Kuna hii twit ya Mtumishi Mungu Godbless lema ya jana , akizungumzia mambo ya sex kabla ya ndoa na baada ya Ndoa, hiyo twit haikuwa na maana hiyo , maana yake ni hii hapa
Ni kwamba tupate katiba mpya kwanza ndo malidhiano yafanyike na pili tufanye malidhiano kwanza ndo tupate katiba mpya ?
Hiyo ndio Maana ya sex kabla ya ndoa na Baada ya ndoa aliyomaanisha Godbless Lema
Watanzania msimamo wetu ni Mmoja na wote tunaujua, kilichopelekea mpaka ndugu zetu kuuwawa ni katiba Ambayo haiendani na matakwa ya Watanzania
Katiba lazima ibadirike ile kuwe na uwanja sawa wa kisiasa kwa vyama vyote
Repost 780
Nendeni jela wanangu. Kuna maisha. Kuna wanetu wameishi kule miaka tele. Sio mwisho wa dunia. Kesi za mchongo zina mwisho. Lakini majitoleo yenu yatakumbukwa milele. Jamhuri inawashitaki. Jamhuri ni sisi. Na sisi hatuwadai. Mungu awalinde. Tutashinda. Ninyi & wenzetu wote.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo Oktoba 16, 2025
Jana tuliishia part 105 so leo tunaendelea na-;
Part 106
Muda huu ni saa tatu asubuhi.
Tumefika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es salaam.
Hali ya Mahakama ni nzuri.
Tunawashuhudia Waandishi wakichukua picha mgando na mnato kwa watu mbalimbali waliopo hapa Mahakamani.
Askari Magereza wale wa Kikosi Maalum yaani KM wako hapa ndani ya Chumba cha Mahakama wanazunguka zunguka kama wanakagua lindo vile.
Wasaidizi wawili wa Majaji tunawaona wako hapo mbele, Mwanamke mmoja na Mwanaume Mmoja kwa wasiofahamu hawa wanaoitwa Wasaidizi wa Majaji kitaaluma ni Mahakimu Wakazi.
Cheo chao ni sawa na Mahakimu waliopo Kisutu pale hawa hufanya kazi ya kuwasaidia majukumu ya kufanya research mbalimbali za masuala ya kisheria.
Wameingia hapa Majaji watatu kama kawaida ambao ni Jaji Dunstan Ndunguru, James Karayemaha na Ferdinand Kiwonde. Wakiwa kwenye magauni yao nasikia yanaitwa majoho mekundu.
Limesomwa shauri hapa na karani na amesimama Renatus Mkude Wakili Mkuu wa Serikali na ametambulisha wenzake muda huu, anasema upande wa Jamhuri wako tayari.
Mhe. Lissu ameulizwa yuko tayari na anaomba akumbushwe shahidi aliishia wapi kujibu maswali yake.
Amekumbushwa anasema anaomba aanze sasa.
Mhe. Lissu: Shahidi umeamka salama?
Kaaya: Nimeamka salama Mheshimiwa Lissu.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kama ulieleza kwamba fomu No. 145 kwamba haikusomwa wakati wa committal Kisutu?
Kaaya: Sikuwepo Kisutu.
Mhe. Lissu: Je umeileta hapa Mahakamani?
Kaaya: Sijaileta pia.
Mhe. Lissu: Sasa turudi tulipoishia jana. Maelezo yako Polisi ulitoa maneno mengi ikiwemo "Baadhi ya maneno mengine aliyotamka Rais alitoa maelekezo kuwa hakikisheni wapinzani hawaendi kokote....."
Naomba majaji shahidi apewe Exhibit D1 ili twende pamoja.
Sasa shahidi baada ya kelele nyingi za wapinzani kuenguliwa akiwemo Nchimbi alisema mambo kuhusu uchaguzi.
Je unafahamu Mchengerwa Waziri wa Tamisemi alisema wakikata rufaa wagombea walioenguliwa watarudishwa?
Kaaya: Sikumbuki.
Mhe. Lissu: je unafahamu Mchengerwa aliongeza muda wa rufaa ili watu wakate rufaa?
Kaaya: Sikumbuki.
Mhe. Lissu: Unafahamu wagombea angalau wa Chadema kwa maelefu walikata rufaa ndani ya huo muda wa rufaa ambao uliongezwa na Mchengerwa?
Kaaya: Sikumbuki.
Mhe. Lissu: Rufaa za Uchaguzi wa serikali za mitaa zinasikilizwa na Kamati za Wilaya?
Kaaya: Sina kumbukumbu.
Mhe. Lissu: Je unafahamu wenyeviti wa kamati za rufaa za Wilaya ni Makatibu tawala wa Wilaya ambao ni wateule wa Rais?
Kaaya: Sina Uhakika.
Mhe. Lissu: wote waliokata rufaa waliorudishwa hawafiki hata 10?
Kaaya: Hilo silifahamu.
Mhe. Lissu: Ila maneno yangu unasema ya uongo kuhusu uchaguzi wakati wewe kila kitu hujui?
Kaaya: Kimya.
Mhe. Lissu: Sasa watu wanaosimamia uchaguzi wote wa serikali za mitaa ni watu wa Rais kama nilivyokuonyesha mimi nakosea wapi?
Kaaya: Rais akishachaguliwa anafanya kazi kwa niaba ya Serikali na sio Chama chake.
Mhe. Lissu: Kwahiyo akikosea na mimi nikimpinga nikisema anafanya mambo ya hovyo kuengua watu wa Chadema nakosea wapi? Hapo anakuwa ameacha kuwa mwana CCM?
Kaaya: Haachi kuwa Mwanaccm.
Mhe. Lissu: Sasa wewe fundi wa Viyoyozi hebu tuambie kazi za Mwenyekiti wa CCM anazifanya nani kipindi akiwa Rais?
Kaaya: Anaendelea kuzifanya mwenyewe.
Mhe. Lissu: unafahamu zaidi ya asilimia 98 ya wenyeviti wa mitaa waliochaguliwa ni wa CCM?
Kaaya: Sifahamu.
Mhe. Lissu: Je unafahamu kwamba mwaka 2014 kwenye Uchaguzi wa Vijiji na mitaa ambao wagombea wa upinzani hawakuenguliwa walipata asilimia 33 ya viti vyote vya serikali za mitaa?
Kaaya: Sina Takwimu hizo.
Mhe. Lissu: Je unafahamu mwaka 2014 asilimia zaidi ya 20 walienda kwa upinzani ulienda kwa upinzani?
Kaaya: Hilo nilisikia.
Mhe. Lissu: Uchaguzi wa 2019 ambao wagombea walienguliwa wa upinzani CCM ilipata wenyeviti wa mitaa 100%?
Kaaya: Sikumbuki.
Part 107 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 105
Mhe. Lissu: Kwahiyo wewe hufahamu mtu anayeteua Mawaziri nchi hii wewe humfahamu?
Kaaya: Mawaziri wanateuliwa na Rais.
Mhe. Lissu: Kwahiyo Mohamed Mchengerwa ni mteule wa Rais Samia? Huyo ni waziri wa TAMISEMI.
Kaaya: Ni kweli.
Mhe. Lissu: Je ni kweli au sio kweli ni Waziri ambae anatoa tangazo la uchaguzi na ratiba yake ya huo uchaguzi wa serikali za mitaa?
Kaaya: Sina Uhakika.
Mhe. Lissu: Ni kweli au sio kweli wasimamizi wakuu wa uchaguzi huo ambao ni returning officer ni wakurugenzi wa halmashauri mbalimbali?
Kaaya: Sijui.
Mhe. Lissu: Ni kweli au sio kweli Wakurugenzi wote wa halmashauri za Wilaya ni wateule wa Rais?
Kaaya: Sifahamu.
Mhe. Lissu ; Askari Polisi mwenye cheo cha Inspector hafahamu wakurugenzi wanateuliwa na nani? Vituko na aibu. (Nimechomekea mimi hii)
Mhe.Lissu: Ni kweli kwamba watumishi wote wa serikali za mitaa wanaohusika na uchaguzi wa serikali za mitaa wanafanya kazi kwa niaba ya Rais au maelekezo ya Rais?
Kaaya: Sina Uhakika.
Mhe. Lissu: Ni kweli uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 kwa maelfu walienguliwa na kuzuiwa kugombea?
Kaaya: Sina uhakika.
Mhe. Lissu: Ni kweli au si kweli baada ya kuenguliwa kelele ikawa kubwa hadi Dr. Nchimbi katibu mkuu wa CCM alielekeza pia warudishwe?
Kaaya: Sina Uhakika.
Mhe. Lissu: Ni kweli baada ya kelele zote hizo Waziri wa Tamisemi Mchengerwa aliomba muda uongezwe na kubadili ratiba ya Uchaguzi?
Anasimama Renatus Mkude anasema Mheshimiwa Jaji imefika saa tano kamili naomba turuhusiwe kwenda msibani na tutafikisha salamu za rambirambi pia za Mshitakiwa.
Jaji Ndunguru: Shahidi tukutane kesho saa tatu asubuhi.
Tunaahirisha shauri hili.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 104
Mhe. Lissu: Sasa waeleze majaji kuwa serikali haihusiki chochote na uchaguzi na uchaguzi uko chini ya Tume huru?
