Top Tweets for #KitengeTv
Wana Simba wanataka ripoti ya mapato na matumizi isomwe na mtu wa Njee.
Sosi #KitengeTV
#BlackWeekSale

Mkurugenzi wa #KitengeTV @mshambuliaji amesema amepokea kwa mshtuko mkubwa kifo cha Master Tindwa aliyekuwa Mtangazaji wa Michezo @CloudsMediaLive
Kitenge amesema Tindwa alifanya naye kazi yeye (Marehemu) akiwa Capital Radio na Kitenge akiwa Radio One Stereo enzi hizo miaka ya 2008-2014.
“Tulimpokea Tindwa alipojiunga na Capital Radio ambayo ni radio ndugu na Radio One na tukafanya naye kazi Newsroom moja ni moja ya vijana waliokuwa tayari kufundishika na hakuwa na papara na alikuwa ni mtu mwenye kiu ya kufika mbali”
“Hakika ndoto zake zote zimezimwa, inaumiza sana sana, nimekosa maneno mengi, ila hili limeniuma mno la Tindwa” amesema Kitenge katika salaam zake akiwa London, Uingereza.
Picha hiyo inaonekana ni wakati ule Hashim Thabeet akiwa anacheza Ligi ya Kikapu ya Marekani alikuja kututembelea Radio One na Master Tindwa akiwepo. Ameondoka Kijana Mdogo na Kifo cha Kijana kinauma sana maana kinazima ndoto nyingi, amesema Kitenge huku akiomba familia yake na Clouds kwa Ujumla wawe wavumilivu katika kipindi kigumu hiki wanachopitia kwa kumpoteza Master Tindwa.
#KitengeUpdates

Jengo linawaka Moto Mtaa wa Nyamwezi na Narung’ombe karibu na Shimoni Kariakoo huku chanzo bado kikiwa hakijulikani nini.
#kitengetv inaendelea kufuatilia na itawaletea taarifa zaidi.
Makamu wa Rais wa Klabu ya Yanga @Arafat__AH kesho anachukua fomu kwa ajili ya kugombea Ubunge katika Jimbo la Shaurimoyo Zanzibar.
Akizungumza na #kitengetv Arafat amethibitisha kuwa atachukua fomu kesho kwa ajili kuomba ridhaa ya kugombea Jimbo hilo.
Itakumbuka kuwa Arafat mbali ya nafasi yake ya Makamu wa Rais wa Yanga pia ni amekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya PBZ.
#KitengeSports

Kuna shabiki wa Yanga ametaka interview yake na #KitengeTV aifanye kwa kiingereza ili wazungu wajue why HAWACHEZI.
Kaka @mshambuliaji hii ikienda hewani nitag.
Vijana wako wanafanya kazi iliyotukuka

#kitengetv tunawatakia watanzania wote Heri ya sikukuu ya Mei Mosi.
Endelea Kuchakarika..!!💪

