Kikao kazi hicho cha Siku tatu kinawashirikisha Viongozi zaidi ya Mia Sita Hamsini kutoka Taasisi, Mashirika na Wakala wa Serikali. Kauli mbiu ya Kikao hicho ni โKujenga Ushirikiano Endelevu katika Mazingira ya Ushindani wa Kimataifa โ Wajibu wa Mashirika ya Umma
Benki ya NMB imedhamini na kushiriki kwenye Kikao kazi cha wenyeviti wa Bodi na watendaji wakuu wa taasisi za umma (CEOs Forum
2025) kinachoendelea katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano Arusha (Arusha International Conference Centre).
Ujumbe wa NMB umeongozwa na David Nchimbi - Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi pamoja na Juma Kimori - Afisa Mkuu wa Fedha na Kaimu Afisa Mtendaji mkuu.
Tarehe 28 Agosti 2025 pale Tanganyika packers, Kawe, jijini Dar es Salaam, tutasimama pamoja kushuhudia ukurasa mpya wa Taifa letu ukiandikwa kwa KISHINDO CHA KIJANI.
#kishindochakijani
Mkutano huo uliendeshwa na Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Bw. Sabasaba Moshingi, na uliwahusisha wadau mbalimbali wakiwemo wateja wakubwa, wafanyabiashara na viongozi wa jamii.
#NewsInfo
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila, ametangaza kumpa zawadi ya gari aina ya Toyota Crown golikipa wa Taifa Stars endapo hataruhusu goli katika mchezo wa Robo Fainali ya Michuano ya CHAN kati ya Tanzania na Morocco unaochezwa leo saa 2 usiku.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mhe. Chalamila alisema zawadi hiyo inalenga kuongeza hamasa kwa wachezaji wa timu ya taifa na kuhakikisha wanapambana kwa nguvu zote ili kuibuka na ushindi.
Mkuu huyo wa mkoa amewataka wachezaji kupambana kwa ari na kuonyesha uwezo mkubwa ili kuipa heshima Tanzania na kufanikisha ndoto ya kusonga mbele katika mashindano hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila ametangaza kuwa wachezaji wote wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) watapewa zawadi ya viwanja wilayani Kigamboni
pamoja na fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni 20.
Chalamila amesema zawadi hizo ni sehemu ya hamasa na motisha kwa wachezaji kuelekea katika mchezo wa robo fainali ya Michuano ya CHAN kati ya Tanzania na Morocco unaotarajiwa kupigwa leo saa 2 usiku.
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Eliakim Chacha Maswi Agosti 21, 2025 ametia saini mkataba wa ushirikiano kati ya Wizara ya Katiba na Sheria ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wizara ya Sheria ya Japan.
Utiaji saini Mkataba wa Ushirikiano kati ya Wizara ya Sheria ya Japan na Wizara ya Katiba na Sheria ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umeshuhudiwa na Makamu wa Waziri wa Sheria wa Japan Morimoto Hiroshi na Katibu Mkuu Eliakim Chacha Maswi
Kwa mara ya kwanza katika historia, kampuni ya teknolojia ya Marekani, Apple Inc, imefanya maamuzi ya kuzalisha modeli zote nne za iPhone 17 nchini India, hatua inayolenga kupunguza gharama kubwa za kodi za uagizaji (tariffs) zilizowekwa na Rais Donald Trump kwa bidhaa zote
Aidha, Apple inategemea kuzindua rasmi iPhone 17 mwezi Septemba mwaka huu, huku tetesi zikidai kwamba simu hiyo itakuja na muonekano mwembamba zaidi (slim body), rangi mpya, maboresho ya kamera, pamoja na mumo mpya wa uendeshaji wa ios 26,