Kaaya: Hapo ni kweli serikali haihusiki ni tume ndio inahusika.
Mhe. Lissu: Sasa naambiwa nilitengeneza nia ya kuhamasisha wananchi wazuie uchaguzi mkuu unalifahamu hilo?
Kaaya: Inategemea.
Mhe. Lissu: Inategemea nini wewe Polisi mi nakwambia kuhusu mashitaka yangu. Hiyo hati umeisoma? Unajua nashitakiwa na nini?
Kaaya: Mimi sijaisoma hiyo Hati ya Mashitaka.
Mhe. Lissu: Kwahiyo hujui mashitaka yanasema nini? Kama hujaisoma huwezi kuijua.
Kaaya: amenyamaza anatoa macho.๐
Mhe. Lissu: Haya umegoma kujibu. Mimi nakuacha tuendelee. ๐
Mhe. Lissu: Kwenye maneno ninayotuhumiwa nayo sijaitaja kabisa serikali?
Kaaya: umeitaja kwa namna fulani hujataja kwa uwazi.
Mhe. Lissu: Hiyo namna fulani ndio wamekufundisha akina Kingai ambao nao pia sio Mawakili wamekudanganya umekalili na unakimbia na haya mambo ya uongo unaona unavoteseka hapa sasa nakusomea maneno yaliyopo kwenye hati ya mashitaka
"Walisema msimamo huu unaashiria uasi ni kweli kwasababau tunasema tutazuia uchaguzi hii ndio namna ya kupata mabadiliko. Tutaenda kukinukisha sana.
Hayo ndio maneno nashitakiwa nayo sasa katika hayo maneno kuna neno serikali?
Kaaya: Hapo neno Serikali lipo kwa maana ukitafsiri
Mhe. Lissu: Nakuuliza kuhusu maneno niliyosema mimi nimetaja serikali?
Kaaya: kwenye maneno hujataja ila lipo.
Anasimama Job Mrema anasema tuna pingamizi tunaona shahidi ameshajibu hili Swali.
Jaji: Hebu tuendelee sioni pingamizi hapo.
Mhe. Lissu: Kwenye hayo maneno ninayosadikika kuyasema kama nimetaja Tume huru ya Uchaguzi?
Kaaya: Hujataja Tume Huru ya Uchaguzi.
Mhe. Lissu: Hii habari ya kutishia serikali sasa ulisema umesoma Criminal Law? Ni kweli?
Kaaya: Ni kweli nimesoma Criminal Law.
Mhe. Lissu: Je umesoma Penal Code? Kanuni ya adhabu umeisoma. Wewe si umesoma LL.B?
Kaaya: Nimesoma.
Mhe. Lissu: Kifungu cha 39(2)(d) cha Penal Code sasa waeleze kwenye kifungu hicho neno kutishia kama limefafanuliwa?
Kaaya: Sikumbuki.
Mhe. Lissu: Neno lililotumika ni intimidation. Je waeleze kama hilo neno limefafanuliwa? Nikupe sheria usome ili unataka kuropoka.
Kaaya: Sikumbuki.
MheLissu: Nikikwambia hilo neno halijajatafsiriwa kokote kwenye Penal Code utasemaje?
Kaaya: Sikumbuki.
Mhe. Lissu: Je kwenye hati ya mashitaka hilo neno kutishia serikali limefafanuliwa?
Kaaya: Sikumbuki.
Mhe. Lissu: Hata kwenye hati ya mashitaka hicho kinachoitwa kutishia Serikali halijafafanuliwa utasemaje?
Kaaya: Sina uhakika.
Mhe. Lissu: Sasa naomba apatiwe maelezo yake exhibit D1 sasa tuyapitie shahidi na usinisumbue.
Je maneno yafuatayo ni ya kihaini yapo kwenye ukurasa wa 2 wa maelezo yako.
Umesema matamshi mengine ni-;
Umesema mambo ya majaji kuwa ma ccm na wanataka vyeo.
Umeyaona hayo maneno?
Kaaya: Ndio nayaona.
Mhe. Lissu: Sasa Je hayo maneno ni uhaini?
Kaaya: Hapana sio ya uhaini.
Mhe. Lissu: pia ulisema maneno mengine ambayo mimi nimeyasema kwamba nilisema wapinzani walienguliwa kwa amri ya Rais. Je hayo nayo ni Uhaini?
Kaaya: Inategemea. Wapelelezi wanajua.
Mhe. Lissu: Nakuuliza wewe hayo ni Uhaini? Kama kuna mtu mwingine anajua wewe umekuja kufanya nini hapa?
Kaaya: Mimi ni Mpelelezi lakini sijapeleleza hilo mimi.
Mhe. Lissu: Na mimi nataka kuchaguliwa kwenye kacheo fulani na nyie mnataka kuchaguliwa pia sasa mnafikiri tunafanyaje kwa mazingira haya. Je hayo pia ni uhaini.
Kaaya: sasa hadi nichunguze ndio nitajua.
Mhe. Lissu: Ulichunguza?
Kaaya: Mimi sio Mpelelezi. Sikuchunguza hili.
Mhe. Lissu: Unajua Uchaguzi wa Serikali za mitaa unaendeshwa na TAMISEMI?
Kaaya: Ni kweli.
Mhe. Lissu: Ni kweli kwamba uchaguzi huo unaendeshwa kwa kanuni za uchaguzi huo zinazotungwa na waziri?
Kaaya: Sifanyi kazi huko kwahiyo sifahamu.
Lissu: Huyo Waziri ni mteule wa Rais?
Kaaya: Mimi sijui.
Part 105, itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 103
Mahakama imetulia sana hata hakohoi mtu baada ya hiyo speech ya Mhe. Lissu.
Watu wameingiwa ubaridi ni kama maneno yamewaingia kila aliyepo hapa.
Jaji amewasha kipaza sauti na kumwambia shahidi uko chini ya kiapo.
Endeleeni.
Mhe. Lissu: Ni kweli au sio kweli hiyo video ya Tarehe 03/04 ilichapishwa kwenye Jambo Tv na mitandao mingine na walichapisha Jambo Tv wenyewe?
Kaaya: Aliyechapisha sifahamu.
๐๐๐ kumbukeni kosa la Lisu ni kuchapisha na kusambaza.
Mhe. Lissu: Ni kweli Mkutano wangu wa tarehe 03/04 ulirushwa mubashara na Jambo Tv?
Kaaya: Ni kweli.
Mhe. Lissu: Na ni kweli au sio kweli mimi sina uhusiano wowote na Jambo TV?
Kaaya: Mimi sikufanya upelelezi wa kuhusu wahusika wa Jambo TV ni akina nani.
Mhe. Lissu: Ile Flash Disk XIOXIA yenye rangi nyeupe unaikumbuka ulisema.
Kaaya: ndio nakumbuka
Mhe. Lissu: Je uliandika aina hiyo ya Flash na rangi yake kwenye maelezo yako Polisi?
Kaaya: Sikuandika.
Mhe. Lissu: Umezungumza sana kuhusu video na kuwaonyesha wakubwa zako na kuipakua na kuweka kwenye flash disk umezungumza sana asa waeleze majaji kama umewasilisha hiyo flash disk au hiyo video mahakamani hapa.
Kaaya: Bado sijaiwasilisha.
Mhe. Lissu: Ni sahihi nikisema hakuna mtu aliyeiona isipokuwa wewe hiyo video, Majaji hawajaona, Mawakili hawajaona na mimi sijaona.
Kaaya: Ni kweli.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kama unafahamu au hufahamu hiyo video vilevile haikuwasilishwa wala kuonyeshwa kwenye committal Kisutu?
Kaaya: Sifahamu.
Mhe. Lissu: Sasa shahidi unakumbuka kwenye ushahidi wako ulieleza jinsi ulivyoona hiyi video na kutoa taarifa kwa mkuu wa kitengo?
Kaaya: Ni kweli.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji kama kwenye maelezo yako Polisi au hapa Mahakamani ulimtaja huyo Mkuu wako wa kitengo kwa jina?
Kaaya: Sikumtaja.
Mhe. Lissu: Unakumbuka nilikuuliza maswali mengi juu ya kesi mbalimbali zilizofunguliwa na watu tofauti tofauti kuhusu masuala ya Katiba na mabadiliko yake.
Kaaya: Nakumbuka.
Mhe. Lissu: Waelelze majaji kama unafahamu au hufahamu kwamba tarehe 13/06/2023 Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Wananchi ilitoa uamuzi kwamba Serikali ya Tanzania ibadilishe sheria ya Uchaguzi ili kuhakikisha sheria za uchaguzi zinakuwa za haki kwenye kesi ya BOB CHACHA WANGWE.
Ni kesi ya Bob Chacha Wangwe akiwa na Legal and Human Right Center wakiwashitaki AG, Tume ya Uchaguzi. Alikuwa anawapa full citation hapo majaji anawatajia na namba ya kesi hiyo.
Mhe. Lissu: sasa kuzuia uchaguzi ni uhaini mnasema hivyo kwenye ushahidi wako ulieleza kuzuia uchaguzi bila kufuata utaratibu wa kisheria kama vile kupata amri ya mahakama ni kuitisha serikali.
