Dunia inafahamu ukweli. Ndiyo maana Tundu Lissu anasema akipatikana na hatia, anyongwe hadi kufa. CCM wanasema adhabu siyo kunyongwa pekee
Tundu Lissu anaeleza Mahakama kwamba adhabu ya uhaini ni kuachiwa huru au kunyongwa hadi kufa. CCM wanasema Mahakama iamue kwa hisia tu
Anyways, tuachane na huo ujinga wa CCM
EPP Group (European People’s Party Group). Ni muungano wa kisiasa wa mwelekeo wa kati-kulia (centre-right) katika Bunge la Ulaya.
EPP Group (European People’s Party Group) ndilo kundi kubwa zaidi na lenye ushawishi mkubwa zaidi katika Bunge la Ulaya (European Parliament).
EPP GROUP (European People’s Party Group) wamempendekeza Tundu Lissu kugombea Tuzo ya Sakharov (Sakharov Prize for Freedom of Thought)
Pia, ECR GROUP (European Conservatives and Reformists Group) wameungana na EPP GROUP kumpendekeza Tundu Lissu kuwa mgombea wao
ECR GROUP ni muungano wa kisiasa wa mwelekeo wa kulia/kihafidhina (right-wing/conservative) katika Bunge la Ulaya (European Parliament)
Kumpendekeza Tundu Lissu kunamaanisha wanamuona ni alama ya ujasiri na kielelezo cha watetezi wa demokrasia wanaopitia vizuizi
Kupendekezwa kwa Tundu Lissu ni tamko kwamba mapambano ya miaka mingi, yametambuliwa katika ngazi ya juu kabisa ya kitaasisi Barani Ulaya
Uteuzi huu TAL akiwa gerezani kwa mashtaka ya uhaini unaiweka diplomasia ya Tanzania na mazingira ya kisiasa ya ndani katika jicho la kimataifa;
Unaiwekea serikali na taasisi za kisheria ‘presha’ ya kuendelea kuheshimu misingi ya demokrasia, uwazi, na haki za kisiasa na michakato ya kiuchaguzi
Mchakato wa kumchagua mshindi wa Tuzo ya Sakharov (Sakharov Prize for Freedom of Thought) unafuata hatua zilizowekwa na Bunge la Ulaya
Kupendekezwa ni hatua ya kwanza katika mchakato mrefu wa utoaji wa tuzo hii. Siyo kwamba Tundu Lissu kupendekezwa ndiyo ameteuliwa mshindi
Ili mteule aingie katika kinyanganyiro, anapaswa kupendekezwa na: Kila kundi au kundi la wabunge linaweza kupendekeza jina moja pekee
Wagombea waliopendekezwa huwasilishwa katika mkutano wa pamoja wa kamati kadhaa za Bunge la Ulaya kwa ajili ya mchujo wa wagombea
Kamati ya Mambo ya Nje, Kamati ya Mandeleo, na Kamati Ndogo ya Haki za Binadamu. Hapa, maelezo ya kila mgombea husomwa mbele ya wabunge
Kamati mbili kuu za Bunge la Ulaya; Kamati ya Mambo ya Nje (AFET) na Kamati ya Mandeleo (DEVE), hufanya zoezi la kura ya pamoja kwa njia ya siri
Kutokana na kura hizo, wanachagua wagombea watatu wenye kura nyingi zaidi ili kuunda orodha fupi ya mwisho (shortlist of three finalists)
Uamuzi wa mwisho wa kumchagua na kumpata mshindi haufanywi na kamati, bali unafanywa na Mkutano wa Marais (Conference of Presidents)
Kundi hili hukutana faragha, kujadili finalists watatu, na kumtangaza mshindi mmoja rasmi kutoka katika orodha fupi ya mwisho (shortlist of three finalists)
Mshindi hualikwa katika ukumbi wa Bunge la
Ulaya mjini Strasbourg, France, wakati wa kikao cha pekee cha Bunge la Ulaya, mwezi Desemba
Huko, mshindi hutunukiwa cheti rasmi cha ushindi pamoja na zawadi ya kifedha ya £50,000. Hii kwa sasa ni sawa na takribani TZS 174,262,600
Tuzo ya Sakharov ni kitu gani?
Tuzo ya Sakharov (Sakharov Prize for Freedom of Thought) ndiyo tuzo ya juu zaidi na heshima ya haki za binadamu inayotolewa na Bunge la Ulaya
Sakharov Prize for Freedom of Thought iIlianzishwa mwaka 1988 kwa heshima ya mwanasayansi na mpinzani wa Kisovieti Andrei Sakharov
Tuzo hizi wamewahi kushinda watu wazito sana Duniani wakiwepo; Nelson Mandela (1988), Kofi Annan (2003), na Malala Yousafzai (2013)
Sakharov Prize for Freedom of Thought hutolewa pia kwa watu au mashirika yanayojitolea kutetea uhuru wa mawazo na haki za binadamu Duniani
Wakati Serikali Katili ya CCM inataka kuaminisha Dunia Tundu Lissu ni mhaini, Dunia inakataa kwa vitendo uongo na ghiliba za serikali ya CCM
Dunia inampendekeza Tundu Lissu kuwa mshindi wa tuzo ya juu zaidi na heshima ya haki za binadamu inayotolewa na Bunge la Ulaya. Kwa heshimaaaa.
MMM, Martin Maranja Masese, Mtikila.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 457
Mhe. Lissu anaendelea kufanya mawasiliano yake ya mwisho (Final submission)
An Act, attempt or omission punishable by law, hayo ndo makosa.
Kama hakijawekewa adhabu na hakijatamkwa sio makosa.
Hayo maneno yanayodaiwa kuwa ya kihaini sio makosa ya kihaini kwa mujibu wa kifungu cha 39 chote na vilevile sio makosa kwa mujibu wa makosa yaliyoorosheshwa kwenye sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Udiwani.
Sio makosa ya Jinai kokote kwahiyo ukiyasema yanakuwaje makosa ya kuchochea mtu kufanya jambo halali? Kosa lilitakiwa jambo lisiwe halali na liwe kinyume na sheria ndio lingekuwepo kosa hapo.
Waheshimiwa Majaji nataka nifunge kwenye hilo suala kwamba Je maneno yanayolalamikiwa ni makosa kwa mujibu wa Sheria?
Na jibu ndio hilo nililolionyesha na sio makosa ya Uhaini wala jinai nyingine.
Jibu la issue no. 4 ni Negative. Maneno niliyosema sio makosa kwa mujibu wa sheria za Tanzania na sio pia ni Uhaini.
Sasa Waheshimiwa Majaji naomba niende kwenye issue no. 5 inahusu uchapishaji yaani PUBLICATION.
No issue ya tano ni Deed yaani kitendo.
Inasema JE KUTAMKA YALE MANENO NI KITENDO KWA MUJIBU WA KIFUNGU CHA 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu.
Whether the alleged words constitute a deed?. Suala hili kwa lugha rahisi upande wa mashitaka wanasema kusema ni matendo.
Issue ni je maneno ni matendo?
Kwanza Waheshimiwa Majaji naomba nifafanue hii confusion imetokea wapi?
Hii ni confusion ya kutengenezwa makusudi na upande wa mashitaka. It is a delinerately confusion created ili kuhalalisha hoja fulani. Iko hivi kifungu cha 39(2)(d) kinasema any person who forms an intention to instigate any lerson or grouo of person to intimidate the executive and manifest such intention by any overt act or deed or by publishing by printing or writing shall be liable of conviction
Masharti ya kifungu lazima uthibitishe kwa kuchapisha maandiko au maandishi au kwa kitendo cha wazi. Khatibu Gandi ilisema mananeo matupu sio Uhaini.
Sasa ili wanitengenezee kosa wakasema maneno ni matendo kumkwepa Khatibu Gandi. Wamedraft mashitaka kwa kusema the accused manifested his intention by his deed of uttery. Kwahiyo namna ya kuhalalisha maneno haya ni kosa wakaona waseme maneno ni matendo. Wanataka kuepuka masharti ya sheria.
Ili kuendana na kifungu cha 39(2)(d) cha Penal Code.
Pia wametengeneza tofauti kwenye maneno ambayo haipo kwamba overt act na deed vinatofautiana. Utofauti wake ni nini?
Hoja yangu ya kwanza ni kwamba acts and deed in their plain meaning means the same thing.
Kwa maana ya kawaida kiswahili chake ni kimoja kwamba ni MATENDO.
Kwenye kingereza in their plain english meaning oxford advanced learner disctionary an act means a particular thing that somebody does.
Hiyo dictionary inasema it is synonimous as an action. Kwa Kiswahili ni kitendo.
What is a deed in the same Dictionary a deed is a thing that somebody does. It is synonimous with an act.
Therefore a deed is essentially the same as an act. Kifungu cha 39(2)(d) kinaposema kitendo kitathibitishwa with an overt act or deed maana inasema inahitaji kitendo na sio kitu kingine.
Hayo maneno mawili kuthibitisha kwamba yanasema ni kitu kimoja twende kwenye Blacks Law Dictionary hiyo ni famous Kamusi ya Kisheria.
Blacks Law Dictiomary 7th Edition what does it say about an action is something done or perfomed. It also a deed.
It is a process of doing or perfoming. Haya ni matendo. Kwahiyo Wahehsimiwa Majaji an act is the same thing as a deed. Something that is done. It can not be something that is said
Maneno hayawezi kuwa ni Matendo. Kwahiyo hii charge inayonikabili inaposema nilithibitisha nia yangu ya uhaini kwa matendo yangu ya maneno haiwezekani. Words can not be deed. Na kwavile haiwezekani hii hati ya mashitaka ni Defective. Ni mbovu kwasababu imetaja kitu ambacho hakipo kwenye sheria.
The charge is defective on this particular point.
