Ni heshima kubwa kushiriki Jukwaa la Uziduaji 2026 lililofanyika jijini Dodoma, likiandaliwa na taasisi ya HakiRasilimali.
Kando ya jukwaa hilo, nilipata pia fursa ya kuhojiwa kidogo kuhusu sekta ya uziduaji na matarajio ya wadau. #JukwaaLaUziduaji2026
Fikiria makabila zaidi ya 100, kuishi katika upendo mmoja, ni neema kubwa. Watanganyika na wazanzibari (watanzania), tuenzi sana tunu hii, tusivurugane wala kuvurugwa.
https://t.co/h4vxQegeHm Wakati tunaadhimisha siku ya kuzuia kuzama maji duniani leo 25 Julai 2025, tusikie visa vinavyowasibu wavuvi kiasi cha kuhatarisha maisha yao na kisha tukumbushane kuchukua tahadhari.
Karibu katika kikao cha kwanza cha 'THE MEETING' hapa BMG Media @bmgonlinetv ikiwa ni kikao bora kabisa cha mjadala kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 ambapo tunajadili nafasi ya vijana katika uchaguzi.
Kuanzia saa 11:00 jioni, karibu ushiriki mubashara kikao hiki cha wazi.