Kaaya: Nakumbuka.
Mhe. Lissu: Utaratibu huo wa namna ya kuzuia uchaguzi upo katika sheria gani?๐
Kaaya: Sifahamu.
Ushahidi ni kazi sana jamani.
Leo kumbukeni kuna ile kesi yetu pia niliyofunguliwa na Viongozi wa Chama ndio inaanza muda huu ila Mimi siendi wataingia Mawakili wetu kwa niaba yetu.๐คฆ๐พโโ๏ธ
Mhe. Lissu: Katiba unaifahamu shahidi?
Kaaya: Ndio naifahamu.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji kama upo utaratibu wa kuzuia uchaguzi mkuu?
Kaaya: Haupo. Haujaanishwa kwenye Katiba.
Mhe. Lissu: kwahiyo utaratibu haupo?
Kaaya: Zipo sheria zingine lakini.
Mhe. Lissu: Hivi unaelewa swali langu au unatuchelewesha kwenda kwenye mazishi?
Kaaya: haupo
Mhe. Lissu: Je ni kweli Uchaguzi mkuu wa Tanzania unaendeshwa na inayoitwa Tume Huru ya Uchaguzi?
Kaaya: Ni kweli.
Mhe. Lissu: Je ni kweli Katiba inasema tume ni chombo huru na haitakiwi kuingiliwa na Mamlaka au mtu yeyote?
Kaaya: Sikumbuki.
Mhe. Lissu: Anasomewa Katiba hapa ibara ya 74(11) kuhusu Tume na uhuru wake na pia anasomewa sheria ya Uchaguzi kuhusu wajibu wa Tume.
Kwamba tume haitakiwi kupokea maelekezo yoyote kutoka serikali wala chombo chochote cha serikali.
Kaaya: Ni sahihi.
Part 104 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo Oktoba 15, 2025.
Last time tuliishia part 101 so leo tunaendelea na
Part 102
Leo Tarehe 15/10/2025.
Mheshimiwa Tundu Lissu ameingia Mahakamani.
Amesimama Kizimbani anauliza Polepole amepatikana na Mama anasemaje si Balozi wake?
Majaji wameingia na Shahidi nae kama kawaida ameingia yupo hapa. Inspector wa Polisi John Kaaya.
Karani anasimama Criminal Session No. 19605 Jamhuri dhidi ya Tundu Lissu.
Iwapendeze naitwa Renatus Mkude Wakili wa Serikali niko na Job Mrema, Ignas Mwinuka, Harrison Lukosi, Winiwa Kasawa tunaiwakilisha Jamhuri. Na Mshitakiwa yupo. Lakini pia tuna jambo tunaomba kuiambia Mahakama.
Mhe. Lissu anasema na mimi niko tayari na pia nitakuwa na jambo la kuieleza Mahakama.
Renatus Mkude, tulipokea taarifa ya Msiba wa Msajili wa Mahakama Kuu kanda ya Shinyanga.
Tumekuwa na utaratibu wa kwenda kushiriki matukio kama haya na tulipanga kuhudhuria kwenye msiba huo kwa vile ni jambo la kibinadamu ilikuwa na rai yetu itakapofika saa tano twende tukamuage huyu ndugu yetu ili tuendelee kesho tena. Ni hayo tu.
Mhe. Lissu anasimama kwenye hilo mimi sina pingamizi lolote na ikiwapendeza wakienda kwenye huo msiba wanipelekee salamu zangu za rambirambi kwa wafiwa.
Lakini pia niwaeleze kuhusu watu waliokuwa wanazuiwa kuingia Mahakaman, nimesema sana jambo hili.
Kasoro juzi Jumatatu sikulizungumzia kwasababu niliambiwa wangeruhusiwa siku hiyo lakini walikuja wakazuiliwa hapo getini.
Kwa taarifa nilizonazo walichukuliwa na maafisa wa uhamiaji na baadae wakafukuzwa nchini ili wasiweze kuingia Mahakamani kushuhudia kesi hii.
Sasa waheshimiwa majaji hii ni mara ya tatu kwa watu wanaotaka kuja kuhudhuria mahakama hii kufukuzwa nchini.
Walianza na Ujumbe uliotoka Kenya ukiongozwa na Jaji Mkuu mstaafu wa Kenya, Willy Munyoki Mutunga.
Wakafuata Boniface Mwangi na Agatha Atuhire walikamatwa na kuteswa na kupelekwa mipakani na kutupwa.
Na sasa hili limetokea kwa raia wa Ujerumani na Marekani walioingia nchini kihalali kuja kutaka kuona kinaendelea nini.
Hii ni kesi kubwa kuliko zote ndivyo inasema Katiba yetu ni kesi inayo draw Regional and International attention.
Haya yaliyofanyika Kisutu tayari yapo kwenye Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa yapo katika mahakama za haki za binadamu na watu Afrika.
Kwahiyo haya sio mambo madogo kabisa. Mahakama inapoingiliwa inasababisha sintofahamu kwenye mfumo wetu wote wa haki jinai ndani ya Taifa letu.
Mwaka 1958 kulikuwa na kesi kubwa sana katika Mahakama ya Wilaya Dar es salaam Kivukoni ambayo ni Regina Vs Julius Nyerere na wenzake wawili mmoja wapo Robert na mwingine Rashid baldell.
Wakoloni wa kingereza did not dare kuzuia watu kwenda kushuhudia kesi ya kiongozi wao na wanaofahamu historia ya nchi hii Mwalimu alitetewa na Wakili kutoka Wingereza.
Wakoloni hawakukataza pia hawakupiga watu wasiingie Mahakamani.
Kesi ya Jommo Kenyata pia ilikuwa kubwa sana ambayo ilifanyika katikati ya Vita vya Maumau, Waingereza did not dare kuzuia watu kwenda kusikiliza the trial of Jomo Kenyata ilifuatiliwa.
Mwaka 1956 mpaka 1961 tulikuwa na kesi ya Uhaini Afrika Kusini imeelezwa kwenye Long Walk to Freedom, Kesi ya Nelson Mandela hakuna mtu aliyepigwa wala kuzuiwa kwenda Mahakamani, hakuna watu walioteswa ili wasiingie Mahakamani.
Sasa nchi hii baada ya miaka 64 ya Uhuru Serikali yetu na vyombo vya Ulinzi na Usalama inazuia watu wasiingie Mahakamani kwenye nchi ambayo sheria zinasema mahakama ni ya wazi.
Tunafanya mambo ya hovyo kuliko wazungu waliotutawala sisi hapa Tanganyika, walioitawala Kenya na wale wa Afrika Kusini sasa mimi niko Gerezani na Mahakama imeshindwa kufanya lolote.
Sasa ili isije kuja kusemwa baada ya mimi na nyie majaji kutoweka hapa Duniani kuwa nilikuwa kwenye dhambi ya watu ambao walinyamaza kimya mambo haya kutokea. Nimesema kutimiza wajibu wangu na sitaki dhambi ya kunyamazia uovu au maovu, naomba kumalizia hapo.
Part 103 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 91.
Mhe. Lissu: waeleze majaji kama hicho cheo cha special seargent kipo kwenye vyeo vya Police hapa Tanzania.
Kaaya: Nilisema nimehudhuria mafunzo ya Special seargent na sio cheo cha special Sergeant.
Mhe. Lissu: Waheshimiwa Majaji someni mlichoandika mtusaidie alisema nini tafadhali sana nawaombeni.
Jaji: anasoma hayo maelezo na kusema kuwa alipandishwa cheo cha rank ya Special Sergeant.
Mhe. Lissu: sasa tuambie katika muundo wa jeshi la polisi kama hicho cheo kipo?
Kaaya: Hicho cheo kipo ndio maana hayo mafunzo yalikuwepo na nilihudhuria.
Mhe. Lissu: Je huo ushahidi wa Special seargent uko wapi kwenye maelezo yako ya Polisi?
Kaaya: Waheshimiwa Majaji hayapo.
Mhe. Lissu: Ni kweli kwamba ulisema ulipokamilisha hayo mafunzo ulipewa cheti cha kushiriki hayo mafunzo na useme kama umeandika kwenye maelezo yako?
Kaaya: Ni kweli nilisema na ni kweli kuwa hayapo kwenye maelezo yangu. Nilisema hapa mahakamani pekee.
Mhe. Lissu: Je ni kweli au si kweli ulisema mwezi October 2021 ulipelekwa kwenda kusomea assistant Inspector kule Moshi?
Kaaya: Ni kweli
Mhe. Lissu: Yako wapi hayo kwenye maelezo yako ya Polisi?
Kaaya: Hayapo.
Mhe. Lissu: Ni kweli au si kweli kwa ushahidi wako baada ya mafunzo ya assistant Inspector ilipofika Feb. 2022 ukafuzu na kupata cheti cha mahudhurio.
Kaaya: Ni kweli.
Mhe. Lissu: Hivi kwanini huongezi sauti?
Kaaya: Sawa nitaongeza.
Mhe. Lissu: haya jibu swali?
Kaaya: Hayo maelekezo hayapo kwenye maelezo yangu ya Polisi.
