Biologist and Wildlife Ecologist,
Professional Hunter,
Mgombea wa Ubunge 2020 (CHADEMA),Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Manyara, Makamu Mwenyekiti Kanda ya Kaskazini
@godbless_lema Hawana watu wenye sifa ya uongozi kwa sababu wote wanakataa mambo ya msingi na kulazisha dhuluma itamalaki. Hawakubaliki! Watabadilisha hadi watafanya recycling.
Tuna taarifa ya kikao cha siri ya Bi Kizimkazi na majaji wa mahakama ya rufaa hivi karibuni - na maelekezo yaliyotolewa!
Ushauri wangu: majaji msikubali kushinikizwa - simameni kwenye haki - and may God help you!
Komaeni!
Soon tunamalizana na huu udhalimu! Msikubali kuwa sehemu ya udhalimu!
#TutaelewanaTu
@godbless_lema@MwauraRobert2 Wazanzibari mbona wako kila mahali katika ofisi za umma huku Tanganyika hadi kwenye nafasi za utendaji wa vijiji hadi mitaa? Hakuna anayelalamika huku. Wana nyumba na ardhi pia kama watanzania. Kule Zanzibar ni mwiko mtanganyika kupata kupata ardhi. Hao hao ndio wanatubagua????
Watoto wa Mwenyekiti Tundu Lissu wamekua wakisikia simulizi za baba yao akiteswa na hata kushambuliwa kwa risasi kwa ajili ya kupigania haki za watu wengine. Leo, mtoto wake yuko barabarani akidai uhuru wa baba yake. Ni hadithi ya kutia moyo, lakini pia ya kuhuzunisha sana.
Agustino Lissu ✊🏽❤️
A fighter like his father Tundu Lissu and courageous like his mother Alice Magabe🔥
Mungu ailinde familia hii wamepitia mengi sana 😢
Nafurahi kuona wamekataa kuwa wanyonge!
#FreeTunduLissu
@MayonLaizer@Sir_Shuma Tunamsubiri tu atoke gerezani. Naamini mpango mkuu wa Mungu juu yake uko karibu kutimia.
".....amewashusha wenye nguvu kutoka viti vyao vya enzi, akawakweza wanyenyekevu". Lk.1:52.
Soma
‼️ALERT‼️
MGOGORO UNAOENDELEA KATA YA IDUKILO, WILAYA YA KISHAPU, MKOA WA SHINYANGA ULIOPELEKEA MAUAJI, WANANCHI KUUMIZWA, KUKIMBIA MAKAZI YAO, KUSHIKILIWA KWA IDADI KUBWA YA WANANCHI NA KUSITISHWA KWA HUDUMA ZA KIJAMII
Mgogoro huu ni wa muda mrefu. Ulianza kutokana na madai ya kuporwa kwa maeneo ya wananchi wa Idukilo mwaka 2022 baada ya mwekezaji aitwaye FANTOM, anayejihusisha na shughuli za uchimbaji wa madini aina ya dhahabu, kuchukua maeneo ya wananchi na kuanza kuweka bikoni katika maeneo hayo.
Kulitokea vurugu kubwa zilizosababisha mwananchi aitwaye COSMAS HAMIS SHILIMWA, mkazi wa Idukilo, kupigwa risasi. Tukio hilo lilitokea tarehe 10 Machi 2022.
Baada ya tukio hilo, wananchi walikusanyika na kutaka maelezo kutoka kwa askari kuhusu hatua hiyo. Viongozi mbalimbali wa serikali walikuwepo katika eneo la tukio, wakiwemo diwani, watendaji na wenyeviti wa vijiji.
Wananchi walipohoji kuhusu mwenzao kupigwa risasi katika maeneo hayo ambayo ni maeneo ya machimbo ya wananchi, viongozi hususan diwani waliwaomba wawe watulivu wakieleza kuwa suala hilo linafuatiliwa. Baada ya wananchi kuridhia kuwaachia viongozi kushughulikia suala hilo, polisi walichukua mwili wa marehemu na kuupeleka katika eneo la mgodi kwa ajili ya kupigwa picha na baadaye kutoa taarifa kwamba COSMAS HAMIS SHILIMWA alikuwa akiiba madini katika mgodi huo kinyume na utaratibu.
Jambo hilo liliwakera wananchi wa Idukilo, ambao walimuita diwani wao na kumuuliza kwa nini aliahidi kufuatilia suala hilo lakini akashindwa kusimamia haki ya ndugu yao COSMAS HAMIS SHILIMWA, ambaye walidai alipoteza maisha yake kwa kupigwa risasi huku taarifa iliyotolewa ikielezwa kuwa si ya kweli.
Wananchi pamoja na Sungusungu walikubaliana kumtoza faini diwani wao, SARAH MHOLI, ng’ombe watano. Vinginevyo wangemtenga katika shughuli zao za kijamii. Diwani huyo hakulipa faini hiyo.