Baada ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita kuimarisha ulinzi katika kijiji cha Lulembela kata ya Lulembela wilayani Mbogwe Mkoani Geita #kitengetv imefika Wilayani humo na kujionea hali halisi ya Kituo cha Polisi kilivyo pamoja na Gari lililoripotiwa kuchomwa na Wananchi waliokuwa wanafanya Maandamano wakishinikiza kuachiwa wananchi wawili waliokuwa wakihisiwa kuiba watoto na kuwatoa Figo.
Na hii ndio hali halisi ya kituo inavyo onekana kwa sasa huku hali ya usalama ikiwa imerejea tayari katika eneo hilo.
#KitengeUpdates
Baada ya Jeshi la Polisi Nchini Kupitia Msemaji wake ACP David Misime kutoa ufafanuzi wa awali juu ya kuuawa kwa watu wawili Wilayani Mbogwe Mkoani Geita akiwemo Theresia John (18) Mwanafunzi wa Kidato cha Nne aliyekuwa akisoma shule ya Sekondari Lulembela, #kitengetv imefika nyumbani kwao na Mwanafunzi huyo kupata undani wa kifo chake.
Akizungumza na #kitengetv Mama mzazi wa mtoto huyo amesema kipindi tukio linatokea mwanaye alikuwa ndani ya nyumba akiwa anachungulia Dirishani kwa bahati mbaya wakati Askari wa Jeshi la pilisi wakijihami walifyatua risasi ambayo ilipita katika dirisha ambalo binti yake alikiwa akichungulia na kupigwa na risasi hiyo sehemu za kifuani na kufariki dunia.
#KitengeUpdates
Sikiliza vijiweni huko watu wanasemaje baada ya Mchezo wa jana wa Watani wa Jadi wa Yanga na Simba ambao Yanga iliipasua Simba kwa bao 1-0 na kuingia Fainali ya Ngao ya Jamii. #kitengetv Iko Vijiweni.
Mkuu wa wa Wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo amepiga marufuku Mamlaka za maji kuwabambikia bili watumiaji wa maji katika wilaya hiyo.
Akizungumza na #kitengetv amesema kuwa wananchi wamekuwa wakilalamika kubambikiwa bili na mamlaka za maji tofauti na matumizi wanayotumia.
#KitengeUpdates
Baada ya Wafanyabiashara wa kariakoo kufunga maduka yao kuanzia asubuhi ya leo 23/06/2024 #kitengetv tumefika hapa Kariakoo kufahamu hasa nini kinaendelea hapa na kilio kikubwa cha Wafanyabiashara wa Kariakoo ni nini.
#kitengetv tumezungumza na baadhi ya wafanyabiashara wa hapa Kariakoo na kutueleza kuhusu hali hii ya Mgomo huu ambao unaoendelea hapa Kariakoo.
#KitengeUpdates
Kutana na Daktari Bingwa kabisa wa Masuala ya Uzazi Dr. Shaffiq ambaye kwake kama una shida yeyote ya uzazi hajawahi kushindwa.
Amefanya mahojiano marefu na #kitengetv na tumekuwekea YouTube mahojiano kamili.
Una shida ya uzazi? Muone huyu.
Mfanyabiashara mkubwa wa Maduka ya Simu #zahor__matelephone Leo amezindua Duka Jipya la Simu Jengo la Salamander Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na #kitengetv Zahor Matelephone amesema wametoa offer mbali mbali kwa Wateja wao wa mwanzo katika Duka hilo.
#KitengeUpdates
#kitengetv tumezungumza na Fortunatus Kasomfi ambaye ni Mwandishi wa Habari kutoka Afrika Kusini anayefanya kazi katika Kituo cha South Africa Broadcasting Corporation (SABC), ameeleza kuhusu muitikio wa Mashabiki wa Mamelodi Sundowns juu ya Mchezo dhidi ya Yanga wa hatua ya Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.
#kitengeSports
Mkuu wa kitengo cha habari wa Azam Fc Thabit Zakaria amezungumza na #kitengetv kuhusu sakata la mchezaji wao Prince Dube kutuma barua ya kutaka kuvunja mkataba na timu hiyo.
Kwenye Youtube ya #KitengeTv tumekuwekea kwa urefu mahojianio haya, nenda katazame.
#kitengeSports
Kufuatia Sakata la Watoa Huduma wa Afya kusema watagoma kesho kufuatia Kitita Kipya toka NHIF, #kitengetv Imezungumza na mmoja ya Wadau wa Afya na kutoa maoni yake.
#KitengeUpdates
Serikali Mkoani Geita imesema Ufaulu wa Wanafunzi kidato cha Nne umepanda kutoka 85.9% mpaka 90.02% kwa Mwaka 2023 ambapo ongezeko la ufaulu ni 4.1% huku jitihada za Walimu kujituma kufundisha zikitajwa kuongeza ufaulu huo.
Akizungumza na #kitengetv Afisa Elimu Mkoa wa Geita Mwl.Anthony Mtweve amesema kati ya Shule 141 Shule 32 zimeweza kufuta Daraja la 0 na wengine hawana Daraja la nne.
#KitengeUpdates
Serikali imekamilisha Mradi wa Maji wenye thamani ya Shilingi Bilioni 6.5 uliokuwa ukijengwa katika Mamlaka ya Mji Mdogo wa Katoro Wilayani Geita Mkoani humo ambao umelengwa kuwafikia wakazi Elfu 68.
Akizungumza na #kitengetv Mhandisi Msimamizi wa Mradi huo kutoka Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Geita (GEUWASA) Bw.Ernest Jackson amesema mradi huo unatarajia kuhudumia Maeneo mbalimbali ya Mji wa Katoro ikiwemo kata ya Nyamigota, Kata ya Buselesele na Kata ya Katoro ambapo wakazi wapatao Elfu 68 ni wanufaika wa Mradi huo.
"Mradi huu ulianza mwanzoni mwa mwaka 2021 na kwa sasa hivi tuko kwenye hatua za Mwisho kabisa tunategemea kukamilka kwa mradi huu utaweza kunufaisha takribani watu elfu 68 kwa hatua hii kama mnavyoona tumeanza kuunganishia watu majumbani kwa ajili ya majaribio mpaka sasa tumeshaunganishia watu 10 mradi mpaka kukamilika unagharimu takribani bilioni 6.5 , " Mhandisi Jackson.
Aidha Mhandisi Jackson amesema kwa sasa wameanza kuunganisha taasisi mbalimbali za Serikali pamoja na wananchi ambapo wananchi 10 tayari wamekwisha kuunganishwa na Mradi huo na tayari wameanza kunufaika nao.
Benjamine Jackson ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi kilimani iliyoko Mamlaka ya Mji Mdogo wa Katoro amesema Mradi huo ni chachu ya kuondoa changamoto katika shule hiyo ambapo toka shule hiyo imeanzishwa haikuwai kupata Maji tofauti na Mradi huo uliokamilika.
Amesema Changamoto iliyokuwepo ilikuwa ni wanafunzi kukosa Maji ya kutumia nyakati za kufanya usafi Madarasani pamoja na maji ya kutumia kwenye vyoo vya shule hali ambayo ilikuwa ikiwapelekea kwenda kujisaidia nyumbani na wengine kupelekea utoro Mashuleni.
#KitengeUpdates

