VIDEO:
Jeshi la Polisi Nchini Tanzania limezingira Kanisa la Ufufuo na Uzima lenye Makao yake makuu Wilayani Ubungo Jijini Dar Es Salaam, linalomilikiwa na Kuongozwa na Askofu Josephat Gwajima ambaye pia ji Mbunge wa Jimbo la Kawe na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM.
Taarifa kutoka kwenye vyanzo vyetu vya habari akiwemo Askofu Dkt.Josephat Gwajima mwenyewe, vimefahamisha kuwa Askari Polisi hao wakiwa na magari zaidi ya matatu, wakivalia kirai na wengine sare za Jeshi la Polisi wamezingira kanisa hilo na wengine wakiendelea kuwahoji baadhi ya waumini wa Kanisa hilo waliokutwa katika eneo hilo la Kanisa wakiendelea na shughuli mbalimbali.
Kuzingirwa kwa kanisa la Ufufuo na Uzima Ubungo Jijini Dar Es Salaam kumekuja muda mfupi mara baada ya uwepo wa taarifa za serikali kulifuta Kanisa hilo, siku moja tangu Kiongozi huyo wa kiroho kutangaza msimamo wake wa kuendelea kukemea na kupambana na vitendo vya utekaji na Watanzania kupotea.
Kulingana na barua ya serikali, sababu ya uamuzi hyo wa Msajili wa Jumuiya za Kiraia Emmanuel Kihampa ni kile kilichoelezwa kuwa Kanisa hilo limekiuka sheria ya Jumuiya sura ya 337 kwa kutoa mahubiri yenye mwelekeo wa kisiasa na yenye nia ya kuichonganisha serikali na wananchi.