Katika kura za maoni za ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, wananchi wanaeleza kuwa wanachama wengi wa CCM katika eneo hilo hawakumchagua SARAH MHOLI. Hata hivyo, kwa mujibu wa maelezo yao, baadaye alipitishwa kuwa mgombea wa uchaguzi wa Oktoba 2025.
Kutokana na hali hiyo, wananchi wengi walionyesha kutoridhishwa na hatua hiyo na wakaamua kumuunga mkono mgombea wa ACT, MUSSA HALUNA MAZIKU.
Katika uchaguzi wa tarehe 29 Oktoba 2025, wananchi walidai kuwa uchaguzi ulipotoshwa baada ya polisi kuchukua masanduku ya kura na kuondoka nayo, jambo lililosababisha hasira miongoni mwa wananchi kutokana na kutangazwa kwa mgombea ambaye walidai hawakumchagua.
Baada ya tukio hilo, wananchi waliandamana na viongozi wa serikali za vijiji katika Kata ya Idukilo walijivua nyadhifa zao kuanzia wenyeviti wa vijiji hadi wenyeviti wa vitongoji, huku wakieleza kutomtambua diwani SARAH MHOLI.
Baadaye Mkuu wa Wilaya alifika katika eneo hilo. Kwa mujibu wa maelezo ya wananchi, alieleza kuwa diwani wao ni SARAH MHOLI na kwamba hawezi kuhangaika na waathirika wa UKIMWI, kauli ambayo wananchi walitafsiri kuwa iliwalenga wao.
Wananchi walionyesha hasira kubwa kufuatia kauli hiyo na baadaye walivamia makazi ya SARAH MHOLI, ambapo nyumba yake ilichomwa moto na mali mbalimbali kuharibiwa.
Siku iliyofuata baada ya tukio hilo, polisi walifika katika maeneo ya Idukilo na kufyatua risasi za moto. Katika tukio hilo, kijana mmoja aitwaye KIJA MAKUNGU alidaiwa kupigwa risasi tumboni akiwa katika shughuli zake na kufariki dunia papo hapo.
MAMBO YANAYODAIWA KUENDELEA KWA SASA KATI YA WANANCHI WA IDUKILO NA POLISI
Kwa mujibu wa taarifa zinazotolewa na wananchi wa Idukilo:
* Polisi hawataki wananchi wa Idukilo kufungua maduka au kufanya shughuli mbalimbali za kijamii.
* Maduka yanaelezwa kulazimishwa kufungwa.
* Polisi wanaelezwa kuingia katika nyumba za wananchi na kufanya vitendo mbalimbali vinavyolalamikiwa na wananchi.
* Wananchi wanadai kuporwa mali, fedha na bidhaa zilizopo madukani.
Part 2 👇
* Vyombo vya usafiri, hususan pikipiki, vinadaiwa kunyang’anywa.
* Watu wengi wanadaiwa kukimbia makazi yao kutokana na hali ya hofu.
* Baadhi ya wananchi wanadaiwa kukamatwa, kupelekwa vituo vya polisi na kupigwa.
* Wananchi wanadai kuwa zaidi ya wananchi 200 wanashikiliwa katika vituo mbalimbali vya Polisi Wilaya ya Kishapu na Wilaya ya Shinyanga kutokana na matukio yanayohusishwa na mgogoro unaoendelea katika Kata ya Idukilo.
* Wananchi wanaeleza kuwa kukamatwa kwa idadi kubwa ya watu kumeongeza hofu na sintofahamu miongoni mwa familia na jamii ya Kata ya Idukilo.
* Mpaka sasa wananchi wengi waliokimbia makazi yao wanaendelea kukosa huduma muhimu za msingi ikiwemo chakula, huduma za afya, maji na mahitaji mengine ya kibinadamu, hali ambayo inaelezwa kuwa imeongeza mateso kwa familia nyingi.
* Wananchi wanadai kuwa hakuna hali ya amani katika Kata ya Idukilo.
Aidha, wananchi wanadai kuwa polisi wanawataka wakubali uongozi wa diwani SARAH MHOLI.
Wananchi pia wanadai kuwa polisi wameweka kambi katika Shule ya Msingi Idukilo na kuitumia kama kituo cha polisi.
Kutokana na hali hiyo, wananchi wanaeleza kuwa idadi kubwa ya watoto wameathirika kielimu. Baadhi yao walikimbia pamoja na wazazi wao, huku waliobaki wakishindwa kuhudhuria masomo yao kutokana na mazingira ya hofu na kutokuwepo kwa mazingira salama ya kujifunzia.
Wananchi wanadai kuwa hali hiyo imesababisha kusitishwa kwa huduma mbalimbali za kijamii katika Kata ya Idukilo, ikiwemo elimu, afya, usafiri na shughuli nyingine muhimu za kijamii na kiuchumi.
