Katika safari kuna wanaosafiri, wanaosafirisha wasafiri, wasindikizaji na wapagazi. Ndivyo ilivyo katika safari ya maisha. Tambua nafasi yako na nafasi za watu wengine katika safari ya maisha yako. Tambua pia nafasi yako katika safari za maisha ya watu wengine.
Ngazi ni vipande vya mbao au chuma vilivyounganishwa kukuwezesha wewe kukwea juu. Tukishafika juu tunaishukuru ngazi na kusahau kushukuru vipande vyake. Katika maisha, ni rahisi kumshukuru wa mwisho kukusaidia ukawasahau waliokusaidia kumfikia huyo wa mwisho aliyekupandisha.
@tonytogolani Bro @tonytogolani hakika umebarikiwa kuwa na hekima sana. Mungu akutunze sana na aendelee kukujaza maarifa zaidi tuendelee kujifunza kupitia wewe.
Afya, Rizki na Umri ndio mambo tunayopaswa kuyaomba sana kwa Mwenyezi Mungu katika umri wa ujana. Ndio mitihani ya rika la ujana. Ndio yanayoamua utu uzima na uzee wako utakuwaje.
Katika maisha yetu ya kila siku watu wana tukosea wanatusemea vibaya na wengine kutuumiza lakin unajua nini hutakiwi kubeba mtu moyoni, semehe kusamehe kuna faida kuliko kubeba mzigo mzito ya chuki na visasi, Samehe ila usisahau, GM Fam ๐
#SikilizaTogolani "Wanaume tunaothamini wanawake tupo wengi tu sema mama na dada zetu ndio wanahisi tumelogwa na tumekaliwa vichwani. Wanaume wenzetu pia wanaona tunaua bendi. Inabidi tujitutumue hivyo hivyo na mfumo dume". Mshauri wangu wa Masuala ya Kipumbafu, Anasa na Starehe
Binadamu hupenda kujipambanua kwa jambo au mambo ambayo yana umati. Ukiona uko peke yako kwenye jambo, jua wako wengi tu wanaoona kama wewe ila wamekosa ujasiri wa kujitokeza wanasubiri umati. Yaani wako wengi wanaokuunga mkono kimya kimya! Watu hupenda kuwa miongoni mwa wengi!
@sonnino123 Hapo nanunua bodaboda kama 16 hivi za TVS na hela itakuwa imeisha. Hizo boda nikiwakabidhi vijana waaminifu waniletee hesabu/day hiyo hela ndani ya week nakuwa nimeirudisha naanza kula faida ๐ช๐ช๐ช
@saza_hassan Hilo suala la kawaida sana ndugu. Nguo za ndani zinashauriwa zikauke kwa mionzi ya jua ili kuua baadhi ya bakteria tofauti na kuanika sehemu ambayo mionzi hiyo haifikii hivyo hao wanawake/wamama wako sahihi kabisa na pia kuanika chupi nje sioni kama ni shida kwa namna yeyote ile