Aloyce Nyanda unaweka mjadala mahali pasipo sahihi. Swali halipaswi kuwa: “CHADEMA ibadili msimamo gani ili Lissu aache kuteseka?” Swali sahihi ni: “Kwa nini Serikali inamtesa Lissu kwa sababu ya msimamo wa kisiasa?”
Kumhurumia Lissu ni jambo la kibinadamu, lakini kuitumia huruma hiyo kuishinikiza CHADEMA ilegeze madai yake ni kuhamisha lawama kutoka kwa anayesababisha mateso kwenda kwa anayeyapinga. Lissu hayuko mahabusu kwa sababu CHADEMA imekataa mazungumzo; yuko mahabusu kwa sababu mamlaka zimeamua kuyafanya madai ya Katiba mpya, uchaguzi huru na haki ya kukosoa Serikali kuwa jambo la kuadhibiwa.
CHADEMA haijakataa mazungumzo. Inakataa mazungumzo yasiyo na ajenda, dhamana, uwazi wala matokeo—mazungumzo yanayotumika kununua ukimya huku sababu za mgogoro zikibaki palepale. Mazungumzo ya kweli hayafanyiki huku mmoja ameketi mezani na mwingine ameshikiliwa gerezani kama dhamana ya kisiasa.
Kujikadiria kisiasa ni muhimu, lakini busara si kumwambia anayedhulumiwa apunguze madai ili dhuluma ipungue. Huo si mwafaka; ni kuifanya haki iwe fidia ya uhuru wa mtu mmoja. Kama mateso ya Lissu yanatumika kuilazimisha CHADEMA kubadili msimamo, basi huo wenyewe ni uthibitisho kwamba tunakabiliwa na shinikizo la kisiasa, si tofauti ya kawaida ya kimkakati.
Lissu asingependa kuachiwa kwa gharama ya wananchi kusaliti madai aliyoyatolea uhuru wake. Njia ya kumsaidia si kuyazika madai yake, bali kuyafanya madai hayo kuwa sauti ya Watanzania wengi zaidi.
Kwa hiyo, wito wa kwanza usielekezwe kwa CHADEMA kujifungia ndani. Uelekezwe kwa Serikali: Mwondoeni Lissu katika minyororo, heshimuni haki zake, kisha wekeni mazingira ya mazungumzo ya kweli. Hakuna mwafaka wa heshima unaojengwa kwa kutumia uhuru wa mwanadamu kama karata ya majadiliano. #aloycenyanda
The IDU is gravely concerned by today's High Court ruling in Dar es Salaam ordering our Vice Chairman @TunduALissu to stand trial for treason — a charge carrying the death penalty.
After 16 months in detention for a speech, this ruling prolongs a politically motivated prosecution designed to silence Tanzania's opposition. We call for his immediate and unconditional release, and urge democratic governments worldwide to do the same. #FreeTunduLissu 🇹🇿
Mtangazaji wa Wasafi Media ambaye pia ni Diwani wa Kariakoo jijini Dar es Salaam kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Haji Manara, nusura azichape na mtangazaji mwenzake Oscar Oscar wakati wa mjadala mkali katika kipindi cha Jana na Leo kinachorushwa na Wasafi FM.
Mjadala huo ulihusu hali ya upangaji wa miji, miundombinu na matumizi ya ardhi nchini, huku Oscar akisema Serikali ndiyo inayopaswa kulaumiwa kwa changamoto hizo.
Oscar alisema kutopangika vizuri kwa nchi ni jambo la kuilaumu Serikali, akitolea mfano changamoto za miundombinu na usimamizi wa matumizi ya ardhi katika Jiji la Dar es Salaam.
“Nchi yetu kutopangika vizuri wa kulaumiwa ni Serikali, shida zote za miundombinu Dar es Salaam alaumiwe Serikali, zaidi usimamizi wa matumizi ya ardhi, Serikali ilaumiwe. Na si Dar es Salaam tu, ni nchi nzima,” alisema Oscar.
Kauli hiyo ilimfanya Manara kumpinga Oscar, akimtaka asitumie nguvu kubwa katika mjadala huo na kumsikiliza kabla ya kutoa hoja zake.