TAARIFA ZA MADAI YA UVUNJIFU WA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU
Kwa mujibu wa taarifa zinazotolewa na wananchi:
* Kuna madai kuwa baadhi ya askari polisi wamehusika katika uporaji wa maduka ya wananchi katika Kata ya Idukilo, Kijiji cha Idukilo; Kata ya Mondo, Kijiji cha Kabila; pamoja na Kata ya Mwadui Ruhumbo, Kijiji cha Mabambasi.
* Kuna madai kuwa baadhi ya maduka yalichomwa moto baada ya matukio ya uporaji yanayodaiwa kufanyika.
* Kuna madai ya uwepo wa vitendo vya ubakaji dhidi ya wanawake katika baadhi ya maeneo yaliyoathirika na operesheni za usalama.
* Kuna madai ya uwepo wa mateso, vipigo na vitendo vingine vinavyodaiwa kukiuka haki za binadamu dhidi ya baadhi ya wananchi.
HITIMISHO
Wananchi wa Kata ya Idukilo wanaeleza kuwa chanzo cha mgogoro huo ni mgogoro wa ardhi na maeneo ya uchimbaji wa madini ya dhahabu uliotokea baada ya mwekezaji FANTOM kuanza shughuli za uchimbaji katika maeneo ambayo wananchi wanadai yalikuwa yakitumiwa na wachimbaji wa eneo hilo.
Wananchi wanaeleza kuwa mgogoro huo umeendelea kwa muda mrefu na umeathiri maisha yao kwa kiasi kikubwa, ikiwemo kupoteza maisha kwa baadhi ya wananchi, majeruhi, kukimbia makazi yao, kushikiliwa kwa idadi kubwa ya wananchi katika vituo vya polisi, kusitishwa kwa huduma za elimu, afya na usafiri, pamoja na kuongezeka kwa changamoto za kibinadamu kwa familia nyingi.
Wananchi wanatoa wito kwa mamlaka husika, taasisi za haki za binadamu, viongozi wa dini, viongozi wa kisiasa na wadau wengine wa maendeleo kufanya uchunguzi wa kina kuhusu madai yote yaliyotolewa, ikiwemo vifo vya wananchi, matumizi ya nguvu, madai ya uporaji, uchomaji wa mali, ubakaji, mateso, kukamatwa kwa wananchi kwa wingi, pamoja na hali ya kibinadamu inayowakabili wananchi wa Kata ya Idukilo, kwa lengo la kurejesha amani, haki na utulivu katika eneo hilo.
Kutoka kwa Mwananchi wa Kijiji cha Idukilo.
JESHI LA POLISI LIMEVAMIA NYUMBANI KWA MBYELLA (ANAYEUZA NGUO NA VIFAA VYA CHADEMA NA KUONDOKA NA TSHIRT, KOFIA, NGUO NA BENDERA ZA CHADEMA.
Nimepata taarifa kwamba usiku wa kuamkia leo mida ya saa nane, Jeshi la Polisi limevamia nyumbani kwa Yoromu Mbyella, mfanyabiashaa ambae huwa anauza sare za CHADEMA wakidai wanamtafuta kwa kosa la kutengeneza Tshirt zenye maandishi “FREE TUNDU LISSU”
Kwa mujibu wa mtoa taarifa, Mbyella mwenyewe hakuwepo nyumbani so Polisi walifanya upekuzi na baada ya kumkosa waliondoka kwa muda.
Baadaye walirejea wakiwa na Gari aina ya Fuso kisha wakabeba nguo zote na vifaa vyenye nembo ya chadema ikiwemo Bendera za Chadema ambazo huwa anauza kisha wakaondoka na mali hizo bila kutoa sababu zaidi.
Kwa mujibu wa mke wa Mbyella (anayeuza nguo na vifaa vya chama) nyumbani kwao kuna duka la kuuza vifaa hivyo ambavyo Polisi wameondoka navyo vyote.
Tunafuatilia kufahamu sababu hasa ya kuvamia nyumbani hapo na kuleta taharuki kwa mtu ambaye hata kama wangemhitaji Polisi, wangempatia wito na angefika kituoni kama Polisi walikuwa na jambo na Mbyella.
Kuuza vifaa vya chama kama nguo, kofia, Bendera siyo kosa kisheria.
REPOST 200
@MariaSTsehai@HildaNewton21 Kwamba hawa wanaoteka wanalichafufua Taifa ni kweli. Wanaoteka Hafahamiki?😂 Cha kushangaza eti wanayo hadi bunduki na pingu. Waliotekwa wengine wamepatika vituo vya polisi. Wengine walikutwa na pingu😂? Eti agenda! Ya nani na nini? Hivi pingu zinamilikiwa na nani? Na bunduki je?
CHADEMA ni sauti ya wananchi. Ni chama pekee kinachowatetea wananchi ni Chama cha wananchi kwa ajili ya wananchi. Kinafuata sheria ya vyama vya siasa. Ukikifuta ni kukiondoa katika mifumo rasmi ya kisheria. Halafu unadhani kitatokea nini. Msijajili ni kosa kubwa hata kufikiria .