Kwenye Maisha ya MwanaDamu,Usingizi mzuri ni ule uliolala kwenye Tumbo la Mama yako;Huu wa Duniani Tabu tupu
Maisha ni Vita,lakini pia ni zawadi.Changamoto ni sehemu ya Safari,si mwisho wa Safari.
Mtegemee Mungu ili upate Amani ya Moyo
Hakuna Mafanikio makubwa ya kusimulia Bila Uthubutu
Watu wengi wanapenda kusikia Hadithi za Mafanikio,lakn husahau kua nyuma ya kila Ushindi kulikua na kipindi cha Hofu,Mashaka na Hatari
Watu wanaosimulia Hadithi za Ushindi Leo ni wale waliokua tayari kuhatarisha kushindwa Jana
Ukitaka kuishi na watu vizuri mtaani;
1. Lipa deni lako kabla hujadaiwa.
2. Usilazimishe urafiki
3. Ata kama uko busy kiasi gani hakikisha unapata muda wa kushiriki matukio ya kijamii mtaani kwako( Misiba na N.k)
Unapokaa Muda mrefu sana kwenye Eneo lako la Mazoea,Unaweza usione Hatari yake Sababu linaonekana Salama.Lakn linaweza kuua Ndoto zako
Maisha hubadilika pale unapoThubutu kufanya jambo ambalo hujawahi kufanya
Fanya kile unachoogopa kufanya lakn unajua ni muhimu kwa Ukuaji wako
Kuhusu wewe ni jukumu lako.
Usipotaka huwezi kupata,
Usipojifunza huwezi kuelewa,
Usiposikiliza huwezi kusikia,
Ukiamua inakuwa usipoamua haiwi,
Kila kitu kinaanza na wewe mwenyewe.
Pesa hupenda watu wanaojifunza kuuza.
Kuuza bidhaa.
Kuuza huduma.
Kuuza idea.
Hata kuuza confidence yao wenyewe.
Ukishindwa kuuza, dunia itakuuzia umasikini kila siku.
Unaweza kuwa na vigezo vyote vinavyotosha kupewa heshima na hadhi ya juu lakini ukakosa kitu kimoja tuu ambacho kitakufanya ujihisi hauna thamani, kutokupendwa.
Maji yakijaa Duniani, hakikisha Mtumbwi wako hauzami.
Usiweke nguvu nyingi kulalamikia hali ya Dunia, weka Nguvu nyingi kuhakikisha Maisha yako hayaangamii kwaSababu ya Hali hiyo.
Kuna a bible verse nimeisahau, watu walimuomba Mungu apigane vita yao, nae aliwajibu, nendeni mkam face adui nami nitawapa nguvu ya kumshinda.
Mungu anataka akukute kwenye mchakato sio umekaa kaa tu kama mbuzi.
Ishi kwa Uwezo wako wa Leo huku ukijenga Uwezo mkubwa wa Kesho
Kila hatua ya Maendeleo ina wakati wake. Hakuna haja ya kuharakisha kuonekana umefika wakati bado unajenga msingi.
Ukiridhika na Uwezo wako wa sasa huku ukiendelea kukua,Utaishi Maisha yenye Furaha na Utulivu zaidi.
HAPPY BIRTHDAY Malkia Wangu, Moyo Wangu unaotembea Nje ya Mwili Wangu, Movie kali niliyo wahi kuiona kwenye Maisha yangu nikukuona wewe unavyo kua …Dad’s Little Angel ❤️❤️❤️.Mungu anakubariki sisi tuna kulea.
Ukubwa ni Pamoja na Kutunza Siri za Mtu Ambae Hamuongei Vizuri Kama Awali
Mwenye Hekima hulinda Siri alizoaminiwa Jana,Hata kama Leo si Rafiki Tena wa yule aliyemwamini.
Uaminifu wa kweli hupimwa Hata baada ya Urafiki wenu kupita.
Pesa ni Matokeo.Akili ndio Mbegu,Ukipalilia Akili yako vizuri,Mavuno ya Pesa yataifuata
Chanzo kikubwa cha Utajiri si Pesa ulionayo mfukoni,Bali ni Mawazo,Maarifa,Ubunifu,na Uwezo wa kutatua Matatizo ulionao Akilini
Ongeza Thamani Akili Yako,Uwezo wa kutengeneza Pesa uongezeke.
Maisha ni kama mfululizo wa kutatua matatizo.
Unapokuwa unamalizana na moja, jingine tayari linafanya warm up😃
Tofauti si kukosa matatizo, bali kujifunza kuyakabili kwa hekima, uvumilivu na moyo wa kusonga mbele.🤛🏼