Umasikini sio Utakatifu,na kuwa Tajiri hakumfanyi Mtu kuwa mwenye Dhambi
Usiogope kutafuta Mafanikio kwa njia halali ukidhani Umasikini ndio ishara ya Utakatifu.Mungu hapewi Utukufu na Umasikini wako,Bali na Maisha yako ya Uaminifu,Bidii na matumizi sahihi ya kile ulichonacho.
Upanga Usio na Kazi utapata Kutu Ukiwa kwenye Ala yake
Kitu kisipotumika hupoteza Ubora,Nguvu au Thaman yake Taratibu
Thamani ya Upanga ipo katka kutumika kwake,na Thamani ya mwanaDamu ipo katika kutumia Vipaji,Maarifa na Uwezo wake kwa manufaa yake na ya wengine
Tafakari Sana
Kabla ya kulala usihesabu tu makosa uliyofanya leo, kumbuka pia hatua ulizopiga.
Wakati mwingine tunajilaumu sana hadi tunasahau kuwa bado tunaendelea kusonga mbele.
Pumzika, kesho ni ukurasa mpya wa kuandika hadithi bora zaidi.
“Ukimuuliza MUONGO kwanini alikudanganya,Anakudanganya Tena.”🙌
Uaminifu hujengwa na Ukweli,lakini Uongo hujijenga juu ya Uongo mwingine.Kadri Mtu anavoendelea kudanganya,ndivo inavokua vigumu kwake kukumbuka na kutetea alichosema awali
USIMUAMINI MUONGO HATA KAMA ANASEMA KWELI
@Maestrowafact Washakuvunja mkali.....ile code ilio funguliwa oct 29...
Ni kama laana au mlango ambao uko wazi ..ku heal unaitaji ukwel na uwajibikaji ..ata uombe yasijirudie kama hauta kili na kusema ukwel ni ngumu kusahau na uenda yakijirudia ..