"Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wote wawajibike, au kuwajibishwa na mamlaka zao za uteuzi. Hasira ya Wananchi ipo katika kuona hakuna anayewajibika kwa matendo maovu waliyofanyiwa raia".-; Askofu Wolfgang Pisa, Rais wa TEC.
November 15, 2025
REPOST
TUTAKUWEPO🫵😎
Kanisa Takatifu Katoliki la Mitume linaendelea kutimiza wajibu wake wa kitume. Hili la kuwaombea waliopoteza maisha, waliojeruhiwa na waliopoteza ndugu na jamaa katika vurugu za uchaguzi mkuu ni ibada njema. Ahsante sana Mhashamu Baba Askofu, Jude Thaddaeus Ruwa'ichi, OFMCap, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Tume ya Haki na Amani ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania…🙏🏾
Mama zetu enzi hizo wakisikia unalia huko nje, walikuita na kutaka kujua nini kimekusibu. Kwikwi sana lakini unajua nafasi ndio hii ya kucheua maumivu. Unalalamika. Unasemea wenzako. Unashitaki. Mama mwema angesema, “Pole” na kukunyooshea kiganja chake, “Tema puu nikamchape.” Kesi inaishi hapo.
Wazazi wetu hawakusoma mambo ya ‘empathy’ lakini walielewa mama ndiye mtu wa kwanza kuonesha utu kwa mwanae anayepitia misukosuko ya kihisia. Mama alikujua anawajibika kuelewa malalamiko ya mtoto, kuonesha anamhurumia na ndiye mfariji wake nyakazi za maumivu.
Kesho yake ilikuwa ukichokozwa huko michezoni, ukatokea mtafaruku, ulijua ukikimbilia kwa mama atakuelewa. Imani uliyonayo kwa mama iliondoa haja ya kugombana na wenzako. Tulikimbilia kwa mama zetu.
Tuliogopa sana vile vijamaa vilivyolelewa na mama asiyejua kusema hata pole. Hawa walikuwa wakikimbilia kwa mama zao waligeuziwa kibao, “Unapigwa? Wewe ulikuwa wapi? Hebu niondokee hapa!” Hawa jamaa walikuwa wakatili sana kwenye michezo. Ukipishana naye kidogo anamalizana na wewe pale pale maana anajua kukushitaki kwa mama yake ni kupoteza muda.
Hatari sana kuwa mzazi usiye na uwezo wa kumfundisha mwanao utu kwa vitendo lakini anajua kumbebesha lawama kwa kuamua kushughulikia matatizo yake mwenyewe. Utu tunajifunza kwa wazazi wanaojali hisia zetu. Utu tunajifunza kwa wazazi wanaosikiliza maumivu yetu.
Rambirambi kwa ajili ya mpendwa wetu Clara, itapokelewa kwenye namba ya kaka yake.
0762156130
Clarence Justine Salama
Baada ya kuaga pale Bochi Hospital, msiba utasafirishwa Mbeya hivyo tuwashike mkono kwa chochote🙏🏾
Kwa muda mrefu kama taifa tumekuwa na changamoto ya kutokuwa na viwango vya pamoja (common standards) vinavyotuongoza kutambua kipi ni cha msingi zaidi katika ujenzi wa taifa letu.
Kuwa na barabara, reli, madaraja na miundombinu mingine ni wajibu wa serikali, si zawadi. Pesa zinazotumika kwenye hiyo miradi si mali binafsi za viongozi na wala hazitokani na vyanzo vyao vya asili vya mapato. Ni fedha za umma, zinazokusanywa kupitia kodi kutoka kwa wananchi wanaofanya kazi kwa bidii kila siku. Kwa lugha nyepesi tunaweza kusema, serikali inapotekeleza miradi ya maendeleo, inatimiza wajibu wake wa kikatiba wa kutumia mapato ya wananchi kwa manufaa ya wote.