Mhe. Lissu: waeleze Majaji kama ni kweli tarehe 09/10 ulisema hapa mwezi June 2025 ulipandishwa cheo na kuwa full Inspector kwasababu ya utendaji kazi mzuri?
Kaaya: Ni kweli Majaji.
Mhe. Lissu: waeleze sasa hayo mambo mema kama yapo kwenye maelezo yako ya Polisi?
Kaaya: Na yenyewe hayapo.
Mhe. Lissu: Ulienda kwenye mafunzo ya miezi miwili kuanzia Januray hadi March 2020 ulijifunza forensic investigation in modern science?
Kaaya: Nilisema lakini hayapo kwenye maelezo yangu ya Polisi.
Mhe. Lissu: Ni kweli au sio kweli kwenye ushahidi wako wa Tar. 09/10 ulisema ulipata mafunzo ya SISSCO certified support in Cyber security?
Kaaya: Ni kweli nilisema.
Mhe. Lissu: yako wapi kwenye maelezo yako?
Kaaya: Hayapo
Mhe. Lissu: Sasa kwanini hutoi sauti Polisi?
Kaaya: Natoa.
Mhe. Lissu: Haya toa basi.
Kaaya: sawa natoa.
Hii leo ni kama ule wimbo wa nauliza UTATOA, HUTOI.๐๐๐
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kama ni kweli ulisema vilevile ulisomea computer Hacking katika chuo cha Unique Academy pale Upanga?
Kaaya: Nilisema kweli hapa Mahakamani.
Mhe. Lissu: Ulisema kama umesomea computer Hacking?
Kaaya: Sikusema.
Mhe. Lissu: kwamba mafunzo yalichukua miezi miwili yaani week 8?
Kaaya: ni kweli nilisema ila kwenye haya maelezo hapa sijaandika.
Mhe. Lissu: Ulisema ili mtu yeyote kuweza kutumia mitandao ya Kijamii mtumiaji huyo anatakiwa kujisajili kwa kuweka taarifa zake ili zionekane na watumiaji wengine?
Kaaya: Ni kweli.
Mhe. Lissu: Piia ulisema ukiwa unajisajili unapata username jina lako, password na email address unaviweka?
Kaaya: Ni kweli ila sikusema unaweka nilisema unaandaa.
Mhe. Lissu: basi ni sawa jibu sasa swali langu kama hayo maelezo yapo kwenye hayo maelezo yako ya Polisi.
Kaaya: Hayapo kabisa.
Mhe. Lissu: baada ya kuandaa yote hayo unaingia kwenye uwanja wa mtandao husika kwa kadri ya maelekezo utakayopewa?
Kaaya: Ni sahihi nilisema hapa lakini kwenye maelezo niliyotoa Polisi haupo, usije sema nisome wakati sikuandika.
Mhe. Lissu : ulisema kuhusu ukurasa wa mtumiaji yaani user page?
Kaaya: Ni kweli.
Mhe. Lissu: Je upo kwenye maelezo yako ya Polisi?
Kaaya: Haupo
Mhe. Lissu: Baada ya hapo ulisema hivi kwamba kwenye YouTube ukiingia, unaweka username na email address na password na baada ya hapo unajaza taarifa.
Kaaya: Sikusema neno kuandaa.
Part 92 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako ujumbe uende mbali.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 92
Mhe. Lissu: Haya tutumie neno la kuandaa. kwahiyo unaandaa nilivyotaja hapo juu. Wakati gani sasa?
Kaaya: Wakati unajisajili.
Mhe. Lissu: Baadae unapewa masharti ya kuingia si ndio baada ya hapo?
Kaaya: Ndio
Mhe. Lissu: Then unapewa URL?
KAAYA: Ni kweli.
Mhe. Lissu: Sasa waeleze majaji kama yapo kwenye maelezo yako, ukisema kwa sauti POLICE inapendeza sana.
Kaaya: Hayapo kabisa.
Mhe. Lissu: kwa ushahidi wako ukishapata hiyo channel system locator ni unique ID isiyoweza kutimika na mtu yeyote?
Kaaya: Ni kweli.
Mhe. Lissu: Je yote hayo yako kwenye maelezo yako Polisi?
Kaaya: Hayapo.
Mhe. Lissu: Ulisoma Data protection na ethical computer Hacking?
Kaaya: Ni kweli?
Mhe. Lissu: Yako wapi kwenye hilo karatasi uliloandika Polisi?
Kaaya: Hayako. Sikuandika
Mhe. Lissu: Kwamba ulipata cheti pia?
Kaaya: Ni kweli
Mhe. Lissu: Yako wapi?
Kaaya: Hakuna.
Mhe. Lissu : Kuhusu maandalizi yako ukifika asubuhi kazini kwenye maelezo uliandika?
KAAYA: sikuandika.
Mhe. Lissu: Police notebook umeisema sana.
Kaaya: Ni kweli?
Mhe. Lissu: Umeileta Mahakamani.
Kaaya: Sijaileta kwasababu
Mhe. Lissu: Sababu isubiri kwanza, utaitoa siku nyingine.
Mhe. Lissu: kuhusu kukagua vifaa vyako kabla ya kazi pia?
Kaaya: Nilisema lakini sikuandika kwenye maelezo yangu ya Polisi.
Mhe. Lissu: Ulisema unayo program na software inayokuwezesha kufanya doria mtandaoni?
Kaaya: nilisema ndio.
Mhe. Lissu: Kwenye maelezo hayo uliyoshika yapo?
Kaaya: Hayapo kabisa huku ameshikilia karatasi yake ya Maelezo Polisi yenye kurasa mbili huyo nayo pale kizimbani.
Mhe. Lissu: twende kwenye ya Tarehe 04/04/2025 ulisema hapa kwamba ulifika ofisini saa 12 asubuhi?
Kaaya: Ni kweli.
Mhe. Lissu: Je umeandika hayo?
Kaaya: Sikuandika.
Mhe. Lissu: kwamba ulikuwa na vitendea kazi pia ulisema?
Kaaya: hayo yapo ila notebook lakin haipo, sikuandika.
Mhe. Lissu: ulivyoanza kuperuzi ulikutana na maneno Tundu Lissu uso kwa uso na watia nia majimboni No Reforms, No Election njia panda.
Kaaya: Ni kweli.
Mhe. Lissu: Na ukaeleza kwamba uliangalia hiyo video yote.
Kaaya: Ni kweli.
Mhe. Lissu: Kwa ushahidi wako ulisema uliangalia hiyo video kwasababu ulikuwa na wasikiliziaji elfu 39?
Kaaya: Si kweli nilisema watizamaji elfu 39.
Mhe. Lissu: Basi twende na hao watizamaji uliosema.
Mhe. Lissu: Kwahiyo kilichokufanya ni hao watizamaji elfu 39 na comment 300?
Kaaya: Ni sahihi.
Mhe. Lissu: Je hayo yapo kwenye maelezo yako Polisi.
Kaaya: Hayapo
Mhe. Lissu: Katika ushahidi wako umeeleza ulivyomaliza kuangalia hiyo video na wakati unaiangalia ulichukua police notebook yako na kuwa unaandika baadhi ya maudhui?
Kaaya: Ni kweli
Mhe. Lissu: je kama uliandika kwenye maelezo yako Polisi wambie majaji?
Kaaya: Hebu rudia.
Mhe. Lissu: Je ulisema ulikuwa na notebook na kuandika uliyokuwa unayaona na kama hayo umeandika kwenye maelezo yako?
Kaaya: taarifa hizo zipo lakini polisi notebook sijaandika kwenye maelezo yangu.
Mhe. Lissu: Ulisema baadae ulimpa taarifa kiongozi wako wa dawati la doria mtandaoni na je upo kwenye maelezo yako Polisi?
Kaaya: sikumbuki.
Mhe. Lissu: Waheshimiwa Majaji naomba mumsomee Shahidi, akumbushwe alichosema.
Mahali aliposema baada ya kutazama hiyo video alipomaliza kutazama na kuandika maudhui kwenye notebook ndipo alimjulisha mkuu wake wa kitengo na akamwambia aende kutoa taarifa kwa George.
Jaji: baada ya kuandika matukio yote kwenye notebook yangu.
Mhe. Lissu: Sasa wambie Majaji kama hayo waliyokusomea yapo kwenye maelezo yako Polisi?
Kaaya: baadhi hayapo.
Mhe. Lissu: Yapi hayo ambayo hayapo.
Kaaya: Hayo ya Polisi notebook.
Mhe. Lissu: Je ya saa nne?
Kaaya: Na yenyewe hayapo.
Mhe. Lissu: Ulisema umeenda kutoa taarifa kwa SSP George? Ambae amepanda cheo juzi hapa?
Kaaya: Sina taarifa kama amepanda cheo.
Part 93 itaendelea kwenye post inafuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 89
Wamesimama Mawakili wa Serikali wanasema tunapinga nyaraka kupokelewa kwasababu hatua hazijafuatwa.
Wanasema Mhe. Lissu hajacontradict anataka ipokelewe.
Mhe. Lissu anawajibu Waheshimiwa Majaji wao wenyewe waliniletea hizi kesi siku ya kwanza leo nimetumia utaratibu huo huo ambao waliusema wao na kuniletea kesi tena wameona nongwa.