“Shida Oscar Oscar husikilizi, unapayuka tu, usitumie nguvu kubwa kupayuka. Unapiga kelele tu. Hakuna anayeitetea Serikali na hatupo hapa kulaumu ama kusifia kila kitu, na si dhambi kuitetea Serikali,” alisema Manara.
Manara alieleza kuwa hoja aliyokuwa akiwasilisha ilikuwa kuhusu makosa yaliyofanywa na baadhi ya watendaji wa Serikali wa zamani katika mipango miji, akisema makosa hayo yamechangia changamoto zinazoonekana leo.
“Mimi nimeanzisha kusema watendaji wetu waliokuwepo zamani walitukosea kwenye mpango mji. Oscar, kuwa na heshima na watu,” alisema.
Hata hivyo, Oscar alisisitiza msimamo wake kwamba Serikali inapaswa kulaumiwa kutokana na changamoto hizo, huku akitaja zaidi masuala ya miundombinu na usimamizi wa matumizi ya ardhi.
Katika kuendelea na mjadala huo, Manara alirudia hoja yake kwamba kuna kizazi cha watendaji kilichofanya makosa makubwa katika mipango miji, akisema, “Kuna kizazi kilitukosea sana.”
Tundu Lissu; Waheshimiwa majaji ni ushahidi wangu kwamba mimi ni mtu wa heshima, mtu wa heshima kubwa ndani ya nchi hii na kimataifa. Na heshima niliyo nayo ni kwa sababu ya msimamo wangu wa kupigania haki, demokrasia na utawala wa sheria. Sio kwa sababu nyingine yoyote.
Tundu Lissu; Waheshimiwa majaji, taasisi nyingi sana. Taasissi za kitaifa, kikanda na taasisi za kimataifa ikiwemo umoja wa mataifa, jumuiya ya Ulaya na jumuiya ya Madola imesema haya mashtaka ni mashtaka ya kisiasa hakuna cha uhaini wala jinai yoyote. Ni siasa tupu. Na wamedai niachiliwe huru bila masharti yoyote. Baraza la haki za binadamu kimataifa limesema sio tu niachiliwe huru bila masharti bali nilipwe fidia kwa usumbufu wote na changamoto zote nilizopata tangu kufunguliwa kwa mashtaka haya.
Tundu Lissu; Naomba iingie kwenye ushahidi kwamba nchi za jumuiya za ulaya, zimesimamisha misaada kwa Tanzania kwa sabbu ya mashtaka haya. Marekani imesimamisha misaada takribani dola milion 700 kwa mujibu wa taarifa zangu kwa sababu ya mashtaka haya. Kwa sasa bunge la Marekani, linajadili mswada wa kuwawekea vikwazo serikali ya Tanzania na viongozi wake kwa sababu ya mashtaka haya
Tundu Lissu; Ukiachana na ushiriki huu, vile vile nimeshiriki kwenye masuala ya uchaguzi kama wakili wa wagombea ubunge wa chama au wabunge walio waliochaguliwa wa chama tangu mwaka 2005. Napenda kuamini kwamba, kwenye masuala ya kesi zinazohusu uchaguzi ni mjuaji. Mjuaji kweli kweli. Mjuaji kuliko mawakili wengi hapa nchini.
Tundu Lissu; Kuna majaji wa mahakama hii na mahakama ya rufani wamejifunza mengi kutoka kwangu. Na kusema hivi sio kujitapa bali ni kusema tu nafahamu sheria nyingi zinazohusiana na uchaguzi. Nje ya ujuzi wa sheria kutokana na kuwa wakili, kuanzia mwaka 2021 mpaka wakati nakamatwa mwaka jana, nimefanya utafiti mkubwa sana kuhusu mfumo wetu wa uchaguzi, sio tu sheria bali mfumo mzima. Tangu enzi za ukoloni mpaka leo hii. Nisingekuwa napotezewa muda gereza la Ukonga, ningeshaandika kitabu kuhusu mfumo wa uchaguzi wa nchi hii na mauchafu yake yote.
Zambia wamepiga kura, Raia 4.9M.
Generally, hakujawa na internet blackout wala any serious atrocities, lakini wamechukua siku 4 kutangaza matokeo.
Tanzania, waliopiga kura walikuwa 32.7M. With no access to internet, violence everywhere… lakini walitumia only 2 days.
Haya ni maajabu!!!