Part 458 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 456
Mahakama imerejea.
Majaji wameingia wapo watatu kama kawaida yao wanaongozwa na Jaji Ndunguru.
Anasimama Katuga anasema corum iko kama asubuhi isipokuwa Ajuaye Zengeli, anasema wako tayari kwa ajili ya kuendeshea.
Jaji Ndunguru anamuuliza Mshitakiwa vipi?
Mhe. Lissu anamjibu niko tayari.
Mh. Lissu anasimama na kusema Wahehsimiwa Majaji tulipobreak nilipendekeza niingie kwenye hoja ya Sheria ya Uchaguzi na kama ambavyo nimeelezea kosa la Uhaini kama lilivyofafanuliwa kwenye Katiba.
Kosa nililoshitakiwa nalo halihusiani kabisa na kilichosemwa kwenye kanuni ya adhabu na ndio sheria pekee kwahiyo kama haya matendo niliyoshitakiwa nayo hayafit katika sehemu yoyote katika mojawapo ya matendo 10 ambayo kifungu cha 39 kimeyataja kwamba ukiyafanya haya unakuwa umefanya kosa la Uhaini.
Maana yake ni kwamba mimi sijafanya kosa lolote la Uhaini.
Sasa Wahehsimiwa Majaji kama sijafanya kosa lolote la Uhaini je nimefanya kosa lingine lolote kwa mujibu wa sheria za Tanzania? Ndicho ninachotaka kujadili kwa sasa.
Maneno ninayoshitakiwa nayo ni kuvuruga Uchaguzi na sheria No. 1 ya 2024 ndio Sheria inayosimamia uchaguzi kwenye nchi hii. Hiyo sheria ilitungwa kwa ajili ya Uchaguzi wa 2025 na sheria hiyo ilitungwa kusimamia uchaguzi ambao kwa mujibu wa DW 5 umekuwa ni uchaguzi ambao watu wengi wamekufa kuliko kipindi kingine chochote toka vita ya majimaji.
Sura ya 7 ya Sheria hiyo ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani. Inasema kwenye kichwa cha habari ni MAKOSA na ADHABU ZAKE.
Makosa yanayohusu Uchaguzi na adhabu zake. Waheshimiwa Majaji sheria hii katika Sura ya 7 imeorodhesha jumla ya Makosa 23 na adhabu zake.
Kuanzia kifungu cha 114 hadi 136 ni orodha ya makosa na adhabu zake. Makosa ambayo ukiyatenda unaweza kushitakiwa na kufungwa au ukapewa adhabu ya kijinai na kufungwa.
Maneno ambayo tunataka kujua ni makosa ni yale maneno tutazuia uchaguzi, tutavuruga uchaguzi na tutahamasisha uasi. Tumesema sio Uhaini hadi sasa kwa hoja tulizotoa. Sasa je ni kosa gani lingine?
Uzuri wa sheria hii umeandikwa Kiswahili kila anayejua kusoma na kuandika anaweza kusoma. Kosa la 1 lipo kwenye kifungu cha 114 linaitwa kosa la uandikishaji wapiga kura,
2. Kutumia wadhifa kushawishi watu wasiwe wagombea kifungu cha 115.
3. Mwenendo usiofaa wa mtendaji wa uchaguzi.
4. Makosa yanayohusu daftari la Wapiga kura kifungu cha 119 hili nalo mimi sihusiki na hayo yote niliyotaja.
5. Mwenendo usiofaa wa maafisa uandikishaji.
6. Kifungu 121 makosa yanayohusu fomu za uchaguzi na karatasi za kura.
7. Kosa la mtu kutangaza amejitoa kwenye kinyang'anyiro.
8. Kifungu cha 123 vishawishi vya rushwa kwa ajili ya kujitoa hilo nalo sihusiki nalo.
9. Kifungu cha 124 margin inasema makosa mengineyo kutoa ushahidi wa uongo wakati wa tamko.
10. Utunzaji wa siri ni kosa pia. Kif. 125
11. Kifungu cha 126 hongo na takrima
12. Impersonation kujifanya mtu mwingine. Kuchukua kadi ya mpiga ya mwenzako.
13. Kupoteza sifa kwa kuhukumiwa kwa kosa la kitendo cha Rushwa.
14. Kosa la 14 liko kifungu cha 129 bad influence ushawishi mbaya.
15. Kosa la kif.130 hongo na rushwa kwa maafisa wa tume.
16. Hatia ya kujifanya mtu mwingine. Mimi ni Tundu Lissu wa miaka yote sijajifanya mtu mwingine.
17. Adhabu ya vitendo vya rushwa na vitendo haramu.
18. Kuingilia Mikutano halali ya hadhara ni kitendo haramu vilevile.
19. Makosa yanayohusu siku ya uchaguzi. Kuvaa nguo za chama siku ya uchaguzi. Hilo pia sijafanya.
20. Unyanyasaji na ukatili wa kijinsia wakati wa uchaguzi. Hilo nalo halinihusu katika kesi hii.
21. Kuchafua matangazo ya uchaguzi. Wagombea wameweka mapicha unararua.
Hayo ndio makosa kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi na ukiyafanya hayo yana adhabu zake zilizoelezwa kwenye sheria.
Hakuna kukinukisha hakuna kuzuia uchaguzi sio kosa kabisa. Na sio makosa kwasababu kifungu cha tano cha kanuni ya adhabu kimefafanua makosa ni vitu gani?
Part 457 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
Kimama haamini anachokiona ,
Alidhani na Lissu akikaa jela long enough basi atauza mechi kama Mbowe….
Yani hawajui wafanye nae nini….
Watanzania tupambane kuweka pressure juu ya Lissu kwa njia yoyote ile…….
Yes, WHERE IS NCHIMBI?????????? NCHIMBI YUKO WAPI?????
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 453
Mhe. Lissu anaendelea kufanya mawasiliano yake ya mwisho (Final submission)
Mhe. Lissu anasema Ushahidi wote huo wa mashahidi hao went largely uncontested by this army of this governement Lawyers. It remain intanct and therefore interm of the aforesaid authorities. Rumima, Nyerere failure to cross examined is deemed to be admission of the veracity of the defence testimony and story.
Hawakuhoji kwasababu walikubali story yetu.
Naomba nimalizie kwenye hoja hii kwa kusema yafuatayo.
Nimeshitakiwa kwa tuhuma ya kutengeneza nia ya kuchochea umma wakati sheria kifungu cha 39(2)d hakitambui umma. Kinatambua nia ya kuchochea mtu au kikundi.
Nimeshitakiwa kwa kutengeneza nia ya kuchochea umma ambao hautambuliki na sheria kuzuia uchaguzi wakati sheria haitambui nia ya kuzuia uchaguzi. Nia ya kuzuia uchaguzi haitambuliki na kifungu husika.
Nimeshitakiwa kwa kutengeneza nia ya kuchochea umma usiotambulika kuzuia uchaguzi usiotambulika kisheria ili kuitishia serikali ambayo sijaisema kokote kwenye maneno yangu na hawajaleta ushahidi wa kuthibitisha hilo.
Nimeshitakiwa kwa sababu ya hisia na sheria hairuhusu mashitaka ya hisia.
Katika mazingira haya hili swala la tatu. Jibu lake sio lingine zaidi ya HAPANA.
The only logical and xorrect answer is and can only be NEGATIVE. That is to say the accused did not inform any intention to instigate any person or group of person to obstruct the 2025 general election for the purpose of intimidating the Executive of the URT.
on the basis of Grey Likungu Mataka to sustain a conviction on the charge of treason the prosecution must prove the intention to commit treasonous conduct.
The prosecution failed to prove the intention to commit treasonous act.
Nimemaliza swala la tatu. Naomba niende swala la nne sasa kwa ruhusa yenu.
Swala la nne linasema JE HAYO MANENO yaliyotamkwa na Mshitakiwa yanatengeneza kosa lolote linalojulikana na sheria?
Hayo maneno hayo yamekuwa maarufu sana, yanatengeneza kosa linalotambulika na sheria za nchi hii. Yanaonesha kosa? Do they constitute any offence known to Tanzania laws?
Nitajibu swali hilo kama ifuatavyo.
Swala hili lilijitokeza kutokana na tuhuma zilizoletwa upande wa Mashitaka kwamba the accused uttered words amounted to criminal offence which determination ilisababisha mkuu wa upelelezi kanda ya Dar es salaam kufanya upelelezi.
Haya ni maneno yao Jamhuri sio yangu.
Maneno yenyewe yakoje yanasema nini?
Kwenye mkutano wa Tarehe 03/04/2025 mtuhumiwa alidhihirisha nia yake kwa kusema maneno yafuatayo "wanasema kitu kimoja sahihi msimamo huu unaashiria uasi tutazuia uchaguzi na hiyo ndio namna .. huu uchaguzi tutauvuruga vibaya sana..."
Haya ndio maneno yanayisemwa yanadhihirisha nia ya uhaini. Na ndio criminal offence.
Wahehsimiwa Majaji kitu cha kwanza kabisa. Kuhusiana na maneno haya. Ni kwamba hakuna mahali kokote ambapo upande wa mashitaka umeyafafanua hayo maneno.
Hawajasema kuvuruga uchaguzi maana yake ni nini na kwanini ni kosa?
Kuhamasisha uasi ni nini na kwanini ni kosa?
Hawajasema kuzuia uchaguzi ni nini na kwanini ni kosa?
Hawajasema kukinukisha ni nini na kwanini ni kosa?
Sio wajibu wangu mimi mshitakiwa kuyatolea maneno hayo ufafanuzi na kuonesha kuwa sio makosa. Sio wajibu wangu kisheria.
Ni wajibu wa upande wa mashitaka kufafanua hayo maneno yana maana gani na kusema kwanini ni makosa. Ni wajibu wao kueleza kwanini wanadhani ni kosa.
