@EsirEid Huu ndio ukweli pia tusisahau wale waliochoka huku usingizi mzito ukiwanyemelea huku wakiendesha chombo cha https://t.co/hIK46OaKs1 vyema wapaki pembeni Sehemu rafiki alafu wauchape usingizi kwa masaa kadhaa na hatimaye waendelee na safari.
Wenye msongo wa mawazo waweke umakini
Shida mnahisi DINI hatuijui. YESU ambae tumesherekea kuzaliwa kwake jana ni kweli ni MFALME WA AMANI ila huyo huyo MFALME WA AMANI alitaka "HAKI ITAWALE ulimwenguni na kukemea MAOVU".
Kwaakili ya kawaida inamaanisha YESU alijua HAKI ikitawala DUNIANI basi AMANI itatamalaki-maana AMANI ni tunda la HAKI.
Kwenu wahubiri na watu mnaojificha kwenye KICHAKA CHA AMANI, mnajua wazi msingi wa AMANI ni HAKI hubirini HAKI na wakumbusheni watawala kutenda HAKI kama kweli wanaipenda AMANI.
With Bishop Henry Mchamungu
Auxiliary Bishop of Dar-es-Salaam, Tanzania( Askofu Mkuu Msaidiizi Jimbo kuu la Dar es Salaam Roman Catholic.
Kanisa la Mungu, Kanisa la Watu na kanisa linalojali haki za Watanzania - Asante kwa huduma yako leo Parokiani kwetu
Kura haipaswi kulindwa inapaswa kujilinda yenyewe kwa mifumo ya kiuchaguzi inayohakikisha usalama!!,
kura inaibwa kwa mujibu wa sheria, lazima ilindwe kwa mujibu wa sheria
kwanza huwa hawaibi kura zetu bali huwa wanaongeza zao 😁😁
Masharti ya kanuni za maadili kwa vyama 👇🏽
Dhana ya kulinda kura ni kiashiria cha mapungufu kwenye mfumo wa uchaguzi. Kwa nini ulinde kura ?? Unatakiwa uzuie kisababishi kiletacho dhana kuwa kura yako haiko salama. Kukiwa na shaka kuhusu usalama wa kura huo sio uchaguzi.
PURITY AND SANCTITY OF ELECTIONS NDIO PA KUANZIA
BARUA YA WAZI KWA VIONGOZI WA DINI NCHINI TANZANIA
Yahusu: Wito wa Kurudi kwa Msingi wa Sadaka Takatifu Si Misaada ya Kisiasa
Waheshimiwa viongozi wa dini,
Kwa heshima kubwa na moyo mzito, nawaandikia barua hii nikiwa kama raia wa Tanzania, muumini, na mtumishi wa umma wa watu. Nawasimamia kwa heshima yenu, lakini pia kwa maumivu ya kuona hali ya kiroho na kijamii ya taifa letu ikiyumba kwa ukimya wa baadhi yenu ukimya unaotufunga sote.
Kwa huzuni tumeona baadhi ya taasisi za kidini zikianza kutegemea misaada ya kisiasa kama msingi wa huduma zao badala ya sadaka ya waumini walioguswa kwa moyo. Misaada hii imekuwa ikipokewa hadharani, ikashangiliwa, na kisha kutumiwa kama ishara ya ukaribu au fadhila kwa watawala. Lakini kwa roho ya kweli, tunajiuliza: hii ni sadaka au ni zawadi yenye masharti?
Maandiko yanatufundisha:
“Lakini wewe utoapo sadaka, mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo wa mkono wako wa kuume.” (Mathayo 6:3)
Sadaka ya kweli haina maneno, haipigwi parapanda, haibebi ajenda ya kisiasa. Inapokuwa na masharti au inakuwa sababu ya kunyamazisha sauti za kinabii, basi si sadaka ni ushawishi wa kifedha.
Na tunazidi kushangazwa na hali nyingine ya kimya. Kanisa ambalo Askofu Josephat Gwajima ni mtumishi wake limefungwa kwa maelezo yasiyoeleweka, bila taratibu za haki wala uamuzi wa wazi, na bado, hata baada ya madhabahu kufungwa, viongozi wa dini wengi mmekaa kimya. Kimya hicho si cha hekima bali ni cha hofu. Je, kama si yeye, bado mngebaki kimya?
Na kama kanisa linaweza kufungwa leo kimyakimya, kesho ni nani atakayefuatwa?
Mtume Paulo alisema kwa ujasiri;
“Je! Nataka kuwapendeza watu au Mungu? Kama ningali nikitafuta kuwapendeza watu, basi mimi singekuwa mtumishi wa Kristo.” (Wagalatia 1:10)
Waheshimiwa viongozi, tunapaswa kuchagua sasa:
•Je, tutaendelea kunyamaza huku madhabahu zikiporwa kwa taratibu?
•Je, tutakubali sadaka zitufunge midomo na misaada itupofushe macho?
•Au tutasimama kwa haki, bila kujali kama anayedhulumiwa ni wa upande wetu au la?
Bwana Yesu alisema:
“Mtu hawezi kutumikia mabwana wawili.” (Mathayo 6:24)
“Nanyi mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.” (Yohana 8:32)
Na sisi leo tunasema:
Kweli ndiyo uponyaji wa taifa. Haki ndiyo ibada ya kweli. Sadaka ya moyo ndiyo sadaka ya Mungu.
Kwa hivyo, tunawaomba muwe kioo cha ujasiri, si kivuli cha mamlaka.
Muongoze kwa Roho wa Mungu, si upepo wa siasa.
Kwa upendo, heshima na imani katika taifa letu na Mungu wetu,
Godbless Lema
If you want #Peace, prepare institutions of peace. This doesn’t refer only to political institutions, whether national or international, but to the entire forum of institutions – educational, economic, and social – that are involved.
Serikali yoyote inayotenda haki kwa Wananchi wake italindwa na hao Wananchi kwa wivu mkubwa mno na kamwe hatotokea yeyote kuitusi au kuidharau..
Ukiona Serikali ndio inatokwa mishipa kujitetea ujue kuna shida kubwa mahali.
📍
Kwa kuwa sisi siyo Malaika wakati mwingine anayekukosoa anaweza kuwa sahihi kuliko anayekusifia kwani anayekukosoa anakuonyesha ni wapi umekosea hivyo unapata fursa ya kujisahihisha.Kumbuka; Kujikosoa na Kukosoana ni silaha ya Mapinduzi &Kujiimarisha na siyo dalili ya udhaifu