Kwa kawaida tu, huwezi kufananisha utekaji, upoteaji wa watu, unyanyasaji na mauaji na ujenzi wa barabara kana kwamba vyote vina uzito sawa. Haki za binadamu na uhai vina msingi wa kimaadili, kikatiba na kimataifa ambao unapaswa kuwa wa juu kuliko miradi ya maendeleo ya miundombinu. Barabara na miundombinu mingine havitokuwa na maana kama wananchi wanaotakiwa kuvitumia hawana uhakika wa usalama wao, na haki zao zinakanyagwa bila ulinzi wa kisheria.
Maendeleo ya kweli ni yale yanayojumuisha:
• Uhuru na usalama wa mtu binafsi (hakuna hofu ya kutekwa au kuuawa).
• Utawala wa sheria na uwajibikaji wa viongozi.
• Heshima kwa utu wa binadamu na haki za msingi.
• Ushirikishwaji wa wananchi katika maamuzi ya kitaifa.
• Uwiano kati ya maendeleo ya kiuchumi na maendeleo ya kijamii na kimaadili.
Sehemu yoyote ile, tunapozungumzia maendeleo, ni lazima tuwe na mtazamo mpana unaojumuisha haki, utu na uhai kama msingi wa ustaarabu. Taifa lenye barabara nzuri lakini watu wake hawana amani, hawana sauti, na wanaishi kwa hofu, si taifa lililoendelea, ni taifa lililojenga miundombinu juu ya msingi dhaifu wa hofu na ukimya.
🚗 Life Way Garage Sinza 🔧
Huduma zote kwa gari lako: full service, wheel alignment, wheel balancing, brakes, suspension, battery ,diagnostic & more!
Haraka, uhakika, na kwa vifaa vya kisasa.
👉 Tupo Sinza Mori
Gari lako, maisha bora!
0753359604-Gipson
#opentowork
Experienced in Communications & Project Dev, Brand Strategist & Creative Fields.
Kama kuna any position out there unahisi I can fit in, kindly let me know.
Msaada to RT
Dear young dads,
USIPELEKE mtoto kanisani halafu wewe ukabaki kwenye gari. Unamharibu. Ibada, hata kama inaboa, huwa na thamani kwao pale watoto wamwonapo baba anashiriki.
Labda home waliwahi kuona unafumba macho, lakini wamwone baba akifunga macho kanisani anakuwaje.
It's the little things that matter - eternally.
🙏
Uzuri wa kiburi ni namna kinavyokuandalia anguko lako kwa ustadi mkubwa. Kwanza, kinakujaza ujasiri uamini wewe ni mtu mwenye akili zisizo za kawaida, unaona wasichoona watu wote na kisha kinakufumba macho usiuone ukweli unaouhitaji kwa kukuletea watu waliobobea kukusifu kama nyenzo ya kulinda maslahi yao.
Hapo kinakuwa kimekujengea imani kuwa unazo nguvu zisizo za kawaida za kufanya chochote unachotaka, kinakutenganisha na kila mwenye hekima unayemhitaji na kukugombanisha na watu ambao kimsingi wangekuwa na ujasiri wa kuona mapungufu yako.
Kikikufikisha hapo unaanza kuamini una uhuru usio na kikomo wa kufanya makosa bila usumbufu wala kuingiliwa. Kila anayeona makosa yako anakuwa tatizo. Unabaki kugombana na watu badala ya kujihami na adui. Unakuja kugundua makosa yako ukiwa umeshachelewa. Hata kile ulichofikiri unakipigania kinapeperuka. Tunakusahau.
Peace be with you all! This is the first greeting spoken by the Risen Christ, the Good Shepherd. I would like this greeting of peace to resound in your hearts, in your families, and among all people, wherever they may be, in every nation and throughout the world.
Last night, we won the “Africa CEO Disruptor of the Year 2025” at the Africa CEO Forum @africaceoforum — among 3,000+ companies.
Huge shoutout to the incredible teams at @NALAmoney and @rafiki_api this one is for all the hard work behind the scenes where no one else sees 🩵🩵
We are just getting started. Give us a couple years, we’ve got some big plans 💪🏾
Time to get back to building Payments for #TheNextBillion