@TogolaniMavura Hongera sana sana sana Kaka Mkubwa. Mungu aendelee kusimamia kazi ya mikono yako. Imani hulindwa kwa imani. Kama ulivoilinda imani ya Mhe Rais ukiwa Korea basi hakuna shaka kwamba utailinda pia ukiwa UN. To God Be The Glory π
@BrendaRupia@ccm_tanzania You can't be serious, kwamba haukusikia kiongozi akisema alikosea na kurekebisha takwimu ?? Why are you trying to capitalize kwenye common human error ?!
@Wakazi Wewe hata harufu ya mafanikio ya kimziki ya Diamond haupati kwa jinsi alivyokuzidi mbali. Jifunze kujishikilia, huna hata chembe ya uhalali wa kumtukana π kwa namna alivyofanikiwa. Utazikwa na chuki dhidi ya wenzako.
@AfricaFirsts We all stand for Senegal. The trophies are won on the pitch not on papers. Senegalese were punished with different sanctions, that could be enough. Its a shame to be crowned a champion by just an email...Its a shame and an unacceptable for the football world.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akihutubia Kikao cha Umoja wa Afrika (AU) kuhusu masuala ya G20, katika Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU), uliofanyika jijini Addis Ababa, Ethiopia, tarehe 14 Februari, 2026.
Rais Dkt. Samia aliwasilisha msimamo wa Tanzania kuhusu vipaumbele vya maendeleo, ikiwemo kuimarisha matumizi ya nishati safi, usimamizi wa madeni ya nchi, ustahimilivu dhidi ya majanga ya tabianchi, uongezaji thamani wa rasilimali za madini, pamoja na kuimarisha usalama wa chakula.
_____
#MaendeleoEndelevu
#DiplomasiaYaKiuchumi
#KaziNaUtuTunasongaMbele
Karibu Tanzania Mheshimiwa Rais.
Ikulu, Dar es Salaam leo nimempokea Kaka yangu, Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni. Ziara yake hii nchini ikiwa ni siku chache tu baada ya Uchaguzi Mkuu wa Uganda inaonesha namna Uganda inavyothamini ushirikiano wake na nchi yetu, ambao umejengwa katika misingi ya udugu, ujirani na kuheshimiana.
Tumejadili maendeleo ya Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP). Mradi huu ambao ni moja ya vielelezo vya uhusiano wetu, unatarajiwa kuanza kufanya kazi Julai mwaka huu. Vilevile, tumejadili mpango wa kuunganisha reli (SGR), ujenzi wa mabomba ya kusafirisha gesi asilia na mafuta, kukuza matumizi ya bandari za Tanzania, ulinzi na usalama, pamoja na namna bora ya kukuza biashara baina ya nchi zetu kwa kuondoa vikwazo visivyo vya kikodi.
Leo jioni nimewasili Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ambapo nitaungana na viongozi wengine katika uzinduzi wa Global Africa Investment Summit (GAIS) pamoja na Mkutano wa Dunia wa Serikali (World Governments Summit - WGS) 2026 unaolenga kujenga mwelekeo wa namna serikali zinavyoweza kuhimili mabadiliko ya dunia na kuchochea maendeleo endelevu.
Ushiriki wa Tanzania katika majukwaa haya ni kielelezo cha uthabiti wake kisiasa, na dhamira yake ya kuendelea kuvutia uwekezaji toka ndani na nje ya nchi, utakaozalisha ajira zaidi na kuchagiza maendeleo yetu. Aidha, ni utekelezaji wa Dira 2050 pamoja Sera mpya ya Mambo ya Nje katika Diplomasia ya Uchumi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiondoka nchini kuelekea Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) leo tarehe 02 Februari, 2026, ambapo atashiriki kwenye mkutano wa World Government Summit (WGS 2026) na uzinduzi wa Global Africa Investment Summit (GAIS).
Ushiriki wa Tanzania katika WGS 2026 unaakisi utekelezaji wa DIRA 2050 na Sera Mpya ya Mambo ya Nje, zinazoweka diplomasia ya kiuchumi kama nguzo ya mahusiano ya kimataifa.
Lengo ni kuoanisha sera, ushirikiano na mitaji ya uwekezaji kwa maendeleo ya taifa.
_____
#DiplomasiaYaKiuchumi
#DIRA2050
#KaziNaUtuTunasongaMbele
@Liberatus80@Happine61746941@BabaMwita Libe, do you even have an economic clue? Hivi mnajadili mambo ya uchumi kisiasa na miehemko tu. We don't reserve Gold for a show off guys. Hatuweki akiba ya dhahabu ili tutengeneze bangili wala hereni mazeeπ its typical economical. Anyways, am the beneficiary, so what?