The EPP Group has nominated lawyer, human rights activist and politician Mr Tundu Lissu as a candidate for the Sakharov Prize.
After surviving a 2017 assassination attempt, Mr Lissu returned to Tanzania to continue advocating democratic reform, only to face arrest, treason charges and exclusion from the 2025 presidential election, while his party was barred from participating.
His case reflects the wider erosion of democratic pluralism and political competition in Tanzania.
For the EPP Group, Mr Lissu represents a powerful combination of personal courage, democratic conviction and geopolitical relevance. His nomination affirms that Europe stands with those defending constitutional democracy and political freedom in Africa and in other partner countries of the EU. Mr Lissu embodies the defence of democracy, political pluralism, the rule of law and fundamental freedoms at extraordinary personal cost.
The Sakharov Prize for Freedom of Thought is the highest tribute paid by the European Union to human rights work.
Taarifa hii ni kutoka Kurugenzi ya Sheria na Haki za Binadamu - CHADEMA inaonyesha orodha ya kesi zinazowakabili wanachama wetu maeneo mbalimbali nchini Tanzania. Chukua hatua: baini eneo ilipo kesi karibu nawe, fika mahakamani, na uwape morali wanachama wenzetu. #PeoplesPower
HEPI, unahoji kwanini CHADEMA hawajafika msibani, Kizimkazi? Lakini umeshindwa kuhoji kwanini Dk. Emmanuel Nchimbi hajafika huko Kizimkazi? Unasema “nadhani lipo tatizo kubwa CHADEMA”. Hiki kisabengo unatoa wapi? Yaani ulione tatizo ndani ya CHADEMA ushindwe kuliona tatizo ndani ya CCM yenu ambayo wabunge wake walimuita Makamu wa Rais, YUDA? Wakamburuza kamati ya maadili ya chama na kumfukuza kama kibaka? STULI KAWAIDA anasema alistahili kufurushwa. HEPI, unatafuta kiki kwenye msiba, bosi akuone akutupe kwenye nishati? HEPI, Yu Bera Wochi Yua Baki. Jishikilie.
Kwenye mirathi ambayo sisi Wanaume tunaandika majina yetu hayapo, maana yake maisha yetu tunasaka kwa ajili ya wengine sasa muhimu ukipata hela usisahau KUISHI, usisahau Kujijali maana utaondoka na nyingi utawaachia, ISHI kidogo.
Yaani eti ccm chawa anawaonya Wenyeviti wa mikoa kutoa tamko🤣🤣!!!
Mmiliki wa chawa anachekea chawa wake kuwaonya hao wanaoitwa Wenyeviti wa mikoa!!!!
Nani amemtuma huyu chawa kama sio mmiliki wa chawa?
Iko siku hawa chawa watamshambulia mmiliki kwasababu siku hiyo mmiliki hatakua madarakani..
Uzuri wao ni kwamba wana phd za unafiki mwenye mamlaka ndio Yuko sahihi kwa kila jambo.
Shame on you.
Wizara ya mambo ya ndichi ina~deal na petty issues….badala ya ku~deal na vitu serious.
Waziri una deal na mashalove & Pipitilda
badala ya kulinda mipakani huko zinaingia pombe feki daily zinaenda kuua figo za maelfu ya mahomeboys na dada zetu, ajira zenyewe hamuwapi vijana wanashindwa kumudu dialysis gharama wanapoteza maisha!
Halafu hapo utasema wizara inalinda raia na mali zake!!?🤷♂️
Unazungumzia maadili ya kuongea lugha chafu mitandaoni, USA 🇺🇸 Rais Trump anatukanwa na raia ile F****word tena public kabisa kwenye press na raia haguswi na ndio nchi ina mahospital bora,shule na vyuo bora, umeme & maji havikatiki,barabara safi, na ajira za kutosha!!
Wewe maadili yamekusaidia nini mtu nina bachelor ya Architecture GPA 3.5 na naendesha boda tena ya mkataba mwaka wa nne huu kazi hamna, kwa siku naingiza elfu saba, utasema kuna maisha hapo?
Wewe unaekazania maadili una population ya watu milioni 70, unatangaza ajira elfu 45!!
Sasa kuna taifa hapo?
Simaanishi kama taifa tusiwe na maadili au utamaduni, lakini ni petty issues….. kundi la wale mates wangu walipaswa kuitwa hata basata tu wakamalizana nao chaap kwa, kama wazazi/walezi……easy tu, lakini sio waziri wa wizara!!
Kama tunataka kukemea maadili, tukemee maadili ya utekaji na ufisadi na mauaji ya ndugu zetu, hayo ndio maadili ya msingi na uwaite wahusika uwakemee live tuone kama tulivyoona kwa wale wasanii!!
