Akizungumza na Veriafya, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na Uzazi, Godfrey Chale wa Dkt. Chale Polyclinic iliyopo Mbezi kwa Msuguri anabainisha kuwa takriban 50% ya matatizo ya uzazi kwa mwanamke husababishwa na mvurugiko wa homoni kwenye vichocheo vinavyodhibiti mzunguko wa hedhi na upevushaji wa mayai, wakati 50% nyingine inatokana na changamoto za kiumbe katika viungo vya uzazi kama vile uvimbe na maambukizi yanayoweza kuharibu kuta za kizazi au kuziba mirija ya uzazi na kuzuia mbegu na yai kukutana au kusababisha mimba kutungia nje ya mji wa uzazi
Ufafanuzi kamili wa mazungumzo haya unaweza kuupata hapa https://t.co/6suc1Tn8TB
VIDEO:
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) amevitaka vyama vya ushirika nchini kuendelea kuboresha utendaji kazi wake ili kujijengea sifa nzuri ya uwepo wa hati safi ambao umeonekana kuongezeka.
CPA Mugeta amesema hayo jijini Dodoma kwenye maonesho ya Nane Nane akieleza kuwa kwa mwaka 2025/26 kuna ongezeko la asimilia 4% kutoka asilimia 16% mpaka 20% kwa vyama vinavyopata hati safi.
Amesisitiza kuwa mafunzo yanayotolewa na COASCO kwa viongozi na watendaji wa vyama vya ushirika yamechangia kuboresha matokeo ya ukaguzi.
VIDEO:
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, ameielekeza Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC) kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika vyama vya ushirika ili kudhibiti ubadhirifu wa mali, kuimarisha uwajibikaji na kulinda maslahi ya wanachama.
Akizungumza jijini Dodoma wakati wa Maonesho ya Kimataifa ya Nane Nane, Dkt. Nchimbi amesema Serikali imejipanga kuhakikisha vyama vya ushirika vinatoa huduma bora kwa wakulima huku mali zake zikisimamiwa kwa uwazi na kutumika kwa manufaa ya wanachama. Amesema ukaguzi wa mara kwa mara utasaidia kubaini mapema changamoto zinazovikabili vyama hivyo na kuchukua hatua stahiki dhidi ya matumizi mabaya ya rasilimali.
Kwa upande wake, Msajili na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC), Dkt. Benson Ndiege, amesema kumekuwa na changamoto za usimamizi wa mali za ushirika ambapo baadhi ya mali ziliuzwa isivyo halali. Amesema TCDC imeanzisha mfumo rasmi wa kutambua na kusajili mali za ushirika ili kuimarisha ulinzi wake, kudhibiti ubadhirifu na kuongeza thamani ya mali hizo kwa manufaa ya wanachama.
Dkt. Pius David Muzzazzi, Bingwa wa Magonjwa ya Watoto ashauri kupitia Youtube Chaneli yake wazazi na walezi wawe na majimaji yenye chumvi "Saline Nasal Drops" ambayo yatawasaidia watoto wakipata Mafua.
DRC fan Michel Kuka Mboladinga, aka "Lumumba Vea," has gone viral at AFCON 2025 for standing completely still during matches, including against Senegal and Botswana, in a powerful tribute to national hero Patrice Lumumba, sometimes remaining motionless for over 90 minutes..
HABARI:
Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetangaza kusitisha kwa muda usafiri wa treni za Standard Gauge Railway (SGR) kati ya Morogoro na Dodoma kuanzia leo, Desemba 31, 2025, kufuatia uharibifu wa miundombinu uliosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Mhandisi Machibiya M. Shiwa, mvua hizo zimesababisha athari katika maeneo ya Kidete (Korogwe, Morogoro) pamoja na Godegode (Mpwapwa, Dodoma), hivyo kufanya njia hiyo kutotumika kwa usalama.
Kutokana na athari hiyo, safari zitakuwa kati ya Morogoro-Dar es salaam na Dar es salaam-Morogoro hadi pale marekebisho yatakapokamilika na usalama kuthibitishwa, hivyo Abiria wametakiwa kubadili ratiba zao ili kuendana na mabadiliko hayo ya kiufundi.
