MUHIMU KUELEWA
Mhudumu afya ngazi ya jamii (CHW) ni mmoja ya wanajamii anayetoa huduma za msingi za afya hasa zinazolenga kinga na kuimarisha afya ya wanajamii.
➡️Ni kiungo kati ya jamii na vituo vya huduma za afya.
➡️Wanajamii hawa wana vigezo na hupata mafunzo rasmi.
Kutumia CHW ni practice ya sehemu nyingi Duniani.
Kwetu Tanzania; tunaenda kuwaingiza kwenye mfumo rasmi wa afya.
Ni hatua nzuri..
Mfumo wa Afya kuanzia ngazi ya jamii.
Fikiria: Siku moja; unapata huduma ya kupima presha nyumbani kupitia mhudumu aliye kwenye makazi yenu.
Leo ni siku ya figo duniani, msisitizo ni kutoa fursa ya huduma kwa wote.
Ila tukumbuke kulinda afya zetu ndiyo linatakiwa kuwa jukumu kubwa zaidi kwa kila mmoja wetu.
Ishi kwa kuzingatia kanuni za afya yako, utatunza afya ya figo zako na mwili wako kwa ujumla.
Muhimu kuhusu ugonjwa wa Saratani
Kwa sasa
➡️Saratani ni miongoni mwa sababu kuu za vifo ulimwenguni, ikiwa chanzo cha vifo karibu milioni 10 mwaka 2020.
➡️Kwa mwaka 2020 kwa kila binadamu sita waliofariki dunia, mmoja alifariki kwa Saratani.
➡️Aina za saratani zinazosumbua watu zaidi ni pamoja na saratani ya matiti, saratani ya shingo ya kizazi, saratani ya mapafu, utumbo na puru pamoja na saratani ya tezi dume.
��️Karibu theluthi moja ya vifo kutokana na saratani vinasababishwa na matumizi ya tumbaku (sigara, shisha), kuwa na unene kupita kiasi, matumizi ya pombe, kutokula matunda na mboga za majani, na kutofanya mazoezi.
➡️Maambukizi yanayosababisha saratani, kama vile virusi vya papilloma (HPV) na virusi vya homa ya ini, ni chanzo cha takriban 30% ya kesi za saratani.
➡️Saratani nyingi zinaweza kupona ikiwa hugunduliwa mapema na kutibiwa kwa ufanisi.
WHO estimates that 296 million people were living with chronic hepatitis B infection in 2019, with 1.5 million New infections each year..with estimated 820,000 deaths mostly from cirrhosis and hepatocellular carcinoma (primary liver cancer)
Umepima homa ya ini na kupata chanjo?