It is a question of burden of proof na lazima tuambiane ni nani ana wajibu wa kuthibitisha. That burden it never shift from the prosecution.
Kwasababu hawajafafanua wameleta hisia zao juu ya hayo maneno. Waheshimiwa Majaji ushahidi wa upande wa mshitaka juu ya haya maneno uko ukurasa 146 in the case of PW 1. Ukurasa 183 na 184 in the case of PW 2, na ukurasa wa 444 hadi 446 in the case of PW 16.
Part 454 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 454
Mhe. Lissu anaendelea kufanya mawasiliano yake ya mwisho (Final submission)
Mashahidi wote hao wamesema hayo maneno yanatengeneza kosa la uhaini. Mtayaona kwenye hizo kurasa. Without exception wametoa sababu zilezile. Sababu ya kwanini wamefanya hivyo ni Sababu za Mapolisi. Ni walewale hakuna jipya.
Kwa upande mwingine mashahidi wote wa utetezi wamesema maneno yale hayana shida yoyote. Na hayo yapo kwenye ukurasa wa 196 na 123 kwa DW1, 671 na 672, 679, 681, 698 to 700, 726 in the case of DW 2. L
Waheshimiwa Majaji DW 3 ipo 764 na anataja kurasa kadhaa hapo pia.
DW 4 upo kwenye ukurasa 810na DW5 930 anataja kurasa kadhaa zinazohusu mashahidi hao.
Wahehsimiwa majaji mashahidi wote wa utetezi without exception hayo maneno yanayodaiwa hayana kosa lolote kwenye sheria za Tanzania.
Waheshimiwa Majaji kwa vile kuna 2 sets of evidence which are diametrically oppose what is the position of the law.
Kujibu swali hili the statrting point on this question must nencesarily article 28(4) of the constitution.
Maneno ya Katiba ni muhimu sana inasema hivi, uhaini kama unavyofafanuliwa na Sheria utakuwa ni kosa la juu kabisa dhidi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Ibara ya 28(4) ya Katiba)
Waheshimiwa majaji, Uhaini kwa nchi hii ni ule uliofafanuliwa na Sheria. Nje ya Sheria ni Maneno matupu. Kwa vile uhaini lazima uwe umefafanuliwa na Sheria, ni sheria ipi inafafanua uhaini? Ni kifungu cha 39 cha Kanuni ya Adhabu ndio kinafafanua uhaini.
Waheshimiwa majaji kifungu cha 39 ni muhimu sana kwenye kesi hii. Kama ninayotuhumiwa kuyafanya hayamo kwenye kifungu hiki hakuna uhaini hapa. Kifungu cha 39 kina vifungu vidogo vinne. Hivyo vifungu vidogo vinne vimetengeneza matendo 10 ambayo ukiyafanya yanatengeneza kosa la uhaini.
Kitendo cha kwanza cha kihaini kwenye kigungu cha 39 (1)(a) ni kumuua au kujaribu kumuua Rais. Kitendo cha pili cha kihaini ni kuendesha vita dhidi ya Jamhuri ya Muungano 39(1)(b).
Kifungu cha 39(2) kimetengeneza matendo manne. Hivyo kitendo cha tatu kinaitwa forming the intention to effect or forming the intention to instigate any person or group wasababishe kifo cha Rais au Rais atiwe kilema au ajeruhiwe au afungwe ni uhaini 39(2)(a)
Kitendo cha nne ni kutengeneza nia ya kuwezesha au ukatengeneza nia ya wengine wawezeshe Rais apinduliwe kwa njia zisizo halali kutoka kwenye nafasi yake kama rais na jina lake kama mkuu wa nchi na amiri jeshi mkuu ni kitendo cha uhaini 39(2)(b)
Kitendo cha tano ni kutengeneza nia ya kuwezesha au kuwawezesha kupinduliwa kwa Serikali ya JMT ni uhaini 39(2)(c). Kitendo cha sita ni hii niliyoshtakiwa nayo, ukitengeneza nia ya kuwezesha au kushawishi watu wawezeshe kutishiwa kwa Serikali, Bunge au Mahakama unakuwa umetenda kosa la uhaini 39(2)(d)
Kosa namba 7,8 na 9 yako kwenye kifungu cha 39(3). Kitendo cha 7 kipo 39(3)(a) ambacho kinasema ukijiunga au kushirikiana nao na maadui wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kosa la uhaini. Kitendo cha 8 kinasema kuchochea mtu yeyote kuivamia Jamhuri ya Muungano kwa silaha au kama wale wakongo wanaitwa M23 ukiwaleta Tanzania ni uhaini.
Kitendo cha 9 cha kihaini kipo 39(3)(b) ukichukua silaha ndani ya Jamhuri ya Muungano kwa lengo la kuibadilisha serikali ili ibadilishe mambo yake ni uhaini typically hapa ni Kama M23 au wale wa Somalia , 39(3)(c)
Kutendo cha 10 kipo kwenye 39(4) ni kusaidia maadui wa Jamhuri ya Muungano kwa kufanya kitendo chochote cha kumsaidia adui kama vile kuhatarisha maisha, ni kitendo cha uhaini, haya ndio makosa ya uhaini kwa Sheria za Tanzania. Nje ya haya ni maneno matupu, ni hisia, ni ignorance and such like.
Part 455 itaendele kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 452
Mhe. Lissu anaendelea kufanya mawasiliano yake ya mwisho (Final submission)
Mhe. Lissu anasema Msimamo huu utaukuta kwenye maamuzi ya Mahakama hii kwenye kesi ya Justin Rutahirwa vs Bulchad Kalumna. Consolidated Criminal Appeal No... 2020 Justice Kilekamajenga alisema
Hisia hata kama ni nzito kiasi gani haziwezi zikawa msingi wa kutia mtu hatiani. Na hasahasa kwenye kesi nzito kama ya Murder.
Sasa hii ya kwangu sio kesi ya Murder.
Hii ni kesi ya Uhaini na Waheshimiwa Majaji UHAINI ni kosa pekee lililotajwa kwenye Katiba ya nchi. Ibara ya 28(4) inasema UHAINI KAMA UNAVYOFAFANULIWA NA SHERIA UTAKUWA NI KOSA LA JUU KABISA DHIDI YA JAMHURI YA MUUNGANO.
Ndio kosa kubwa kuliko yote kwneye nchi hii na adhabu yake ni kifo. Walionishitaki wanataka mnihukumu kifo kwasababu ya hisia zao. Kwasababu wanahisi nilikuwa nalenga kuitishia Serikali.
Waheshimiwa Majaji Mahakama hii kwa misingi hii ya kisheria haiwezi kuwakubalia. Na nawaomba Majaji msiitikie wito wao, wito wao ni wito wa hisia msiwakubalie mwaliko wanaoutaka. Kunitia hatiani kwasababu tu wanahisi nililenga kuitishia serikali.
Ushahidi wa Utetezi unasemaje juu ya hii hoja? Ushahidi wangu ulikuwa simple, straight foward and consistent kwenye hii hoja.
DW 1 589 na 590 nilizungumzia nia ya kuitisha huo mkutano kwamba told the court the meeting was inteded of bring together all prospective candidate of the party from across the country ams it was called with the intention of exolaining the party no reforms no election resolution made by the party conglese.
Ndio ilikuwa nia yetu na ndio ilikuwa nia yangu. Tuliitisha watia nia kuwaeleza msimamo wetu. That was the intention.
Specifically on those words nilisema yafuatayo ukurasa wa 596 wa records
In that discussion i did not refer to the governement and what intended to do to the governement. Nikaendelea kusema ghe allegation that our objective was to threten the govenrnrmt is therefore misplaced.
My purpose was to explain kwa watia nia kuhusu changamoto za masuala ya uchaguzi na ili waelewe msimamo wa Chama wa no reforms no Election.
There was no intention to threaten the governement because threatening the governement was never part of my agenda. I did not mobilize people to engage in violence or disorder. Nilisema tutapambana kutaka mageuzi hadi reforms zitakapopatikana.
I was extensively and vicious cross examined nilikaliwa kooni kwelikweli lakini naomba muangalie kwenye record kama huo ushahidi wangu juu ya nia yangu kwamba ulihojiwa hata mara moja.
Mimi nimeangalia hiyo rekodi yote sijaona these governement lawyers cross examined me juu ya nia yangu kwenye mkutano ule. Hakuna hata mara mija walipofanya hivyo. Waliniuliza maswali alfu lela ulela. That aspect complitely remain unchallenged Justice Rumima Katiti, Nyerere Nyague, Chora Samson Kiberit Mahakama ya Rufani all those cases from Court of Appeal have established a principle that failure to cross examine a witness on a material point is an admission of his version of the story.
Kutonihoji kuhusu nia yangu huwezi kusema hukubaliani na nia yangu ya kuitisha ule mkutano. Hiyo nia umeikubali kabisa.
Ushahidi wangu umeungwa mkono na DW 2 Kwenye ukurasa wa 161 wa rekodi. Na ukiangalia nae pia aliulizwa maswali mengi lakini hakubadili msimamo wake kabisa angalia ukurasa wa 691 he never waver the position. Alisema tuliazimia bagamoyo na tulihitaji kuuelezea kwa watia nia.
Msimamo huo huo uliungwa mkono na DW 3 ukurasa wa 732 na 779 na 791 na 795 of the record. Kwenye swala la nia nae hakushake kwenye suala la nia.
Msimamo wa Utetezi ulishikiliwa pia na DW 4 ukurasa 799 na 800 wa hizo rekodi za Mahakama.
Part 453 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 451
Mhe. Lissu anaendelea kufanya mawasiliano yake ya mwisho (Final submission)
Mhe. Lissu anasema, PW 17 alikuwa ni shahidi wa mafichoni nina shida na hilo na kwamba shahidi huyu alitoa ushahidi wake mafichoni lakini in all fairness sio yeye aliyejipeleka mafichoni aliwaambieni hakuna mtu hata mmoja aliyemtishia.
