Producer @s2kizzy amenyoosha maelezo kuhusu wadau wa muziki ambao wamekuwa wakimsema kuwa ni bingwa wa kucopy nyimbo za watu wengine na kuzirudia kwenye ngoma zake
🎤 @mkogoty 🎥 @nickymeena_
#EastAfricaTV#HainaKuchoka
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda amesema wameanza mazungumzo na UNESCO pamoja na uongozi wa Meta kuitambua rasmi lugha ya Kiswahili kwenye majukwaa yote duniani ili vijana wanaotengeneza maudhui kwa lugha ya Kiswahili waweze kulipwa vizuri.
VIDEO:
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limetoa onyo kali kwa askari wake wanaokiuka maadili kwa kuingilia majukumu ya taasisi nyingine za serikali kwa lengo la kujipatia rushwa na maslahi binafsi.
Kamanda wa Kanda hiyo, SACP Jumanne Muliro, ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la Kariakoo. Muliro amesisitiza kuwa askari hawaruhusiwi kisheria kujifanya maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Shirika la Viwango (TBS), wala Mkemia Mkuu wa Serikali.
Kamanda Muliro amebainisha kuwa ameshatoa maelekezo ya kiutendaji kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala na OCD wa Kariakoo kuhakikisha askari wanabaki kwenye majukumu yao ya msingi ya ulinzi wa raia na mali zao.
Muliro amefafanua kuwa endapo kuna taarifa za uvunjifu wa sheria katika nyanja za kikodi au viwango, jukumu la polisi ni kufanya uchunguzi na kushirikiana na mamlaka husika, na si kuchukua nafasi ya mamlaka hizo.
🟢 Pamoja na surprise za Uteuzi wa Wagombea Ubunge na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, tutegemee KATIBU MKUU wa CCM mpya leo kutoka Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa!!
Tusubiri🧭⌛️
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, imepitisha rasmi majina ya wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi, ikiwemo ubunge na uwakilishi kwaajili ya kwenda kupigiwa kura na wajumbe watakaochagua mgombea mmoja ambaye atasimama kukiwakilisha Chama katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 29 Oktoba mwaka huu.
Taarifa rasmi iliyotolewa Jumanne Julai 29,2025 katika Ofisi za Chama hicho Jijini Dodoma na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM CPA Amos Makalla imeeleza kuwa katika Jimbo la Ilemela walioteuliwa uteuzi wa awali ni tisa huku Mbunge wa jimbo hilo anayemaliza muda wake Dkt. Angelina Mabula akikatwa katika mchakato huo.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kampeni za uchaguzi zitaanza rasmi Agosti 28 na kumalizika tarehe 28 Oktoba 2025.
VIDEO:
Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla amesema Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imeshakamilisha mchakato wa ujenzi wa barabara ya Mbande–Kongwa–Mpwapwa kwa kiwango cha lami, na utekelezaji wa mradi huo utaanza hivi karibuni baada ya mkandarasi kuingia kwenye hatua za maandalizi.
Makalla ametoa kauli hiyo leo, Juni 23, 2025, katika mkutano wa hadhara na wananchi uliofanyika wilayani Mpwapwa, mkoani Dodoma, ambapo amesisitiza kuwa utekelezaji wa mradi huo ni sehemu ya jitihada kubwa zinazofanywa na serikali chini ya uongozi wa Rais Samia kuimarisha miundombinu nchini.
"Kwa miradi mikubwa kama hii ya barabara, unamwachaje Dkt. Samia? Tunawaahidi, Chama cha Mapinduzi kitaendelea kutimiza wajibu wake kwa Watanzania. Kama kuna changamoto yoyote iliyobaki, hakuna chama mbadala chenye uwezo wa kuzitatua zaidi ya CCM," amesema Makalla.
Mwanamke aitwae Kagwa Mahigi (25) mkazi wa kijiji cha Lugubu kusini wilaya ya Igunga mkoani Tabora, anadaiwa kuwaua watoto wake wanne kwa kuwanywesha sumu na yeye kujiua kwa kunywa sumu hiyo, kwa madai kuwa ni baada ya mume wake kumjengea mke mdogo nyumba ya Kisasa.