#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo February 9, 2026
Last time tuliishia Part 150 so leo tutaendelea na-;
Part 151.
Ameingia Mheshimiwa Lissu, zimepigwa kelele nyingi sana hapa Mahakamani ni kelele za Rais! Rais! Rais!
Mhe. Lissu amepiga kombati ya kaki, ameingia kwa vibe sana.
Amebeba makabrasha yake, mavifurushi mengi sana ya vitabu.
Imepigwa sauti ya Courttttt ikiwa na ukali watu hawanyamazi wanaendelea na minong'ono fulani ya kushangilia.
Wameingia Majaji na kuketi eneo lao.
Jaji anasema tuendelee
Karani anasoma namba ya shauri.
Anasimama Renatus Mkude wakili wa Serikali Mkuu, yuko na Ajuaye, Nasoro Katuga, Cathbert Mbiringe, Thawabu Issa wanawakilisha upande wa Jamhuri na Mshitakiwa Tundu Lissu yupo.
Leo tumekuja kujibu hoja za Tundu Lissu kama yeye atakuwa tayari, sisi upande wa Serikali tuko tayari Waheshimiwa Majaji.
Mhe. Lissu anaulizwa uko tayari?
Anasema niko tayari lakini nahitaji kuzungumza mambo yaingie kwenye rekodi za Mahakama.
Niwatakie heri ya Mwaka Mpya nyie Majaji, Mawakili wa Serikali na wote waliopo hapo.
Maswala mawili kati ya matatu ninayotaka kuzungumza nitasema kwasababu kifungu cha 11(1)(2) cha sheria ya magereza nyie majaji ni visiting justices kule magereza.
Majaji wanaodhuru magereza mna wajibu wa kuhakikisha magereza yanaendeshwa kwa mujibu wa sheria na wafungwa iwe wamehukumiwa au mahabusu kama mimi wanapata treatment kwa mujibu wa Sheria.
Na kwa mujibu wa kifungu hicho mna mamlaka ya kutoa maelekezo na mapendekezo kuhusu treatment ya wafungwa na mahabusu.
Sisi tunaoishi huko magerezani tumepewa Haki kwa mujibu wa kifungu cha 48 cha sheria hiyo kuwaeleza juu ya mambo yalivyo na tunavyotendewa huko magereza.
Jambo la 1 ni kuhusu haki ya mfungwa kuwasiliana na Mawakili wake.
Wafungwa wana haki ya kufanya mawasiliano na mawakili au washauri wa kisheria bila kusikilizwa na maafisa wa magereza Kanuni ya 13 ya kanuni za uendeshaji wa magereza GN. NO. 60/1987. (Prison Management Regulations)
Kanuni inasema kila mfungwa atapewa fursa ya kuwasiliana na mwanasheria wake na atakapomtembelea maafisa wanaweza kumuona ila sio kumsikiliza. Anaisoma hiyo kanuni kwa kingereza hapa.
Sasa Waheshimiwa majaji kumekuwa na tatizo kubwa kuhusiana na haki yangu ya kuzungumza na mawakili wangu bila kusikilizwa na maafisa wa magereza.
Muda wote wako pembeni yangu hadi ninapozungumza na mawakili.
Tatizo hili sio jipya lilianza toka niko Kisutu.
Anasimama Nasoro Katuga anasema tulikuwa na concern aliweka pingamizi halijaamuliwa anaanza kusema mengine. Naomba mwongozo katika hili.
Jaji anaandika kidogo.
Anamuuliza Lissu unasemaje?
Lissu anasema kifungu cha 48 nilichosema kinasema ni draw attention yenu sio kuomba chochote. So i'm drawing the attention to you. Mkiona mnachakufanya fanyeni mkiona hamna msifanye. Wajibu wangu ni kuwaeleza kinachoendelea.
Jaji anasema nafikiri uendelee haya madai ya Katuga ameeelewa baada ya jibu lako.
Tarehe 12/11/2025 tulivyoahirisha kesi mambo yakabadilika tena wakili akifika anapelekwa ofisi ya Mkuu wa Usalama wa Gereza na mimi na Wakili wangu tunapelekwa huko huku wakitusikiliza nikiwa nazungumza na kikundi, kuanzia Mkuu wa Gereza, maafisa wengine zaidi ya watano wanatusikiliza wakati sheria haitaki hivyo.
Siku 88 toka kesi imeahirishwa mwaka jana wananisikiliza kila Mawakili wangu wanaponitembelea.
Mimi na Mawakili wangu tukiuliza, tunaambiwa ni Maagizo kutoka juu, Huko juu ni wapi juu mbinguni au wapi? Mungu anajua.
Hilo ni jambo langu la kwanza.
Nimewapa taarifa kwa mujibu wa kifungu cha 48 mtajua chakufanya ili kuhakikisha sheria inalindwa.
Jambo la Pili, linahusu kutembelewa na watu wengine wasiokuwa wanasheria. Kanuni zinasema unaruhusiwa kutembelewa na watu sio ndugu pekee.
Part 152 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako kwenye tweet hii.
Kila nikiiangalia afcon afu nikiwaangalia Tanzania😂 nasikitika ila sijui nasikitika nn ngj tuone kesho. Si tumekubaliana kama taifa tunasaka point 1😂 haya tupeni maelekezo wawekezaji. Ni point moja ya GG au nyau nyau
@Jambotv_ Nini mama raisi mtoto naibu waziri wa elimu mume wa mtoto waziri wa afya. Mtoto wa kiume mratibu wakikosi maalumu😂😂 tukishindwa kuikomboa hiii nchiiii. Bas keki ya taifa wataimega sana
Nimetoka Ukonga kumuona Mwenyekiti, Yuko imara na anawasalimia wote.
Anatoa pole kwa Watanzania wote waliopoteza maisha, familia ndugu na marafiki.
Anatambua watu waliopoteza viungo na kubaki na ulemavu.
Ametoa pole kwa wote waliopoteza mali pia.
Damu ya wenzetu haijamwagika bure na hakuna atakaefunika jambo hili bila uwajibikaji.
Msimamo wa Mwenyekiti uko thabiti, Yuko imara na mwenye afya njema.
“Nimesimuliwa na bado nacheka, kumbe ile tarehe 29 Bashite alikurupushwa mahali, unaambiwa alitimua mbio hata Eliud Kipchoge asingeweza kumfikia.
Akakimbilia ndani ya ambulance nayo ikawa inamkimbiza ikipiga ving'ora kama imebeba mgonjwa 🤣🤣 🤣”
Chezea 🇹🇿Gen-Z #MD9