Kwanza wanasoma sana kesi ya High Court wakati kesi ninayoitumia mimi ni kesi ya Mahakama ya rufani.
Kwahiyo naomba maelezo ya shahidi yapokelewe.
Wanarudi kufanya rejoinder Mawakili wa Serikali amesimama Igans Mwinuka, anasema Majaji mimi sipingi kabisa alichosema kuhusu kesi ya Mahakama ya rufani nakubaliana nayo kabisa.
Hivyo hata hiyo kesi utaratibu wake ni huo kabisa.
Hajaonesha hizo contradiction ni hayo tu.
Majaji wanaandika hapa kidogo.
Jaji anasema na sisi tunahitaji muda kidogo tuweze kwenda kuandika uamuzi mdogo.
Tutaendelea Jumatatu asubuhi itakuwa ni tarehe 13/10/2025.
Kesi imehairishwa mpaka siku ya Jumatatu asubuhi.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 88
Mhe. Lissu: Je unafahamu tarehe 31/05/2023 CCM ilikataa mapendekezo yote ya Chadema na mazungumzo yale yakaishia hapo?
Kaaya: nimeona kwenye vyombo vya habari kuna mambo yalifanyiwa kazi na serikali.
Mhe. Lissu: Nimeuliza mapendekezo ya Chadema kuhusuu Katiba mpya?
Kaaya: sikushiriki kwahiyo sifahamu.
Mhe. Lissu : December 2021 Rais Samia aliunda kikosi kazi kuangalia matatizo ya mfumo wetu wa Uchaguzi na kumteua Prof. Rwekaza Mkandala kuangalia matatizo hayo?
Kaaya: Hilo nilisikia.
Mhe. Lissu: na mapendekezo ya kikosi kazi yalikataliwa na CCM na samia huyu huyu?
Kaaya: Hilo nalo sifahamu.
Mhe. Lissu: Sasa jitihada hizi toka mwaka 1991 hadi leo nikikwambia Chadema na mimi tumejaribu mahakamani imeshindikana na njia ya mazungumzo imeshindikana utasemaje?
Kaaya: SI KWELI.
Mhe. Lissu : waeleze majaji tuna Katiba Mpya au hatuna? Fanya haraka jibu.
Kaaya: tunatumia katiba ile ile ya zamani.
Mhe. Lissu: je uliwahi kuandika maelezo yako Polisi?
Kaaya: Niliwahi kuandika
Mhe. Lissu: je kama ukionyeshwa utayatambua?
Kaaya: Ni kweli nitayatambua.
Mhe. Lissu: anamsomea maelezo yake shahidi yote hapa, anasema nataka kutumia zile stages zote, anamsomea hapa.
Mhe. Lissu : Waheshimiwa Majaji sasa naomba nianze kumuonyesha maeneo ninayotaka kumcontradict.
1. Eneo la kwanza alisomea chuo cha upolisi Zanzibar
2. Alipewa Cheti cha Competence.
3. Ushahidi wake juu ya masomo
aliyoyasoma kama vile kusomea masuala ya military and safety skills, sheria ya ushahidi.
5. Cheti alichopata baada ya training.
6. Alipelekwa kwenda kusomea nafasi ya assistant Inspector Moshi na kusomea community policing.
Anamsomea maeneo zaidi ya 10 ambayo anataka kumcontradict huyu shahidi.
Hapa ataonesha ushahidi wake mahakamani alisema nini na kwenye maelezo yake ya shahidi ameandika nini?
Mhe. Lissu anaendelea kusoma maeneo anayotaka kumcontradict na muda huu ameshafikisha mambo 40 ambayo yanatofautiana kati ya maneno aliyosema mahakamani na yale aliyoandika kule kwenye maelezo yake.
Huyu shahidi sijui tutamalizana nae lini. Maana zoezi tu la kumuonesha maeneo yenye shida linachukua karibu nusu saa. Je maswali yenyewe itakuwaje?
Lazima kiwake ๐๐๐
Part 89 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 87
Mhe. Lissu : waeleze Majaji kama unafahamu kama mwezi January 1991 Rais Mwinyi aliunda tume ya Rais ya kama twende na chama kimoja au vingi?
Kaaya: Sina kumbukumbu hizo.
Mhe. Lissu : Tarehe 17 Feb. 1992 tume hiyo maarufu kama Tume ya Nyalali iliwasilisha taarifa yake kwa Rais Mwinyi?
Insp. Kaaya: Sifahamu.
Lissu anasema tukiwa vituoni huko mnatukoromea sana, Ongeza Sauti na usiwe na wasiwasi kusema hufahamu HAUTAFUNGWA.
Mhe. Lissu : Unafahamu kwamba Nyalali na tume yake walipendekeza kwamba nchi hii iwe na Katiba Mpya itakapofika September 1993?
Insp. Kaaya: Sijawahi kusikia kabisa hicho kitu.
Mhe. Lissu : Unafahamu kwamba serikali ya Rais Mwinyi ilikataa mapendekezo ya tume ya Jaji Nyalali kuipatia Katiba Mpya?
Insp. Kaaya: Sina kumbukumbu.
Huyu shahidi majibu yake ni sifahamu na sina kumbukumbu yani akibadili sana ni Sijui.๐๐๐
Acha twende.
Mhe. Lissu : Umewahi kusoma kitabu cha Rais Mwinyi kunaitwa Mzee Rukhsa kinazungumzia historia yake?
Kaaya: Nimekisikia.
Lissu: Umekisoma Je?
Kaaya: Hapana sijasoma.
Mhe. Lissu: Mzee Mwinyi kwenye kitabu hicho alieleza CCM na serikali walikataa mapendekezo ya Baba wa taifa kuwa mgombea binafsi aruhusiwe?
Kaaya: Sio kweli.
Mhe. Lissu: Umejuaje wakati hujasoma?
Kaaya: Ni kweli sijasoma kwahiyo unaniuliza maswali ambayo sijasoma. Kwahiyo kiukweli sijasoma na sijui hayo mambo.
Watu wanacheka.๐๐
Mhe. Lissu: Baada ya CCM kukataa mapendekezo ya Nyalali Mkapa mwaka 1998 aliteua tume nyingine ya Jaji Kisanga ili kuangalia upya mfumo wa kikatiba.
Kaaya: Mimi sio mwanasiasa ndio maana siyajui hayo.
Mhe. Lissu: Jaji Robert Kisanga alikuwa ni mwanasiasa?
Kaaya: Sifahamu.
Mhe. Lissu: sasa Unafahamu Jaji Kisanga aliteuliwa na Rais kuongoza tume hiyo mwaka 1998?
Kaaya: Huyo Jaji simfahamu na kazi zake sizifahamu.
Mhe. Lissu anasema mimi siwezi kukufunga ila napenda kukamata waongo kwahiyo hufahamu pia hata maamuzi ya tume yake?
Kaaya: Hayo yote sifahamu.
Mhe. Lissu: mwaka 2003 Rais Mkapa akaunda tume ya Jaji Mac Bomani kuongoza tume nyingine ya mabadiliko ya Katiba?
Kaaya: Sio sehemu yangu ya kazi.
Mhe. Lissu: unafahamu au hufahamu?
Kaaya: sio sehemu ya kazi yangu kwahiyo sijui.
Lissu: yalipokataliwa hujui pia?
Kaaya; sijui kila kitu yani.
Mhe. Lissu: December 31, 2011 Jakaya Kikwete alitangaza ataunda tume ya Katiba ili ikusanye maoni ya Watanzania na kuandaa rasimu ya Katiba na itakapofika mwaka 2014 tuwe na Katiba Mpya?
Kaaya: sijui.
Lissu: unanfahamu Jaji warioba aliteuliwa kuongoza tume hiyo?
Kaaya: Hilo nafahamu.
Mhe. Lissu: Tume ya warioba ilipendekeza kuwe na katiba mpya na kuandaa rasimu?
Kaaya: Hilo nafahamu lilikuwepo.
Mhe. Lissu : Bunge maalumu la Katiba lilikaa zaidi ya miezi 6?
Kaaya: Nafahamu na wewe ulikuwepo pia.
Mhe. Lissu: usiwe na kiherehere sasa. Nimeuliza unafahamu tu?
Mhe. Lissu: Pamoja na kazi yote hiyo ya miaka minne CCM na serikali walikataa mapendekezo ya warioba na hakuna katiba mpaka leo?
Kaaya: Waheshimiwa majaji mchakato wa katiba ulianzishwa na serikali na bado upo kwenye utaratibu.
Mhe. Lissu: kwahiyo kuna utaratibu unaendelea toka 2013?
Kaaya: Mchakato unaendelea ulifika Bungeni lakini taratibu zingine sifahamu kabisa.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji kama unafahamu baada ya Kikwete kuondoka Akaja Magufuli na baadae Samia. Mwaka 2022 Rais Samia walianzisha maridhiano mwaka huo?
Kaaya: Hayo nilisikia.
Mhe. Lissu: je unafahamu kama hayo mazungumzo yaliongozwa na watu wazito kama Kinana wa CCM na Freeman Mbowe kwa Chadema?
