Ukiwa kwenye mahusiano yawe ni urafiki au mapenzi halafu sio two way traffic (give and receive) mpaka unaonekana kama unajipendekeza ni bora ukala kona tuu.
Maisha yenyewe mafupi haya.
Kwenye circle yetu kuna watu uwa wanatupiga tuff kila mara tukikwama.
Tujitahidi tusiwe tunawatafuta tukiwa na shida pekee, tuwajulie hali, tuwashirikishe mipango yetu na kupeana uzoefu, pia siku moja moja kama upo vizuri, you do something for them out of your pocket.
Sisi #wanaume ni kama chumvi ikitajwa basi imezidi, imemwagika, imeisha, imepungua au haina madini joto. Umuhimu wetu huonekana zaidi tusipokuwepo au tusipotimiza wajibu wetu. Tusipotajwa tajwa haina maana hatuthaminiwi bali ni kwamba matarajio juu yetu ni makubwa. #MenDay19Nov