TRC imeomba radhi kwa usumbufu unaoweza kujitokeza na imehakikishia umma kuwa wataalamu wake wanafanya kazi kwa kasi ili kurejesha huduma hizo haraka iwezekanavyo.
VIDEO:
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe, Dkt. Benson Bagonza, ametoa wito kwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuchagua Spika atakayekuwa daraja la maridhiano badala ya kuwa kiongozi wa mihimili, akisisitiza umuhimu wa kuwa na kiongozi anayejenga umoja na kuheshimu misingi ya katiba na demokrasia.
Kupitia andiko lake lililochapishwa katika ukurasa wake wa Facebook, Askofu Bagonza amesema Bunge linapaswa kumpata Spika ambaye “atakaa mbele, lakini moyo wake ukae katikati ya wabunge wote,” ili kurejesha imani ya wananchi kwa chombo hicho cha uwakilishi.
“Tunataka Spika asiyenuka uchama wala uspika. Afikike, ahojiwe, anuniwe na akubali kutopongezwa mpaka amalize kazi. Akatae kuwa yeye ndiye Bunge na asiwe juu ya Bunge. Akae mbele lakini moyo wake na mawazo yake yakae katikati miongoni mwa wabunge”, ameandika Bagonza.
Amesema Bunge la 13 linapaswa kumpata kiongozi mwenye hekima, uzalendo na uwezo wa kujenga daraja la maelewano miongoni mwa Watanzania, akionya kuwa hatari kubwa ni kulifanya Bunge kuwa la chama kimoja badala ya kuwa la wananchi wote.
Askofu Bagonza pia amewataka wabunge kumchagua Spika mwenye uelewa wa kizazi kipya, ambaye ataweza kujenga daraja na vijana wa Gen Z, akisisitiza kuwa wakati umefika kwa viongozi waandamizi kutambua mabadiliko ya kijamii na kizazi.
“Spika ajaye ajenge daraja na vijana au ‘wahuni wa Gen Z’. Asiogope Panki wala Milegezo yao, atambue Bunge lijalo laweza kuwa na Spika Gen Z,” ameandika kwa utani uliochanganyika na ujumbe mzito.
Aidha, amewataka wabunge kumpata Spika atakayeheshimu mgawanyo wa mihimili ya dola bila ya kile alichokiita ndoa ya mihimili akisema kila mhimili unapaswa kubaki kwenye mipaka yake huku ukiheshimiana bila kuogopana.
“Spika wetu kwa hekima na uzalendo, aitilie mashaka ndoa ya mihimili. Kila mtu abaki kwake, tutembeleane kwa mialiko. Huyu atunge, yule atafsiri na yuleee atekeleze. Tuheshimiane bila kuogopana. Ikibidi kuogopana iwe bila kutishana. Spika ajaye ajue siyo wa kwanza na hatakuwa wa mwisho. Waliwahi kuwapo ambao tusingekula mpaka wafike. Hivi sasa wakiwapo hatuli mpaka waondoke. Walinyima watu swali la nyongeza, sasa wananyimwa swali la msingi. Tanzania simama nishuke nimefika!”, ameandika.
Andiko hilo la Bagonza limekuja wakati taifa likijiandaa kwa kikao cha kwanza cha mkutano wa kwanza wa Bunge la 13, kinachotarajiwa kufanyika Novemba 11, 2025.
Katika wakati huu, mjadala wa nani ataongoza Bunge hilo umeendelea kushika kasi, ambapo majina ya wanasiasa kama Mussa Zungu na Stephen Masele yanatajwa kuwania nafasi hiyo, kufuatia Dkt. Tulia Ackson kujiondoa kwenye mbio hizo.
