote unavyoona hapa duniani viliumba na YEYE na akawapa ruhusa uumbaji kuvifinyanga. unaona viti, magari, vyote vinatokana na nchi na katika nchi yapo madini ili kutengeneza hivi vitu. Nguo tulizonazo zinatokana na pamba, chochote unachoona chanzo ni Mungu ukimwelewa au ukimfahamu Mungu ndipo unapata maarifa ya kufanya kitu fulani kiwe na maana katika maisha yako.
Ndege anatengeneza kiota chake mwenyewe cha kujilinda ila wewe ujafanya chochote, hii inamaanisha ndege wanamjua Mungu wao. Wadudu wanakusanya chakula kwa ajili ya ubaadaye wao pale njaa itakapotokea ila mwanadamu anatapanya chakula na kumaliza chote. Je ndege si zaidi ya mwanadamu? Binadamu wanaishi pasipo kuwa na ubaadaye. Jinsi maisha yanavyoendelea watu wanamsahau Mungu kuliko wadudu wanavyomkumbuka muumba wao.
Mwanzo 2:1 “Basi mbingu na nchi zikamalizika, na jeshi lake lote. Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya.”
Tunapaswa kujua kwa nini Mungu aliumba na akaweka mpango wa usalama? ni kwa ajili ya ulinzi. Mungu alielewa umuhimu wa usalama. Linda chochote unachofanya hapa duniani ila naona jamii ya wanadamu hawalindi chochote wanachofanya, hawalindi watoto wao, afya zao, ndoa zao, biashara zao, kazi zao yaani hawalindi chochote na usalama ni lazima katika maisha ya mwanadamu na mwanzo wa uumbaji wake, Mungu aliongeza kipengele cha ulinzi yaani usalama.
@ MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA
IBADA YA SIKU YA JUMAPILI | KANISA LA EFATHA MWENGE | 07.06.2026
1 wakorintho 14:2 "Maana yeye anenaye kwa lugha, hasemi na watu, bali husema na Mungu; maana hakuna asikiaye; lakini anena mambo ya siri katika roho yake.”
@ MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA
Zaburi 103:1-4 “Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA. Naam, vyote vilivyo ndani yangu Vilihimidi jina lake takatifu. Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA, Wala usizisahau fadhili zake zote. Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote, Aukomboa uhai wako na kaburi, Akutia taji ya fadhili na rehema,”
Sitakufa bali nitaishi niyasimuliye matendo yake makuu maana Bwana Yesu amenisamehe na kuniponya na mauti na leo nipo hapa kulitukuza Jina lake.
@ MTUME ELIAKUNDA MWINGIRA