Pole kwa Agnes Zakaria kwa kusumbuliwa na uvimbe kwa muda wa miaka 27, Pongezi kwa Madaktari Bingwa maarufu kama "Madaktari wa Samia" kwa kazi nzuri ya upasuaji wa uvimne waliyoifanya kwa Agnes.
Asante Rais Samia kwa wema huu, karibuni tena Buchosa wema na kazi uendelee.
Serikali imeanza matengenezo ya barabara ambazo zimeathiriwa na mvua katikia Jimbo la Buchosa.
Tumeanza na Barabara ya Nyakaliro - Kishamba yenye urefu wa kilometa 32 ambayo ni mkombozi wa uchumi kwa Wananchi wa Buchosa.
Kazi iendelee
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la TAG VCCT ameandaa Kongamano la Uamsho Revival Conference kuanzia Ijumaa ya Mei 17, 2024 hadi Jumapili ya Mei 19, 2014 litakalofanyika katika kanisa hilo lililopo Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
.
Ahadi yangu niliyoiahidi Machi 2, 2024 ya kutoa magunia 10 ya mahindi katika Shule ya Msingi Kasisa, Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema - Mwanza nimeitimiza. Natoa wito kwa wazazi kushiriki katika kuwasimamia watoto wao kwenye masuala ya kielimu ili kuongeza ufaulu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassani kwa akizindua Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam tarehe 08 Mei, 2024.
ARE YOU READY FOR HSM?
HEDHI SALAMA MARATHON
11th May 2024 @ Green Grounds – Oysterbay, Dar es Salaam
Theme: *“MAZINGIRA RAFIKI KWA HEDHI SALAMA*
Race categories: NOW ONLY: *10km Challenge Race; 5km Fun Run: 2.5km* Children and Elders.
Tickets selling out soon!
Register Now!
Kifo ni safari yetu sote, kinachotokea ni kwamba tunapishana muda wa nani ameanza na nani anafuata.
Dini zote zinasema kufa ni haki kwa kila kiumbe kinachoumbwa na Mwenyezi Mungu, hata hivyo ni vyema tukatiana moyo kwenye matatizo.
Pumzika kwa amani ndugu yangu, Marco Zagalo.
Uamuzi wa serikali kupitia Wizara ya Afya kupiga marufuku uvutaji wa sigara hadharani ni uamuzi mzuri unaopaswa kupongezwa kwani utahakikisha nguvukazi ya taifa haipotei, hususani vijana.
Vijana ndiyo nguvu kazi ya Taifa letu, Kazi iendelee
@samia_suluhu_hassan
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amezindua Kitabu cha Miaka 60 ya Historia ya Ofisi ya Makamu wa Rais pamoja na Kitabu cha Safari za Picha ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 60 kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.
Jana April 23, 2024 nilipata nafasi ya kuchangia hoja bungeni kwenye Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira kwa Mwaka wa Fedha 2024/25.
Hoja yangu ilijikita zaidi katika kuwalinda wanawake wanaojishughulisha na uchimbaji wa madini.
Uchapaji wako wa kazi na uwajibikaji katika kuitumikia jamii ndiyo nyenzo ya maendeleo.
Leo unapoadhimisha kumbukizi ya siku yako ya kuzaliwa @ridhiwani_kikwete, nakuombea kila la heri katika kuwatumikia wananchi.
Kazi iendelee
#CCMImara#TunaendeleaNaMama#KaziIendelee
Imetimia miaka 40 sasa tangu tulipoondokewa na aliyekuwa Waziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Edward Moringe Sokoine.
Naungana na wananchi wenzangu wa Buchosa kuwapa pole wanafamilia na watanzania kwa ujumla na kuendelea kumuombea kwa Mungu apumzike kwa amani.
Naungana na wananchi wenzangu wa Buchosa kutuma salamu za pole kwa waathirika waliokumbwa na mafuriko nchini yaliyotokea kulingana na uwepo wa mvua za El - Nino, Na salama za pole kwa wanafunzi walipata ajali ya gari.
.
@samia_suluhu_hassan @ikulu_mawasiliano
@ccmtanzania
Thamani yako haitokani na watu kusema una thamani, bali inatokana na wewe kujitambua bila kujali mazingira ukaionyesha thamani hiyo mbele ya umma.
.
@samia_suluhu_hassan @kassim_m_majaliwa @biteko @wizara_elimutanzania @wizara_sanaatz @millardayo@tbc_online@globaltvonline
Asante Ndugu Boniventura Destery Kiswaga kwa kuwasilisha swali langu leo Bungeni, Shukrani kwa Wizara ya Maliasiri na Utalii kupitia kwa Naibu Waziri Mhe. Dunstan Kitandula (@dunstankitandula) kwa majibu mazuri ya swali langu leo Bungeni.
#VitendoVinaSauti#TunaendeleaNaMama