Kaaya: Sikushiriki.
Lissu; unafahamu?
Kaay; sikushsiriki kwahiyo sifahamu
Mhe. Lissu : Unajua Chadema ilipeleka mapendekezo ya namna ya kufufua mchakato wa katiba mpya ili hadi 2024 tuwe na katiba mpy?
Kaaya: Sikuwepo kwahiyo sifahamu.
Part 88 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo Oktoba 10, 2025
Jana tuliishia Part 84 so leo tunaendelea na
Part 85
Mhe. Lissu ameingia,
Majaji wote watatu wameingia.
Leo humu ndani wameweka Ma TV mengi sana.
Sijui ndio wanataka kucheza hizo video lipo lingine la kama inch 70 huko lipo katikati ya Judge na Mh. Lissu.
Linawafanya wasionane kabisa.
Naona Jaji kama anaongea na Karani kuwa inapaswa hiyo ihamishwe hapo.
Inatukinga hajazungumza kwa sauti lakini tunamuelewa alichokuwa anakisema. Kwasababu ndio kinachotekelezwa hapa.
Sasa kesi inasomwa na karani hapa.
Anasima Renatus Mkude ni Wakili wa serikali Mkuu, Niko na Ajuaye Zengeli, Job Mrema, Ignas Mwinuka, Harrison Lukos, Cathbert Mbiringe na Winiwa Kasawa. Lissu yupo na ajitetea Mwenyewe.
Shauri linakuja kwa mshitakiwa kumuhoji maswali ya Dodoso.
Mh. Lissu wale wageni wangu wameambiwa hawawezi kuingia ndani ya Mahakama hii hadi wapate kibali cha idara ya Uhamiaji.
Sasa wataendelea kuwepo hadi watakapofukuzwa kuwepo nchini hadi kibali chao cha kuwepo Tanzania kitakapoisha.
Tunataka tujue Dunia ijue kama kweli uhuru wa Mahakama upo kweli au ni maneno tu.
Kwahiyo nitaendelela kusema na naomba mnisamehe kwa hilo na mnivumilie.
Majaji wanateta hapa kidogo.
Mahakamani hapa yupo Makamu Mwenyekiti wa Chama, John Heche, Naibu Katibu Mkuu Amani Golugwa, Mjumbe wa Kamati Kuu God bless Lema, Katibu Mkuu wa Bavicha Dua Lyamzito na viongozi pamoja na wanachama wengine wengi.
Majaji wanateta kama dakika tano hivi hapa Mahakamani.
Wamemaliza kuongea.
Jaji Ndunguru amewasha kipaza sauti chake anasema naomba tuisemee hii hoja kwamba sisi tunafuata utaratibu tuliojiwekea kwa kuzingatia idadi ya watu pia.
Kwahiyo tumeambiwa jambo hilo linashughulikiwa na ofisi ya Msajili naomba ndugu zako wawasiliane na Ofisi ya Msajili ili wakalimalize.
Jaji Ndunguru Nadhani tuko vizuri sasa tunaweza kuendelea.
Mhe. Lissu anamjibu tuko vizuri kabisa.
Sasa Jaji anamuonya Shahidi hapa kuwa uko chini ya kiapo.
Ukumbuke hilo.
Haya Mshitakiwa karibu sana umuulize Maswali Shahidi.
Shahidi amevaa kisweta fulani cha damu ya Mzee muonekano wake haeleweki kama anataka kulia au kucheka.
Mhe. Lissu : Insp. John Kaaya ni majina yako.
Kaaya: Ndio.
Mhe. Lissu : Nikikuuliza ndio au hapana jibu hivyo. Nikisema fafanua unafanya hivyo.
Tukienda hivyo tutamaliza upesi. Usipofanya hivyo tutaenda mpaka week ijayo.
Mhe. Lissu: Jana ulisema maneno yafuatayo ndio yalikufanya uone kauli yangu ya tar. 03/04 yalikuwa na lengo la kuitisha Serikali "Tunahamasisha uasi, tutavuruga sana sana......" ulisema hivyo.
Kaaya: Ndio kwa sauti ya chini sana.
Mhe. Lissu: Ongeza sauti Bwana we si ni askari.
Mhe. Lissu: Uchaguzi upo kwa sheria ulisema. Ni kweli au sio kweli?
Kaaya: Anajibu kuwa ni Kweli.
Mhe.Lissu : ulisema kuzuia uchaguzi bila kufuata utaratibu kama vile kupata order ya mahakama nia yake ni kuitisha serikali?
Kaaya: Ni kweli.
Mhe. Lissu: Sasa eleza mahakama kwamba kwa miaka mingi zaidi ya miaka 30 viongozi na wanachama wamekuwa wakitumia njia ya mahakama kupinga mfumo huu wa Uchaguzi?
Kaaya: Hilo sifahamu.
Mhe. Lissu : Unafahamu kama 1993 aliyekuwa Mwenyekiti wa Democratic Party Mtikila akipinga sheria za uchaguzi alifungua kesi mahakama kuu na kesi nyingine kupinga zuio la vyama vya siasa kuzuiwa kufanya mikutano ya hadhara?
Kaaya: Mimi SIJUI.
Mhe. Lissu: Unanfahamu kama Mch. Mtikila vilevile alifungua mashauri hapa mahakama kuu kupinga zuio la watu wasio wa vyama vya siasa kugombea nafasi za kisiasa?
Kaaya: Nilikuwa Shule.
Mhe. Lissu: We polisi nimekuuliza unafahamu au hufahamu?
Kaaya: SIJUI.
Mhe. Lissu : Jibu hivyo ili twende harakaharaka. Je kwenye kesi hiyo ya Mtikila mahakama kuu hii ilisema hicho kifungu cha Katiba kinachokataza watu kugombea wasio na vyama hakipo sahihi unafahamu hilo?
Kaaya: Mwaka gani ilikuwa?
Part 86 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 84
Job Mrema: Hiyo Flash utaitambuaje pia?
Kaaya: Nitaitambua ina GB 8 na ina rangi nyeupe.
Job Mrema: Waheshimiwa Majaji ni hayo tu kwa shahidi huyu.
Vituko sana. Muda wote shahidi anatusumbua nitaitambua video, nikiona kitu fulani na kitu fulani. ๐
Mwisho wa siku kumbe video yenyewe na flash hiyo italetwa na shahidi mwingine sio yeye.
Makaratasi mengi wanatumalizia misitu tu bila sababu ya msingi.๐
Ngoja sasa aanze kusokotwa.
Kinachofuata sasa ni CROSS EXAMINATION yaani maswali ya DODOSO kutoka kwa CRISTIANO RONALDO AU MESSI wa Sheria Mh. Lissu.
Jaji anasema Mshitakiwa unasemaje?
Mhe. Lissu: Mh. Jaji huyu Shahidi asiende hivi hivi naomba mnipatie nusu saa nianze nae leo leo au hata kama mkiniruhusu niendelee nae hadi saa mbili usiku niko tayari.
Jambo lingine off record jana niliwaahidi nitawaleteeni kitabu nilichoandika miaka mitano iliyopita kinaitwa "Remaining in the Shadow" kuhusu mambo ya Uchaguzi pia.
Nimebeba copy tatu hapa naomba niwape na Mawakili wa Serikali Copy moja nao wakasome ili wajue mambo mengi wasidhani mimi ni mtu wa mchezomchezo na waache kutumika tu.
Majaji pia nawapatieni copy moja.
Jaji Ndunguru anasema sasa unatupatia copy moja tunasomaje si bora ungetoa copy mbili?
Mhe. Lissu: Waheshimiwa Majaji nikiwapa mbili mtagombana sana maana mko watatu.
Watu wanacheka.
Jaji Ndunguru: Sasa wewe ugomvi wetu haukuhusu, tupe hizo copy mbili sisi tutajua cha kufanya.
Watu wanacheka. ๐๐๐
Mhe. Lissu: Basi nyie Vijana anawanyooshea Wakili Kisabo na Mahinyila kuwa hakikisheni kesho mnaongeza copy zingine 4 zije hapa.
Jaji Ndunguru anasema sasa jamani tutaendelea kesho.
Muda umeshakwenda.
Shahidi kapumzike na Mshitakiwa na wewe kajiandae na kesho tuendelee na Cross Examination saa tatu kamili asubuhi.
Inapigwa Courttttttt kubwa sana.
Majaji wanasimama na kutoka.
Kesi imeahirishwa hadi kesho asubuhi saa tatu.
Tukutane kesho wandugu.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 83
Job Mrema: Tarehe 07/04/2025 nini kilitokea?
John Kaaya: Nakumbuka nilikuwa zamu kazini. Wakati naendelea na majukumu ya kila siku. Alinipigia afande SSP George majira ya asubuhi akinielekeza niende Ofisini kwake.
Ulivyofika ofisini ikawaje?
Kaaya : Alinikumbusha kuhusu ile taarifa niliyompelekea aliniamuru nirudi Ofisini ninapofanyia kazi za doria mtandaoni na kupakua video ile katika ukurasa wa Jambo TV niipakue na baadae nimpelekee.
Nilivyopokea amri ile nilirudi ofisini kuifanyia kazi.
