Femina Hip partners with Plan International to empower over 28,000 adolescent girls and young women in Rukwa Region, Tanzania, through the ‘Girls Get Equal’ project, focusing on education, empowerment, and resilience (2025–2029).
@PlanTanzania#feminahip#partnership
Meet the faces of the 2025–2026 #IrelandFellows!
From civil servants and health professionals to tech innovators and economists, they represent the best of Tanzania 🇹🇿, DRC 🇨🇩, and Seychelles 🇸🇨.
Stay tuned as we #MeetTheFellows & share their journeys!
🔗https://t.co/8HmL403dUv
Delighted to visit Embassy partner @FeminaHip today and discuss challenges and opportunities for girls and boys in Tanzania. @FeminaHip doing really impactful work
Today, we had the honor of welcoming H.E. Nicola Brennan, the Ambassador of Ireland to Tanzania, to our offices, accompanied by Helen Counihan (Deputy Head of Development Cooperation), Oliva Kinabo (Gender Program Manager), and Isa Sekro (Programme Officer, Development Cooperation).
This meaningful visit was a wonderful opportunity to showcase the impactful work Femina Hip is doing to empower young people across Tanzania, some of whom were present and shared their powerful stories. #BuyuniFemaClub #JuhudiFemaClub #UjanaSalamaChampions #FemaAlumni. We held rich and reflective conversations, unpacking the realities young people in Tanzania face.
A heartfelt thank you to Ambassador Brennan and her team for spending time with us, listening deeply, and sharing in our mission to uplift young people. We value the connection, and the conversation! It’s partnerships like these that keep the energy flowing and the ideas growing, all in service of young people leading change.
@IEAmbDar@IrlEmbTanzania
#feminahip
Wavulana hawapaswi kuachwa nyuma. Katika jamii ambayo mara nyingi huwasahau au kuwawekea matarajio yasiyozingatia hisia zao, tunasema kwa nguvu – MSITUSAHAU PIA.
Wiki hii tunasimama na wavulana kuelekea Siku ya Mtoto wa Kiume Duniani. Tuwaunge mkono, tuwasikilize, na tuwajenge kuwa baba bora wa baadae.
#sikuyamtotowakiume #msitusahaupia #feminahip
Kuelekea siku ya mtoto wa kiume kimataifa tuwaandalie vijana wa kiume mazingira ya kuwa wao —bila woga, bila kubezwa. Wakilia, wasikilize. Wakihitaji kuongea, watie moyo. Huo ndio upendo wa kweli.
Tusifundishe wavulana kuficha maumivu. Tuwafundishe kuwa ni sawa kuwa na hisia. Ni sawa kulia. Ni sawa kuhitaji msaada.
#SikuYaMtotoWaKiume #KuliaSioUdhaifu #feminahip
Leo vijana kutoka Mradi wa Ujana Salama kata ya Mbaramo, wilayani Muheza, wameshiriki kikamilifu kwenye Kongamano la Vijana.
Vijana walijadili kwa ujasiri na kueleza maoni yao kuhusu mambo muhimu yanayowahusu, kama vile:
•Maendeleo ya kiuchumi kwa vijana
•Afya ya uzazi
•Ukatili wa kijinsia
•Ulinzi na usalama wa mtoto
Ni jukumu letu sote kuhakikisha vijana wanapata maarifa sahihi juu ya maisha yao ili waweze kuijenga kesho iliyobora na imara.
@IrlEmbTanzania
#UjanaSalama #Feminahip #PazaSautiYako
Leo tulikuwa na kikao cha Tathmini ya Kati ya Utekelezaji wa Mradi wa Ujana Salama Muheza!
Kikao hiki kimefanyika wilayani Muheza kikihudhuriwa na: Viongozi kutoka Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Ubalozi wa Ireland, Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza, Wanakamati wa MTAKUWWA, Dawati la Jinsia la Polisi – Muheza na Mkoa wa Tanga, Mkuu wa Polisi Wilaya, Hakimu mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya, Watendaji Kata, Madiwani na Afisa elimu kata, Viongozi wa dini na Ujana Salama (Youth Champions).