Breaking News:
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Pwani na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho Boniface Jacob (Boni Yai) muda mfupi uliopita leo, Jumamosi Novemba 08.2025 amekamatwa na Jeshi la Polisi Goba, jijini Dar es Salaam akiwa njiani kwenda kuripoti kituoni
Wakili Hekima Mwasipu ameithibitishia Jambo TV kuhusu kukamatwa kwa kiongozi huyo wa upinzani ambaye pia ni Meya wa zamani Manispaa za Kinondoni na Ubungo, Dar es Salaam
Itakumbukwa kuwa, usiku wa kuamkia leo Jeshi la Polisi kupitia kwa Msemaji wake lilitoa orodha ya watu 10 linaowasaka kufuatia uchunguzi na ushahidi uliokusanywa na Jeshi hilo kutokana na matukio ya vurugu, uporaji wa mali na uvunjifu wa amani yaliyotokea Oktoba 29.2025 katika maeneo mbalimbali nchini
Katika orodha hiyo wapo viongozi waandamizi wa CHADEMA akiwemo Katibu Mkuu John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara Amani Golugwa (ambaye amekamatwa na Polisi asubuhi ya leo), Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi Brenda Rupia Brenda Jonas Rupia, Mjumbe wa Kamati Kuu Godbless Jonathan Lema, Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa Wakili Deogratias Mahinyila na Mjumbe wa Baraza Kuu Hilda Newton
Wengine walioko kwenye orodha hiyo ni pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima ambaye pia ni Kada wa CHADEMA Askofu Machumu Maximilian Kadutu (Askofu Mwanamapinduzi), na Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) Askofu Josephat Gwajima, ambapo taarifa ya Jeshi la Polisi ilieleza kuwa inawasaka vigogo hao, lakini pia wakapewa tahadhari ya kujisalimisha kwenye Vituo vya Polisi mara moja pindi waonapo taarifa hiyo.
Jambo TV inaendelea kufuatilia na itakuletea undani zaidi wa taarifa zinazowahusu vigogo hao.
Breaking News:
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tanzania Bara Amani Golugwa amekamatwa asubuhi ya leo Novemba 8, 2025 akiwa nyumbani kwake
Wakili wake Hekima Mwasipu ameithibitishia Jambo TV kukamatwa kwa kiongozi huyo wa upinzani nchini akieleza kuwa kwa sasa wanafuatilia kujua ni Kituo kipi cha Polisi amepelekwa ili taratibu zingine za kisheria ziendelee
"Kwa sasa naweza kuthibitsha tu amekamatwa" amesema Wakili Mwasipu kwa kifupi.
Jambo TV inafuatilia na itakuletea undani zaidi wa taarifa hiyo.
Jeshi la Polisi Nchini limeutangazia umma wa Watanzania kuwa kufuatia matukio ya vurugu, uporaji wa mali na uvunjifu wa amani yaliyotokea Oktoba 29.2025 katika Majiji ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza na Mbeya, na pia katika mikoa ya Shinyanga, Geita, Songwe, Ruvuma, Mara Dodoma, Kilimanjaro na Iringa ambazo zimesababisha madhara kwa binadamu, kuharibu mali nyingi za umma na za watu binafsi kumeleta athari kubwa
Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi hilo Novemba 07.2025 imeeleza kuwa mbali na athari kwa uhai na maisha ya watu, waliofanya uhalifu huo pia wameharibu na kuchoma moto mali za umma kama vile Ofisi za TRA, TAKUKURU, Mahakama, ATM za baadhi ya Benki, Vituo vya Polisi, Vituo vya Mabasi ya Mwendokasi kutoka Kimara mwisho hadi Magomeni na kutoka Magomeni hadi Morocco, Ofisi za Serikali za Mitaa, kuchoma moto barabara za lami na za zege kwa kutumia matairi na majengo kadhaa ya Chama cha Mapinduzi (CCM)
Aidha Jeshi laPolisi limeendelea kueleza kuwa, baadhi ya mali za watu binafsi zimeharibiwa na kuchomwa moto kama vile Vituo vya mafuta, Maduka mbalimbali, Magari makubwa na madogo, pia wamehusika wamefanya uporaji wa mali na pesa za watu kutoka maeneo mbalimbali ya biashara
"Pamoja na kwamba baadhi ya waliopanga kutekeleza uhalifu huo wamekamatwa na kuanza kufikishwa Mahakamani, Jeshi la Polisi Nchini kwa kushirikiana na Vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama linaendelea na msako mkali wa kuwatafuta wale wote waliopanga, kuratibu na kutekeleza uovu huo, aidha wakati hatua hizo zikiendelea, jamii inaombwa kuendelea kutoa ushirikiano wa dhati katika kutoa taarifa za watu wote waliohusika ili hatua sahihi za kisheria zichukuliwe dhidi yao" -Jeshi la Polisi
Kupitia taarifa hiyo pia, Jeshi hilo limesema kufuatia uchunguzi na ushahidi uliokusanywa hadi sasa linawasaka kwaajili ya kuwakamata Josephat Gwajima, Brenda Jonas Rupia, John Mnyika, Godbless Jonathan Lema, Machumu Maximilian Kadutu, Deogratias Cosmas Mahinyila, Boniface Jacob, Hilda Newton, Award Kalonga na Aman Golugwa, ambapo watu hao wametakiwa kujisalimisha katika vituo vya Polisi mara moja pindi waonapo taarifa hiyo popote pale walipo
Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi limesema hatua za kisheria kwa wahalifu ambao wameshakamatwa zinaendelea nchini kote na kwamba Novamba 07.2025 baadhi yao wamefikishwa Mahakamani
Jeshi hilo limetoa onyo kwa mtu au kikundi cha watu kinachopanga kufanya uhalifu wa aina yoyote ile kuwa halitasita kuchukua hatua za kisheria dhidi yao.
