Watanzania wameyakataa kabisa majiko ya umeme na kutumia Majiko ya Gesi
Mfano
Kuna majiko ya single burner yana 1000 watt
1000 watt ni sawa na 1kWh kwa saa
Tuseme kwa kadirio la juu unatumia jiko kwa masaa 2 kila siku yaani 2kWh
Kwa siku 30 za mwezi utakuwa umetumia 60kWh
Kwa sasa Tanesco wanachaji 1kWh kwa Tshs 100-290 kwa wateja wa kawaida
60kWhรTshs 290 unapata 18,000/=
Kwa mwezi unaweza kutumia gesi ya shilingi ngapi?
Pia siku hizi kuna majiko janja ya umeme ya induction haya kwenye matumizi ya nishati ya umeme ni rafiki sana na ni teknolojia ya kisasa. Ukinunua induction cooker hautajuta