Katika kikao hiki, tumeona mafanikio muhimu ya mradi hadi sasa: Vijana waliofikiwa wameongezeka kutoka 5,498 mwaka 2022 hadi kufikia jumla ya 19,262 mwaka huu 2024.
Kesi za ukatili wa kijinsia (GBV) zilioripotiwa dawati la jinsia polisi zimeongezeka kutoka 64 hadi 76, kuonyesha kuongezeka kwa uelewa na ujasiri wa kuripoti, kesi zilizopelekwa mahakamani zimeongezeka kutoka 27 hadi 29.
Tumeshuhudia kupungua kwa ndoa za utotoni na mimba za utotoni, ushiriki wa vijana katika shughuli za kujikimu zinazozingatia mabadiliko ya tabianchi umeimarika, ushiriki wa wanawake vijana katika maamuzi ya jamii umeongezeka na mradi umepanuka kutoka kata 6 hadi 12 na shule 2 hadi 7.
Mradi wa Ujana Salama unaendelea kuonyesha kuwa mabadiliko yanawezekana yakianzishwa na jamii yenyewe.
@ortamisemitz@maendeleoyajami@IrlEmbTanzania
#ujanasalama #feminahip
Leo tumefanya ziara ya kutembelea mradi wa ndani ya shule uitwao KIJANA JITAMBUE. Ziara hii ilifanyika katika shule ya sekondari Tanga Technical, iliyoko jijini Tanga, ambapo tulishuhudia mafanikio ya moja kwa moja ya mradi huu kwa vijana wanaonufaika nao.
Wanufaika wakuu wa mradi ni wanachama wa Fema Club, ambao walitushirikisha maigizo yenye jumbe za kuelimisha kuhusu changamoto halisi zinazowakabili vijana, kama vile athari za ujauzito kwa wanafunzi wa kike.
Pia tulitembelea bustani za mboga zinazoendelezwa na wanafunzi hao kama sehemu ya kujifunza stadi za maisha. Kupitia shughuli hizi, vijana wanajengewa uwezo wa kujitambua, kujitegemea, na kufanya maamuzi sahihi kwa maisha yao ya sasa na ya baadae.
Mradi huu unaonesha mafanikio makubwa na ni mfano bora wa uwekezaji katika maendeleo ya vijana nchini Tanzania.
Ziara hii ilihusisha wawakilishi kutoka; Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Halmashauri ya Jiji la Tanga na Ubalozi wa Ireland, Tanzania.
@ortamisemitz@maendeleoyajami@IrlEmbTanzania
#kijanajitambue #feminahip
Leo tunaungana na Watanzania wote katika kusherehekea maisha na uzalendo wa Rais wa kwanza wa Zanzibar, Sheikh Abeid Karume.
Daima tutakuenzi!
#HappyKarumeDay#FeminaHip
Aisha Omari Kerefu, a Fema Club Champion under the Kijana Jitambue project in Tanga, is passionate about advocating for sexual and reproductive health and rights.
She envisions a world where all adolescent girls and young women can access #SRHR services without shame or judgment.
Let’s stand with her in breaking barriers and ensuring every girl has the right to safe and stigma free healthcare!
#feminahip #kijanajitambue #SRHForAll
Girls have a right to be heard and involved in decisions that shape their lives and futures! At Femina Hip, we are dedicated to advocating for a world where girls and women can live free from violence and discrimination.
Zawadi Hasibu Mvungi shares her vision of a future where every girl and woman feels safe and empowered. Let’s work together to make this a reality!
#GenderEquality #FeminaHip
Ni rahisi kuijenga kesho yako ikawa bora kwa kujaribu mambo mbalimbali kuliko kutokuthubutu kufanya jambo lolote.
Ikawe wiki ya heri kwa kila jambo unalofanya.
#feminahip