Top Tweets for #dfmupdates
Umoja wa Ulaya unasema umemuita mjumbe wake nchini Tanzania kwa mashauriano pamoja na kutathmini upya uhusiano wake na nchi hiyo kutokana na kuongezeka kwa ukiukwaji wa haki za binadamu Tanzania. #dfmupdates #economy #politics #HumanRights #Equality #EuropeanUnion #Tanzania

Tanzania imekua nchi ya mfano katika utekelezaji wa mradi wa mabasi yaendayo kasi jijini Dar es salaam, Kenya inatarajiwa kua nchi ya pili katika ukanda wa Afrika Mashariki kupata mradi huo. #dfmupdates #technology #advancement #innovation #economy #HealthyLiving #Kenya #Tanzania

Serikali ya #Tanzania imejitenga na kampeni ya kuwakamata na kushtaki mashoga inayoongozwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda. Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania inadai kampeni hiyo ni mawazo binafsi ya Makonda na si msimamo rasmi wa serikali.#dfmupdates

Mahakama Iringa imemuachia aliyekua Mwenyekiti wa Mtandao wa wanafunzi Abdul Nondo baada ya upande wa jamhuri kushindwa kuwasilisha maelezo juu ya mashtaka. Nondo alikua anakabiliwa na mashtaka ya kutoa taarifa za uongo kuwa alitekwa na watu wasiojulikana. #dfmupdates #Tanzania

Serikali yatangaza baraka kwa wakulima wa korosho mkoani Mtwara. Ni baada ya zao hilo kupata bei mpya kutoka shilingi 2717 kwa kilo hadi shilingi 3016 kwa kilo. #dfmupdates #agriculture #farming #crop #economy #politics #Tanzania

Baraza la Taifa la usimamaizi wa Mzingira (NEMC) limekifungia Kiwanda cha usindikaji nyama ya punda cha Huwachen Company Limited kilichopo Dodoma kwa kutochukua hatua za utunzaji wa mazingira. #dfmupdates #environment #life #Health #Tanzania

Makamu wa Rais, Mh Samia Suluhu amepongeza uongozi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) kwa kuendelea kutekeleza agenda ya uchumi wa viwanda ambapo limeanza kufanya kazi na wamiliki wa viwanda kutoa huduma za bima. #dfmupdates #technology #insurance #development #tanzaniayaviwanda

Takribani simu 4,340 zimefungwa ndani ya miezi mitatu iliyopita baada ya TCRA kugundua ziliibiwa ama zingine kutokidhi viwango. #dfmupdates #mobilephone #technology #Tanzania

Albamu yangu ya 'Dunia Kwaheri' ilisababisha kamera ziungue wakati wa kurekodi, wabeba kamera walikufa ndoa zilikufa kwasababu ilibeba ujumbe wa maamuzi magumu - Paschal Cassian. #dfmupdates #gospel #worship #faith #love #JesusChrist #God #Tanzania

Kama bahari ya Shamu haikumzuia Musa kuvuka, ukuta wa Yeriko haukumzuia Joshua, kama kifo hakikumzuia Yesu kufufuka basi hakuna kitu kitakachokuzua wewe kufanikiwa kiroho na kimwili kwa Jina la Yesu kristo. #dfmupdates #faith #believer #worship #love #JesusChrist #God #Tanzania

Mwenyekiti wa bodi ya kampuni ya IPP, @regmengi amesema kuwa kampuni yake inakamilisha maandalizi ya kuanza kutengeneza smartphones, kompyuta, na vifaa vingine vya umeme ikiwa ni jitihada za kuunga mkono mkakati wa uchumi wa viwanda. #dfmupdates #technology #development #Tanzania

Mtu akinitumikia Baba atamheshimu. Ukitaka heshima duniani utakachokipata ni dharau lakini ukitaka heshima ya kweli, mtumikie Mungu wa mbinguni kwa uaminifu, utaheshimiwa Duniani na Mbinguni. #dfmupdates #worship #faith #love #JesusChrist #God

Baraza la Makanisa Duniani (WCC) sasa limeanza kupambana na matumizi mabaya ya Biblia. Imegundua inatumika kunyanyasa wanawake makanisani na kugundua viongozi wa makanisa wanaopiga wake zao. Isabela A. Phiri Naibu Katibu Mkuu Wa WCC. #dfmupdates #worship #faith #Jesus #God

Mwili wa mwandishi kutoka Tanzania aliyekuwa anafanyia kazi Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Ujerumani (DW) marehemu Isaac Gamba umewasilishwa uwanja wa ndege Dar es Salaam na safari ya kuusafirisha hadi Mwanza inakaribia kuanza baada ya ibada kufanyika. #dfmupdates #Tanzania

Ndege mpya aina ya Boeing 737 yaanguka baada ya kupaa Jakarta, Indonesia.
Ndege iliyokuwa imewabeba abiria 188 ilikuwa safarini ikielekea Pangkal Pinang. Ilitoweka kutoka kwenye mitambo ya rada saa kadha baada ya kupaa, ilipokuwa inavuka bahari. #dfmupdates #Boeing737 #Tanzania

Shirika la SOS Childrenβs Village Tanzania limetambua wanafunzi 600 wa shule za msingi nane za halmashauri ya Wilaya ya Iringa waliopoteza malezi bora kwa wazazi na walezi wao na kuwawezesha kupata mahitaji muhimu ya shule. #dfmupdates #youth #EducationForAll #Equality #Tanzania

Wabunge nchini Ethiopia wamemchagua Sahle-Work Zewde kuwa rais wa kwanza mwanamke Ethiopia. Bi Sahle-Work ni mwanadiplomasia mwenye uzoefu ambaye sasa amekuwa kiongozi wa kipekee mkuu mwanamke barani Afrika. #dfmupdates #empoweringwomen #Diversity #Ethiopia #Tanzania

Trends for you
Most Popular Users

Elon Musk 
@elonmusk
241.7M followers

Barack Obama 
@barackobama
119M followers

Cristiano Ronaldo 
@cristiano
114.4M followers

Donald J. Trump 
@realdonaldtrump
111.9M followers

Narendra Modi 
@narendramodi
107.2M followers

Rihanna 
@rihanna
98.7M followers

NASA 
@nasa
92.4M followers

Justin Bieber 
@justinbieber
91.8M followers

KATY PERRY 
@katyperry
90M followers

Taylor Swift 
@taylorswift13
83.9M followers

Lady Gaga 
@ladygaga
75.4M followers

Virat Kohli 
@imvkohli
73.4M followers

Kim Kardashian 
@kimkardashian
70.9M followers

YouTube 
@youtube
68.8M followers

Neymar Jr 
@neymarjr
66.4M followers

Bill Gates 
@billgates
65.2M followers

Selena Gomez 
@selenagomez
63.1M followers

The Ellen Show
@theellenshow
62.3M followers

CNN 
@cnn
61.8M followers

X 
@x
60.7M followers






