Madereva wafunguka sababu za mgomo: Trafiki, VTS, kufungiwa leseni, miundombinu, mfumo wa point vyatajwa.
"Kuna dereva mmoja hapa amenyang'anywa leseni, leo mwaka wa tatu. Mpaka tunajichanga kila siku kumpa yeye na familia yake. Mke wake anakwenda kudanga huko ndio aje amlishe mwanaume na watoto. Haiwezekani kitu cha namna hii. Ni uonevu, na sisi ni wana uchumi wa nchi hii. Sasa tumefika mahali tumechoka. Tunataka serikali itutambue, sisi ni wanauchumi wa nchi hii. Serikali haiwezi kusonga mbele pasipo kuwa sisi madereva."
Maamuzi sahihi yasipo fanyika wakati sahihi siyo sahihi tena sio kila mvumilivu huwa anakula mbivu wengine hula maumivu (only for who knows)๐๐๐