@Mkunga_Og Binafsi naona shawaha za mwanaume zipo na faida san kweny mwili wa mwanamke kwaiyo withdraw ni kam unamnyima mwenza wako proteins za kimsaidia kujenga mwili wake ..kwa mm nashauri ni bora kutumia calenda means period menstruations circle
🚨AUGUSTINE OKEJEPHA, Dogo kutoka Nigeria ana miaka 20 tu ndio anaenda kuzima eneo la Kiungo Mkabaji pale Simba Sports kutoka Rivers United, alikuwa na mashindano bora sana msimu uliopita ya klabu barani Afrika.
Simba mpaka sasa hakuna Mchezaji aliyesajiliwa amevuka miaka 25, hii ni project inapikwa ni suala la muda na kuwa na Kocha bora ambaye anaweza kuendana na Vijana wengi kwenye kikosi ambao wana njaa ya mafanikio, Simba wanarudia walichofanya miaka minne nyuma.
Kiukweli Mwekezaji MO akishirikiana na Mwenyekiti, Baba yangu MANGUNGU wameamua safari hii! Kifupi Mzee wangu yupo tayari hata kuuza viwanja vyetu Kilwa kule😀💪
MANGUNGU JR.
Kocha Rulani Mokwena jana kwenye Interview yake na Gwiji Robert Marawa, amesema hakutaka kuondoka Mamelodi Sundowns ila alilazimishwa kuondoka, lakini pia sababu nyingi hawezi kuziweka wazi kwakuwa kabla ya kuondoka alisaini kifungu cha kutosema chochote kuhusu Mamelodi huko nje (Confidentiality clause).
Hivyo amelipwa chake na klabu imehodhi taarifa zote kuwa hapaswi kwenda nje kuzungumza chochote, nje na hapo atakuwa matatizoni kisheria kwakuwa amesaini kifungu hicho cha kisheria, klabu imechagua kujiwahi kulinda taswira yake kisheria😀! Wajanja sana Masandawana.
🚨 UONGOZI wa klabu ya Simba umempa mkataba wa miaka miwili aliyekuwa kocha msaidizi wa Raja Casablanca, Fadlu David anayeelezwa atatua nchini Ijumaa sambamba na wasaidizi wake.
.
Kocha huyo ambaye amethibitisha ujio wake Tanzania baada ya kutumia ukurasa wake mtandao wa kijamii ‘Instagram’ kuwaaga viongozi, wachezaji na mashabiki wa timu aliyokuwa akiifundisha.
.
“Ulikuwa ni wakati mzuri, msimu mzuri, wachezaji bora, wafanyakazi wenzangu tulikuwa na benchi bora bila kuwasahau mashabiki.” Ni ujumbe wa kocha huyo akiwaaga.
MAGETONI ndipo Wanangu wamechill muda huu, wanatazama juu kuamini Mwenyezi Mungu aliye hai ambaye ndie aliyempa rizki Mzee Bakhresa na MO, tunamtazama kwa kuamini kuwa hajatusahau kesho atatupa rizki yetu, nawapa tano Wanangu kwa kuendelea kuvuka vipindi vigumu ambavyo wengi waliamini tupo sawa ila moyoni tuna vita zetu kali sana.
MAPENZI, yamekuwa machungu sana, kuna namna mpya ya ‘kujiuza’ inaitwa kuhudumia, utasikia Mwanaume asiye na pesa siwezi mpa nafasi, ndio hivyo Wanangu wana real love ila dunia inataka pesa, ugali dagaa kwenye amani sio utani, Dada zetu wamekubali wali nyama motoni sio vitani tena, mkono mtupu wa Mwanangu hauwezi kulambwa.
INSTAGRAM, ni chaka ambalo tunatazama wenzetu walioshinda huku sisi tukiwapigia makofi kwa bidii mpaka pale zamu yetu itakapofika, tukiona wapo Dubai tunacomment kwa furaha, tukiona wapo Ulaya tunashangilia, maisha yetu yana vita nyingi sana kwahiyo tumechagua furaha kwakuwa chuki ni mzigo mwingine ambao hatuwezi kuubeba.
HARAKATI, zimetusaliti sana Wanangu mfumo unataka tuwe Machawa, ajira zinataka tuvunje nazi na kuoga njia panda, Utajiri sometimes unataka kafara, wanaotupa nafasi wanapenda tufanikiwe ila sio kuzidi wao, wanaodai haki wanaitwa wajeuri, Chawa anaitwa Mchapakazi na Wanangu wapo mtu kati mbele kiza na nyuma moto.
MICHONGO, imekuwa msamiati mgumu sana Wanangu, walioshika mpini wanavuta sana kisu kinatukata, Dada zetu wanashusha sana sketi kwakuwa vyeti sio kitu tena, Wanetu wanapiga Interview lakini hakuna nafuu bado kombolela halijalipa na kila tukijitokeza kubutua wanatuwahi.
MITAA, inatudai sana Wanangu kwakuwa waliamini kuna sehemu tunaelekea lakini maisha yametupa njia mpya na mfumo haujatupa machaguo, bado wanatuona kitaa licha ya vyeti vyetu, kuna muda wanatucheka kuwa kiko wapi, kuna muda tuliowaacha kitaa wana maisha kuliko sisi.
Unaona nini ukiwaona Wanangu? Fahamu unawatazama Washindi hao wapo vitani, hawana michongo ila wanavaa wanapendeza, wanakula na wanaishi, mioyo yao imejaa upendo wakiamini kesho nayo siku🫡