Unaacha kuwaita askari walioua ndugu zetu october 29 uwakemee na kuwawajibisha, unamuita yule sista du anayeuza jeans, unamuita Nicole….kisa anaonyesha kifua!!?
Nini kifua babu, nchi za wenzetu unakuta striper anacheza uchi kabisa usiku club na mchana ni daktari / nurse anatibu watu na ndio ajira yake na analipa kodi na hela anayotengeneza humgusi….na ana degree kasoma na husikii kaitwa na waziri wala Mkuu wa mkoa! Dunia ndio ipo huko!!
CAG kila mwaka anasoma report wizi wa Billions of bags 💰 na huoni mtu akiwajibishwa…..sasa hayo ndio maadili ya kukemea public tena, sio mtuambie tunamalizana kwenye vikao vya kamati sijui za halmashauri…NO!!
Watu wanatekwa kiholela, wanapotea wanakufa….kila kiongozi anayehojiwa anakataa kuwa hakuna utekaji….husikii hata mmoja akikemea…..then leo wizara ya mambo ya ndani head liner unakaa kikao na GiGi money, Anko T unawakemea na mnalazimisha kabisa iwe news kubwa!!
Yani hukemei mtu anaua watu, unakuja unamkemea gigi kavaa mpasuo!?
Hivi tuna taifa kweli hapa jamani!?
Hii nchi ina maigizo sana!!
“The truth is an offense, but not a sin”
Mwenyekiti Tundu A.M Lissu amenukuu maneno ya Bob Marley & The Wailers kutoka katika wimbo wa ‘Jah Live’ ambao ulitoka mwaka 1975 kufuatia kifo cha aliyekuwa Mfalme wa Ethiopia, Haile Selassie I (kifo chake kilitangazwa 27 Agosti 1975).
Katuga: Shahidi shule si ulikuwa unafundishwa multiple choice?
Mhe. Lissu: Mimi sijafundishwa multiple choice. Mimi nimefundishwa critical thinking. Sheria unafundishwaje multipe choice? Ndio maana unakuwa mjinga.
Kuna hatari leo wakazinesa kavukavu mbele ya Pilato
Nassoro Katuga; Unamjua Julius Ndyanabo?
Tundu Lissu; Namfahamu Julius Ishengoma Francis Ndyanabo namfahamu
Nassoro Katuga; Unamfahamu vipi?
Tundu Lissu; namfahamu kuwa alifungua kesi kupinga sheria ya uchaguzi kupinga kifungu cha mtu aliyekuwa anapinga uchaguzi kulipa fedha na alishinda
Nassoro Katuga; unamfahamu Mtikila?
Tundu Lissu; namfahamu
Nassoro Katuga; unafahamu nini kuhusu kesi ya mgombea binafsi?
Tundu Lissu; Christopher Mtikila alifungua kesi ya mgombea binafsi akaishinda serikali na Serikali ikaenda mahakama ya rufani akaenda Mahakama ya Afrika akashinda na serikali unayoitumikia mpaka leo imekataa kutekeleza hukumu ya Mahakama ya Afrika
Baadae baadae hapo tutaanza kuona Hashtag za Flani anafaa kuwa Msaidizi mpya, Flani anafaa kuchukua makablasha au Flani anafaa kuchukua Vibuyu
Hakuna anayefaa wajomba kama mifumo bado ni ile ile
Nchimbi hakuomba radhi na/au kuwapa pole Watanzania kwa serikali yao kuuwa maelfu, kutesa, kupoteza na kuwapa kesi za uongo.
Mamlaka ilikuwa muhimu kwake vs our collective good.
Leo ni victim wa mfumo alioulea, hana hakika na usalama wake.
A good road is good for all of us!
Wafuasi wa MBOGAMBOGA wenyewe wamechanganyikiwa kama raia wengine tu. Hata wao hwaelewi mambo yanayotokea. Wanashangaa mtandaoni tu. Mambo ni mzobe mzobe. Ipo hivi, hamuwezi kuua watu wengi kwa kiwango kile halafu mkatawala watu kwa amani na utulivu. Damu za watu zitawatesa sana.
Kuna jamaa anafanya “boys mentorship camp” pale Chugga namkubali sana. Ukiwa na boys above 8 peleka huko wakajifunze namna ya kujitegemea na kua wanaume. Safi sana 👊🏿
Tundu Lissu; Kwa hiyo Waheshimiwa Majaji hakuna afisa yeyote wa Serikali ambaye hawezi kupelekewa summons. Wala siyo Rais wala siyo Makamu wa Rais Mstaafu wala siyo waziri Mkuu Mstaafu wote hao wanawajibika mbele ya Mahakama.