Tofauti na mashahidi wengine huyu PW 17 yeye hakuwa muhalifu kabisa, mashahidi wengine wote wa vificho walikuwa ni watuhumiwa, yeye alikuja kama Shahidi huru.
Kwa ushahidi wake na uzito wa ushahidi wake ni mkubwa sana. Waheshimiwa Majaji muhimu zaidi kuhusu shahidi huyu ni kwamba ushahidi wake unaunga mkono ushahidi wote wa Utetezi. His entire evidence is in substantial agreement with the evidence of defence side in all major issues.
Mambo yote ya Msingi amepingana na mashahidi wa Jamhuri na kuungana mkono na mambo yote ya Utetezi.
Hawa mashahidi wanne niliowataja PW 1,2 na 16 ushahidi wao umetofautiana fundamentally na PW 17.
Hii ina maana kwamba ushahidi wote wa mashitaka ni totally unreliable kwasababu ni NDIMI MBILI KAMA ZA NYOKA.
Ulimi mmoja unasema ni Uhaini na Ulimi mwingine unasema maneno haya hayana shida yoyote, hakuna kitu. On the basis of the authority cited yesterday.
This is a life or death of this case suala hili ninalosema kwa sasa kama ushahidi wao hauna credibility kwahiyo swali la JE KULIKUWA NA NIA YA KUTENDA KOSA LA UHAINI?
Kama ushahidi haushikiki basi kesi inakufa. Hoja sio hiyo peke yake.
Hii nadharia kwamba serikali inasimamia sheria ni hoja ya maana kiasi gani?
Kesi yote ya Mashitaka kwenye suala hili imejengwa kwenye hisia, supposittions kwenye suspicions sio kwenye ushahidi. Ni hisia kwamba analenga kuitishia serikali. It is based on suspicious. It is based on their beliefs and spoken words.
Serikali haikutajwa kokote wala kiongozi yeyote hajatajwa lakini kwenye vichwa vyao wana imani hiyo na kwasababu Lissu anailenga Serikali na Katiba inasimamiwa na Serikali.
Huu ni msingi wa hewa sio msingi wa mawe na kokoto.
Kesi imejegwa kwenye msingi wa hewa na sio mawe na Kokoto.
Nasema hivyo kwasababu hawa mashahidi wamerudia rudia sana na mawakili wao wamerudia rudia sana mambo ya kutaka kuzuia uchaguzi ni kuitishia serikali?
Je Serikali ni chombo pekee kinachosimamia Sheria?
Tuzungumze na mambo ya wazi.
Judiciary Administration Act Sheria ya usimamizi wa Mahakama. Je hii sheria inasimamiwa na nani? Inasimamiwa na Mahakama na sio Serikali wala chombo kingine.
Sheria ya Tume ya Utumishi wa Mahakama imasimamiwa na nani? Inasimamiwa na Judiciary.
Sheria ya Parlimentary Powers and Immunity Act inasimamiwa na nani? Na Bunge.
National Assembly Adminstration Act 2008 inasimamiwa na nani? Inasimamiwa na Bunge.
Sheria za uchaguzi zinasimamiwa na nani? Na Tume ya Uchaguzi. Sasa Tume ni Serikali?
Nchi hii kuna sheria inaitwa Kanuni ya Maadili ya Uchaguzi zinasimamiwa na nani? Na Tume.
Tanganyika Law Society Act inasimamiwa na nani? Inasimamiwa na Chama cha Mawakili.
Hii nonsense ya kwamba Serikali ndio inasimamia sheria imeletwa na Mapolisi. PW 1 ameianzisha ikabebwa na Mapolisi wengine na ikapelekwa kwa ofisi ya DPP nao wakaibeba wakaja nayo Mahakamani bila kufikiri. Nonsense!.
Jaji anasema tulia kidogo.
Mhe. Lissu anasema nina haki ya kukasirika nimekaaa gerezani kwa mwaka mzima na nusu, niache nizungumze.
Miaka 55 iliyopita kesi ya Amin Sam Mrisho Nasoro Mzava alisema Suspicion no matter how strong can not be the basis of conviction in criminal charge.
Msimamo huo wa miaka 55 iliyopita uliungwa mkono na Mahakama ya Rufani, Nathaniel Mapunda vs R 2006 TLR 395
35 years baadae kutoka kwenye kesi ya Amin Sam Mrisho mahakama ya rufani ilisema suspicion alone however grave it may ben be it not enough to sustain conviction kwneye kosa lolote iwaje kwenye kosa kama la Mauaji?
Part 452 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 450.
Mhe. Lissu anaendelea kufanya mawasiliano yake ya mwisho (Final submission)
PW 16 ndie alichukua uongozi baada ya George. Alisema hivi. Huyu nae ni polisi. Ukurasa wa 434 the accused intended to intimidate the govt in to doing what he wanted or pursuing the cause of action he intended. By threatening to obstruct general election amount to treason.
Aliendelea kuelezea kwanini haya maneno ni uhaini ukurasa 485 anasema the words used by the accused such as tutazuia uchaguzi, tutahamasisha uasi were intended to intimidate the govt which is vested with the repsonsibility and authority to protect the country and by uttering those words he deliberately intended to intimidate the governemnt.
Under re examination alisema yafuatayo what i meant is that the words complained of i meant the govt is vested with the power to enforce the law of the country kwahiyo kusema maneno yale ni kuitisha serikali.
Msimamo wao ndio huo ukitishia uchaguzi ni uhaini na hiyo ndio Police thinking na sio thinking ya Wanasheria.
Waheshimiwa Majaji sio kila shahidi wa Upande wa mashitaka walikuwa na msimamo huo.
The eye witness PW 17 ni kwamba hakuunga mkono hiyo theory ya Mapolisi, hakuiunga mkono kabisa. He differed with the prosecution case.
Alipingana na msimamo wa Mashitaka ni shahidi wao lakini alitofautiana nao kabisa.
Kwenye ushahidi wake ni tofauti kabisa.
Alisema yafuatayo kuhusu lengo la Mkutano wa Tarehe 03/04/2025
"The meeting was intended to bring together Chadema aspiring candidate to discuss election related matters and the partys slogan No reforms, No Election.
Akaendelea kusema alot was discussed during meeting hower the main issue included the slogan No reforms and how Chadema inteded to approach the forthcoming general election i recall they stated that without reforms they would not participate in the general election.
Furhermore the Chairman Lissu spoke on how they plan to obstruct election and said tutazuia uchaguzi na tutakinukisha.
Huo ni ukurasa wa 481 na hayo ndio maneno ya aliyekuwepo, aliyesikia na kurusha matangazo hayo. Hakuna Uhaini wala kosa lolote.
PW 17 was also Extensive cross Examined. sasa when cross examined kwamba aliona chochote kuwa ni uhaini alisema yafuatayo, 498 ukurasa
"It is true in my statement i did not state the words spoken by Lissu constituting treasonous statement" Ni kweli maneno yale sikuandika kokote kuwa maneno ya Lissu yalikuwa ni makosa na yalitengeneza kosa la Uhaini.
Huyu PW 17 Sio shahidi wangu. Hakuona uhaini na hakusikia uhaini. Exhibit D16 ni muhimu sana katika pieces of Evidence ni muhimu sana katika kesi hii.
Kielekezo hicho D16 is complitely silence on the words tutazuia uchaguzi tutahamasisha uasi ni maneno hayapo kabisa kwenye hicho kielelezo.
Nilimuuliza kwanini haya maneno hayapo kwenye maelezo yako? Ukurasa wa 497 na 498 anasema hivi "the words are not contained in exhibit D16 it is true i was at the meeting i heard and saw what was going on personally and in the exhibit i recorded what was going on ....... "
Nilikuwepo nilisikia na kuona kilichokuwa kinaendelea mimi mwenyewe na kwenye kielelezo niliandika mambo ya No Reforms, No Election na akasema kwamba pia
The Leaders were not wrong to discuss no Reforms and Challenges facing election in their constituences.
Shahidi angekuwa wangu wangesema nilitegemea nini lazima angesema hivyo. Sasa huyu ni shahidi wao. Kifungu cha 67 kinasema ushahidi wa moja kwa moja. Ushahidi bora. Best Evidence Rule.
Kama ni ushahidi wa kuona ni aliyeona, kunusa basi aliyenusa, kuonja basi aliyeonja.
Sasa PW 17 alikuwepo, aliona, alisikiliza na alirusha matangazo yeye. Amesema sikuwa na kosa. Nimekaa mwaka mzima na nusu Gerezani halafu Mapolisi walikuwa na ushahidi huu wa PW 17.
Nisipozungumza haya kwa UKALI MAWE YATAZUNGUMZA.
Hapa Mhe. Lissu amekasirika kabisa, Jaji anasema kwa upole tuendeleee.
Part 451 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo September 24, 2026
Last time tuliishia part 446 so leo tunaendelea na -;
Part 447
Majaji wameingia Mahakamani na Mhe. Tundu Lissu nae ameingia Mahakamani na kupokewa kwa makofi mengi hapa.
Amepiga kinyaturu na ndugu zake waliopo hapa Mahakamani, amesema NINA KWETU NA NILIAGA VIZURI.
Yupo Mlinzi wa Katuga alikuwa anamzuia Dr. Rugemeleza Nshala kupita kwenye njia. Dr. Amempelekea moto sana na kumwambia anapaswa kuwa na adabu hata kama anajiona yeye ni usalama asimtishe kwa lolote.
Majamaaa haya yana viburi sana yani mtu wa usalama ana ujasiri wa kuingia Mahakamani na kufanya ujinga anaoutaka. Bahati nzuri amejichanganya amekutana na Dr. Nshala hajamlazia damu kabisa.