Watu 172 wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Nyamagana, mkoani Mwanza, wakikabiliwa na mashtaka mbalimbali yakiwemo uharibifu wa mali, kuchoma moto na unyang’anyi wa kutumia silaha.
Kwa mujibu wa taarifa za mahakama, watuhumiwa hao wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Oktoba 29 na 30, 2025, siku ambazo ziliambatana na matukio ya vurugu katika maeneo kadhaa nchini.
Watuhumiwa hao walifikishwa mahakamani Novemba 7, 2025, chini ya ulinzi mkali wa Jeshi la Polisi na kusomewa mashitaka yao kwa makundi tofauti, kulingana na maeneo wanayodaiwa kutenda makosa hayo.
Akisoma mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Raula Shehagilo, kiongozi wa jopo la waendesha mashtaka wa serikali Jaines Kihwelo, akisaidiana na Helen Mabula na Sara Heperias, alieleza kuwa baadhi ya watuhumiwa wanadaiwa kutenda kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha kinyume na kifungu cha 287(a) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 (marejeo ya 2023).
Pia, kwa nyakati tofauti, watuhumiwa hao wanadaiwa kuharibu mali kwa makusudi, kinyume na kifungu cha 326(1) cha sheria hiyo, pamoja na kufanya fujo na maandamano bila kibali, kinyume na vifungu vya 74(1), (2), 76 na 37 vya Kanuni ya Adhabu.
Mashitaka mengine ni pamoja na kuchoma moto mali, kinyume na kifungu cha 319(a)(b) cha Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 (marejeo ya 2023).
Kutokana na uzito wa baadhi ya makosa hayo, ambayo hayana dhamana, mahakama imeelekeza watuhumiwa wote kurudishwa rumande hadi kesi hizo zitakapotajwa tena Novemba 17, 19 na 20 mwaka huu.
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) leo Novemba 7, 2025, imetangaza orodha ya Wabunge Wanawake wa Viti Maalumu 115 walioteuliwa kushiriki katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Uteuzi huo umefanywa kwa mujibu wa masharti ya Ibara ya 66(1)(b) na 78(1) za Katiba ya mwaka 1977, pamoja na kifungu cha 112 cha Sheria ya Uchaguzi wa mwaka 2024.
Miongoni mwa walioteuliwa ni Cecilia Daniel Paresso na Bonnah Ladislaus Kamoli wote kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambapo Bonnah awali alikuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Segerea. Wengine ni Devotha Minja na Sigrada Mligo kutoka Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), waliopata nafasi hizo kupitia orodha ya viti maalumu.
Kwa mujibu wa taarifa ya INEC, idadi kamili ya wabunge wa viti maalumu inapaswa kuwa 116, ambapo uteuzi wa nafasi moja bado unasubiri kukamilika kwa uchaguzi wa ubunge katika majimbo ya Fuoni (Zanzibar) na Siha (Tanzania Bara).