Nilipofika ofisini niliandaa vitendea kazi vyangu kama vile computer na notebook. Nilikagua utendaji kazi wa computer yangu na nilichukua police notebook yangu na kuchukua ile link na kuinakili kwenye program maalumu kwa ajili ya kupakua yale maudhui.
Job Mrema: Halafu ikawaje?
John Kaaya: Niliandaa Flash mpya aina ya XIOXIA yenye ukubwa wa GB 8 niliiweka kwenye computer na kuifanyia virus scanning na baadae nikaifanyia formating ili kuondoa data yoyote iliyomo mle kwenye flash.
Ndipo nikaichukua ile video na kuihifadhi katika flash hiyo.
Job Mrema: wakati unaipakua hiyo video ilikuwa na muonekano gani?
John Kaaya: ilikuwa na watizamaji elfu 52 na waliocomment mia tatu.
Kingine nilibaini ile video ilichapishwa tar. 03/04/2025 kwenye ukurasa wa Jambo TV.
Job Mrema: Kuhusu maudhui yake ulifanya nini?
John Kaaya: Niliweza kuisecure flash ile kwa ku encrypt na password.
Nilichukua pia PF 145 ambayo ni Exhibit label na niliilabel kile kielelezo na kukipa alama DM.
Radio call la askari limeanza kuita humu ndani mahakama imesimama kidogo.
Majaji hawajasema kitu wanasema haya tuendeleeee. ๐๐
Kuna mambo majaji wanakausha ila Katuga huwa ni mnoko sana angekuwepo angeweza msingizia hata Chadema yeyote hapa maana anatuchukia sana.๐
Job Mrema: Baada ya kufanya labelling uliendelea na hatua gani nyingine?
John Kaaya: Niliondoka ofisini na kuonana na afande SSP GEORGE na kwamba nimeshapakua na kuyahifadhi.
Hiyo ilikuwa ni tarehe 07/04 majira ya saa 9 mchana baada ya kufika ofisini kwa George nilionana nae na kumjulisha kwamba maelezo aliyonipa nimekamilisha.
Baada ya kumjulisha afande George alichukua diary yake na kunijulisha kuwa ameshafungua kesi ambayo ina Reference No. DSMZ/CID/PE.101/2025
Pia aliniambia niorodheshe hiyo kesi namba kwenye kile kielelezo ambacho niko nacho yaani flash aliniambia niandike maelezo yangu nimpatie.
Job Mrema: nini kikafuata?
John Kaaya: Aliniambia nikipeleke kielelezo kwa ACP Malugala mtunza vielelezo. Nilijaza namba ya jalada kwenye kielelezo. Nilichukua kielelezo DM na kukipelekea kwa ACP Malugala.
Job Mrema: Tar. 08/04 kilitokea nini sasa?
John Kaaya: Nilikuwa zamu kazini na nikiwa naendelea na majukumu yangu.
Alinipigia afande SSP George akiniamuru niende Ofisini kwake, nilisitisha shughuli zangu na kwenda kuonana na Afande George.
Job Mrema: Nini kiliendeleaa ulipofika?
John Kaaya: Nilimkuta yupo na Mpelelezi.
alinikumbusha kuhusu tukio la Tarehe 07/04/2025 kuhusu uwasilishaji wa kielelezo kwake.
Aliniambia nimpatie yule mpelelezi password katika kielelezo DM.
Nilichukua POLICE NOTEBOOK yangu kwa ajili ya kujikumbusha password yangu na kuinakili kwenye notebook ya mpelelezi niliyoamuriwa nimpatie.
Job Mrema: Je hiyo video ya tarehe 04/04/2025 utaitambuaje ukiiona?
John Kaaya: Hiyo video naweza kuitambua kwa maudhui yanayotamkwa, mzungumzaji amevaa kombati ya Kaki, nyuma ya mzungumzaji kuna rangi za Bendera ya Taifa pia itakuwa kwenye flash disk.
Job Mrema: Kwani Maudhui yaliyokuwepo kwenye hiyo video ni yapi?
Hawa watu wanatupotezea muda kabisa wanaulizana maswali yale yale yani, Wanakera sana.
John Kaaya: Anaanza kusema yale maudhui ya Lissu.
Part 84 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 82
John Kaaya: Pia aliposema Mahakamani hakuendeki ila Mahakama ni chombo cha kutoa haki na kutoa maamuzi ya mambo mbalimbali yanayobishaniwa.
Hivyo anavyojulisha umma kwamba hakuendeki ni kutoa taarifa ya uongo kwa umma na kuitishia serikali ๐
Kaaya ana akili hata kidogo huyu yani Mahakamani hakuendeki eti ni kuitishia serikali.๐๐๐
Job Mrema: Baada ya kuitizama hiyo video nini kingine ulikisikia.
John Kaaya: Lissu alisema Tutaenda kuzuia uchaguzi, tutazuia uchaguzi kwasababu wanasema tunahamasisha uasi na tutaenda kuuvuruga sana sana.
Natamani mngekuwa mnamuona huyu shahidi aiseee, kituko cha mwaka.๐
John Kaaya anaendelea: Kwa matamshi hayo niliyosema waheshimiwa majaji niliona kuna viashiria vya jinai.
Uchaguzi huandaliwa kwa mujibu wa Katiba na Sheria hivyo kuzuia uchaguzi kwa kuhamasisha uasi bila kufuata utaratibu ni kosa.
Haya yote aliyafanya lengo lake ni kuitisha serikali ambayo ndio msimamizi mkuu wa Sheria na kulinda amani.
Nilichogundua TANZANIA haitakuja kushinda kesi yoyote kimataifa kama mashahidi wetu ndio hawa na Mawakili wetu wa serikali ndio hawa akina Job Mrema kama nchi tunasafari ndefu.๐ฅน
Anaendelea hapa John Kaaya: Baada ya kuona hayo maudhui nilichukua POLICE NOTEBOOK yangu na ku note maudhui hayo niliyosema na nilinote link ambayo hayo maudhui yanahusika.
Hapa namaanisha ni ukurasa wa Jambo TV pamoja na mtoa maudhui ndugu Tundu Lissu.
Job Mrema: Kila muda unasema Tundu Antipas Lissu unamfahamu yuko wapi?
John Kaaya: anasema namfahamu na yupo hapa mahakamani.
Job Mrema: Yuko wapi?
John Kaaya: Yule pale anampungia.
Majaji wanasema ukipunga mkono maana yake umemuonesha nani?
Watu wanacheka. ๐๐๐
Shahidi ananona aibu kumuonesha Lissu kwa kidole.
Hawa watu wanawasababishia watu watende dhambi wasizotaka.
Huyu shahidi kiukweli usikute hajataka kabisa kuja kufanya hii kazi maana namuona kama hana amani๐
John Kaaya anaendelea: Baada ya kuona hayo nilimjulisha mkuu wangu wa kazi ambae ni mkuu wa kitengo cha doria mtandaoni.
Job Mrema: Hiki kitengo kipo ofisi gani?
Kaaya: Kipo ofisi ya DCI.
Job Mrema: Hiyo picha mjongeo alimaliza kuitizama muda gani?
John Kaaya: Nilimaliza kuyatizama kwenye majira ya saa nne asubuhi siku ya tarehe 04/04/2025.
Job Mrema: Ulitoa taarifa kwa mkuu wako wa kazi ulitoa taarifa saa ngapi?
Jibu: Nilipomaliza kuitizama ndio nilitoa taarifa kwa mkuu wangu wa kazi.
Job Mrema: ulivyotoa taarifa ulipata matokeo gani?
John Kaaya: Nilielekezwa kwenda Polisi kanda maalumu Dar es salaam kwa ajili ya kwenda kumjulisha Afande SSP George. Juu ya maudhui yale.
Job Mrema: Utekelezaji wa majukumu yako ikawaje?
Kaaya: Nilisimama kutekeleza majukumu mengine nilienda kuonana na Afande George ambae kwa siku ile alikuwa ni Naibu Kamanda wa Upelelezi Kanda ya Dar es salaam na ilikuwa tarehe hiyo hiyo Tar. 04/04/2025.
Job Mrema: Ikawaje?
John Kaaya: Nilivyofika nikamkuta Afande George na kumjulisha dhumuni la ujio wangu kwake.
Nilimwambia nimeelekezwa na mkuu wa kitengo cha makosa ya mtandao kuwa nije kukupa taarifa ya nilichokiona huko mtandaoani.
Baada ya kumjulisha alinielekeza, nimuonyeshe picha mjongeo zile na nilimuonyesha kupitia simu janja yake kwa kuingia kwenye ukurasa wa Jambo TV.
Job Mrema: Ikawaje tena?
John Kaaya: Basi nilichezesha picha mjongea ile kwa kumuonyesha baadhi ya vipande nilivyobaini vina viashiria vya jinai.
Hapa nazungumzia ile video ya tundu lissu uso kwa uso na watia nia majimboni No reforms, no election.
Job Mrema: Nini kikafuata?
John Kaaya: Afande George alichukua Police Notebook yake na kujaza taarifa kuhusiana na picha mjongeo ile na baada ya kuchukua baadhi ya taarifa muhimu, aliniamuru kurudi eneo langu la kazi kuendelea na majukumu mengine.
