Kwenye Maisha Changamoto Kubwa Ni Kwamba Wapo Watu Ambao Wataamua Kupambana Na Umasikini Walionao.
Lakini Vile Vile Wapo Watu Ambao Badala Ya Kuunga Mkono Juhudi Za Kupambana Na Umasikini Huo Wao Wataamua Kupambana Na Watu Ambao Wameamua Kupambana Na Umasikini. @ManenoIzaak
MUHIMU NI KUZIJUA NA KUZIISHI📌.
1.Ukipenda kupita kiasi – utaumizwa
2.Ukiongea kupita kiasi – utadanganya
3.Ukijali kupita kiasi – utadharauliwa
4.Ukifikiria sana – huo ni msongo wa
mawazo
5.Ukikaa kimya kupita kiasi – utanyanyaswa
6.Ukifanya kazi kupita kiasi – utachoka na kubomoka
7.Ukitumia pesa kupita kiasi – utakufa na deni
8.Ukisamehe kupita kiasi bila kujifunza – utadhulumiwa kila siku
9.Ukitoa siri zako kupita kiasi – utapoteza heshima yako
Watu dhaifu watafikiria kulipiza kisasi kila wakati
Waache wafanye wanachotaka
Watu wenye nguvu husamehe maishani
Ni chaguo lao kufanya
Lakini watu wenye akili watapuuza maishani
Kwa sababu ndiyo njia yao ya kufanya
Kwa hivyo chagua kutoka kwa waliotajwa hapo juu wewe ni nani?
Pindi utakapoelewa nguvu ya maneno yako, hutazungumza kila unachofikiria.
Pindi utakapoelewa nguvu ya fikra zako, hutawaza kila kitu kinachokuja akilini.
Pindi utakapoelewa nguvu ya uwepo wako, hutapatikana kila mahali.
Tambua Thamani Yako
"Kuna watu ni daraja la kuivusha riziki kwa wengine na kuna watu ni tuta la kukinga riziki isiwafikie kirahisi wengine. Ukiwa na nafasi ya kumsaidia au kumuinua mtu mmoja tu, msaidie na muinue yule ambaye kwa kuinuka kwake atakuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kuinua wengine."
"Binadamu tunaishi kwa kusudi. Tukikosa kusudi, maisha yanapoteza maana. Tafuta kulifahamu kusudi lako, lilinde kwa wivu mkubwa lisikuponyoke, maana kusudi lako ndio bando lako." ~Togolani Mavura.
"Maisha ya binadamu hayakamiliki bila lile shaka moja, jambo moja au tatizo moja linalomuumiza kichwa na ambalo hana majawabu yake ya moja kwa moja au ujasiri wa kulikabili kwa wakati huo na kuamua kuliweka katika mabano ama kuliahirisha. Kila binadamu ana lake. Hauko peke yako!"
"Katika uongozi ni muhimu sana sana kutambua ni wakati gani una cheo tu, wakati gani una mamlaka tu, na wakati gani una vyote viwili, yaani cheo na mamlaka. Muhimu zaidi, kutambua nafasi yako na ukomo wa unachoweza kufanya katika mazingira yote hayo matatu!" ~Togolani Mavura.
"Fursa ijayo inaweza kuwa ndio ufunguo na mwanzo wa fursa nyingine nyingi kumiminika katika maisha yako, au ndio fursa ya mwisho kukutembelea katika maisha yako yaliyosalia. Mitizamo hii miwili ni mtihani wa utu wetu, imani yetu na hatma yetu." ~Togolani Mavura.
Tatizo lako kubwa linalokufanya ushindwe kubadilika,
Unalazimisha kubaki mtu wa zamani kwenye mazingira mapya
1. Badili mtazamo wako
2. Badili tabia zako
3. Badili marafiki zako
4. Badili mambo unayofatilia
MABADLIKO >> MAFANIKIO