Nov 16, 1982 - May 28, imepita miaka 13 tangu tumpoteze Rapper Albert Kenneth Mangweha ๐๏ธ, Endelea kupumzika kwa amani ๐
#Tbt hapo alikuwa anafanya Freestlye katika Jukwaa la Dar Live, akiwa pamoja na Fid Q na Mzungu Kichaa , 2008.
Siku ya kwsnza naliskia lile goma la @FidQ "SIHITAJI MARAFIKI"
Ilipoanza tu ile intro *MACHIZI SKUSOMA NAO TULIKUTANA TU MTAANI,UDOGONI SKUCHEZA NAO ILA NDIO MACHIZ WA UKUBWANI*
Lile dundo bana ngosha katufokea sana walimwengu sio siri๐ ๐
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Muziki Tanzania, Farid Kubanda maarufu kama Fid Q, amesema moja ya sababu kubwa inayofanya Muziki wa Tanzania kushindwa kupata Tuzo za Kimataifa kama Grammy ni Wasanii wengi kushindwa kudumisha utambulisho wa muziki wao na badala yake kuiga mifumo ya muziki kutoka Mataifa mengine kama Amapiano na Afrobeat.
Fid Q ameyasema hayo leo Mei 21, 2026 wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Miaka 30 ya Bongo Flava, litakalofanyika Julai 10, 2026 katika Ukumbi wa Mlimani City, Jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa Tanzania ilisimama kidete kupitia muziki wa Bongo Flava uliokuwa na utambulisho wa kipekee uliobeba lugha, utamaduni na simulizi za maisha ya Mtanzania, hali iliyoufanya muziki huo kutambulika ndani na nje ya mipaka ya nchi.
โMiaka ya mwanzo ya Bongo Fleva ilijengwa na vijana waliokuwa wakielezea maisha halisi ya mtaani, ndoto, changamoto, mapenzi na matumaini ya jamii lakini kwa sasa aina hiyo ya muziki imepungua nguvu, huku baadhi ya wasanii wakiegemea zaidi katika maudhui yasiyo na uhalisia wa maisha yetu na kuhamasisha ngono, tujiulize swali, ukisikiliza Bongo Flava ya sasa, kweli inawakilisha sauti ya Tanzania? Wakati wasanii wengi wanafanya Amapiano na Afrobeat, bado tunaweza kusema tuna sauti yetu ya kipekee?โ amesema Fid Q.
#MillardAyoUPDATES