Anasimama Ajuaye na kuwataja wenzake anaoshirikiana nao na kusema wako tayari kuendelea.
Majaji wanateta kidogo pale juu kidogo na kumuuliza Mshitakiwa kama yuko tayari. Mh. Lissu nae anajibu niko tayari Waheshimiwa majaji akiwa amekaa na anaandika andika pale kizimbani.
Jaji Ndunguru tuendeleee sasa.
Mhe. Lissu anaanza.
Waheshimiwa Majaji nikumbushwe nilipoishia.
Uliishia pale kwenye kesi ya Mbowe.
Sasa Wahehsimiwa Majaji naomba kabla sijasema kuhusu ushahidi naomba niseme kitu muhimu ambacho Mahakama hii ilisema kwenye kesi ya Freeman Aikael Mbowe.
Madhara ya kutofafanua essential elements ambazo zimetajwa kwenye sheria wakati unaandaa hati ya Mashitaka. Ni muhimu hiki nitakachokisoma kiingie kwenye rekodi sawasawa.
Kama nilivyosema Mahakama Hii ilikuwa inajadili kushindwa kwa upande wa Mashitaka ku disclose essential particulars za lawful authority kwamba maana yake ni nini hizo mamlaka halali.
Ukurasa wa 53 wa Hukumu kwenye hiyo kesi ya Freeman Aikael Mbowe ilisema statute must give fair notice or warning to those subject to them. They must guard against arbitrary and discriminatory enforcement and they must not unreasonably guard people .....
Zilinde watu dhidi ya matumizi holela mamlaka ndio sheri zinapaswa kufanya kazi hiyo.
Muhimu zaidi Mahakama hii ilisema yafuatayo; Such statute must be intepreted strictly under the overbread doctrine. Lazima zitafsiriwe kwa umakini mkubwa ili kulinda haki za watu.
Over bread dotrine if the statute is broadly written that it deter free speech then it can be strucked out on its face because of its chill effect. Even if it also prohibit acts that may legitimately be forbidden.
Kama sheria imeandikwa haina limit na inanyima watu haki yao ya kusema Hii Doctrine inasema Mahakama inaweza kuifuta.
Hii overbread maana yake iko kwenye Blacks Law Dictionary 7th Edition.
Mahakama hii kwenye kesi ya Freeman Mbowe ilimalizia kwa kucite Isdory Patrice kwa kusema maneno yafuatayo ukurasa wa 58. The failure to name lawful authority targeted by the utterances prejudiced the first accused in his defence and denies the Court an objective criterion upon which it can evaluate if the the words in question were calculated to achieve the act of conduct said to seditions. In view of the aforesaid the charge was defective.
Nairudia tena. Anarudia tena kusoma Mahakama Kuu ilichosema kwenye kesi ya Mbowe kama ilivyo hapo juu.
Kwa kifupi.. Hati ya Mashitaka inayosema alichochea umma. Umma ni watu wote wa Tanzania Bara, wageni wasio wageni, watoto wachanga. Kila mtu aliyepo Tanzania bara ni umma. Hayo maneno yasipofafanuliwa hakuna namna ya kujitetea. Kwahiyo Mtuhumiwa hawezi kujitetea.
Leo unaambiwa wa Mtwara, kesho kutwa wa Nanyumbu ndo maana Mahakama inasema lazima yafafanuliwe na yasipofafanuliwa hati ya mashitaka ni batili.
Maneno yaliyopo kwenye hati ya mashitaka kwenye shitaka langu imeingiza neno umma halipo kwenye sheria na pili halijalifafanua. Kwasababu hiyo ni hati ya mashitaka batili.
Waheshimiwa Majaji baada ya kusema hivyo nijibu swali nililoliacha jana. Je ushahidi unasemaje?
Ukiachana na kuwa legally defective je ushahidi nao pia unasema nini?
Part 478 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 448
Mhe. Lissu anaendelea kufanya mawasiliano yake ya mwisho (Final submission)
Hapa Nazungumzia ushahidi unaohusu nia ya kuchochea umma iliyoletwa na hawa walionishitaki.
Nia ya kuchochea umma kuzuia Uchaguzi mkuu wa mwaka jana kwanza nilishasema nia yenyewe haipo kisheria hiyo ya kuzuia uchaguzi nitaelezea baadae.
Sasa jambo la kwanza.
Katika mashahidi 17 wa Mashitaka waliokuja kutoa ushahidi ni mashahidi wanne tu ambao walitoa ushahidi kuhusiana na suala hili.
Mashahidi hao ni PW1 George Bagyemu; PW2 John Kaaya, PW16 Amin Mahambana PW 17 aliyepewa jina la gizani la P.
Hao ndio walitoa ushahidi juu ya nia ya kuchochea umma kuzuia uchaguzi mkuu.
Jambo la Pili.
Watatu kati ya hao mashahidi wanne ni Mapolisi, mmoja tu PW17 ndio hakuwa polisi.
Jambo la tatu.
Watatu kati ya hao wanne hawakuwepo kwenye huo Mkutano, hakuhudhuria na mmoja tu PW 17 ndio alikuwepo kwenye Mkutano.
PW 17 ni shahidi pekee ambae ni eye witness katika mashahidi wote 17 aliyeona na kusikia yaliyotokea kwenye Mkutano. Wengine wote sio eye witnesses, wameona mitandaoni.
Hayo mambo matatu ni muhimu kama nitakavyoonesha shortly.
Huyo PW 17 sio tu aliona na kusikia ndo aliyerusha Matangazo. For now it suffices to say PW 17 ni mwandishi wa habari aliyesema kuwa alirusha matangazo kwenye mtandao wa Jambo TV.
Waheshimiwa Majaji kesi ya Upande wa Mashitaka imejengwa kwenye nini?
Kesi yao imejengwa kwenye ushahidi wa PW 1, PW 2 na PW 16. Hao Mapolisi ambao hawakuwepo kwenye mkutano. The theory of the case is built on their Evidence, what is this theory of the case.?
Dhana ya kesi hii ni kwamba Mimi mshitakiwa nilichochea umma kwa kuzungumza maneno yale yapo kwenye hati ya mashitaka kwa lengo la kuitishia Serikali kwasababu moja tu. Serikali ndio inasimamia Sheria za nchi na kwasababu Uchaguzi upo kwa mujibu wa sheria basi niliitishia serikali.
Hiyo ndio dhana yao. That is their theory. Ukiuvuruga Uchaguzi unakuwa umeitishia serikali. That is entire basis of this case.
Hiyo nadharia imetokana na ushahidi wa hawa Mapolisi watatu.
Tuanze na PW 1 George Bagyemu Waheshimiwa Majaji PW 1 ndie aliyepewa taarifa kwamba kuna video ina maneno ya kijinai na alipewa taarifa na PW 2. Tar. 04/04 siku moja baada ya ule mkutano.
Kwenye ushahidi wake PW1 alisema nini juu ya nia ya kuichochea serikali. Ukurasa 146 wa rekodi. Anazungumzia kilichomfanya aamini kuna nia ya uhaini.
The factors which led me to conclude it was a treason offence is
"The accused words that atahamasisha uasi, atavuruga sana, atazuia uchaguzi, atakinukisha sana sana, atakinukisha vibaya sana"
Hicho ndio kilimfanya askari Polisi George Bagyemu kusema ule ni uhaini.
Kwa maoni yake akasema pia These words were communicated with the intention of threatening the Executive.
Akaendelea kusema I say so because the election is held as per constitution and the law.
Akaendelea kusema The Executive Enforces the Law. He intimidated the Executive for the purpose of violating the Law which it enforces.
Kesi yote ipo hapo.
Mtakumbuka kwamba PW 1 was subjected to weathering cross Examination.
Kwenye Cross Examination PW 1 alisema kwamba sio kusema alikiri kwamba kwenye hayo maneno hakuna neno SERIKALI wala hakuna Serikali ya JMT, Wala Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Hakuna Rais wa JMT Samia, wala Makamu wa Rais, Isdory Mpango, wala Mkuu wa Mkoa Chalamila na zaidi ya hayo hakuna maneno Halmashauri ya Jiji Dar es salaam Temeke au Ubungo.
Na kwa maneno yake alisema no desgnation of any Executive leader mentioned by the treason words kwahiyo hiyo serikali wanayosema ilitishiwa hiyo Serikali yenyewe haipo na viongozi hawapo.
PW 1 licha kusema Serikali haipo lakini alisisitiza words to EXECUTIVE was intended to be intimidated.
Alisema yafuatayo kwenye ukurasa wa 166 wa record when a person says kukinukisha sana he commits Treason.
Part 449 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 449
Mhe. Lissu anaendelea kufanya mawasiliano yake ya mwisho (Final submission)
Anasema Shahidi huyo akaendelea kusema the words kukinukisha sanasana, vibaya sana are not provided in section 39(2)(d) of Penal Code lakini uchaguzi unasimamiwa na Sheria kwahiyo ni kosa.
Amekubali maneno hayo hayapo kwenye kifungu kinachotengeneza kosa la Uhaini na ukiyasema tu umefanya kosa la Uhaini.
Huo ndio ushahidi mnaoshawishiwa mtoe hukumu ya Kunyongwa? Huo ndio ushahidi wa Uhaini.? Ushahidi wa kunyonga mtu. hawana hata aibu.
Jaji sasa mshitakiwa huko usiende sana
Mhe. Lissu anajibu Perfectly ligitimately mimi kuumizwa na maneno haya kwamba nimekaa ndani kwa mambo haya. Acha niseme.
Anaendelea.
The evidence on record suggest once PW 1 complained ghat words was treasonous kila mtu hadi mawakili wa serikali akili zao zikawekwa mfukoni na wakaamini kila kitu kuwa yale maneno ni uhaini. Hawakuwahi kufikiria vinginevyo.