Part 83 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 81
Mahakama imeanza muda huu.
Majaji wameingia.
Mheshimiwa Lissu alivyoingia kabla ya Majaji amewaambia Mawakili anzeni kuandaa submission ya No Case to Answer maana hakuna kitu hapa.
Mawakili wa Serikali wanacheka.
Anasema Jaji Ndunguru kuwa sasa kabla hatujaahirisha kulikuwa na suala hapa la kulitolea uamuzi mdogo atasoma mwenzangu hapa Jaji Kiwonde.
Anaanza hapa Jaji Kiwonde. Shahidi alisema habari za vibegi vya kura feki na mshitakiwa alipinga hapa.
Baada ya sisi kutafakari swali la msingi tulijiuliza kama mahakama hii ilishatoa amri ya kuzuia maudhui yaliyoonwa yasitolewe ushahidi.
Mahakama siku ya Jumatatu ilisema masuala yanayohusu vibegi vya polisi na utendaji kazi wa mahakama ya Tanzania.
Hicho ndio tulichokizuia siku ya Jumatatu.
Kwenye kesi hii tumeona shahidi namba mbili anasema alichokiona kwenye mtandao wa Kijamii.
Lakini yule wa kwanza yeye alikuwa anatoa ushahidi kama anafahamu mambo hayo.
Huyu anaeleza alichokiona na sisi tunamwambia asifike mbali aishie kwenye kusema alichoona.
Pingamizi halina mashiko.
Shahidi aendelee kutoa ushahidi wake.
Hiyo ndo ruling mtaelewa wenyewe maana binafsi nimejitaidi kuelewa lakini naona Jaji ananivuruga tu hapa ila ndo Mahakama zetu tutafanyaje.
Haya tuendelee
Job Mrema: Sasa shahidi endelea
Kaaya: Lissu alisema hawa mapolisi mnawaona wana vibegi vya kura
Maneno mengine alisema.. kwakuwa majaji nao ni watu wa Rais na wao ni MACCM. Wanataka wapandishwe vyeo kwenda kwenye mahakama za rufani kuteuliwa kwenye commissions na kwenye tume ndiko kuna hela.
Hayo maneno niliona akisema Mshitakiwa.
Akaeleza tena kwahiyo MAHAKAMANI HAKUENDEKI.
Maudhui mengine aliyotamka ni kwamba NA MIMI NATAKA NITEULIWE KWENYE KACHEO FULANI NCHI HII,
UKisema na mimi unamaanisha nini shahidi?
Jaji anaingilia sasa ndugu MREMA Shahidi anasema hayo maneno aliyasema Lissu wewe ukisema anamaanisha nini akisema NA MIMI unamuuliza hilo swali kwani ni yeye ndio ameyasema huyo si ana quote tu?
Job Mrema: Sawa Mheshimiwa Jaji naomba nisamehewe nilidhani ni maneno yake anasema.
Anaendelea Kaaya: anaanza kusema maneno mengine lissu alisema "Mkutano wetu unasema NO REFORMS NO ELECTION, Wamesema Kitu kimoja sahihi hapa kwamba tunapanga kufanya uasi, ni kweli tunaashiria uasi.
Tutakinukisha vibaya sana, tutakinukisha sana sana.
Kitu nimegundua ni kwamba haya Mapolisi yamekaa huko kituoni kukariri Hotuba ya Mh. Tundu Lissu ambayo yeye hata hakatai hayo maneno wa kila siku ya Mungu wanayarudi tu kama Sara ya Baba yetu.๐
Nafikiri hawana kitu cha kukitolea ushahidi.
Eniwei tuendelee
Job Mrema: Ulivyomaliza kusikiliza Video ulibaini nini?
John Kaaya: Nilibaini matamshi yale yana viashiria vya jinai.
Job Mrema: Shida gani?
John Kaaya: Maneno yavibegi niliona yanapotosha umma.
Jaji Kiwonde: sasa mnaona huko mnaanza kuelekea tena kwenye vibegi.
Mhe. Lissu: Mhe. Jaji huu ushahidi aachwe aendelee kuutoa tu maana nilipinga mkasema ni sahihi aendelee sasa nafikiri asikatazwe acha aseme tu. ๐
Jaji Ndunguru: Basi aendelee hakuna shida.
Job Mrema: Ieleze Mahakama Shahidi ulikuwa unaelezea viashiria vya makosa kwenye maneno hayo.
John kaaya: Waheshimiwa Majaji pamoja na hayo matamshi niliyosema, pale aliposema kuwa mahakamani hakuendeki kwasababu majaji ni watu wa Rais na ni MACCM niliona taarifa hiyo ina viashiria vya jinai. ๐๐
Anaendelea pia shahidi kusema kanuni za utumishi wa umma zinakataa watumishi kuwa wafuasi wa vyama vya siasa.
Yani Job Mrema na John Kaaya wamekutana hapa ni pipa na mfuniko. Wanzingua sana yani wanapa uvivu kuandika maana kuna muda wanaongea hivi havieleweki
Kaaya kuna muda anaongea sauti ya chini hadi Jaji anamwambia ongeza sauti ni muoga muoga sijui Polisi wa wapi huyu au ndio mjanja akiwa anapiga doria mtandaoni.
Part 82 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 80
Job Mrema: ukawa unafanya nini?
Inspector Kaaya: nikawa naperuzi na niliingia YouTube. Nilivyoingia YouTube nilibaini machapisho mbalimbali ya video. Mojawapo ya Chapisho ni katika ukurasa uliosajiliwa kwa majina ya JAMBO TV na niliona picha iliyokuwa imeambatana na maneno TUNDU LISSU USO KWA USO NA WATIA NIA MAJIMBONI. NO REFORMS NO ELECTION NJIA PANDA.
Baada ya kuona picha mjongeo hiyo niliweza kuchezesha picha mjongeo hiyo ili niweze kuona maudhui yaliyochapishwa.
Lengo la kuchezesha lilikuwa ni nini?
Kaaya; Ili nione maudhui yaliyopo humo ni nini?
Sasa ili iweje ukishaona hayo maudhui?
Kaaya: Lengo ni kubaini kilichozungumzwa.
Kwanini uliingia sasa?
Kaaya: Nilishangaa kuona video ile ina watizamaji wengi elfu na 39 nikaona ngoja na mimi niingie kuona kuna nini na watizamaji 300 niliona wamecomment.
Sasa shahidi unaweza kueleza mahakama majukumu yako ni yapi?
Kaaya: Majukumu yangu ni kuperuzi kwenye mitandao ya kijamii kubaini makosa yanayofanywa.
Sasa ieleze mahakama hiyo sjju ya tarehe 04/04 uliingia kule kufanya nini?
Anasimama Lissu kuwa hilo swali lilishajibiwa alishasema aliingia kuwa video ile ilikuwa imetizamwa na watu wengi na waliocomment nikashawishika ni maudhui gani yamechapishwa humo.
Baada ya kuingia ulibaini nini humo ndani shahidi?
Kaaya anajibu nilivyotizama niliweza kubaini baadhi ya matamshi yenye viashiria vya jinai.
Viashiria hivyo ni vipi?
Shahidi anasema viashiria ni aliposema kuwa kwa kuwa hatuna access na hizo server za tume na Mapolisi ndo hao mnawaona na vibegi vya kura feki.
Mhe. Lissu anasema haya mambo ya vibegi feki yalishakataliwa na Mahakama siku ya juzi hauwezi kuletwa leo tena unahusiana na kesi iliyopo kisutu.
Naona Majaji wanajadili kidogo.
Job Mrema anajibu kwamba kwa upande wa Jamhuri tunapinga hilo pingamizi kwasababu kesi ya Mukisa Biscuits imeeleza pingamizi lazima liwe na sheria iliyotajwa.
Kuibuka ubishani wa kisheria hapa kati ya Mawakili wa Serikali na Mhe. Lissu
Sasa anasimama Mh. Lissu kuwajibu mawakili wa Serikali kuhusu hilo pingamizi dogo la namna ya kutoa ushahidi.
Waheshimiwa majaji nimesikiliza majibu marefu ya hawa wenzangu: nilidhani wasingebisha.
Cha ajabu wamemuachia anijibu huyu Job Mrema wakati yeye hakuwepo sasa mkimkubalia huyu na mlikataa kwa yule PW1 ambae ni George.
With all due respect nafikiri Mrema alikuwa anaongea jambo ambalo halifahamu.
Unaleta kesi ya Mukisa ambayo yenyewe inahusu mapingamizi ya mamlaka ya Mahakama.
Sasa hiyo kesi unatutajia leo ya nini kwenye hatua hii ambayo tupo sasa?
Waheshimiwa Majaji naomba mlikubalie ombi langu.
Majaji wanajadiliana hapa
Kwenye chuma cha Mahakama kuna ukimya fulani hivi nakumbuka tukiwa watoto mkiwa darasani mnapiga kelele ghafla mnajikuta wote mpo kimyaaaaa, tulikuwa tunasema shetani kapita ndo kama huo sasa.๐
Tunasubiri Majaji wamalize kujadiliana then watoe uamuzi kuhusu ombi la Mhe. Lissu.
Part 81 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba Repost yako.