There is Forex,there is Stocks market and then there is whatever in Gods name goes on in the vegetable market pale soko mjinga. Kwa kimombo tunaiita Thoko ya Itharù. Buana mkiskia watu wanasema wanaenda soko mjinga sio mcheso,ile soko ni mjinga cha ukweli. Sukuma wiki prices are like Millicent omangas sendes,yani iko very slippery. Sukuma gunia moja asubuhi inatokanga mia moja. But past 8am,brokers start mentioning prices that will put you in ICU for cardiac arrest
When I lived in ocha,I remember one time I had 6 gunias. According to my mathematicos,after paying nduthi guy 50kes for each gunia,I would remain with about 300 shillings,which was good money. Nakwambia nilianika mboga namna hii,broker akakuja akakagua akaniambia hii nitakupea 40. Nikamuuliza Forty? Akasema yes. Na unajua broker hawakubembelezangi,ni uchukue 40 ama ulale na maskuma yako. Na anakuonesha mboga ilimwagwa jana na watu walikosa wanunuzi
Broker akachukua gunia mbili. Akanipatia 80. Hii nikapiga hesabu nikaona pesa pesa nitapata hapa,yote nitalipa jamaa wa nduthi na nibaki na deni yake ya ishirini. Nilichukua 80 yangu nikaingia mkahawa kwanza,juu niliamka six kuingia shamba na baridi,nikajisunda mandazi sita na chai mbili. Jamaa wa nduthi kumbe nyuma pia anapiga hesabu,akaniuliza wewe utanilipa pesa yangu kweli na naona ni mandazi tu unakula?
Nikamuuliza Kìragú kichwa yako ni mzuri,nikulipe pesa yako na unaskia bei ni gani? Nikamwambia ingia hapa utafute zako pia. Nikauza gunia ingine moja nikateremka nyumbani na forty yangu,jamaa wa nduthi nilimuacha akipigana na soko. Hatujai ongea mpaka leo,ata gunia zangu sijai muuliza alipeleka wapi. Farming is not for the weak buana,soko ni mjinga
Khabusie!