Angel Wariael, binti aliyejeruhiwa Oktoba 29, afariki dunia Muhimbili
Dar es Salaam. Angel Wariael,13, binti aliyekuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kutokana na kujeruhiwa na risasi kwenye matukio ya Oktoba 29 akiwa nyumbani kwao Manzese amefariki dunia.
Hospitali imethibitisha kifo chake leo Novemba 18, 2026, kupitia Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano, Irene Charles Mbonde, pamoja na taarifa kutoka kwa mmoja wa wanafamilia.
Katika taarifa kwa waandishi wa habari, Hospitali ya Taifa Muhimbili, (MNH) imetoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na wote walioguswa na msiba huo, ikiwaombea nguvu na faraja katika kipindi hiki kigumu.
Oktoba 31, 2026, The Chanzo, iliripoti taarifa ya Angel na mama yake mzazi kuhitaji msaada ikiwemo wa matibabu kutokana na hali ya afya yake iliyomsababisha kukatisha masomo. Kufuatia taarifa hiyo, alipatiwa msaada na kuanza matibabu Muhimbili hadi mauti yalipomkuta.
@nickyrabit I would say that is suicidal at this point in time😊watu wengi bado wanatumia viswaswadu na hata wenye smartphone asilimia kubwa wana viswaswadu, ongeza na internet yetu inayoweza kukusaliti muda wowote nadhani bado tunaihitaji sana ussd.
@KennedyMmari Na pia kuna hawa wa "wanaume wote ni mbwa"
Unajiuliza kwani huyu hana baba, babu, mjomba, Na wengine wana wapenzi sasa unajiuliza anakuaje na mtu ambae ni hasara na laana au anakuaje na mtu anamtizama kama mbwa🤔