Alipoamua kuwa huu ni Uhaini hakuna kitu chochote ambacho kingebadili mawazo yake.
Mfano unamuhusu alipoulizwa PW 17 aliyekuwa shahidi wa kuona na kusikia wala hakuona tatizo lolote la kihaini wala kikosaji huyu PW 1 alisema yafuatayo;
Ukurasa wa 169 alisema hivi it is true that in his statement P ndio PW 17 said you were discussing challenges facing you in your constituency he were also said you were airing up your police of no refomrs no election. I read his statement and decided to open up the treason case. It was me who ordered the open up of the file of treason case.
Ni kweli P alisema mlikuwa mnajadili sera yenu ya no reforms nimesoma maelezo yake na nikaamua kufungua kesi ya Uhaini. Ni mimi ndie niliyeamua kufungua file la Uhaini baada ya kupitia ushahidi wote. Kielelezo D16 ndio maelezo ya PW 17. Hayo maelezo hayajasema kulikuwa na kosa lolote.
Huyu Polisi amesoma maelezo ya shahidi wake na kwa vile alishaamua kuwa ni uhaini huu akasema fungua file la Uhaini. Nothing was going to change him. Alipoulizwa baada ya mimi kumuhoji sana. Katuga alimure examine.
Kwamba unasemaje kuhusu hayo maneno yanaweza kuicover serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa vile alishasema serikali haipo sasa ukurasa wa 176 majibu yake yakawa hivi.
The words quoted contexually reffred to Executive. Kwa muktadha wake sio yanasema ila muktadha.
Muktadha ni intepretation, akaendelea kurudia ile Mantra yale maneno unasema kila siku Baba yetu uliye mbinguni.
Kwamba Serikali inasimamia Sheria na uchaguzi unaendeshwa kwa katiba.
Election is held as per law and Constitution and the Executive is the only arm enforces the law. The word Executive exists.
Kwenye maneno tunayolalamikia hayapo lakini yapo. Contexually. Na baadae tukaambiwa constructive. Kisichokuwepo kinaletwa.
Huo ni ushahidi wa PW 1. Na aliposema hayo huo ndio ukawa msimamo wa kila Polisi aliyekuja hapa kutoa ushahidi.
Pw1 testimony set the tone for the three other police witness. For the two sio three.
Yeye PW 1 aliposema kwamba maneno yale ya uhaini kila polisi alisema hivyo hivyo. Ushahidi wao ulifanana kama sare zao za Polisi.
PW 2 alisema hivi, I construed the words tutaenda kuzuia uchaguzi kwasababu tunasema tutaenda kuhamaisha uasi as contain elememt of criminality because th election is conducted according to the constitution and the law.
Therefore kuharibu uchaguzi obstruction without comply to the law manifest the intention to intimidate the Executive which is the principle enforcer of the law and maintainer of peace...
Hayo maneno kwamba uchaguzi unaendeshwa kwa katiba na Serikali ndio inasimamia sheria ni maneno yaleyale kutoka kwa George Bagyemu. Ukurasa wa 183 uko hivyo.
Kwasababu ilishakuwa artice of faith huyo PW 2 kwenye cross examination PW 2 hakubadilika ndio yakawa majibu yake kwamba ni uhaini kwasababu uchaguzi upo kikatiba na serikali inasimamia kwahiyo umeitisha.
Part 450 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 446
Halafu baadae ndio wanasema kutishia Serikali. Hili lengo lao la kuzuia uchaguzi halipo lengo kama hilo kwenye sheria za nchi yetu.
Clearly on this ground too nimeshitakiwa kwenye kitu ambacho hakipo Kisheria. Waheshimiwa Majaji tatizo la tatu la hiyo charge sheet ni hii inayoitwa sheria ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Maana naambiwa nimewachochea watu waitishie.
Swali hili ni muhimu lijibiwe kwasababu nilizosema zimeelezwa kwenye isdory patrice. Reason to disclose particulars so that the defence could prepare their own defence.
Hili sio jambo rahisi kama walivyodhani hawa Upande wa Mashitaka.
Hiyo Serikali imeelezwa kwenye Katiba ya Nchi yetu. Hilo neno Serikali ya Jamhuri ya Muyngano wa Tanzania. Sura ya Pili ya Katiba inaelezea hiyo serikali ya JMT.
Hiyo Serikali ni pamoja na watu wafuatao Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na viongozi wengine hadi watendaji wa vijiji na kata huko chini kabisa ni Serikali.
Ukisoma ibara ya 59 DPP pia ni Serikali na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Baraza la Mapinduzi Zanzibar ni Serikali na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar nayo ni Serikali. Sura ya 6 yote ya Katiba nayo ni Serikali.
Waheshimiwa majaji sura ya nane inahusu local governments nayo ni Serikali. Waheshimiwa Majaji sura ya 9 majeshi ya ulinzi Polisi, Magereza, JWTZ hiyo nayo ni Serikali.
Ili kuonesha kwamba sizungumzii off my head naomba angalieni ibara ya 151 ya Katiba hii ni pamoja na serikali ya Muungano, ile ya Zanzibar na mtu yeyote anayetekeleza majukumu yake.
Kwahiyo upande wa mashitaka walitakiwa kuniambia from the President to village executive officer. Hao watendaji wa vijiji should have disclose in the information hiyo Serikali iliyotishiwa ni ipi?
Rais, Waziri Mkuu, Makamu wa Rais, Mapolisi au ni nani? Nilimtishia nani haswaa? Mwenyekiti wa Kijiji gani hicho niliyemtishia?
Sasa Wahehsimiwa Majaji katika mazingira hayo hii hati ya mashitaka hii information ambayo inazungumzia public wakati sheria inasema tk instigate person or group of person, hati ambayo haisemi who is this animal Executive?
Isdory Patrice imesema you must provide particulars how can it be in light of the case of Freeman Mbowe na Isdory Patrice.
Nafahamu Freeman Mbowe ni maamuzi ya Mahakama hii haiwalazimishi lakini alisema ili kulinda haki za watu ni lazima watoe particulars ili kosa lieleweke kwa mtuhumiwa.
Nimejulishwa kwamba saa 11 imefika. Kesho nataka nizungumzie ushahidi ulioletwa kuhusu jambo hili.
Kwahiyo nitaendelea kesho.
Ajuaye anasema kuwa tuendelee kesho lakini mshitakiwa azingatie huo muda wa siku mbili uliobaki.
Mh. Tundu Lissu anasimama kuwa hili sio suala la kwangu pia ni majaji pia. Hii ni kesi ya adhabu ya kifo. I must defend myself with all what i have.
Nb. Wao wamepoteza muda mwaka mzima kwenye hii leo inawauma Lissu kufanya final submission hadi kesho na siku yote ikakamilika? Majaji wanateta na watu wanasonya humu wamekerwa na kauli ya Ajuaye. Majaji wanateta pale juu.
Jaji: Tunasisitiza huko Mwanzoni kuwa wakati sisi tunaendelea na shauri hili tunaobserve utulivu kwamba tusipige makofi sana wakati watu wengine wanapotumia Mahakama hii na shauri linaahirishwa hadi kesho saa tatu asubuhi.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 445
Mhe. Lissu anasema kwenye kesi niliyoisema ya Uhuru ya Amin Son of Mrisho 1971 alipatikana na kosa la kawaida la wizi. Akahukumiwa kwa kosa lililopo kwenye minimum sentence act. Mahakama kuu ikasema HAPANA. A penal statute must be stricly construed unless expressly provided by the law and charged for it.
Usipomuhukumu mtu kwa kosa hilo huwezi kumshitaki kwa kosa hilo. Stricly construction of the penal statute inalinda uhuru wetu raia. Hawa wanaotutawala tukiwaachia magereza yatajaaa. Watasema umechochea umma wakati sheria inasema hakuna kitu kama kuchochea umma.
Waheshimiwa Majaji naomba nipendekeze uamuzi wa Mahakama hii kwenye kesi ya Freeman Aikael Mbowe and 7 others vs Jamhuri. CA/2020 Ni muhimu kwa Precedent na muhimu kwa ushahidi wa kesi hii.
Proof ni hii kesi ya Freeman Mbowe and 7 others for the purposes za kisheria. Sio umuhimu wake wa kuonesha namna wapinzani tulivyoonewa.
Kuanzia ukurasa wa 52 hadi 59 Jaji Mugeta. Facts were that the appellant were charged of making statements which caused hatred to lawful authority of the governemnt.
Na maneno waliyosema pia lawful authority ni kitu gani?
Mahakama hii ilisema Lawful authority kwenye shitaka la aina hiyo the prosecution must specify what is the lawful authority targeted?
Lazima upande wa mashitaka wafafanue hicho kinachoitwa lawfual authority ni kitu gani?
Kwenye kesi hii hii ya Freeman Mbowe ilicite the decision of the Court of appeal in Isdory Patrice Supra. Na ikasema kwenye Isdory Patrice Mhakama ya Rufani the prosecution must always provide particulars to eneable the accused person to prepare his defence.
Na Mahakama ya Rufani ilisema hati ya mashitaka isipotoa hizo particulars basi ni shitaka batili. Na kwa Freeman Mbowe shitaka waliloshitakiwa nao lilikuwa batili ndio Mahakama hii ilisema hivyo. Hawakuambiwa Lawful authority ni kitu gani?
Sasa waheshimiwa Majaji kuna sababu mbili zinazofanya the information iliyopo Mahakamani kwenye kesi hii kuwa na makosa yale yale ambayo mahakama hii iliyaona kwenye kesi ya freeman mbowe na Isdory Patrice.