Tume imesema uteuzi huo umezingatia uwiano wa kura zilizopatikana na vyama vya siasa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, sambamba na masharti ya kikatiba yanayolenga kuongeza ushiriki wa wanawake katika uongozi wa kisiasa.
INEC imewapongeza wote walioteuliwa na kuwataka kutumia nafasi hizo kwa uadilifu, uwajibikaji na kujenga umoja wa kitaifa kupitia mchango wao ndani ya Bunge.
HABARI:
Watu 9 wakazi wa Makambako - Njombe wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Njombe wakikabiliwa tuhuma za kosa la uhaini na kuzuia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, makosa ambayo waliyalifanya kwa kipindi cha kati ya mwezi March mpaka Octoba 30 mwaka 2025.
Akisoma mashitaka hayo, Wakili wa serikali Magdalena Whella amesema watuhumiwa hao ni Erasto Nzenge (31), Japhet Kimbe (27), Saimon Mlelwa (23), Masondole Manyama (33), Stanley Mbembati (39), Anord Tunduru (30), Fadhil Nguvila (25), Patrick Mpagike (37) na Prosper Mbwilo (26)
Washitakiwa hao wamepandishwa kizimbani leo Novemba 7 na kusomewa mashitaka mawili ya kesi namba 26483/2025 mbele ya hakimu mfawidhi wa Mahakama ya wilaya Njombe Mheshimiwa Matrida Kayombo.
Akisoma mashitaka hayo Mwanasheria wa Serikali Magdalena Whella amesema kosa la kwanza ni kuwa kwa nyakati tofauti ya mwezi Machi mpaka tarehe 30 Oktoba mwaka 2025 katika maeneo tofauti ndani ya mkoa wa Njombe walikula njama na kutenda kosa la Uhaini chini ya kifungu cha sheria namba 384 cha mwenendo wa makosa ya jinai marejeo ya kifungu cha 16 cha mwaka 2023.
Katika kosa la Pili, Wakili wa Serikali amesema washitakiwa hao walitenda kosa la uhaini chini ya kifungu cha 39 cha pili cha sheria ya kanuni ya adhabu, sura ya 16 marejeo ya mwaka 2023, ambapo maelezo ya kosa ni kuwa washitakiwa mnamo tarehe 30 ya mwezi wa kumi mwaka 2025 katika mji wa Makambako walikuwa na nia ya kuzuia uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 na kuitishia serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kujiingiza kufanya fujo na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali za serikali zinazotumika kutolea huduma muhimu.
Baada ya kusomewa mashitaka hayo, Hakimu mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Njombe, Matrida Kayombo amewataka washitakiwa hao kutojibu chochote hadi hapo shauri hilo likapokwenda kusikilizwa kwenye Mahakama Kuu
Aidha, upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika kwa makosa hayo mawili na kwamba makosa yote hayana dhamana na washitakiwa wamerudishwa mahabusu hadi tarehe 12 Mwezi wa Kumi na Moja mwaka 2025 kesi itakapo tajwa tena.
VIDEO:
Kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam muda huu, leo (Ijumaa, Novemba 07.2025) washtakiwa wengine 95 wamefikishwa Mahakamani hapo na kusomewa mashtaka mawili ya uhaini
Shtaka la kwanza ni kupanga njama za kutenda la uhaini ambapo inaelezwa kuwa kati ya Aprili hadi Oktoba 29 mwaka huu washtakiwa walikuwa wanakula njama za kutenda kosa hilo, shtaka la pili ni kutenda kosa la uhaini kwa kuitishia serikali na kufanya vurugu kwa lengo la kuzuia uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2025, na hivyo washtakiwa walifanya vurugu zilizosababisha pia uhalibifu wa mali
Kwa ujumla, watuhumiwa 240 wamefikishwa Mahakamani hapo leo na kusomewa mashtaka ya uhaini.
HABARI ZA HIVI PUNDE:
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson ametangaza kujiondoa rasmi katika kinyang'angiro cha kugombea nafasi hiyo kwa mara nyingine tena, leo tarehe 7 Novemba 2025.
Vyanzo vyetu vya habari kutoka wandani wa Spika huyo vimethibitisha jambo hilo, hata hivyo havikuweka wazi sababu za yeye kutogombea nafasi hiyo.