Baada ya Waziri wa Utamaduni sanaa na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro kuitangaza Kamati ya hamasa ya Taifa Stars watu wengi wamehoji juu ya uwepo wa Babalevo, Mwijaku pamoja na Joti, Ni kwa namna gani wataweza kuisaidia timu ya Taifa.
#kitengetv tumefanya Mahojiano na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo @MsigwaGerson na kufafanua namna ambavyo Kamati hiyo itakwenda kufanya kazi.
#kitengeSports
Hakika kupitia #kitengetv Mmeendelea kupata taarifa kem kem na katika muda mchache imeonekana kupata wafuasi wengi wanaofuatilia habari zake. Endeleeni kutuunga mkono na siye hatutachoka usiku na mchana kuwapa habari za aina zote kutoka kona zote za Ulimwengu. Ahsante sana kwa kutuunga mkono #kitengetv 🙏
Kutoka kwa Mkurugenzi wa #kitengetv @mshambuliaji 🤝

Last Seen Hashtags on Sotwe
momson(***)***+filter:native_video
Seen from Argentina
drunkmom
Seen from Norway
privacy
Seen from Brazil
lowlvl
Seen from United States
PrayforLEOs
Seen from United States
大胸肌
Seen from United States
monkeyapp
裏アカ女子
Seen from Japan
TrenchSweeper
Seen from United States
BingoLikeaBoss
Seen from United States
Trends for you
Most Popular Users

Elon Musk 
@elonmusk
241.1M followers

Barack Obama 
@barackobama
119.1M followers

Cristiano Ronaldo 
@cristiano
112.3M followers

Donald J. Trump 
@realdonaldtrump
111.8M followers

Narendra Modi 
@narendramodi
107.1M followers

Rihanna 
@rihanna
98.1M followers

NASA 
@nasa
92.2M followers

Justin Bieber 
@justinbieber
91.3M followers

KATY PERRY 
@katyperry
88.6M followers

Taylor Swift 
@taylorswift13
82.5M followers

Lady Gaga 
@ladygaga
74M followers

Virat Kohli 
@imvkohli
71.4M followers

Kim Kardashian 
@kimkardashian
70.3M followers

YouTube 
@youtube
68.7M followers

Bill Gates 
@billgates
64.4M followers

Neymar Jr 
@neymarjr
64.3M followers

The Ellen Show
@theellenshow
62.4M followers

CNN 
@cnn
61.8M followers

Selena Gomez 
@selenagomez
61.7M followers

X 
@x
60.8M followers