Sababu hizo mbili za kusema shitaka hili ni batili ni hizi zifuatazo:
1. Sababu ya kwanza ni ile ambayo nimeielezea kwa kirefu kuwa sec.39(2)(b) haijasema kuinstigate memebers of the public bali imesema a person or members of the public. interm of Bahame Sitta amd Isdory Patrice.
2. Sababu ya pili ya kwanini shitaka ni batili vilevile nimezungumzia kuwa hilo neno public ni pana sana na hati ya mashitaka haijadisclose hiyo public ni ipi? Walioko vilabuni, sokoni au eneo lingine lolote. Walitakiwa kuniambia.
Kama hawajafanya hivyo basi kosa ni batili na shitaka ni batili hili.
Linakiuka hiyo principle ya legality la uhalali wa kosa kisheria.
Kwahiyo Waheshimiwa Majaji katika suala hili la tatu on these third issue on the first limb ya to instigate any person or group of person is NEGATIVE. Sijachochea mtu wala kikundi cha watu.
Hakuna kitu kama kuchochea umma.
What about the second limb of this issue?
Sehemu hii inasema hivi lengo la hiyo instigation. Shitaka linasema nilichochea umma kwa nia ya kuzuia uchaguzi mkuu.
The objective ya huo uchochezi wa umma ilikuwa ni kuzuia uchaguzi Mkuu. Sasa Sheria inasemaje?
Kuhusu hiyo intention to instigatigate sheria inasema any person who form intention to instigate person or group of person .......
Hapo inasema lengo ni INTIMIDATION TO EXECUTIVE.
The intention to instigate person or group is to effect the intimidation of executive.
Mimi nimeambiwa nimeinstigate umma kuzuia uchaguzi.
Sheria inasema nimeinstigate umma kuitishia Serikali.
Narudia tena for effect.
Waheshimiwa Majaji nimesema shitaka ni muhimu kulisoma the accused person forms an intention kuwezesha kuzuia uchaguzi mkuu wa 2025.
Sheria inasema unachochea mtu au kikundi cha watu kuitishia Serikali na sio kuzuia uchaguzi Mkuu
Part 446 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 444
Mhe. Lissu anaendelea anasema
Waheshimiwa Majaji sheria inasema unachochea mtu au kikundi cha watu.
Mtu inajulikana sasa what is a group of persons? Natumia oxford advanced learners dictionary group means a number of leople who are together in certain place and connected in certain way.
It is not all. Watu wote hawawezi kuwa group of people. A group may be defined as a subset of all.
Nimeshitakiwa kwa kitu ambacho hakipo kisheria, sheria iko very specific.
Hili kosa lilivyokuwa drafted haiwezi kujibika. Hakuna mtu anayeweza kujitetea kwa watu wa namna hii. Wageni na wasio wageni walioko nyumbani kwao na wanaotembea. It is incapable of being defended.
Hii kesi haipo kwenye kifungu cha 39(2) cha Penal Code.
Waheshimiwa Majaji kwasababu ya upana wa hilo neno Public hilo neno Umma. Upande wa Mashitaka walikuwa na wajibu kisheria ku specify huo umma ni upi kwenye hati yao ya Mashitaka.
Ili kumuwezesha mshitakiwa kuandaa utetezi wake the orosecutio had a duty to specify what exactly that public alleged is? They did not so specify. In fact they had a duty to charge me to instigate a persons or a group of persons.
Wameleta mashitaka ambayo hayapo kwenye sheria.
Sasa turudi kwenye the first principle. Nilisema kitu kinachoitwa kosa la jinai ni kile kilichokatazwa na sheria. Sect. 5 an offence is an act attempt or an omission punishable by law.
Ni kitendo, jaribio au omission ambayo imetolewa adhabu na sheria. Kifungu cha 39(2) kimetengeneza kosa la Uhaini kwahiyo mtu anyechochea mtu au kikundi kuitishia Serikali.
Sheria haijatengeneza kosa la kuchochea watu wote yaani umma. Haipo hiyo.
Hakuna sheria inayosema ukichochea watu wote inasema mtu au kikundi kwahiyo nimekaa jela mwaka na nusu kwa kitu ambacho hakipo kwenye sheria za nchi hii.
Waheshimiwa Majaji ibara ya 13(6)(c) ya Katiba yetu inasema "ni marufuku kwa mtu kuadhibiwa kwa kitendo chochote ambacho alipokitenda kilikuwa sio kosa chini ya Sheria"
Nimeshitakiwa kwa kuchochea umma lakini hakuna sheria inayosema kuchochea umma bali inasema kuchochea mtu au kikundi cha watu. Nimekaa mwaka mzima kwa kitendo ambacho wala sio kosa.
Waheshimiwa Majaji nilisema PGO O. I para. 25 inasema crimes are actions defined as such by the laws.
Makosa ni matendo ambayo sheria imeyatamka kwamba matendo haya ni makosa. Kama sheria haijatamka kwamba tendo hili ni kosa. Haiwezi kuwa ni kosa kabisa.
Waheshimiwa Majaji kesi ya Bahame Sitta inaeleza kuhusu jambo hili.
Mahakama ya Rufani ilisema ilizungumzia principle of legality na ikasema kwamba
Walitumia Latin Marxim kwamba Nullum Crimen Sine Lege kwamba a person should not serve criminal punishment unless that act punishable by the law.
No one should be punishable by an act which is not punishable by the law at the time committed.
Kwenye kesi ya Bahame Sitta. The Appellants walishitakiwa kwa kuingia kwenye hifadhi ya taifa kinyume cha Sheria illegal entry into a National Park. There was no such offence. You cannot charge people on non existed offence.
Ninakabiliwa na kosa la jinai waheshimiwa Majaji ambalo ibara ya 28(4) ya Katiba kuwa Uhaini kama unavyofafanuliwa na sheria utakuwa ni kosa la juu kabisa ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Uhaini kama unavyofafanuliwa na sheria ni ule uliofafanuliwa na kifungu cha 29 cha kanuni ya Adhabu na 39(2) nilioshitakiwa nao mimi umesema ni uhaini gani napaswa kushitakiwa nao hili la kusema nimechochea umma sio kosa lililopo kwenye Sheria.
Waheshimiwa Majaji wakati nazungumzia principles nilisema kwamba penal statute must be construed stricly in favour of the accused.
Nilitaja kesi ya Rex vs Mwanangomeni. Sheria inasema wanawake hawatakiwi kulipa kodi ya kichwa. Na Mwanangomeni alishitakiwa kwa kutolipa kodi ya kichwa.
Mahakama kuu ya kikoloni ikasema penal statute must be construed strictly. Haiwezi kuwa kosa. Hiyo ilikuwa miaka 93 iliyopita. Wakati wa Ukoloni.
Part 445 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 443
Mahakama imerejea.
Mhe. Lissu anaulizia alipoishia.
Jaji Ndunguru anamkumbusha.
Sasa kwenye hiyo quotation naomba muweke kwenye blacket kuwa the same position was taken in the case of Mahomed Matura supra and in Marano Slaa Hofu.
Waheshimiwa Majaji kumalizia hiyo issue ya contradictory testimony of the prosecution witness. Kwasababu hizo contradictions na inconsistences zinahusu jambo kubwa linalohusu ushahidi wa prosecution.
Jambo kubwa la whether the accused person invited the journalist. The effect of this render the prosecution evidence unreliable. Ni ushahidi usiokuwa na thamani yoyote kabisa.
Waheshimiwa Majaji what about the defence testimonies on this issue?
Ushahidi wa utetezi umefuta shaka yoyote juu ya mshitakiwa kuwaalika waandishi wa habari kwenye mkutano wa tarehe 03/04/2025. Kama kulikuwa na doubt anywhere kwamba mshitakiwa alihusika.
Hiyo shaka haipo tena kutokana ba ushahidi wa utetezi. Ushahidi wa mashahidi wote wa Utetezi without exception unasema kwamba waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo walialikwa na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema Brenda Rupia.
Upo ukurasa wa 592 DW1, 661 mpaka 662 hui ni wa DW 2, na DW 3 upo ukurasa wa 693, DW 4 uko ukurasa wa 800 wa mwenendo wa shauri hili. Wote mashahidi hawa walisema aliyealika waandishi wa Habari ni DW 4 Brenda Rupia.
Crucially, that testimony was left intact no cross examination , haukuhojiwa hata mara moja. Hakuwa cross examined at all.
What is the effect of not examining on a particular point? Jibu lake lipo katika kesi ya Director of Public Prosecutions vs Justice Lumima Katiti na wenzake 3 CA No. 15/2018 CAT at Dar es salaam page 16.
It is a well known principle of law failure to examine on a material point of law is taken to be admission of the fact in question.
Kuna kesi zingine mbili on that principle. Nyerere Nyague vs R CA no. 67/2010 na Chora Samson alias Kiberiti vs Republic CA 516/2019.
Waheshimiwa Majaji kwa sababu hizi. Jibu la swala la pili je mshitakiwa aliwaalika waandishi wa habari kwenye mkutano huo wa Tarehe 03? Jibu lake ni negative. HAPANA.
The accused did not invite any of the media personnel who attended the meeting.
Kwa ruhusa yenu waheshimiwa Majaji nitaenda kwenye suala la tatu.
Nb. Kumbukeni yako maswali 9.
Je mshitakiwa alitengeneza nia ya kuchochea mtu yeyote au kikundi cha watu kuzuia uchaguzi mkuu wa 2025 kwa lengo la kuitishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?
Waheshimiwa Majaji kwa kesi hii hili ni suala la kufa au kupona kwa kesi hii. Is a question of life or death with regard to a case at hand.
It is one of the central issue of the entire case. Taarifa iliyoko Mahakamani inayonishitaki inatuhumu kwamba nilitengeneza nia ya kuhamasisha umma. Anarudia tena KUHAMASISHA UMMA.
