THE BLACK DEATH ☠️ (KIFO CHEUSI)
🧵
Kifo cheusi kilikuwa janga la tauni lililotokea Ulaya kuanzia 1346 hadi 1353. Lilikuwa mojawapo ya magonjwa hatari zaidi katika historia ya binadamu; kama watu milioni 50 waliangamia, labda 50% ya wakazi wa Ulaya wa karne ya 14.