Haki haiombwi kwa hofu, inadaiwa kwa ujasiri.
Hatutanyamazishwa na vitisho, kesi za mchongo, wala ukandamizaji unaofanywa na serikali kupitia vyombo vya dola na Mahakama.
Tunataka Katiba Mpya na Tanzania yenye haki kwa wote. ✊🏿⚖️🇹🇿
#KatibaMpya#FreeTunduLissu#justice
Safari ya jana Kilwa kumpumzisha Mh. Bwege imetukumbusha msimamo wake thabiti kwa watu wake na rasilimali zao. Tumempa heshima mwanamapinduzi wa kweli.
Tulizungumza pia na Wakojani kuhusu siasa na uchumi, na kuwaunga mkono. 🕊️⚓
#RIPBwege#Kilwa#StandForJustice#HakiKwaWote
Imani imetuunganisha, dua zinatuongoza 🤲🏾🤍
Istamaa’ la wajada (ٱسْتَمَعَ لَوَجَدَ).
Kiongozi bora husimama kwenye haki, husikiliza watu wake, na hutenda kwa uadilifu.
Hatutaongozwa na hofu, bali na imani. ✊🏾
Haki yetu ni silaha, ukweli ni dira.
“Wala msikubali udhaifu ushinde, bali simameni imara kwa ajili ya haki.” – Surah Al-Hajj 22:41
“Tenda haki, penda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako!” – Mika 6:8
#standforjustice
Tumepokea kwa masikitiko kifo cha Muasisi wa CHADEMA, Baba yetu Mzee Edwin Mtei.
Leo tunalia, lakini hatuyumbi.
Urithi wako unaishi ndani ya CHADEMA na mioyoni mwa vijana.
Pumzika kwa amani, Baba yetu. Mapambano yanaendelea. ✊🏽🔥🕊️
#FreeTunduLissu#StrongerTogether
Miaka 33 ya CHADEMA.
Vijana tumesimama.
Hatubebi woga — tunabeba mabadiliko.
Hatutorudi nyuma mpaka haki, uhuru na maendeleo ya kweli vitawale nchi yetu.
Sasa ni wakati wetu. ✊🏽🔥
#FreeTunduLissu#KatibaMpya#FreedomOfSpeech
Assalaam Alaikum Warahmatullahi Wabarakaatuh.
Hakuna amani bila haki.
Haki ikinyamazishwa, taifa hulipuka.
Haki ikisimama, amani hudumu.
Qur’an 16:90
“Hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha uadilifu na anakataza dhuluma.”
Jumaa Kareem 🤲🏽
“Hesabu 35:33
Hivi hamtaitia unajisi nchi ambayo mwakaa; kwa kuwa damu huitia nchi unajisi; wala hapana sadaka itoshayo kwa ajili ya nchi, kwa ajili ya damu iliyomwagwa ndani yake, isipokuwa ni damu ya huyo aliyeimwaga.”
Oktoba 29, 2025 — Tanzania
Damu ya vijana na wananchi isiyo na hatia imeacha doa kwenye ardhi yetu.
Haki isiposimama, taifa linajeruhiwa.
Ukimya wetu hauponyi nchi—uwajibikaji ndio uponyaji.
Vijana tuseme:
Hatutakubali mauaji na utekaji viendelee kuwa kawaida.