Kuchochea umma kuzuia Uchaguzi Mkuu wa 2025 kwa lengo la kuitishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Waheshimiwa Majaji kifungu cha 39(2)(d) cha Penal Code ambacho kimetumika kunishitaki kinasema.
Mtu yeyote anayechochea mtu au kikundi cha watu.
Kinachochochewa ni mtu au kikundi cha watu.
Shitaka dhidi yangu linasema nimechochea umma. Waheshimiwa Majaji kifungu cha 39(2)(d) hakuna umma kuna mtu au kikundi cha watu.
Sasa Waheshimiwa Majaji hiki kinachoitwa umma ni kitu gani?
Kanuni ya adhabu imetoa tafsiri ya kimachoitwa neno umma. Public means kwa kifungu cha 5 Public refer to not only all persons but also to persons using particular place or to such indeterminate person to be affected by persons.
Umma ni watu wote na ni pamoja na watu wanaokaa mahali popote au wanaotumia eneo lolote ikiwemo Bar, Guest au vilabuni na ni pamoja na watu wote ambao huwezi kuwajua. Huo ndio umma ninaodaiwa kuuchochea uzuie uchaguzi.
Part 444 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 441
Mhe. Lissu anaendelea kufanya mawasiliano yake ya mwisho (Final submission)
Waheshimiwa Majaji ushahidi huo wa DW2 umeungwa mkono na DW3 na DW4 yaani Amani Golugwa na Brenda Rupia ambao ni Naibu Katibu Mkuu Bara na Mkurugenzi wa Habari hawa ndio maafisa wa Chama walioandaa huo Mkutano.
Hii tuhuma kuwa ni mimi ndio niliandaa mkutano ni tuhuma ya uongo na ninachoweza kusema kwa upole ni kwamba haijathibitishwa kabisa. Na nikisema hivyo nasema kwa upole.
The answer to the first issue must necessarily be answered in negative. Jibu la swali la kwamba mtuhumiwa ndio aliandaa mkutano huo jibu lake ni HAPANA. Sio mimi niliyeandaa huo mkutano.
2. Naomba niende kwenye issue ya pili sasa.
Ni je ni mtuhumiwa ndie aliyealika waandishi wa habari kwenye huo mkutano wa Tar. 03/04/2025? Ndio swali linalopaswa kujibiwa.
Waheshimiwa Majaji suala hili pia ni muhimu sana kujibiwa.
Kama lengo la mkutano lilikuwa la kihaini kualika waandishi wa habari ili waje wacover huo mkutano basi hicho ni kitendo cha wazi yaani overt act.
Hivyo na waandishi wa habari waliokuja kwa mwaliko wangu wanakuwa accessory after the fact. Washirika wa kosa na misprision of treason itakuwa inawahusu. Hawawezi kupona kwenye kosa hilo.
Hii tuhuma sio ya bahati mbaya na haijaletwa bure ina lengo la kuthibitisha an overt act kwamba wakithibitisha overt act wanathibitisha kosa la uhaini. It is not innocent at all.
Waheshimiwa majaji tuhuma ya kwamba mimi ndio niliyealika huo mkutano ipo kwenye ukurasa wa 131 wa record za Mahakama Hii (Court Proceedings) mkiangalia walichokileta waendesha mashitaka kwenye preliminary hearing hawakusema clearly kwamba mimi ndie niliyealika waandishi wa habari. Kwenye hayo maelezo ya ziada.
The only say members of the media they were invited. Hawakusema walialikwa na nani?
Waheshimiwa Majaji i take it that not mentioning person of the media it was not dental to innocent haikuwa bahati mbaya na haikuwa innocent. Ilikuwa na nia mbaya na haikuwa innocent.
Wakati wa ushahidi walileta mashahidi wa kusema mimi ndio niliitisha waandishi wa habari. Mimi ndio nilialika hao waandishi wa habari.
PW 1 George Bagyemu alisema hivi wakati anaongozwa kwenye ushahidi wake ukurasa wa 147 wa rekodi. Alisema on this particular point said "Ni mtuhumiwa aliwaalika waandishi wa habari ili hotuba yake iweze kusikilizwa na watanzania na wasio kwenye jambo tv channel" kingereza mlichosema " accused person imvited journalist so that his speak to be heard by Tanzanians and non Tanzanias..
Waheshimiwa Majaji ushahidi wa PW 1 kwenye hoja hii uliungwa mkono na PW 2 Insp. John Kaaya kuhusu hoja hii angalia ukurasa wa 210 na 221 za rekodi ya Mahakama hii.
Waheshimiwa Majaji mtakumbuka nilimuhoji sana PW 1 and on this particular point alisema it is true that is you who imvited the journalist and i dont know the means used to invite them.
Jaji leo hatuna break?
Mhe. Lissu namalizia tu hapa.
Alijibu kuwa sijui ulitumia njia gani kuwaalika lakini ninachojua ni wewe uliyealika waandishi wa habari ukurasa wa 161 na ukurasa wa 210 na 221 PW2 nae aliunga mkono mambo haya.
Ushahidi wa PW1 na PW 2 ulipingwa na PW 16 na PW 17. The testimony of PW 1 and 2 was flately contradicted by the testimony of PW 16 and 17. Ulipingwa moja kwa moja na hao mashahidi wengine.
PW 16 Amin Mahamba ndie alikuwa mpelelezi mkuu wa kesi hii. Alisema yafuatayo kuhusu nani aliyealika waandishi wa Habari na ukurasa 467 wa rekodi. Anasema hivi
"P and P1 they said they instruxted by the director to go and record and live strim the accused speech meeting. John Marwa was informed and invited by director of information and publicity of Chadema Brenda Rupia"
Part 442 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 442
Mhe. Lissu anaendelea kufanya mawasiliano yake ya mwisho (Final submission)
Hao Waandishi wa Jambo TV aliyekuja kutoa ushahidi na yule ambae hakuja walipata taarifa kutoka kwa John Marwa aliyeambiwa na Brenda na niliwauliza kuwa mimi ndie Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa CHADEMA wakajibu Tundu Lissu sio Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Chadema.
Waheshimiwa Majaji kwa upande wake PW 17 alisema nini for his part a protected witness who testified named P as PW 17 could not have been clearler about who invited the jouranlist to the meeting
PW 17 said that, ukurasa wa 439 "the information about the meeting was communicated to our director to our director John Marwa by the Chadema Communication Officer it is not true that the accused was the communication officer of CHADEMA.
Alisema pia the communication officer of Chadema is Brenda Rupia na akamalizia kwa kusema it is not correct for someone to say the meeting was organized by Tundu Lissu and that he was responsible for sending out the invitations.
Mtu akisema Mkutano uliandaliwa na Lissu na kwamba ni yeye ndie aliyetuma mialiko kwa waandishi wa habari. Hayo ni maneno ya PW 17. Ukurasa wa 496. Kwahiyo kwenye suala hili tuna hadithi mbili kwenye ulimi wa mashitaka.
Kuna ulimi mmoja unasema mshitakiwa ndio alialika waandishi wa habari na kuna sehemu nyingine inasema sio yeye. Hizi ndimi mbili za mdomo mmoja wa mashitaka ni kama ndimi za nyoka. Nyoka ana ndimi mbili.
Ni ulimi upi Mahakama hii iende nao? Wao upande wa mashitaka walipaswa kuwa na ushahidi wa aina moja.
Ni upande gani kati ya PW 1 na PW 2 au ule wa PW 16 na PW 17 tuuamini? Hasa kwenye suala crucial ambalo wao wamelileta kwamba mimi ndio nilialika waaandishi wa habari.
Kesi ya Said Hamis Adam Supra. Mahakama ya Rufani Tanzania ilisema kwenye ukurasa wa 11 Jaji Lila alisema "it is now settled that descrepancies and contradictions in the evidences of the witnesses are the bases for a finding of lack of credibility.
Ndimi mbili za aina hii hakuna ubishi tena ni uthibitisho kwamba huo ushahidi hauaminiki.
Waheshimiwa Majaji hii mikanganyiko ya upande wa mashitaka katika suala hili sio mdogo. Sio minor unahusu issue itself nani aliyealika waandishi wa habari?
Huo mkanganyiko wa suala lililotolewa ushahidi the contradictory is not minor or inconsequencial . The my are the major and they gk to the root of the issue on whether the accused invited the media personnel to the meeting. Sio jambo dogo kabisa.
Mahakama ya Rufani ilisema yafuatayo ilisema kwenye kesi ya Makonyo alias Kibona. Kwamba hii contradiction ni ndogo au kubwa ilisema hivi:
Mahakama ya Rufani ilisema ukurasa wa 26
"The law on inconsistent and contradictions is that where a part rises an issue that they were inconsistencies or contradictions in the evidence implicating him the duty of the trial court is to address the contradiction and determine whether they are minor or major contradictions. If the Court makes a finding that the contradictions are minor and inconsequential, it may go ahead to rely on the evidence as tendered. However if it find the inconsistent goes to the root of the case to the extent of shaking its very substractum the trial court shall not take that evidence and credible or reliable."
Mahakama inatakiwa ipime hiyo mikanganyiko na kuamua kuwa ni ya mambo madogo au ni mikanganyiko inayoenda kwenye mizizi ya kesi. Ukiwa ni mkanganyiko wa mambo ya msingi Mahakama haiwezi kuchukulia huo ushahidi ni wa kupuuzwa.
Jaji Ndunguru naomba uishie hapo.
Lissu naomba lisaa limoja na nusu niongee na Mawakili wangu pia nahitaji pia kupumnzisha miguu.
Jaji vipi Jamhuri?
Ajuaye: Hatuna shida.
Jaji basi twende tukapumnzike kwa huo muda tafadhali.
Inapigwa Court tukutane saa tisa kamili hapa kuendelea kula shule kutoka kwa Mh. Tundu Lissu.
Naomba Repost yako.